Wape wanafunzi wafanye mtihani uliooneshwa kwenye somo lililopita. Wanafunzi wanatakiwa waandike majibu yao kutoka katika kumbukumbu zao tu bila ya kunukuu kutoka mahali popote au mtu kuzungumza na mwenzake.
Wakati tunapofanya kila linalowezekana katika kupokea mafunzo ya huduma na njia za kujifunza, kuna hatari ya kutaka kutegemea uwezo wa kibinadamu kwa ajili ya huduma. Lakini, kama Mtume Paulo alivyosema, “Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu” (2 Wakorintho 3:5).
Paulo alisema kwamba hakuwa anafundisha kwa hekima za kibinadamu au kwa kutegemea ushawishi wa kibinadamu; lakini alitumainia kwenye udhihirisho wa Roho Mtakatifu ili kwamba imani ya msikilizaji wake isiweze kutegemea kwenye hekima za kibinadamu, bali hekima za Mungu (1 Wakorintho 2:4-5). Paulo alikuwa mwanazuoni, lakini hakutegemea ufahamu na ujuzi wake katika kutengeneza matokeo ya kiroho.
Akiandika kwa Wathesalonike, Paulo alisema, “Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi” (1 Wathesalonike 1:5). Waliridhishwa na injili kwa sababu ya nguvu ya Mungu.
Yesu aliwaahidi mitume kwamba Roho Mtakatifu atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” (Yohana 16:8). Yesu alisema kwamba, hakuna watu wanaoweza kuja kwake, wasipovutwa na Baba (Yohana 6:44).
Vipengele vichache vinavyohusiana na Kazi za Roho Mtakatifu
Anamwona na hatia mwenye dhambi (Yohana 16:8).
Anambadilisha mwenye dhambi aliyeonekana ana hatia (Yohana 3:5).
Anatawala matendo ya matamanio ya mwili ya mtakatifu anayeongozwa na yeye na kwa jinsi hiyo anamfanya kuwa mwenye haki (Warumi 8:13).
► Je, ni kwa jinsi gani utegemezi wa Roho Mtakatifu unatuongoza sisi katika njia yetu ya kufikia kwenye uinjilisti? Ni mambo gani tunayafanya tofauti kwa sababu tunamtegemea Roho Mtakatifu?
Thamani ya Mafunzo
► Je, tufikirie nini kuhusiana na mafunzo na mbinu za uinjilisti?
Tumeitwa ili kuwakilisha ukweli wa Mungu. Tunatakiwa tuwasilishe katika njia ambayo ni nzuri sana ili tuweze kueleweka.
Hatupaswi kufikiria kwamba kwa kuwa sisi ni tegemezi kwa Roho Mtakatifu hatupaswi tena kuendeleza uwezo wetu kwa njia ya mafunzo.
Paulo alisema alijaribu kuwashawishi watu (2 Wakorintho 5:11). Alimwagiza Timotheo kujifunza ili awe na uwezo wa kuwasilisha ukweli wa Mungu kwa usahihi (2 Timotheo 2:15). Mojawapo ya sifa za askofu ni kwamba ana uwezo wa kufundisha (2 Timotheo 2:24).
Apolo alikuwa na ufanisi mkubwa sana kama mwinjilisti. Anaelezwa kuwa ni mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa, alikuwa hodari katika Maandiko, na mwenye roho iliyokuwa ikiwaka kwa hamasa (Matendo 18:25-26). Uwezo wake wa asili, ukichanganya na karama za kiroho, zilimfanya awe mtu aliyekuwa wa baraka sana.
Mtume Petro anatuambia kwamba tuwe tayari siku zote kumjibu kila mtu aulizaye habari za tumaini lililo katika injili (1 Petro 3:15).
Maandiko haya yanatueleza kwamba Mungu atabariki na kutumia uwezo wetu wa asili pamoja na mafunzo kama tutakuwa tumejitolea kabisa kwa ajili ya kusudi lake. Anatuita tuzitoe nguvu zetu na uwezo wetu kwa ajili ya kazi yake.
Kujazwa Roho Mtakatifu
Katika Matendo 1:4-5, Yesu aliwaambia wanafunzi wake kungojea ubatizo wa Roho Mtakatifu, ambao aliuita “Ahadi kutoka kwa Baba.” Tukio hili litajumuisha pamoja na ujazo wa nguvu za kustahimili zitakazowafanya wawe mashahidi wa ulimwengu wote (Matendo 1:8).
[1]Ingawaje wanafunzi walikuwa wameokoka, walikuwa na hitaji la ndani ambalo lilikuwa ni lazima lipatikane kabla ya kuwa tayari kwa ajili ya huduma bila ya uongozi wa kimwili wa kuonekana wa Yesu. Hata miaka mitatu ya mafunzo chini ya Mwalimu mkuu Yesu haikuweza kuwakamilisha kabisa kwa ajili ya huduma, hivyo, hitaji hili la ndani bado lilikuwa limesalia. Kabla hawajaweza kuwa na huduma iliyopewa nguvu na kuongozwa na Roho Mtakatifu, kama vile Mugu alivyopanga, walihitajika kuwa na hitaji maalumu ndani ya moyo kutokana na kazi maalumu ya Roho Mtakatifu.
Tatizo lilikuwa limejidhirisha lenyewe kwenye nyakati tofauti wakati wa miaka mitatu ya mafunzo. Mara nyingine katika tabia walikuwa watu wa kutaka kulipa kisasi (au wasiotaka kusamehe) kama walivyotaka waite moto ushuke juu ya watu waliokuwa wanawakataa (Luka 9:54-55). Mara nyingine walijivunia kuwa katika kikundi cha mtazamo wa dini fulani tu, kama vile walivyomnyima mtu mmoja kuhudumu kwa vile tu alikuwa hajapata kibali kutoka kwao (Marko 9:38). Walikuwa wabinafsi na wakijivunia matamanio yao, kama vile wanafunzi wawili walivyoomba wapewe nafasi za juu na wakakasirikiwa na wenzao (Marko 10:35-41).
Walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa (Marko 9:33-34). Ukweli ni kwamba walikuwa wameaibishwa na jambo hilo wakati Yesu alipouliza jambo lilelile walilokuwa wanalijadili, na walikuwa na ufahamu moyoni kwamba makusudio yao yalipaswa yawe mazuri zaidi.
Kwenye chakula cha mwisho cha pamoja, Yesu aliwatawadha miguu wanafunzi wake na kuwataka wawe na tabia hiyo hiyo ya utumishi kama yeye alivyokuwa akiwadhihirishia (Yohana 13:14). Walikuwa bado hawajaweza kuwa na aina hii ya unyenyekevu; walikuwa wamekataa kuhudumiana siku hiyo jioni. Tatizo halikuwa ukosefu wa ufahamu, bali walijawa na majivuno na kiburi.
Yesu aliwaambia kwamba wanapaswa wawe na upendo utakaokuwa na nguvu za kutosha ili kuweza kutoa maisha yao kwa ajili ya wengine (Yohana 15:12-13). Walikuwa wakijidhania kwamba wanao upendo huu, lakini haikuwa hivyo; kwa kuwa walikimbia wakati Yesu alipokamatwa, ingawaje walikuwa wamedai kwamba watakuwa tayari kufa pamoja naye (Marko 14:31, 50).
Hawa ni watu ambao walitegemewa kuwa na jukumu la kuongoza na kuliongeza kanisa bila ya uwepo wa Kristo pamoja nao kimwili. Yesu alitambua kwamba hawakuwa tayari kwa ajili ya huduma hii hadi hapo hitaji lao la ndani litakapokamilishwa, kwa hiyo aliwapa maagizo ya kusubiri Yerusalemu hadi watakapoipokea “Ahadi ya Baba” (Matendo 1:4-5). Ahadi hii inatambuliwa kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu. Ilikuwa ni muhimu sana kwamba hawakutakiwa kuondoka na kwenda kuanzisha kanisa bila ya kupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu.
Hakuwaambia kwamba walichokuwa wanatakiwa wawe nacho ni mafunzo zaidi, au mchakato wa ukuaji wa muda mrefu. Walitakiwa tu wasubiri Yerusalemu kwa ajili ya tukio la kiroho/kufikia kilele cha ahadi.
[2]Kile walichokutana nacho wanafunzi kwenye siku ya Pentekoste kinaelezewa kuwa ni ujazo wa Roho Mtakatifu (Matendo 2:4). Ingawaje mambo mengi yalitokea wakati wa tukio hilo, baadaye Petro alidhihirisha kwamba kazi muhimu ya Roho Mtakatifu ilikuwa ni kutakasa mioyo yao (Matendo 15:8-9). Hili ndilo lililokuwa hitaji la wanafunzi. Ushahidi wote wa hitaji lao la ndani lilionyesha kuwepo kwa tatizo katika moyo, uharibifu wa tabia uliorithiwa, ambao walihitajika watakaswe. Wakati utakaso huu ulipofanyika kwa ubatizo (ujazo) wa Roho Mtakatifu, hawakufikiria tena kuhusu usalama wao wenyewe au madaraka kuwa kama ndio lengo lao kuu.
Tukio la wakati wa Pentekoste, lilizindua kanisa kwenye enzi ya uinjilisti wa nguvu. Kwa furaha na kwa ushindi mkubwa kanisa lilisonga mbele pamoja na kuwepo kutokukubaliana kwa mambo mengine ya imani, majungu ya Wayahudi, malalamiko ya ndani, unafiki, uwepo wa nguvu za giza, mateso, na mazingira mengi magumu.
Mwamini anaweza akawa na hitaji linalofanana na lile la wanafunzi walilokuwa nalo. Hitaji hili linaweza kuondoka kwa kujazwa na Roho Mtakatifu.
Hii haina maana kusema:
1. Kwamba mwamini huwa hana Roho Mtakatifu hadi apokee huu ujazo maalumu.
2. Kwamba hakuna kazi za Roho Mtakatifu zinazoendelea ndani ya mwamini hadi huu ujazo wa Roho Mtakatifu utakapotokea.
3. Kwamba hakuna aina nyingine ya ujazo wa Roho Mtakatifu zaidi ya huu ambao hutakasa moyo.
4. Kwamba kila mtu ambaye amejazwa nguvu za Roho Mtakatifu atakuwa na huduma ya kitume.
Hatupaswi kuwa na dhana kwamba uzoefu wetu utakuwa sawasawa na ule wa wanafunzi. Hata hivyo, uhitaji wa utakaso wa moyo na uwezeshwaji wa nguvu kwa ajili ya huduma bado ni jambo muhimu sana kwetu.
Kutokana na mfano wa wanafunzi tunaweza kuona:
1. Kwamba kama mtu analo hitaji hili, hayuko tayari kikamilifu kwa ajili ya huduma au kuishi maisha matakatifu.
2. Kwamba Mungu hapendi amwache mtu katika hali hii.
3. Kwamba suluhisho siyo mafunzo au muda mrefu wa kukua kiroho.
4. Kwamba inawezakana hitaji hili likawezeshwa kwa kitambo, baada ya kutafuta kwa uhakika.
Je, inawezekanaje kwa mwamini kupokea kazi hii ya Roho Mtakatifu?
Petro alisema ilipokelewa kwa imani (Matendo 15:8-9). Yesu aliwaandaa wanafunzi wake kuwa na imani kwa kuwapa ahadi na kuwapa matarajio.
Kwa hiyo, kama mtu ataona hitaji lake na akaona utayari wa Mungu katika kulitimiza, anaweza kuipokea neema hii kwa Imani.
“Kulichukua jukumu hili kubwa kabisa ambalo Bwana alikuwa analikabidhi mikononi mwao lilikuwa juu ya uwezo wa nguvu za mwanadamu. Kwa hiyo, aliwapa nyenzo isiyokuwa na kikomo ya Roho Mtakatifu. Alikuwa aushawishi ulimwengu kwa ajili ya dhambi, haki na hukumu; kwa hiyo, aliambatana nao kwenye huduma yao kwa uimara wa nguvu na matokeo ya kushangaza.”
Walikuwa watu walioungana pamoja, timu ya mashahidi wenye nguvu ya upako:
Kufuatia mwito wa Mungu, wakitegemea nguvu za Mungu, na wakifanya kazi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Kazi ya Kufanya
Kila mwanafunzi ajitathmini mwenyewe kwa maombi na ajibu maswali haya kwa maandishi. Karatasi ya majibu haitahitajika iwasilishwe kwa kiongozi wa darasa.
Je, mimi ni tegemezi kwa Roho Mtakatifu, au ninatumainia kufanya tu yale ambayo uwezo wangu unaruhusu?
Je, ninazo baadhi ya tabia zilizoonyesha kwamba wanafunzi walihitaji ujazo wa nguvu za Roho Mtakatifu?
Je, kunayo matendo yoyote, tabia, mwenendo au malengo ambayo sijayasalimisha kwa Mungu?
Je, niko tayari kwa uamuzi wangu mwenyewe Roho Mtakatifu anitakase kabisa, ili niweze kutumiwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu?
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.