Somo hili linatoa tabia za kanisa lililokua katika mfumo wa maswali. Kanisa linapaswa lifikirie au lizingatie maswali haya kwa ajili ya kuwa na ufahamu wa jinsi wanavyohitajika kuendelea.
Kundi la wanafunzi katika darasa hili wanaweza wasiwe wote wanatoka katika kanisa moja na wanaweza wasiweze kufanya maamuzi kuhusu mabadiliko katika kanisa. Wanaweza wakatumia maswali haya kwa ajili ya kufanya tathmini ya kiwango cha ukuaji wa kanisa na kuweka malengo kwa ajili ya huduma zao wenyewe.
Kwa kila swali lililoko hapa chini, jadili swali linamaanisha nini, ukitumia maelezo ya ufafanuzi yaliyotolewa. Kisha, fikiria ni kwa jinsi gani kanisa linaweza kuendeleza tabia linazozihitaji.
(1) Vikundi vidogo vinavyoleta uhai wa kiroho kwa kanisa viko wapi?
Kanisa lililo na nguvu na lenye uhai lina aina fulani ya vikundi vidogo ambapo maisha endelevu ya kiroho yanasimamiwa. Vikundi hivi vinaweza kuwa ni makanisa ya nyumbani, madarasa ya Jumapili, au vikundi vya aina nyingine. Vikundi hivi vinaweza kuwa ni vile vilivyoandaliwa au vile vinavyojitokeza vyenyewe. Uamsho wa kiroho kwa kawaida huanzia kwenye vikundi vidogo. Maisha ya kiroho ya kanisa hayaendelezwi au kuhuishwa tu katika huduma za ibada. Uwajibikaji wa kiroho na mabadiliko ya maisha kwa kawaida hutokea katika vikundi vidogo. Viongozi wa kanisa wanapaswa wahakikishe kwamba vikundi vidogo vinakuwepo na vinatekeleza haya malengo. Kama muundo uliopo ndani ya kanisa hauwezeshi uwepo wa maisha ya kiroho, mabadiliko yanahitajika.
(2) Nani mmiliki wa kanisa?
Kanisa halitakuwa limekua isipokuwa kumekuwepo na kikundi cha wanachama waliomaanisha na waliojitoa kabisa kwa ajili ya kanisa ambao huchukua jukumu kwa ajili ya huduma ya kanisa na uwezeshwaji wake wa kifedha.
Endapo huduma ya kanisa inaendeshwa kama ni biashara binafsi ya mchungaji, kamwe kanisa halitakaa likue. Kama jengo la kanisa ni la kupangisha, kanisa halitakuwa limekua kama mtu binafsi au shirika la nje ndio wanaolipia kodi ya jengo.
Kwa kweli, jengo na huduma ya kanisa vinapaswa viwe vinamilikiwa na kikundi cha wanachama wa kanisa. Kama jengo litakuwa limekodishwa, kusanyiko linatakiwa lichukue jukumu la pamoja kwa ajili ya kulipa kodi ya jengo.
Huduma ya kanisa la mtaa inatakiwa ianzishwe ili iendelee kama shirika hadi hapo atakaporudi Kristo.
(3) Ni kwa jinsi gani huduma ya mtaa inawezeshwa kifedha?
Hali ya kifedha iliyo nzuri sana kwa ajili ya kanisa inapasa isaidiwe na utoaji wa zaka kwa wanachama wake. Kama kanisa linawezeshwa na shirika la kutoka nje hilo siyo kanisa komavu na liko hatarini. Kama linawezeshwa na mchungaji au na watoaji wachache na siyo kusanyiko lote kwa ujumla, hili kusanyiko litakuwa halijafikia katika kiwango cha familia ya imani iliyokua.
Utoaji wa zaka ni mpango wa Mungu wa kusaidia katika uwezeshaji wa kanisa la mtaa. Viongozi wa kanisa wanatakiwa wafundishe kuhusu utoaji wa zaka na hatua kwa hatua wajenge uwezeshaji wa ndani kwa ajili ya huduma ya kanisa. Kanisa halipaswi litegemee uwezeshwaji kutoka nje kwa ajili ya utendaji wa shughuli zake. Msaada wa nje unatakiwa utumike katika miradi ya kujenga uwezo wa kanisa.
(4) Je, kanisa linatoa uwezeshaji kwa mchungaji anayetumika kwa muda wote?
Mpango wa kibiblia kwa ajili ya mchungaji ni kwamba anautoa muda wake wote kwa ajili ya huduma yake. Wakati mwingine hilo siyo rahisi kwa kanisa jipya, lakini kanisa linapaswa liwe na lengo la kukuza uwezeshaji ambao utamruhusu mchungaji kuendelea kuweka malengo yake kwenye huduma yake bila ya kuwa na wasiwasi wa mahitaji ya kifedha.
(5) Je, ni mfumo gani unaotumika kwa ajili ya kuwajibika kifedha?
Sadaka zinatakiwa zikusanywe na zihesabiwe na zaidi ya mtu mmoja. Watu kadhaa walioaminika wanapaswa wahusike katika kuweka vipaumbele vya kifedha na kanuni za kanisa. Washirika wanapaswa wajue ni kwa jinsi gani mfumo wa kifedha wa kanisa unavyofanya kazi.
(6) Je, ni njia gani zinazotumika kupeleka injili kwa watu walioko nje ya kanisa?
[1]Jukumu la kwanza la kanisa ni kuhudumia washirika wa kanisa waliomaanisha na waliojitoa kabisa kwa ajili ya kanisa katika kusanyiko. Hata hivyo, kanisa ni lazima liweze kuwafikia watu walio majirani na wanaolizunguka kanisa. Kanisa ni lazima liwe na shughuli ambazo watu walioko nje watakuwa na hakika na kazi zinazofanywa na kanisa pamoja na kuisikia injili. Baadhi ya shughuli hizi zinaweza kuwa zisizotarajiwa na zisizopangwa. Viongozi watahitaji kuandaa shughuli zingine, pia. Washirika walio na uwezo wanapaswa waalikwe na wapewe mafunzo kwa ajili ya kuendesha shughuli hizo.
(7) Je, ni kwa jinsi gani kanisa linawajibika na mahitaji ya watu wanaolizunguka kanisa?
Kanisa linatakiwa litafute njia za kushughulika na mahitaji ya watu majirani wanaowazunguka. Kipaumbele kinapaswa siku zote kiwe ni kuonyesha upendo wa Mungu na kudhihirisha kanuni za kibiblia.
(8) Je, kunao watu wa kabila fulani au wengine wenye viwango fulani vya kiuchumi wasiohusishwa kwenye mpango wa kanisa wa kuhubiri nje?
Je, watu maskini hujisikia kukaribishwa kuhudhuria katika kanisa na hali ya nguo zao walizo nazo? Je, watoto walioko katika jumuiya hukaribishwa kuhudhuria hata kama wazazi wao hawapo? Je, kunalo kundi lolote la watu wa kabila fulani wanaojihisi kwamba kanisa halipo kwa ajili yao?
(9) Je, wageni wa kanisa wanasalimiwaje?
Kanisa linapaswa liwape mafunzo watu wake jinsi ya kusalimia wageni wanaotembelea kanisa. Lengo kuu la msingi la kusalimia watu ni kumfanya mgeni ajisikie amekaribishwa vizuri na katika njia ya kustarehesha. Watu kadhaa watapaswa washikamane na kuzoeana na mgeni. Hatapaswa tu kualikwa aje kwenye ibada nyingine, lakini pia akaribishwe ajiunge kwenye kikundi kidogo cha nyumbani au wanapokutanika kusanyiko la nyumbani mahali ambapo anaweza kujifunza na kuuliza maswali.
(10) Je, kanisa linatumia mfumo gani wa kuwaingiza kwenye uanafunzi mara moja watu wapya waliookoka?
Wakati mtu anapookoka, aidha akiwa katika kanisa au mahali pengine popote, hapaswi tu kualikwa kuhudhuria kwenye ibada, bali kwenye mfumo wa haraka wa kuwafanya kuwa wanafunzi. Jambo hili linaweza kuanza kwa ziara binafsi za mchungaji za kutembelea. Anaweza akaalikwa kwenye kikundi kidogo kinachokutana kila wiki. Kanisa linapaswa liwe tayari kuwahudumia watu wapya wanaookoka.
(11) Je, kanisa linaweza kuelezeaje kuhusu kukua kiroho?
Je, watu ambao wamekua kiroho wanaonekanaje? Kusanyiko linatakiwa lifundishwe tabia za kukua kiroho. Tabia hizi siyo kwamba siku zote zinaambatana na uwezo wa uongozi au vipaji, bali watu walio na tabia hizi watapaswa waheshimike kama mifano.
(12) Je, kuna mfumo gani uliopo wenye kusudi la kuendeleza ukuaji endelevu wa kiroho?
Jukumu kubwa na muhimu la kanisani kusaidia katika ukuaji endelevu wa kiroho wa washirika wake wa kanisa (Waefeso 4:11-13). Viongozi wa kanisa hawawezi wakawa ni watu wa kutegemea tu kwamba maendeleo ya kiroho yanatokea. Hawapaswi kuwa ni watu tu wa kuhubiri kwenye makusanyiko na kuacha mambo mengine yote ya maendeleo ya kiroho kuwa ni juhudi ya mtu binafsi. Wachungaji wanapaswa wawe na mfumo kwa ajili ya kuwatia moyo watu kutumia nidhamu za kiroho (mf maombi, utoaji, kusoma maandiko nk). Wanapaswa watoe majukumu ya uwajibikaji kwa watu wote wanaokubaliana nayo. Mambo haya yanaweza kufanyika kupitia mazungumzo ya binafsi, vikundi vidogo, uwepo wa madarasa na njia nyingine zozote zitakazoweza kutumika.
[2](13) Je, kuna muundo wowote wa uanachama ambao unawapa watu njia ya kuwa na msimamo na kujitoa kabisa kwa kanisa?
Watu wanaotaka kuweka msimamo na kujitoa kabisa kwa kanisa wanahitaji hasa kujua msimamo wao huo una maana gani. Baadhi ya makanisa yanadai kwamba hayana muundo wa uanachama, lakini kila kanisa lina njia ya kujua watu wake. Kila mmoja anahitaji kujua watu wanaolifanya kanisa liwepo ni watu wa namna gani.
(14) Je, vigezo vya uanachama au mshirika viko wazi na kujulikana kwa watu wote?
Kila mtu anatakiwa afahamu ni vigezo gani muhimu kwa ajili ya uanachama. Vigezo pamoja na maelekezo ya mchakato wa kuweza kuwa mwanachama unapaswa uchapishwe.
(15) Je, vigezo vya uanachama vinaruhusu mtu mpya anayeokoka kuanza kushiriki kwa haraka?
Mtu ambaye ameokoka na yuko tayari katika msimamo na kujitoa kabisa kwa kanisa anahitajika aweze kulisaidia kanisa haraka inavyowezekana. Hiyo haimaanishi kwamba atahitajika kupewa nafasi fulani ndani ya kanisa au majukumu ya uongozi, lakini atapaswa ajue kwamba yeye ni sehemu ya kanisa.
(16) Je, ni kikundi gani chenye jukumu la kuweka thamani na viwango kwa ajili ya kanisa?
Kunakuwepo na kikundi cha wanachama wenye msimamo miongoni mwa kusanyiko la kanisa ambao hutathmini hali na mwenendo wa kanisa. Wanaweza wakawa ni baraza la mashemasi, au wanaweza wakawa ni wanachama wenye hadhi ya kupiga kura ambao wanaweza wakaitwa ni baraza la uongozi. Viongozi ni lazima waweke umakini mkubwa katika kukuza kikundi hiki. Mabadiliko kwenye kikundi hicho yatakuwa ndicho kipimo cha hali ya baadaye ya kanisa. Mchungaji ni lazima awajibike kwao na kuwa anawapa taarifa wakati wote. Wao pamoja na timu ya uongozi ya kanisa ni lazima wawe na vipaumbele vinavyofanana kwa ajili ya kanisa.
(17) Je, kanisa linashirikisha majukumu yake kwa njia ya maono yaliyo wazi?
Mchungaji, timu ya uongozi, na kikundi cha wanachama wenye wajibu ni lazima watumie muda wao mwingi katika kujadili kusudi na malengo ya kanisa. Watapaswa waendeleze maono kwa ajili ya kanisa ambayo wanaweza wakatoa msaada wao. Kusanyiko linahitajika liwe na uzoefu na maono ya kanisa.
(18) Je, washirika wa kanisa wanajua vyema mafundisho ya imani ya kanisa?
Kanisa ni lazima lifanye jambo la ziada kwa ajili ya watu wake kuliko tu kuongoza ibada na kuwa na uzoefu wa kiroho. Wakati mtu aliyeko nje ya kanisa atakapouliza, “Kanisa lako linaamini nini?” mshirika wa kanisa anapaswa awe na jibu zuri la kumjibu. Washirika wa kanisa wanapaswa wawe na uwezo wa kuelezea misingi ya mafundisho ya imani ya Kikristo na mafundisho ya imani yaliyo maalumu ya kanisa.
(19) Je, washirika wa kanisa wanaelewa uhusiano uliopo baina ya kanisa na dhehebu lao?
Kanisa linapaswa liwe linatimiza ahadi zake kwa shirika au dhehebu lake. Ushirika wa kwenye shirika au dhehebu unaweza ukasaidia katika kutegemeza mafundisho ya imani ya kanisa. Watu wa kanisa wanatakiwa watiwe moyo wa kushiriki kwenye matukio ya shirika au dhehebu.
(20) Je, ni kwa jinsi gani ibada zinapangwa na kufanyiwa tathmini?
Viongozi wanatakiwa waombe sana katika kupanga ibada. Kama Roho Mtakatifu ataongoza ibada katika njia isiyotegemewa, litakuwa ni jambo zuri sana; lakini vinginevyo, viongozi ni lazima wawe na mpangilio wa kufuata. Inapaswa kuwepo na vikao ambavyo viongozi mbalimbali wa kanisa hufanya kazi ya pamoja ya kuandaa dondoo kwa ajili ya huduma za ibada.
Kama kanisa lina ibada nzuri ya kuabudu, kusanyiko linahusishwa na linavutiwa. Kanisa linatakiwa lijaribu kutumia watu wengi tofauti kwenye sehemu mbalimbali za ibada ili kusaidia kuwaweka watu kwenye mvuto na kuwajibika.
(21) Je, ubatizo na Meza ya Bwana vinafanyika kwa mujibu wa maandiko na kwa njia yenye maana?
Kila mtu aliyeokoka kiukweli anatakiwa awe tayari amebatizwa au awe yuko kwenye mpango wa kubatizwa karibuni. Meza ya Bwana inapaswa kutolewa kwa wale walio na ushuhuda wa neema. Meza ya Bwana inapaswa itolewe katika njia ambayo itasaidia washiriki katika kuabudu.
(22) Je, kanisa linatendea kazi nidhamu ya kanisa ya kibiblia?
Kanisa ni lazima liwe kinyume na dhambi. Kama mshirika wa kanisa amepatikana na hatia ya kutenda dhambi, ni lazima akabiliwe katika dhambi yake. Lengo liwe kumleta kwenye toba na kumrejesha kwenye ushindi wa kiroho.
(23) Je, iko timu inayoshirikisha majukumu ya huduma?
Huduma haitakua kama itakuwa haijajenga timu ya uongozi. Kila mtu ana mipaka kwenye kiasi fulani cha watu anachoweza kuwashawishi na majukumu anayoweza kuyabeba. Huduma ya kanisa haipaswi iwe ni huduma ya mtu mmoja.
[3](24) Je, kuna mfumo gani wa kuchagua, kufunza, na kuongeza washirika kwenye timu ya huduma?
Huduma haiwezi ikakua bila ya kuendeleza wanachama wapya kwa ajili ya uongozi wa timu. Wanachama katika timu wanatakiwa wachaguliwe kwa makini sana, lakini kanisa ni lazima siku zote liwe linafanya kazi katika kutafuta na kuendeleza watu ambao wataweza kuchukua majukumu ya baadaye. Ukuaji wa huduma unategemeana na uendelezaji wa viongozi wengi zaidi.
(25) Je, kuna mfumo gani wa kushughulikia migogoro na matatizo ndani ya kanisa?
Migogoro ambayo haijapatiwa ufumbuzi hulidumaza kanisa. Kusanyiko linatakiwa lifundishwe jinsi ya kutatua migogoro binafsi kwa watu. Viongozi wa kanisa hawapaswi kupuuza migogoro lakini uwe tayari kusaidia kuleta upatanisho.
(26) Je, kanisa linatoa msaada kwa huduma za umisheni kwa ushirikiano na makanisa mengine?
Kama kwa ukweli kanisa lina matarajio ya kutaka kuundeleza ufalme wa Mungu, halitahusika katika kufanya tu kazi ya kutaka lijulikane na kupata ushawishi katika mtaa, lakini litatoa msaada kwa huduma nyingine. Kanisa hudhihirisha kwamba ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu wakati linapojitolea kwa ajili ya huduma ambayo haitakuwa ni faida kwa ajili yake peke yake.
(27) Je, kanisa linatoa msaada kwa kanisa lingine jipya linaloanza?
Kanisa lililokua au lililokomaa linapaswa liwe linasaidia kanisa lingine jipya linaloanzishwa katika eneo hilo la karibu. Kanisa hilo jipya litaweza kuwafikia watu ambao hawangeweza kufikiwa na kanisa lililopo.
(28) Je, huduma ya kanisa inahudumia watu wa marika yote na aina zote za watu katika kusanyiko?
Mahitaji ya watoto, wazee, vijana, familia changa, wanaume, watu ambao hawajaolewa, na wengine wanapaswa wawe watu muhimu katika kanisa. Kanisa linapaswa pia lifikirie kuhusu mahitaji ya watu wa ngazi zote za ukuaji wa kiroho.
(29) Je, watu katika kusanyiko wanafanya kazi kwa pamoja katika kuangalia mahitaji ya washirika wa kanisa?
Kanisa ni lazima liweze kujali kuhusiana na mahitaji ya kifedha ya watu walio wahitaji katika kusanyiko. Mahitaji mengi yanapaswa yatolewe na watu walio tayari kusaidia watu wengine pasipokuwepo na usimamizi wa viongozi wa kanisa. Kama washirika wengi wa kanisa hawatajisikia kuwa na jukumu la kuwasaidia watu wengine walio wahitaji katika kanisa, watakuwa bado hawajatengeneza kanisa lililokomaa.
(30) Je, ni kwa jinsi gani kanisa linahakikisha kwamba mahitaji ya watu walio na uhitaji ya kifedha katika kusanyiko yanashughulikiwa?
Kanisa linapaswa liwe na mashemasi ambao watahakikisha kwamba mahitaji ya wahitaji katika kanisa yanatambulika. Kanisa katika kitabu cha Matendo liliwachagua mashemasi wa kwanza kwa ajili ya huduma hii.
Miongoni mwa njia zote za kiungu ambazo zimewekwa kwa ajili ya kukamilisha umisheni wa Ukristo ni kupitia kwa watu wa eneo fulani maalumu waliopewa jukumu kwa ajili ya kuhubiri Injili.”
“Yesu alilianzisha kanisa kwa yeye mwenyewe kuwaita na kuwakusanya pamoja watu wa kufanya utume waliokuwa karibu na yeye mwenyewe, akiwapa mafunzo, nidhamu, na kuwasimika kwenye huduma ya kulitangaza au kulieneza Neno na kushirikisha sakramenti, akieleza wazi nia yake isiyoweza kutenguliwa ya kujenga jumuiya endelevu ambayo itasimikwa ikiwa na nguvu na mamlaka ya kubatiza, kuhubiri, kutunza nidhamu, na kusherehekea chakula cha Pasaka pamoja na Bwana aliyefufuka.
“Mwili huo mmoja unaofanana unapigana na mamlaka na nguvu za kipepo, na kwamba unategemea hata madhara mengine makubwa zaidi kwa siku za baadaye, ndiyo kwa wakati huo huo tayari uko na ushindi kutokana na uwezo wake wa sasa wa kuungana na kichwa kwenye jiji la mbinguni, kwa mategemeo ya furaha iliyokamilika katika Bwana ambako wote walio waaminifu watamtukuza Mungu kwa pamoja kwenye mwisho wa nyakati.”
- William Pope, Ufupisho Kamili wa Teolojia ya Kikristo
(A Compendium of Christian Theology)
Print Course
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.