► Je, ni kwa jinsi gani kanisa lihusike ndani ya jamii?
Yeremia aliandika kwa Wayahudi akiwa utumwani akiwaambia kuhusu uhusiano wao utakavyokuwa kati yao na jamii ya kipagani waliokuwemo. Wayahudi hawa walikuwepo utumwani pasipo matakwa yao; dini ya jamii iliyokuwepo ilikuwa ya kipagani; serikali iliyokuwepo ilikuwa ya ugandamizaji iliyoharibu taifa lao; na, walikuwa wakingojea siku ambayo wangeondoka. Labda walifikiri hawangejihusisha na matatizo yeyote ya jamii ile.
Sikiliza ujumbe ambao Mungu alimpa Nabii kwa ajili ya watu hawa:
Kautakieni amani (shalom) mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa Bwana; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani (Yeremia 29:7).
[1]Shalom, neno hili kwa kawaida likiwa linatafsiriwa kwamba ni amani, halirejelei tu amani peke yake, bali pia baraka zinazoambatana na amani. Linarejea baraka zinazotoka kwa Mungu. Hawa watu waliokuwa wakimwabudu Mungu katika nchi ya wapagani wanaenda kupata baraka wanapokuwa wanajaribu kuzileta baraka hizo kwa watu wa jamii ya makafiri!
Matatizo ya dunia yanatokana na chanzo chake cha ndani cha tatizo la dhambi. Watu binafsi na mataifa yenye nguvu yaliyojipanga vizuri hawaheshimu Neno la Mungu. Kanisa ndilo pekee lenye sifa ya kuweza kuzungumzia matatizo ya dunia kwa sababu kanisa lina uwezo wa Kufafanua Neno la Mungu na kudhihirisha hekima ya Mungu. Kanisa halipaswi tu kuzungumzia na kuwa kinyume cha dhambi zilizopo katika jamii, bali pia kufafanua na kudhihirisha ni kwa jinsi gani jamii inapaswa ifananie.
“Kanisa la Kikristo ni jumuiya ambamo Roho Mtakatifu hupitia kwa ajili ya kuongoza ukombozi na ugawaji wa karama, njia ambayo Mungu huitumia kufanyia kazi yake ya upatanisho katika Kristo aliyeko kwa wanadamu. Kanisa limeitwa kutoka katika dunia ili kusherehekea ujio binafsi wa Mungu, na limetakiwa lirejee duniani kwa ajili ya kutangaza ufalme wa Mungu ulio kiini cha ujio binafsi wa Mungu na tegemeo la kurejea tena alikotoka.”
► Je, ni alama gani zinazoonyesha mafanikio kwa ajili ya kanisa?
Kutokana na kuwepo kwa dhana ya mafanikio ya kidunia, mtu anaweza akafikiri kwamba kanisa lina mafanikio kama lina mahudhurio ya watu wengi, bajeti kubwa, na jengo kubwa sana.
Walio Wakristo kamili wanajua kwamba mambo hayo hayana maana yeyote mbele za macho ya Mungu, bali tu mara nyingi tunavutiwa na mambo hayo. Kwa kawaida tunafikiria kwamba mchungaji anakuwa amefanikiwa kama atakuwa na kanisa kama hilo.
Kipimo muhimu cha kupima mafanikio ni idadi ya watu wanaookoka kwa uhakika kwa sababu ya huduma ya kanisa. Kukua kiroho kwa waumini pia ni jambo muhimu sana, lakini lililo na ugumu wa kupima. Udhihirisho wa kweli wa mafanikio ya kanisa ni mabadiliko yanayoonekana kuletwa na kanisa kwa majirani waliolizunguka.
► Je, unafikiria nini kuhusu taarifa hii?
Mafanikio ya kanisa la mtaa yanapaswa yashikamane moja kwa moja kwenye kiwango kwamba linaleta mabadiliko ya ujumla na ya haraka kwa ujirani unaolizunguka. Hiki ni kigezo muhimu, Kigezo kingine chochote cha mafanikio kinafuata baada ya msingi huu.[1]
Injili huleta matokeo makubwa nje ya watu ambao tayari wameshaokoka. Kila mtu aliyeokoka na kuanza kuishi maisha yanayoendana na kanuni za Ukristo huwa ni kivutio kwa watu wengine. Yesu alisema kwamba wafuasi wake ni chumvi na mwanga wa ulimwengu.
Kanuni za Ukristo ndizo zilizo msingi wa uhuru na haki, na ndizo zilizo kigezo kikuu cha kuweza kuleta mabadiliko kwenye jumuiya. Kama kanisa linawashawishi watu kufuata kanuni za Ukristo, jumuiya itakuwa tayari kushawishika kuanzishwa kwa uhuru na haki.
Hali hii pia inahusika kwenye jumuiya ya mtaa. Kama watu walio majirani watakuwa wameokoka, kwa vyovyote kutakuwepo na mabadiliko kwenye ujirani wote.
► Je, kuna mabadiliko gani yatakayotokea kwenye majirani wako kama watu wengi wangeweza kushawishika kufuata kanuni za Ukristo?
Itakuwa na maana gani kwa majirani wanaokuzunguka kushawishiwa na huduma ya kanisa lako? Kutakuwepo na upungufu wa uhalifu, kuwanyanyasa watoto na kuwapuuza, tabia zisizo za kimaadili, machafuko, ubaguzi wa rangi, biashara haramu, biashara za uyanyasaji, na mambo ya kishenzi (uharabu). Wapangaji watakuwa waaminifu zaidi. Wapangishaji watatoa nyumba zilizo na usalama zaidi. Watu wengi watakuwa na uwezo wa kumiliki maskani yao wenyewe. Wafanyabiashara watakuwa tayari kutengeneza nafasi za kuwaendeleza watu wao waliowaajiri. Watu walioajiriwa watakuwa na tabia nzuri zaidi kwa ajili ya kazi.
Matokeo ya kiroho kwa ajili ya kanisa ndiyo kipaumbele cha kwanza, lakini kama matokeo hayo yatakuwa ni halisi, yatadhihirishwa kwenye mabadiliko yatakayoonekana kutoka kwa majirani waliolizunguka.
[1]John Perkins, akinukuliwa na Daniel Hill katika “Church in Emerging Culture,” in A Heart for the Community. Kimfanyiwa uhariri na John Fuder na Noel Castellanos. (Chicago: Moody Publishers, 2009), 203.
Huduma kwa Watu Maskini
► Je, Yesu alisema kwamba amri kuu ya pili ni ipi?
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Luka 10:25-29 kwa ajili ya darasa.
Mwanasheria alimwuliza Yesu jinsi ya kuupata uzima wa milele. Yesu akamwuliza, “Imeandikwa nini katika torati?” Katika kujibu, mwanasheria alichanganya sheria kuu mbili. Alisema kwamba unapaswa kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na jirani yako kama nafsi yako (Luka 10:27). Yesu alimjibu kwamba jibu lake lilikuwa sahihi, kisha akamwambia, “Fanya hivi nawe utaishi”. Mtu aliye na upendo wa aina hiyo anao uzima wa milele.
Kisha mwanasheria akauliza, “jirani yangu ni nani?” Hakuwa anafikiria kwamba alitakiwa ampende kila mtu. Alikuwa anataka apate upenyo mwembamba wa aina fulani ya watu ambao ni lazima awapende, ili aweze kujisikia kwamba alikuwa anatimiza matakwa yote ya sheria. Yesu alijibu swali hili kwa kutumia hadithi.
► Je, ni hadithi gani Yesu aliyotumia kama mfano wa kumpenda jirani yako?
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Luka 10:30-37 kwa ajili ya darasa.
Yesu alielezea hadithi ya Msamaria Mwema kama mfano wa kile kinachomaanisha kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Upendo unaleta hamasa au motisha kwetu sisi kwa ajili ya kuwajibika kwa mtu aliye mhitaji.
Yesu alielezea kazi yake maalumu katika Luka 4:18-19:
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Taarifa hii inajibu swali linaloulizwa kwamba, Kwa nini Yesu alikuja? Yesu alisema kwamba hili ndilo alilotiwa mafuta ili alifanye. Lilikuwa ni kusudi lililokuwa limetabiriwa kwa ajili yake katika Agano la Kale.
Kazi ya Yesu maalumu inatoa mwelekeo kwa kanisa, lililo “mwili wa Kristo” ulimwenguni. Jambo la kwanza Yesu alilolisema lilikuwa ni kuwahubiri maskini habari njema. Kanisa litakuwa halikamilishi kazi yake maalumu kama litakuwa linazembea au kuwatenga watu maskini. Yesu alisema kwamba maskini ni watu waliobarikiwa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni (Luka 6:20). Mtume Yakobo alisema kwamba Mungu aliwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani (Yakobo 2:5). Mungu amechagua kudhihirisha uwezo wake kwa kuwatumia maskini na wanyonge wa dunia hii (1 Wakorintho 1:27-29). Kanisa lina sababu nyingi za kufanya jitihada maalumu kwa ajili ya kufanya uinjilisti kwa watu maskini. Sababu mojawapo ni kwamba injili huenea kwa haraka zaidi miongoni mwa watu walio maskini.
Maelezo kuhusiana na huduma ya Yesu yanaonyesha kwamba alikuwa anategemea pia kubadilisha hali zilizopo za ulimwengu.
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Mika 6:6-8 kwa ajili ya darasa. Nabii alikuwa anauliza swali gani?
Nabii Mika alilitafakari swali ambalo Mungu kwa uhakika anataka kutoka kwa watu wake wanaomwabudu. Baadhi ya watu waliuliza kama mafahali ya wanyama yangeweza kutosha kwa ajili ya dhabihu. Mika akaeleza kwamba siyo suala la kutafuta dhabihu ambayo ni kubwa mno kwa ajili ya kuwa na thamani mbele za Mungu. Mungu ameshatoa mahitaji yake. Tuna wajibu wa kutenda haki na kusaidia watu wengine katika kupata haki.
Huruma hairejei tu kwenye aina ya matumizi ya mamlaka. “Huruma hurejea kwenye unafuu wa mahitaji. Yesu alisema kwamba yule Msamaria Mwema alikuwa ni mfano wa upendo ambao Mungu anaagiza kwa sababu “alionyesha upendo.” Wakati mwingine makanisa yanadhania kwamba yanapaswa yawe katika mtazamo wa mahitaji ya kiroho tu. Wanadhania kwamba hawana wajibu katika masuala ya umaskini. Hata hivyo, Biblia inataja maskini mara 400. Matatizo ya maskini yanahusika na Mungu. Kama ilivyokuwa kwa Msamaria Mwema, Makanisa yanapaswa yaonyeshe upendo kwa wale watu wanaoonekana kwamba wanahitajika kupewa msaada.
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Ezekieli 16:49-50 kwa ajili ya darasa. Aya hizi zinataja dhambi gani ya Sodoma?
Jiji la Sodoma linakumbukwa kwa ajili ya dhambi ya matendo ya uasherati; lakini uovu wa jiji hilo haukuwa matendo haya peke yake. Watu wa Sodoma walitumia mafanikio yao katika kujipatia starehe wao wenyewe na hawakutafuta njia ya kuwawezesha maskini ili waweze kubadilisha hali zao za maisha.
Dhana ya Parishi au parokia/usharika
Wakati kanisa linapokuwa na wajibu kwa ajili ya aina fulani ya majirani wanaowazunguka, eneo hilo la kanisa linaitwa Parokia au usharika. Kihistoria, mashirika makubwa ya makanisa walitegemea kila kanisa la mtaa litumike kwa ajili ya eneo maalumu la kijiografia. Hii ni tabia ya Kanisa Katoliki katika maeneo mengi duniani, Kanisa la Kilutheri la Ujerumani, na Kanisa la Uingereza nchini Uingereza. Madhehebu mengi ya Kiprotestanti hayana parishi au Parokia/usharika kwa njia sawa.
Jaribu kufikiria itatokea nini kwa kanisa kujifikiria lenyewe kama ni kanisa kwa ajili ya jamii. Kila mtu katika parishi au usharika huo atakuwa amejua mchungaji ni nani na kwamba alikuwa anapatikana kwa ajili ya maombi, kufariji na kutia moyo, kushauri, aidha wakiwa wanahudhuria kwenye kanisa lake au la. Anapokuwa anafanya ziara miongoni mwa jamii, lengo lake la msingi halitakuwa kushawishi watu wahudhurie kwenye kanisa. Badala yake, atakuwa anapeleka huduma ya kanisa kwao.
[1]Kanisa linatakiwa lipeleke huduma ambazo zinakubaliana na mahitaji ya majirani wanaowazunguka, kama vile, ushauri wa kifamilia, kutoa nasaha kwa vijana, na mafunzo ya kazi yanayohusiana na mienendo ya tabia. Haya siyo kwamba hayahusiani na kusudi la kanisa. Ni maeneo ambayo Biblia hujibu masuala yote nyeti, na kanisa linapaswa lishirikishe hekima ya Neno la Mungu kwenye maeneo ya matendo. Ni rahisi kunyooshea kidole mambo ya uovu yaliyoko ndani ya jumuiya, lakini kanisa linapaswa litoe ufafanuzi wa jinsi jumuiya inavyotakiwa iwe.
► Je, ni mahitaji gani yaliyopo kwenye jamii inayokuzunguka ambayo yanaweza yakabadilishwa na Neno la Mungu?
Manabii wa Agano la Kale waliona kwamba ardhi na watu waliopo ni mali ya Mungu, na kumtaka kila mtu alishike Agano la Mungu. Walihubiri kuhusu baraka zilizokuja kwenye jumuiya wakati zikifuata mpango wa Mungu na kuhusu laana ambazo zilikuja kutokana na kukosa utiifu.
Mchungaji anapaswa aione jumuiya yake kama ni parishi au usharika wake ulio chini ya Mungu. Mungu ndiye Mmiliki na Mtawala anayetoa baraka kama wataishi kwenye mpango wake. Mchungaji anatakiwa aendelee kuwataka watu wa jumuiya waishi ndani ya maelekezo ya Mungu. Atapaswa aelezee inamaanisha nini kuishi na baraka za Mungu na kuwatia moyo kuja kwenye uhusiano na Mungu.
Dhana ya parishi au usharika haimaanishi kwamba kila mtu kwenye majirani wanaokuzunguka ni mwanachama wa kanisa. Kanisa linahusisha tu wale ambao wamemaanisha na kujikabidhi kuishi maisha yenye uhusiano na Mungu, lakini jumuiya hushawishiwa na kanisa.
Dhana ya parishi au usharika haimaanishi kwamba majirani wanaokuzunguka wanathibiti kanisa na kuweka vigezo vyake. Kanisa limesimikwa na Mungu, linafuata Neno Lake, na kwamba linawakilisha ufalme wa Mungu kwa majirani wanaolizunguka.
Kwa kuwa kanisa limetakiwa kuwa chumvi na nuru inayoangaza, kanisa limetakiwa kuleta mabadiliko kwa majirani wanaolizunguka.
“Kama mwili wa Yesu, kanisa ni kikundi cha ushirika wa kuabudu ambacho kipo katika kutimiza mapenzi ya Mungu na kuwakilisha matarajio ya Ufalme wake.”
- Larry Smith, I Believe: Fundamentals
of the Christian Faith
Kipaumbele cha Injili
Huduma nyingi zinatoa programu ambazo zinakidhi mahitaji kwa majirani wanaowazunguka. Wanahudumia mahitaji ya jumuiya na kufikiri kwamba kuwahudumia watu kwa njia za vitendo kutawafanya wawe marafiki na kusababisha wawe makini kwa ajili ya kupokea injili. Malengo yao ni kutengeneza nafasi za kushirikisha injili. Wanataka waonyeshe kwamba ni watu wanaojali.
Mpangilio wao ni kama ifuatavyo: Programu, kisha Mahusiano, kisha Injili. Hata hivyo, kuna njia nyingi zinazosababisha programu hizo kwenda vibaya. Msaada labda hautaunda uhusiano wowote isipokuwa uhusiano wa mtoaji na mpokeaji tu.
Wakati mwingine injili inaonekana kutengwa kutoka katika vitu vingine vinavyotolewa, na watu wanaweza kupata msaada bila ya kuwa na hamasa kwa injili. Watu wanaokuwa watendakazi katika huduma wanaweza kuwa na harakati kubwa sana za kutoa msaada na siyo kushirikisha injili. Wapokeaji wa misaada wanaweza wakapokea vitu vingi sana kisha wakaondoka tena kwenda kutafuta msaada mahali pengine.
Mpangilio huo unabidi ubadilishwe. Kanisa linapaswa liweke msisitizo wa injili kwanza kama kipaumbele chake cha kwanza cha kukutana na kila mtu.
► Injili ni nini?
Wakati kanisa linawasilisha injili kwa ulimwengu, ni lazima waweze kuwa waaminifu kuhusisha pamoja na maelezo ya maisha mapya ndani ya kanisa. Wokovu siyo maamuzi binafsi ambayo yanamwacha mtu peke yake katika hali ya maisha mapya yasiyoeleweka ni kitu gani. Watenda dhambi kwa kawaida hawatakubaliana na injili hadi hapo watakapokuwa wamevutiwa kwenye jumuiya ya watu wa imani ambao wanawasilisha injili.
Kwenye huduma ya Yesu na mitume, tunaona kwamba injili ni “habari njema” za ufalme wa Mungu. Ni ujumbe ambao mwenye dhambi anaweza kupokea msamaha na kuja kwenye uhusiano na Mungu. Anakombolewa kutoka kwenye nguvu ya dhambi na kufanywa kiumbe kipya. Anaingia kwenye familia ya watu wenye imani, mahali ambapo kaka na dada zake wa kiroho watamtia moyo na kumsaidia katika mahitaji yake.
Kanisa linapaswa lione kusudio lake la msingi la kuwasilisha injili. Kila mtu anatakiwa afahamu kwamba kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa roho za watu ni kitu ambacho kiko kwa ajili ya kanisa. Kisha, kanisa linawavutia watu ambao wako kwenye utayari wa injili. Huduma ya injili inatengeneza uhusiano.
Kisha baada ya hapo kanisa linasaidia watu walioko kwenye uhusiano na kanisa. Inawezekana ikawa siyo watu wote ambao watakuwa tayari wameokoka, lakini wakavutiwa na huduma ya injili ya kanisa.
Kwa hiyo, huduma ambayo imebadilishwa ni Injili, kisha Uhusiano na kisha Msaada (na siyo programu). Kanisa halipaswi kuwa kama shirika linalotoa huduma za kusaidia. Badala yake, kanisa ni kikundi cha watu ambacho kinasaidia watu walioko kwenye uhusiano pamoja na wao. Endapo wataanzisha programu mbalimbali, watu watajitokeza kwa ajili ya programu hizo bila ya uhusiano.
Taarifa Saba kwa Muhtasari
1. Kanisa lenye matokeo yanayotarajiwa husababisha mabadiliko kwa majirani wanaowazunguka.
2. Ni lazima tuonyeshe upendo wetu kwa majirani zetu kwa kuwajibika katika mahitaji yao.
3. Kanisa linapaswa liwahudumie watu walio maskini ili kukamilisha umisheni wake.
4. Kanisa linapaswa liwahudumie watu walioko kwenye eneo lao la kijiografia.
5. Kanisa linapaswa lielezee na lidhihirishe ni kwa jinsi gani jumuiya inapaswa iwe.
6. Huduma ya injili ni kipaumbele cha kwanza cha kanisa.
7. Kanisa linapaswa liwe na msaada kwa watu kwenye muktadha wa uhusiano.
Kazi za kufanya Somo la 7
1. Kariri taarifa Saba kwa Muhtasari kwa ajili ya somo la 7. Andika aya moja inayoelezea maana na umuhimu wa kila kipengele katika hizi Taarifa Saba kwa Muhtasari (jumla aya saba) kwa mtu ambaye siyo wa darasa lako. Wakilisha kwa kiongozi wako wa darasa kabla ya kuanza kwa kipindi cha darasa kinachofuata. Kuwa tayari kushirikisha aya moja kwa kikundi kama kiongozi wa darasa atakutaka ufanye hivyo wakati wa majadiliano. Andika taarifa hizi kutoka kwenye ufahamu wako bila ya kuangalia mahali popote mwanzoni mwa kipindi cha darasa kinachofuata.
2. Kumbuka kutengeneza ratiba ya nafasi yako mwenyewe ya kufundisha kwa wakati ambao utakuwa nje ya darasa na utoe mrejesho wako kwa kiongozi wa darasa baada ya kuwa umemaliza kufundisha.
3. Masailiano: Zungumza na watu kadhaa wasio hudhuria kanisani. Watake wakuelezee ushawishi wa kanisa kwa majirani wanaolizunguka. Andika muhtasari wa mahojiano hayo.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.