Kuomba Maombi ya Paulo kwa Waamini Wapya.
Maombi ya Paulo kwa waamini wapya yanaelezea zaidi kazi ya ufuasi. Maombi haya yanatuongoza sisi kuomba kwa ajili ya Wakristo wachanga kwa sababu tunapaswa tuombe mambo yale yale ya kufanana kwa ajili yao ambayo Paulo alikuwa anaomba. Maombi haya pia yanaongoza huduma zetu kwa sababu tunapaswa tushiriki kile Mungu anachokifanya kwa ajili ya huduma hizo.
Tuangalie maombi ya Paulo kwa ajili ya vikundi vitatu.
Wathesalonike
► Soma 1 Wathesalonike 5:23-24.
Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike unatoa mwito kwa ajili ya utakatifu. Kila mwamini anaitwa kuishi katika maisha ya utakatifu na usafi, na ahadi za Mungu ambazo zinaweezekana kwa njia ya imani. Tunapaswa kuomba na kufundisha kwa lengo la kumleta kila mwamini kwenye ushindi na usafi.
Wafilipi
► Soma Wafilipi 1:9-11.
Aya hizi zinaelezea kuhusu mchakato endelevu katika maisha ya mwamini. Upendo wake unatakiwa uwe unaoendelea kukua mfululizo. Wakati hilo likifanyika, uwezo wake wa kutambua yaliyo mema unatakiwa nao uongezeke. Akiwa anaendelea kutambua, anayaweka maisha yake katika kutazama kilicho bora zaidi. Hali hii inatakiwa iwe inafanyika kwa kusudi la yeye kuwa msafi (mwenye moyo safi) na bila kuwa na kosa.
Watu ambao Paulo aliwaandikia katika aya hizi tayari walikuwa wameshakuwa Wakristo kwa muda kadhaa. Lakini, bado Paulo alikuwa akiomba kwamba wawe wakiongezeka katika upendo wao kwa Mungu, na, kwa upendo huo, waweze kuelewa vizuri zaidi mapenzi ya Mungu yaliyo kwa ajili yao.
Hapa kuna maswali ambayo mwamini mchanga anapaswa atafakari;
- 
	
Je, kuna mfano gani wa mabadiliko ambao nimeufanya katika maisha yangu wakati Mungu aliponionyesha kwamba tabia, silika au kitendo hakikuwa kitu kizuri sana?
 - 
	
Je, kuna jambo lolote katika masha yangu ambalo nina mashaka kuhusiana nalo?
 - 
	
Je, niko tayari kumruhusu Mungu anionyeshe katika maombi mabadiliko yeyote ambayo ninapaswa niyafanye?
 
Wakolosai
► Soma Wakolosai 1:9-12.
Aliomba kwamba waweze kupata maarifa ya mapenzi ya Mungu katika hekima yote na ufahamu wa rohoni. Mtu mpya aliyeookoka bado huwa hawezi kuelewa mambo yote kuhusu mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yake. Atakuwa anaona hatua kwa hatua kwamba baadhi ya mienendo, maneno na tabia katika maisha yake vinabadilika. Kwa kuwa anampenda Mungu, atakuwa mara kwa mara anapatanisha zaidi maisha yake kwenye mapenzi ya Mungu. Mtumishi wa huduma ya ufuasi atapaswa kuwa anaomba na kwa uangalifu akifundisha waamini wapya kuyatambua mapenzi ya Mungu.
Alisema kwamba waweze kufanya, kama matokeo ya ufahamu mzuri wa mapenzi ya Mungu, “waenende kama ulivyo wajibu wao kwa Bwana.” Watakuwa ni wawakilishi wa Mungu wa kufaa zaidi. Maisha yao yatafanana zaidi na ujuzi wa kubadilishwa kwa neema. Anachotakiwa kukumbuka mhudumu wa uanafunzi ni kwamba hadi hapo mchakato huu utakapokuwa umeendelea kwa muda fulani, baadhi ya mambo yenye kukinzana yatajidhirisha kwenye maisha ya Mkristo mchanga.
Sehemu ya “kutembea kuliko na manufaa” hujumuisha pamoja na “kuwa mtu mwenye kuzaa matunda kwenye kila kazi njema.” Hatupaswi kuwa na mshangao wakati tunapomwona mwamini mchanga bado hajaweza kuzaa matunda kwenye kila kazi njema. Atakuwa bado hajaweza kuwa tayari kuwajibika na kuwa makini katika kazi kama ambavyo ingetakiwa awe.
Aya hizi vilevile hutueleza kwamba tunaweza kuwa na, “uvumilivu na mateso ya muda mrefu kwa furaha.” Mtu ambaye anaweza kuwa na furaha ya kikristo anapokuwa anahudumia na kuvumilia atakuwa amepata kiwango kidogo cha ukuaji wa kiroho.
Hitimisho kuhusu Maombi ya Paulo
Maombi ya Paulo kwa Wakristo wachanga yanatuelezea zaidi kuhusu kazi a ufuasi. Tunapaswa tuwe na malengo sahihi kwa ajili maendeleo ya waamini. Tunapaswa tuwe na uwezo wa kutambua maendeleo, Hatupaswi kushangaa tunapoona mambo ya kukinzana, kutokuelewana, na kutowajibika ndani ya vijana wadogo wa Kikristo. Tunapaswa tusitegemee kuona sifa zote za Mkristo zitajitokeza ghafla.
Tunapaswa tutambue kwamba Paulo hakuwa anajihusisha sana na huduma zao za mafunzo au kuendeleza ujuzi wa huduma. Alihusika sana na maendeleo ya imani yao na tabia ya Mkristo. Hatupaswi kuendelea kuridhika na watu ambao wanaweza kufanya kazi za huduma lakini wanakosa kuwa na tabia ya Mkristo.
Mwalimu ni muhimu kwa sababu ya mfano wake, na kwa sababu ya thamani ya taarifa. Kujifunza kunasisitizwa katika aina mbili za maombi hapo juu. Ujuzi unahusika kwenye mchakato wa kiroho. Mwalimu ana mguso mkubwa kutokana na matumizi yake ya ukweli.
Tunapaswa tuombe maombi ya Paulo kwa ajili ya Wakristo wachanga tunaowapatia hamasa. Tunapaswa tushirikiane na Roho Mtakatifu ili kuwezesha michakato yote kujitokeza ndani ya maisha yao.
Maombi yafuatayo hapa chini yanatokana na maombi ya Paulo kwa ajili ya Wakristo wapya.