Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 11: Kuhubiri Kiuinjilisti

11 min read

by Stephen Gibson


Utangulizi

► Mwanafunzi atapaswa kusoma 1 Wakorintho 1:17-25 kwa ajili ya kikundi. Je, mbinu ya Mungu ya kuokoa watu waliopotea ni ipi?

Wayahudi walikuwa wanatafuta nguvu za kulikomboa taifa lao. Walihitaji ujumbe wa nguvu pamoja na alama za nguvu kuthibitisha kwamba itafanya kazi.

Mataifa walikuwa wanatafuta hekima ya kuelewa maisha na kwa ajili ya kupata mafanikio katika dunia. Walihitaji ujumbe ambao ungewafafanulia jinsi ya kupata kile walichokuwa wanahitaji.

Msalaba uliwakilisha kujisalimisha na dhabihu. Kwa Wayahudi ambao walikuwa wanataka nguvu, ilionekana kama ni udhaifu. Kwa Mataifa ambao walitaka hekima ya kidunia, ilionekana kama ni upumbavu. Kiuhalisia, nguvu na hekima ya Mungu ilidhihirishwa katika kifo cha Kristo. Msalaba ulionekana kama ni udhaifu na upumbavu wa Mungu, lakini ulikuwa ni bora zaidi kuliko juhudi nyingi sana za wanadamu.

Ujumbe wa injili uko kinyume na vitu, na tamaa za dhambi za kibinadamu. Unatoa wito wa kutubu na kujisalimisha kwa Mungu. Unaonekana kama ni ujumbe wa kipumbavu, kwa sababu watu wanataka kusikia kuhusu jinsi ya kupata kile wanachokitaka.

Mungu amechagua kutumia injili kwa ajili ya kuokoa watu. Ametoa jukumu la mawasiliano kwa waamini. Neno kuhubiri halina maana ya kurejelea kwa mtu anayezungumza na umati wa watu tu, bali ni kwa mawasiliano ya injili kwa njia mbalimbali. Kiini cha kifungu siyo kwamba kuhubiri hadharani ndiyo mbinu ya Mungu iliyochaguliwa. Kiini ni kwamba injili ni mbinu ya Mungu.

► Je, kifungu kinamaanisha nini kinaposema kwamba kuhubiri kuhusu msalaba ni upumbavu kwa wale wasioamini?