Mafundisho Na Mazoezi Ya Kanisa
Mafundisho Na Mazoezi Ya Kanisa
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 4: Mashirika ya Kanisa

10 min read

by Stephen Gibson


Elekezo kwa kiongozi wa darasa

Vifaa vinahitajika katika maandalizi ya somo hili. Somo hili linajadili kuhusu uhusiano kati ya makanisa na shirika lao. Kama wanafunzi wanatoka katika kanisa ambalo liko ndani ya shirika, kiongozi wa darasa atapaswa alete nakala ya mambo yanayohitajika katika shirika huo kwa ajili ya kufanya marejeo au tafakuri darasani.

Ufafanuzi kuhusu mashirika ya Kanisa.

► Je, jina la shirika la kanisa au dhehebu lako ambalo uko linaitwaje?

Wakati Mkristo anapokutana na Wakristo kutoka katika makusanyiko mbalimbali ya makanisa ya mahali maswali hujitokeza. Anauliza ni kwa nini yale anayoyaamini na matendo yake yanatofautiana na wengine? Anagundua kwamba kuna tofauti za mafundisho ya imani kati ya aina mbalimbali za makanisa. Kuna tofauti kubwa sana za aina za kuabudu na au ibada.

Mshirika wa kanisa anaweza akaangalia utambulisho wa kidini ambao ni mkubwa kuliko kanisa lake la mahali. Anapenda kuona kwamba kanisa lake ni sehemu ya kundi la makanisa ambayo yanaamini katika mafundisho ya imani inayofanana, lenye kushirikiana na kuwa na ushirika unaofanana wa kuabudu pamoja. Hataki kujisikia kwamba kusanyiko lake la mahali pamoja ndilo peke yake duniani ambalo lina aina yake maalumu ya imani na matendo.

► Mwanafunzi mmoja au wawili wanaweza wakaelezea jinsi wanavyofaidika na kukutana kwao na makanisa mengine yanayofanana na kanisa lao.

Katika somo la Kwanza, tulijifunza kuhusu taarifa zifuatazo:

Kwa ajili ya kuwa na uthabiti wa mafundisho ya imani, Kanisa la mtaa linapaswa lizingatie mambo matatu:

1. Kuwa na imani kwamba Biblia ndiyo mamlaka iliyo kamili.

2. Mafundisho ya imani yaliyokuwa muhimu katika historia ya Ukristo.

3. Kuwa na ushirika na jumuiya ya makanisa yaliyo na teolojia nzuri inayokubalika.

Katika somo hili tutazungumzia kuhusu kipengele cha tatu kilichoko katika orodha hii.

Tafsiri ya shirika la Kanisa

Shirika la kanisa ni kundi la makanisa yaliyojiunga pamoja na kuwa na uongozi mkuu mmoja, wanashirikishana baadhi ya mambo ya imani, wanajitoa kwa pamoja kukamilisha baadhi ya malengo, na wanakuwa na aina fulani ya kuabudu pamoja.

Aina za Shirika Dhaifu na Zenye Nguvu

Shirika linaweza likaitwa “dhaifu” au “lenye nguvu” hutegemeana na nguvu ya mambo yanayoweka ushirika pamoja.

Katika shirika dhaifu, uongozi mkuu unakuwa na mamlaka kidogo sana juu ya kanisa la mahali; orodha ya imani za pamoja inaweza ikawa ni fupi sana na ya msingi; malengo ya pamoja yanaweza yasihitaji ushiriki mkubwa kutoka kwa makusanyiko ya mahali pamoja ya mitaa; na wawakilishi kutoka makanisa hukutana mara kwa mara tu. Katika shirika hilo, mali za kila kanisa inamilikiwa na kanisa la mahali. Na kanisa la mahali linaweza kuchagua kujitoa kwenye shirika hilo wakati wowote. Makanisa yaliyojiunga yanaweza kujitoa kwenye shirika hilo kama yakijisikia kwamba hayana hitaji la kuendelea kuwa katika shirika hilo.

Washiriki wa shirika dhaifu kwa kawaida husisitiza uhuru wa kujitawala wa kanisa la mahali (autonomy). Huwa hawataki shirika kutawala kanisa la mahali, kwa hiyo, kwa uangalifu sana wanapunguza mamlaka ya shirika. Kwa hiyo, kuita shirika “dhaifu” haina maana ya kusema kwamba unashindwa kwenye malengo yake. Washirika wa shirika dhaifu wanataka uongozi mkuu wa shirika uwe mdhaifu. Mamlaka yanagawanywa na kushikiliwa na makanisa ya mahali.

► Je, unafikiria ni nini kizuri kuhusiana na shirika “dhaifu”? Ni mambo gani ambayo siyo mazuri kuhusiana nao?

Katika “shirika lenye nguvu” uongozi mkuu wa shirika hilo wanakuwa na mamlaka kamili juu ya viongozi wa makanisa ya mahali; orodha ya imani za pamoja zinahusisha mambo mengi; makanisa ya mahali yanategemewa kutoa fedha kwa ajili ya malengo ya pamoja; na makanisa ya mahali yanakutana mara kwa mara. Mali za kanisa zinaweza kumilikiwa na shirika. Kama ndivyo, makanisa binafsi hayawezi kuchagua kuachana au kujiondoa kwenye shirika.

Washirika wa “shirika zenye nguvu” wanategemea kuona uongozi mkuu wa shirika ukishughulika na utatuzi wa baadhi ya matatizo yao mbalimbali. Wanasisitiza kujikabidhi na kutumika kabisa kwa ajili ya shirika na kanisa la mahali.

Kuna aina mbalimbali zilizopo za shirika za makanisa. shirika linaweza lisiwe na tabia zote za kulifanya kuwa shirika dhaifu au lenye nguvu, lakini linaweza kuwekwa kwenye kundi la dhaifu au lenye nguvu kutegemeana na tabia ambazo shirika hilo linazo. mashirika yenye nguvu mara nyingi yanaitwa “madhehebu.”

► Je, unafikiria ni nini kizuri kuhusiana na “shirika zenye nguvu?” Ni mambo gani ambayo siyo mazuri kuhusiana nao?

► Je, ni mashirika gani ya kanisa ambayo unajua kuhusu habari zake? Je, unaweza kuziainishaje?

Majukumu ya Dhehebu

Shirika la kanisa lenye nguvu linaitwa dhehebu. Hiyo haimaanishi kwamba shirika hilo linazo tabia zote zinazohusiana na shirika lenye nguvu, bali unaweza kuelezewa kwamba ni lenye nguvu badala ya kuwa mdhaifu.

Dhehebu zuri linakuwepo kwa ajili ya kuhudumia makanisa ya mahali. Dhehebu linasaidia makanisa katika kukamilisha mambo ya pamoja ambayo makanisa mengi ya mahali hayawezi kufanya vizuri yakiwa yenyewe.

[1]1. Linatoa ufahamu wa utambulisho ulio tofauti na aina nyingine za makanisa. Washiriki wa kanisa la mahali wanafahamu kwamba wako tofauti na makanisa mengine katika eneo lao. Wanahamasishwa kujua kwamba wao ni sehemu ya kundi la makanisa ambayo yanashirikishana mafundisho yao ya imani.

2. Linaanzisha mafundisho ya imani. Kanisa la mahali halipaswi kujiona wako huru kubadilisha na kukuza mafundisho yake ya imani bila ya kusikiliza kutoka kwa mtu mwingine tena. Dhehebu linapaswa lishikilie mafundisho ya imani ya kihistoria na yaliyo ya msingi ya Ukristo, lakini pia wanapaswa wawe na mafundisho ya imani ya kina ambayo wanaamini kwamba ni ya Kimaandiko.

3. Linaweka viwango vya sifa kwa ajili ya wachungaji na washiriki wa kanisa. Dhehebu linapaswa liweke viwango vya sifa ili kwamba Wachungaji na washiriki wa makanisa waweze kuwa na mfano endelevu wa Ukristo. Viwango vya sifa vinapaswa viwe katika msingi uliotolewa katika 1 Timotheo 3 na Tito 1, lakini vinapaswa viwekwe wazi kutokana na kila mila au utamaduni.

4. Linatoa mpangilio wa uongozi wa kanisa. Dhehebu linapaswa litoe kwa kanisa la mahali mpangilio wa kuchagua watu kwenye nafasi mbalimbali ndani ya kanisa na kwa ajili ya kudumisha uwajibikaji

5. Linatoa msingi wa mafunzo kwa wachungaji. Makanisa mengi hayana vianzo vya mapato na maandiko ya kufundishia kwa ajili ya kuwafundisha wachungaji wa baadaye. Dhehebu linapaswa liendeleze programu za mafunzo ambazo zitakuwa rahisi kupatikana na ziwe za vitendo.

6. Linatoa mwongozo wa uwekaji wa wachungaji kwenye makanisa. Wachungaji wasiokuwa na makanisa na makanisa yasiyokuwa na wachungaji yanaweza kusaidiwa kwa msaada wa viongozi wa dhehebu. Viongozi wazuri wa dhehebu wataheshimu viongozi wa kanisa kwenye maeneo yote ya maamuzi yao.

7. Linatoa mwongozo wakati kanisa la mahali linapokuwa linapitia kwenye mgogoro. Kama kanisa la mahali litakuwa na mgawanyiko kwa ajili ya jambo fulani au halina uongozi unaoaminika, viongozi wa dhehebu wanapaswa kutoa msaada.

[2]8. Linaunganisha na kutoa misaada ya umisheni na juhudi za uanzishwaji wa makanisa mapya. Kundi la makanisa wanapaswa kushirikishana maono ya kazi ya umisheni. Wanapaswa kuunganisha vianzo vyao vya mapato na nyenzo mbalimbali na kusaidia watu katika kukamilisha malengo ya umisheni.

9. Linafanya ushirika wa kiwango cha juu kuliko ilivyo kwa kanisa la mahali. Washirika wanashawishiwa na kutiwa moyo wa kushirikishana muda wao na makanisa mengine yaliyo katika dhehebu hilo.

10. Linaandaa matukio ambayo yatayaweka makanisa yake kuwa kitu kimoja. Dhehebu linapaswa liandae makongamano na mikutano ambayo itasaidia ushirika wa makanisa na kupanga malengo pamoja.

11. Linatuma viongozi kwenda kwenye makanisa kutoa ushauri na kuwatia moyo. Atapaswa atoke kiongozi wa kanisa kutembelea kila kanisa la mahali angalao mara moja kwa mwaka, na ikiwezekana kufanyika mara kwa mara itakuwa vizuri zaidi.

12. Linatoa ushauri kwa ajili ya kukuza mpango endelevu wa kifedha wa huduma ya mahali. Shirika linapaswa liweke mkazo kuhusu uthamani na umuhimu wa kanisa la mahali na kuwaongoza jinsi ya kukua katika mambo ya kifedha.

Kama dhehebu litawajibika vizuri na kwa ukamilifu katika malengo haya, inaweza kuwa ni msaada wa thamani sana wa kukamilisha malengo ya kanisa. Itakuwa ni jambo lisilowezekana kwa makanisa mengi ya mahali kuweza kutimiza majukumu yote yaliyotajwa hapa juu peke yao. Viongozi wa madhehebu wanapaswa wakumbuke kwamba dhehebu lipo kwa ajili ya kutumikia makanisa ya mahali.

► Kwa kuwa sasa tumeshaona ni kitu gani ambacho madhehebu yanaweza yakafanya kwa ajili ya makanisa yake, tutafakari swali hili: Je, ni kwa jinsi gani kanisa linaweza kufaidika na shirika dhaifu wakati wakijiepusha na matatizo ambayo kwa kawaida huambatana pamoja nao?

► Je, ni kwa jinsi gani kanisa linaweza kufaidika na shirika lenye nguvu wakati wakijiepusha na matatizo ambayo kwa kawaida huambatana pamoja nao?


[1]

“Kanisa lina mamlaka ya kutoa maagizo kuhusiana na ibada za dini, sherehe, na kuwa na mamlaka juu ya utata wa kiimani, na bado siyo sheria kwa kanisa kuamua kitu chochote ambacho ni kinyume au kinachopingana na Neno la Mungu lililoandikwa…”

- Vifungu vya dini
vya Kanisa la Uingereza

[2]

“Uinjilishaji kwa ajili ya ulimwengu ni wazi kwamba ndio umisheni wa Ukristo. Lakini ukamilishwaji wa huu umisheni unategemea kanisa, kwa sababu maajenti wa kutumika kwa ajili ya ukamilishaji wake kwa njia nyingine haiwezekani.”

- John Miley,
Systematic Theology

Kuwajibika kwa Kanisa la Mtaa kwenye Dhehebu

Orodha iliyoko hapa haiwezi ikawa ni ya kufanana kwa kila dhehebu, lakini ni maelezo ya ujumla ya kile ambacho dhehebu kama kawaida huhitaji kwa ajili ya makanisa yake.

Kanisa la mahali linajitoa kabisa kuwajibika katika mambo yafuatayo:

1. Kukubaliana na taarifa ya fundisho la imani la dhehebu, kufundisha mafundisho ya imani, na kutoruhusu mafundisho ya imani yaliyo kinyume kufundishwa kwenye kanisa.

2. Kufundisha na kuwataka washirika kuendelea kuishi katika maisha endelevu ya Mkristo.

3. Kushiriki kwenye makongamano na matukio mengine, na kusaidia katika gharama kwa jinsi itakavyowezekana.

4. Kutoa taarifa ya mwaka iliyo sahihi inayohusiana na mahudhurio, watu walipoamua kuokoka, watenda kazi, na mapato.

5. Kudumisha umoja wa mikusanyiko ya makanisa ya mahali pamoja ya ya dhehebu na viongozi wake na kushughulikia migogoro kwa kuzingatia njia za kibiblia.

6. Kutojishirikisha na shirika lingine lolote ambalo litahitaji kuwa na uwajibikaji unaofanana.

Kama wanafunzi wanatoka katika kanisa ambalo limejumishwa kwenye mahali wa makanisa, chukua dakika chache za kuangalia mambo yanayohitajika kwa ajili ya muungano huo.

► Je, shirika la kanisa lako lilikuwa limeanzishwa na shirika la kimisheni la kimataifa? Kama ndivyo, elezea uhusiano uliopo kati ya makanisa na hilo shirika la kimisheni.

Uhusiano kati ya Shirika la Kimisheni na Muungano wa Makanisa yake.

Wakati mwingine makanisa huwa kwenye mahusiano na shirika la umisheni la kimataifa. Shirika linaweza likaanzisha makanisa, au makanisa yaliyopo yakaamua kujiungamanisha na shirika hilo. Makanisa yaliyounganika na shirika la umisheni hutengeneza shirika wa makanisa.

Mwanzoni, wamishonari wa kigeni wangeweza kuishi nchini na kuwa viongozi wa shirika. Baada ya muda, uongozi unakua kutoka kwa wachungaji wenyeji. Umisheni unapaswa uwe na lengo la kutengeneza wachungaji ili wamisionari wa kigeni wasiendelee kuongoza shirika la makanisa yao moja kwa moja.

Wakati viongozi wa kitaifa wa shirika yanapoendelezwa, kunakuwepo na ngazi tatu kwenye shirika: viongozi wa umisheni, viongozi wa shirika wa makanisa hayo, na wachungaji wa makanisa ya mahali. Viongozi wa shirika hufanya kazi moja kwa moja na wachungaji wa makanisa ya mahali. Mara nyingi viongozi wa umisheni hufanya kazi na viongozi wa shirika.

Baadhi ya mashirika ya kimisheni hutoa uongozi wenye nguvu ambao hutengeneza shirika wenye nguvu wa makanisa. Mashirika mengine ya umisheni hutoa msaada kwa mashirika ya makanisa dhaifu na hawadai kuwa na madaraka yeyote juu yao.

Kama mahusiano yaliyopo kati ya haya madaraja matatu ya uongozi hayatafafanuliwa kwa uwazi kunaweza kukatokea mikanganyiko ya kutoelewana. Mara nyingine watu kutoka kwenye makanisa hayo ya mahali huwasiliana na viongozi wa umisheni kuhusiana na vigezo vyao badala ya viongozi wa kitaifa wa dhehebu kwa sababu wanafikiria kwamba shirika la kimisheni limejaa ukarimu katika vianzo vyake vya mapato. Wakati mwingine viongozi wa umisheni hufanya kazi moja kwa moja na makanisa, wakiwavuka viongozi wa dhehebu. Hali hii inaleta mchanganyiko kwa viongozi wa dhehebu kwa sababu inafanya majukumu yao kutokuwa wazi.

Kwenye sehemu iliyotangulia tuliorodhesha majukumu ya dhehebu. Kwenye dhehebu lililoanzishwa na umisheni, majukumu hukamilishwa kwa viongozi wa muungano na viongozi wa umisheni kufanya kazi kwa pamoja. Kwa kipindi cha muda, viongozi wa dhehebu watapaswa kwa polepole kuendelea kuchukua majukumu zaidi. Hali halisi ya dhehebu liliokomaa ni kwamba unaweza kufanya kazi vizuri sana hata kama hautapata msaada kutoka kwenye misheni husika.

Taarifa Saba kwa Muhtasari

1. Shirika la makanisa/dhehebu husaidia kuwepo na uthabiti wa kanisa la mahali.

2. Shirika linaweza kuwa “dhaifu au “lenye nguvu” kutegemeana na jinsi uongozi mkuu wa shirika/dhehebu unavyokuwa ni muhimu.

3. Washirika wa dhehebu “dhaifu” kwa kawaida husisitiza uhuru wa kujitawala wa makanisa ya mahali.

4. Washirika wa dhehebu “lenye nguvu” wanasisitiza kujikabidhi na kutumika kabisa kwa ajili ya dhehebu na kanisa la mahali.

5. Kanisa haliwezi kuwepo kwenye dhehebu na wakati huo huo likawepo kwenye shirika lingine ambalo linahitaji uwajibikaji kamili wenye nguvu.

6. Dhehebu linakuwepo kwa ajili ya kusaidia makanisa kukamilisha malengo yao kupitia njia ya ushiriki.

7. Shirika la kimisheni la kimataifa linapaswa kuhamishia majukumu yake pole pole kwa viongozi wa dhehebu.

Kazi za kufanya Somo la 4

1. Kariri taarifa Saba kwa Muhtasari kwa ajili ya somo la 4. Andika aya moja inayoelezea maana na umuhimu wa kila kipengele katika hizi Taarifa Saba kwa Muhtasari (jumla aya saba) kwa mtu ambaye siyo wa darasa lako. Wakilisha kwa kiongozi wako wa darasa kabla ya kuanza kwa kipindi cha darasa kinachofuata. Kuwa tayari kushirikisha aya moja kwa kikundi kama kiongozi wa darasa atakutaka ufanye hivyo wakati wa majadiliano. Andika Taarifa hizi kutoka kwenye ufahamu wako bila ya kuangalia mahali popote mwanzoni mwa kipindi cha darasa kinachofuata.

2. Kumbuka kutengeneza ratiba ya nafasi yako mwenyewe ya kufundisha kwa wakati ambao utakuwa nje ya darasa na utoe mrejesho wako kwa kiongozi wa darasa baada ya kuwa umemaliza kufundisha.

3. Mtihani: Kwenye mwanzo wa kipindi kingine cha darasa, unahitajika kuandika kutoka katika kumbukumbu za ufahamu wako majukumu kumi ya dhehebu na angalau mambo matano ambayo kanisa linapaswa kuwajibika kabisa kwa dhehebu lake.

Next Lesson