Utangulizi
► Itampasa mwanafunzi asome hadithi ifuatayo ya kufikirika kwa ajili ya darasa.
Wakati mmoja kulikuwepo na jiji ambalo lilikuwa hatarini kukumbwa na mafuriko ya mto. Watu wa jiji hilo walijipanga katika vikundi mbalimbali vya kujaza mifuko ya mchanga na kuiweka kwenye kingo za mto huo. Watu walifanya kazi kwa shauku kubwa, na hamasa ya kila kikundi iliongezeka. Baadaye vile kikundi vilijipa majina. Kulikuwa na kikundi cha waokoaji wa jiji, Wasawazishaji Mchanga, na Wathibiti Mto. Utambulisho wa kikundi ulikuwa jambo muhimu sana. Wanachama wa kila kikundi walivaa fulana zinazofanana. Walizungumzia ni kwa jinsi gani kikundi kimoja kilikuwa ni bora kuliko kikundi kingine. Kila kikundi kililaumu kazi ya kikundi kingine.
Wakati kikundi cha wathibiti Mto kilipokwenda kuomba toroli kutoka kwenye kikundi cha Waokoaji wa Jiji, hawakuwaruhusu kulichukua toroli hilo, kwa sababu walidhania kwamba wanaweza wakalihitaji tena baadaye. Wakati kikundi cha Wasawazishaji Mchanga walipopungukiwa na mifuko ya kuwekea mchanga, ilibidi wasubiri kwa takribani saa moja kwa ajili ya mifuko kuletwa, ingawaje vikundi vingine vilikuwa na mifuko ya ziada. Vikundi vyote vilikuwa vimejisahau kwamba wote kwa pamoja walikuwa na jukumu moja. Mafanikio ya kila kikundi yalionekana ni muhimu zaidi kuliko matokeo ya ujumla ya jukumu lote lililokuwepo.
► Ni kwa jinsi gani makanisa yanafanya kama ilivyokuwa kwa vikundi vilivyoko kwenye hadithi hii?
Biblia inasisitiza kwa kina sana kuhusu thamani ya umoja wa Kikristo. Paulo alikemea utengano au mafarakano ya kanisa la Korintho kwa kuuliza swali, “Je! Kristo amegawanyika?” (1 Wakorintho 1:13). Aliwaambia Waefeso kudumisha umoja wa Roho. Akionyesha kwamba, “Mwili mmoja... Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Waefeso 4:4-5). Yesu aliomba kwa bidii sana ili kwamba waumini kuwa kitu kimoja, ili ulimwengu upate kuamini kwamba Yesu alitoka kwa Baba (Yohana 17:21).
Tangu mwanzo, kanisa lilijifikiria lenyewe kuwa ni moja. Imani ya Mitume inahusisha pamoja na taarifa hii: "Naamini… kanisa takatifu la Kikristo (katholiko) lililo moja tu; ushirika wa watakatifu.” Imani ya Nikea inahusisha pamoja na taarifa hii: "Twaamini Kanisa moja (katholiko) la Kikristo la ulimwengu wote na la kimitume.” Neno katholiko lina maana ya kamilifu na ulimwengu wote. Neno kimitume linamaanisha kwamba kanisa lilianzishwa na mitume na hata sasa linafuata mafundisho ya mitume.
Matamko ya imani ya awali yalionyesha imani muhimu za mafundisho ya Kikristo. Kanisa halikuhusika na mtu yeyote ambaye hakukubaliana na matamko haya ya imani, kwa kuwa yalikuwa yamekusudiwa kutoa ufafanuzi wa mambo muhimu ya Ukristo. Kwa hiyo, mtu alionekana kuwa ni mwenye ukengeufu kama alikuwa anafikiria kwamba kuna makanisa ya kweli ambayo siyo sehemu ya kanisa moja la ulimwengu wote.