Kumbukumbu kwa Kiongozi wa Darasa: Mwanzoni mwa kipidi hiki, wanafunzi watapaswa kutoa taarifa ya uzoefu wao wa ushirikishaji wa Injili kwa kutumia mbinu iliyoko kwenye somo lililopita. Kumbuka kwamba wanafunzi wanahitaji kutiana moyo mmoja kwa mwingine. Kila mwanafunzi aliyeshirikisha injili amekamilisha jambo fulani la muhimu sana hata kama msikilizaji wake hakuonyesha uwajibikaji ulio chanya.
Kwenye maandalizi ya somo hili, hakikisha kwamba una ubao wa kuandikia kwa chaki, ubao mweupe au makaratasi makubwa kwa ajili ya kuelezea michoro kwa wanafunzi wa darasa.
Hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo (1 Yohana 1:3).
► Je, kuna sababu gani aliyoitoa mtume kuhusiana na kushirikisha injili?
Tumepata uzoefu wa nini maana ya kukutana na Mungu na kuokoka, kwa ajili ya kuanzisha uhusiano pamoja naye. Pia tuna uhusiano na watu wengine ambao nao wako kwenye uhusiano na Mungu. Tunaposhirikisha injili, tunawakaribisha watu wengine kuja kwenye uhusiano ambao na sisi tunao pamoja na Mungu na wngine wanaomjua yeye.
Uwasilishaji huu wa injili ni wa maneno machache na ya kukumbuka. Uwasilishaji unatumia mchoro ambao utaweza kukumbukwa na mtu yeyote anayeuona jinsi unavyowasilishwa.Unaweza ukawasilishwa kwa dakika mbili, au muda ukaongezwa kwa ajili ya majadiliano na utolewaji wa maelezo endapo msikilizaji ni mwenye uhitaji wa kusikia.
Siyo lazima uwe mchoraji mwenye ujuzi. Mchoro wenyewe ni mrahisi, na kutokana na urahisi wake kunamsaidia msikilizaji kuweza kukumbuka.
Sasa tutaenda kwenye hatua za uchoraji, pamoja na maelezo ya maneno yatakayokwenda na kila sehemu itakayochorwa.
Kumbukumbu kwa Kiongozi wa Darasa: Onyesha uwasilishaji wakati wanafunzi wakiwa wanaangalia. Jitahidi usiongeze maneno ya ziada kwenye uwasilishaji wako. Uwasilishaji unapaswa uwe mfupi ili wanafunzi waweze kujifunza kwa urahisi. Wanafunzi hawapaswi kuandika kwenye mchoro wakati wakiwa wanaangalia ukitolewa maelezo kwa mara ya kwanza.
Katika kutoa maelezo kwa mara ya pili, wanafunzi watapaswa kuchora kila hatua ya mchoro wakati kiongozi wa darasa atakavyokuwa anauchora kwenye karatasi au ubao mkubwa zaidi ambao darasa wataona. Usijaribu kuongeza maelezo ya ziada kwenye uwasilishaji. Baada ya maelezo ya mara ya pili, wanafunzi wataendelea kugundua maelezo yaliyotolewa kwenye sehemu ya pili, kisha watarejea tena nyuma kufanyia mazoezi uwasilishaji.
“Mungu alimwumba kila mtu awe kwenye uhusiano pamoja naye na kuishi maisha yaliyobarikiwa. Hakupanga maisha yawe ni ya matatizo na mateso chungu zima.”
Sehemu ya 2
“Mwanadamu ametenganishwa na Mungu kwa sababu ya dhambi. Watu wa mwanzo walitenda dhambi, na tangu hapo kila mtu ametenda dhambi dhidi ya Mungu.”
Sehemu ya 3
“Mungu ni hakimu wa haki, na siku moja wenye dhambi watahukumiwa kwenda kwenye moto wa milele isipokuwa wawe wametafuta rehema za Mungu na kurejea kwenye uhusiano tena pamoja na Mungu.”
[Chora mshale na andika neno “motoni.”]
Sehemu ya 4
“Hakuna lolote tunaloweza kulifanya kwa ajili ya kuturejesha tena upya kwa Mungu au kupata rehema ‒ siyo kwa matendo mema, siyo kwa kwenda kanisani, siyo taratibu za kimadhehebu, na wala siyo kutoa fedha....”
[Chora mshale kuonyesha kila kilichotajwa kwenye orodha.]
Sehemu ya 5
“Hali yetu ingekuwa mbaya sana kama Mungu hangefanya njia kwa ajili yetu ya kurejea kwake. Yesu, Mwana wa Mungu alikufa juu ya msalaba ili tuweze kusamehewa. Baada ya siku tatu, alifufuka kutoka kwa wafu.”
[Chora msalaba.]
Sehemu ya 6
“Lakini haitoshi tu kujua haya. Kila mtu binafsi atapaswa kufanya chaguo la kuokoka na kurejea tena kwa Mungu. Mtu ni lazima atubu, ikimaanisha kwamba ni kujutia kikamilifu kuhusu dhambi na kuwa tayari kwa hiari yake mwenyewe kuachana nazo. Mtu anayetubu anaweza kupata msamaha kwa kumsihi Mungu kwenye maombi.”
[Chora mshale kisha andika maneno “tubu” na “pokea.”]
Sehemu ya 7
"Ni wapi unapofikiri kwamba upo katika mchoro huu? Je, kumewahi kutokea kuwepo na muda maalumu katika maisha yako ambao ulitubu dhambi zako, ukapokea msamaha wa Mungu, na ukaanza kuishi kwa ajili ya Mungu; au bado umetengwa na Mungu kutokana na dhambi yako?”
[Subiri kupata jibu. Watu wengi watakiri kwamba bado wametengwa na Mungu.]
"Uko tayari kufuata hatua hii—Kutubu, kupokea msamaha, na kuanza kuishi kwa ajili ya Mungu? Nitapendezwa sana kuomba pamoja nanyi sasa hivi."
[Fanya maombi yanayokaribia kufanana na haya yafuatayo.]
"Bwana, ninajua mimi ni mwenye dhambi na ninayestahili adhabu ya milele. Ninajutia dhambi zangu na niko tayri kuachana nazo. Ninaomba unisamehe, siyo kwa sababu ninastahili, bali kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yangu. Asante kwa wokovu wako. Kuanzia sasa, nitaishi kwa ajili yako tu.”
Maelezo
Sehemu ya 1
Mwanzo wa kuwasilisha unaweza kurekebishwa ili kuendana na mahitaji ya msikilizaji. Badala ya “maisha yawe ni ya matatizo na mateso chungu zima” mwinjilisti anaweza kutumia kitu kingine cha uhakika zaidi ambacho kitafanana na uzoefu wa msikilzaji.
Sehemu ya 2
Ni muhimu kwa msilizaji wako kutambua kwamba yeye binafsi ni mwenye hatia kutokana na dhambi na ametengwa na Mungu. Hayuko kwenye hali ambayo imetokana na dhambi ya Adamu.
Sehemu ya 3
Hii inaonyesha hali mbaya ya mwenye dhambi.
Sehemu ya 4
Kusudi la sehemu hii ni kumwonyesha msikilizaji kwamba hapaswi kuweka utii wake kwenye kitu kinachopotosha kwa ajili ya wokovu. Sehemu hii inaweza kutumika katika kufananisha na mahitaji ya msikilizaji. Mwinjilisti atapaswa ajitahidi kutaja vitu ambavyo inawezekana msikilizaji akaweka utii kwake.
Sehemu ya 5
Njia rahisi ya kuelezea mateso na kifo cha Yesu msalabanini kusema kwamba “Yesu alikufa juu ya msalaba kama dhabihu ili kwamba tuweze kupata msamaha.” Kusudi la sehemu hii ni kumsaidia msikilizaji ajue kwamba anapaswa kutegemea kwenye wokovu ambao Mungu aliutoa.
Sehemu ya 6
Mwinjilisti anajaribu kumleta msikilizaji kwenye kipindi cha kuweza kufanya maamuzi. Msikilizaji anahitaji kutambua kwamba atapaswa afanye maamuzi binafsi. Anahitajika afahamu tafsiri sahihi ya toba, ili awze kujua kwamba toba ni zaidi ya kuwa na majuto na ni zaidi ya kusema anaomba samahani. Anahitajika ajue kwamba anapaswa aombe ili amsihi Mungu kwa ajili ya msamaha.
Sehemu ya 7
Kwenye hatua hii, Mwinjilisti anajaribu kumleta msikilizaji kwenye kukiri hitaji lake la kuokoka. Uwasilishaji umepangwa katika kumsaidia mtu ambaye hajaokoka kutambua kuwa bado hajaokoka. Swali limeandliwa kwa umakini mkubwa sana. Watu wengi wanafikiri wanaweza kila siku wakaomba kwa ajili ya msamaha wakati wanaendelea kuishi kwenye maisha ya dhambi. Swali linauliza kuhusu muda maalumu ambao mtu anaokoka na kuhusu maisha mapya anayoanza. Anatakiwa atambue kwamba kama bado hajawahi kuwa na uzoefu wa mabadiliko, ametengwa na Mungu kwa dhambi yake. Kisha mwinjilisti atapendekeza kufanya maombi pamoja naye kwa ajili ya wokovu.
Kama msikilizaji haelewi hitaji lake au hayuko tayari kutubu, mwinjilisti asimhimize kuingia kwenye maombi. Kama atajilazimisha kuomba bila ya kutubu kwa kumaanisha na kujionea mabadiliko, anaweza akawa na wokovu wa uongo au anaweza akaamini kwamba mabadiliko hayawezi yakatokea kwake. Kwa vyovyote vile, inawezekana asije kuokoka hapo baadaye.
Mchoro unaweza kuwasilishwa kwa haraka. Kama unayo nafasi ya kushirikisha injili, kwa wepesi tu unaweza ukauliza, “Je, ninaweza kuchukua angalau dakika mbili za kukuonyesha mchoro unaoelezea kile ambacho Biblia inaelezea kwamba ni njia ya kujua kwa uhakika kama kweli umeokoka? Kwa hatua hiyo kunamfanya mtu ajue kwamba hutaenda kutumia muda wake mwingi. Kama ataonyesha kuvutiwa na anataka kuzungumzia kuhusu hiyo, hapo unaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kwa kawaida, watu wengi huvutiwa na michoro. Mara nyingi mtu ataomba kuuhifadhi mchoro huo baada ya mwinjilisti kumaliza huduma.
Kumbukumbu kwa Kiongozi wa darasa
Onesha uwasilishaji tena kwa mara kadhaai. Epuka kuingiza ushauri wa zida au ufafanuzi kwenye uwasilishaji kwa sababu wanafunzi watajifunza kwa urahisi zaidi kama utakuwa mfupi. Baada ya maonesho kadhaa, wanafunzi baadhi wanaweza wakafanya maonesho kwa kubadilishana kwenye kikundi, wakati wanafunzi wenzao katika kikundi wakiwasaidia kukumbuka mambo muhimu kwa undani zaidi. Kisha, wanafunzi wanaweza wakagawanyika kwenye vikundi vya watu wawili wawili na kufanya mazoezi ya uwasilishaji kila mmoja na mwenzake.
Kazi za Kufanya
(1) Wasilisha injili kwa kutumia daraja la mchoro kwa angalau watu watatu ambao hawajaamini. Andika aya moja kuelezea kila uzoefu na ujiandae kuelezea kuhusu uzoefu huo kwenye kipindi kingine cha darasa kitakachofuata.
(2) Katika maandalizi ya somo litakalofuata, soma na utafakari katika Warumi 1-3, Warumi 5, na Warumi 10.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.