Mafundisho Na Mazoezi Ya Kanisa
Mafundisho Na Mazoezi Ya Kanisa
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 1: Mungu Mmoja na Kanisa Moja

12 min read

by Stephen Gibson


Utangulizi

► Kwa nini unaenda Kanisani?

Wakati watu wanapozungumzia kuhusu “kwenda kanisani” wanamaanisha kwenda kwenye nyumba ya ibada kwa ajili ya ibada iliyopangwa.

Watu wengi Wanasema wanatenda kanisani kwa ajili ya kujifunza kuhusu Mungu. Watu wengine wanaojisikia wako mbali na Mungu huenda kanisani wakitegemea kuusikia uwepo wa Mungu. Watu wanaomjua Mungu huenda kanisani wakitegemea kuusikia na kuupata uwepo wake Mungu kwenye sifa. Kanisa ni kuhusiana na Mungu. Watu wanapaswa waweze kuusikia na kupata uwepo wa Mungu kwenye ibada za kumsifu Mungu za kanisa.

Lakini kanisa siyo jengo, na vile vile siyo mahali pa makutaniko ya kusifu. Kanisa ni kusanyiko la waumini ambao wamedhamiria kwa pamoja kuwa kanisa. Kwa hiyo, Tunaposema kuhusu watu kuliona kanisa au kwenda kanisani, tunamaanisha ni kikundi cha watu walioamini. Tunaposema kwamba kanisa ni kuhusiana na Mungu, hatumaanishi tu kwamba jengo na ibada ya kusifu ni kuhusiana na Mungu. Maisha ya kikundi cha watu waliodhamiria waliyo nayo kwa pamoja ndiyo kuhusiana na Mungu.

Asili ya Neno

Msamiati wa kigiriki ekklesia (G1677)[1] ni neno ambalo kwa kawaida hutafsiriwa “kanisa” katika Agano Jipya. Wakati likitolewa tangazo la watu wakusanyike pamoja katika jiji kwa ajili ya kukutana, mkusanyiko huo ulikuwa unaitwa ekklesia.

Ekklesia ni neno linalotumika kwa ajili ya kanisa katika Agano Jipya. Neno hili limetumika mara 117 kwenye Agano Jipya, lakini siyo matukio yote yanayorejea kanisa. Baadhi yanarejea kwenye aina nyingine za mikusanyiko (Matendo 19:32, 39, na 41).

Injili inatolewa kwa watu wa rangi zote, jamii zote, maeneo yote na kazi zote. Kama ambavyo kila mtu kwenye jiji anaweza kusikia tangazo la kukusanyika, hakuna kikundi cha watu kinachotengwa katika kupokea injili.

Kanisa ni kikundi cha watu ambacho kimekubaliana na wito wa injili. Watu wake wanatoka katika makundi mbalimbali ya watu ili kuunda kikundi maalumu chenye watu tofauti ambao wamejiachilia kabisa kwa ajili ya Kristo na kanisa lake.


[1]Hii ni namba ya Strong’s Concordance kwa neno la kigiriki.

Mungu Baba katika Kanisa

Nafsi za Utatu Mtakatifu wa Mungu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu – zinahusiana na waumini kwa njia za kipekee katika kanisa.

Mungu atatukuzwa milele kwa ajili ya kazi anazozifanya ndani ya kanisa.

Naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina (Waefeso 3:21).

Kwa kuwa kanisa lipo kwa ajili ya utukufu wa Mungu, hakuna jambo lolote linalotakiwa lifanyike ambalo siyo la kumpa Mungu heshima. Kanisa halipaswi kufanya jambo lolote litakalowapa watu ufahamu usiotakiwa kuhusiana na Mungu alivyo, au jambo la kumfanya mtu awe ndiyo dira badala ya Mungu.

Kanisa ni familia ya Mungu

Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio (Wagalatia 6:10).

Basi ninyi salini hivi: “Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe” (Mathayo 6:9).

Kwa kuwa kanisa ni familia ya Mungu, haiwezekani kwa ukweli mtu kuwa katika kanisa isipokuwa awe ana mwamini Mungu na yuko kwenye uhusiano na yeye. Mtu haingii katika kanisa tu kwa kuwa anawajua watu waliomo ndani ya kanisa. Mtu anaingia katika kanisa kwa kuingia kwenye uhusiano na Mungu, na kisha, kuingia kwenye uhusiano na watu wa Mungu waliopo.

► Je inamaanisha nini kuwa na Mungu kama Baba?

Kristo katika Kanisa

Yesu ndiye aliyelianzisha na kulijenga kanisa. Yesu anaahidi mafanikio ya mwisho ya kanisa.

[1]Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda (Mathayo 16:18).

Yesu anaahidi kuwa na kanisa.

...Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:20).

Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao (Mathayo 18:20).

Kristo ndiye kichwa cha Kanisa. Kanisa ndiyo mwili wake hapa duniani. Uhusiano binafsi wa Yesu alio nao na kanisa ni wa kina sana kuliko tunavyoweza kuelewa.

Akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote (Waefeso 1:22-23).

Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake (Waefeso 5:30).

[2]Kwa kuwa mshirika wa kanisa ni sehemu ya mwili wa Kristo, haiwezekani kihalisia mtu kuwa sehemu ya kanisa isipokuwa yeye binafsi awe ameiweka imani yake kwa Yesu kama Mwokozi na amekubaliana na mamlaka ya Kristo kama Bwana.

► Je, ni aina gani ya mtu anayeweza kuitwa sehemu au mjumbe wa mwili wa Kristo?


[1]

“Kifungu binafsi cha ‘kanisa langu’ kinaonesha kwamba Yesu, kwa mujibu wa Mathayo, kwa makusudi alionesha kutaka kutengeneza jamii endelevu ya maombi, kuhubiri, na nidhamu. Aliwaita na kuwafundisha wanafunzi wake na kuwapa ahadi ya kuja kwa Roho Mtakatifu ili kuwaongoza baada ya yeye kuondoka na kupaa mbinguni.”

- Thomas Oden,
Life in the Spirit

[2]

“Mahali popote Yesu alipo, kuna kanisa katholiko [la ulimwengu wote].”

- Ignatius
(katika barua yake kwa Smirna)

Roho Mtakatifu katika Kanisa

Kitabu cha Matendo kinaonesha kwamba kanisa la kwanza lilikuwa linatambua uwepo wa Roho Mtakatifu pamoja na nguvu zake. Roho Mtakatifu alitoa uvuvio na nguvu kwa ajili ya kuhubiri (Matendo 2:11). Aliwaita watu kwenye wito wa huduma maalumu (Matendo 13:2). Aliwaongoza watu kuwa kwenye maeneo sahihi ya huduma zao (Matendo 16:6-10). Alitoa ufumbuzi masuala yaliyohusu fundisho la imani (Matendo 15:28).

Roho Mtakatifu ni mwongozaji mkuu wa kanisa katika kukamilisha umisheni wake wa dunia nzima.

Hakuna shirika lolote binafsi la kibinadamu linaloweza kutegemea kukamilisha kazi yote. Mungu amewaita na kuwatuma wamisionari, na anajua vigezo vya kila eneo la kijiografia.

Mtu ataingia katika kanisa kwa kuona miujiza ya kuzaliwa upya inayotokana na Roho Mtakatifu. Kwa kuwa uwepo wa miujiza ya kuzaliwa upya ni uzoefu unaopita ufahamu wa kawaida, uinjilisti unaongozwa katika njia isiyokuwa ya kawaida na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu. Matokeo ya uinjilisti hayawezi kuelezeka kwa njia za kawaida.

Uhai wa kanisa unategemea Roho Mtakatifu.

Kuabudu kwa kanisa la kwanza kullkuwa kunaongozwa na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu alizungumza kupitia watu wake mbalimbali (Matendo 4:30-31). Utaratibu wa ibada ulikuwa unaweza kubadilishwa wakati wowote na Roho Mtakatifu.

Kanisa ni tofauti na shirika la aina yeyote ile la kibinadamu. Washirika wa kanisa wanakuwa kwenye ushirika wa kila mtu na mwenzake kwa sababu wako kwenye ushirika na Mungu na wana maisha ya kiroho. Mtu ambaye hajaokoka kiuhalisia hayuko kwenye huo ushirika hata kama atalipenda kanisa na rafiki wa watu walioko katika kanisa hilo.

Roho Mtakatifu hugawa karama za kiroho ili kwamba watu wanaohusika nazo waweze kuzitumia katika kuhudumiana mmoja kwa mwingine (1 Wakorintho 12:4-7). Kwenye siku za kwanza za kanisa la kwanza katika Yerusalemu, kuwajibika kwa washirika pamoja na umoja wao kulikuwa ni kwa nguvu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa waumini wa wakati huu kuweza kufikiria ilivyokuwa. Watu waliuza mali zao na kuzikabidhi hizo fedha kwa kanisa ili washirika wa kanisa waweze kushirikishana maisha kwa pamoja. Wakati Anania na Safira walipoamua kusema uongo, waliuawa kwa sababu dhambi yao haikuheshimu kazi ya ajabu ya Roho Mtakatifu aliyokuwa anaifanya kwa kanisa (Matendo 4:32-35, Matendo 5:1-4).

Umoja wa kanisa unakamilishwa kwa uwepo wa uhai wa Roho Mtakatifu.

Kanisa (ambalo siyo jengo, bali kundi la watu alioamini) linaitwa “hekalu la Mungu” kwa sababu Roho Mtakatifu huishi ndani ya kanisa kwa njia maalumu (2 Wakorintho 6:16). Hukumu iliyo kali hutangazwa kwa mtu yeyote anayeliletea madhara kanisa la kiroho mahali ambapo umoja wa Kikristo unakaa (1 Wakorintho 3:16-17).

► Je, utasemaje kwa mtu anayedai kwamba amewezeshwa nguvu na Roho Mtakatifu lakini analipiga vita kanisa pamoja na kuligawa?

Mungu hudhihirishwa na Kanisa

Kanisa lina msaada kwa watu katika kumkumbuka Mungu, kumwelekea Mungu, na kuwa na uzoefu wa mabadiliko yanayofanywa na Mungu.

Kanisa limeundwa na kuanzishwa na Mungu. Zaidi ya mahali pengine popote ulimwenguni, kanisa ni mahali ambapo mapenzi ya Mungu hufanyika kwa makusudi na watu wanaompenda Mungu. Kwa hiyo, kanisa linauonesha ulimwengu ni kwa jinsi gani Mungu alivyo.

► Je, ni mambo gani kadhaa ambayo watu wanapaswa kuyaona kuhusiana na Mungu wanapoliangalia kanisa?

Kwa kuliangalia kanisa, watu wanapaswa wamwone Mungu kwamba ni wa upendo na mwenye huruma, anawajali watu wote, anasamehe, anapenda ukweli, anatimiza ahadi zake, na anachukia dhambi wakati anawapenda wenye dhambi.

► Je, ni makosa gani ambayo watu wanatakiwa wayaepuke kwa kukumbuka kwamba kanisa ni kuhusiana na Mungu?

Kuabudu

Kwa kuwa kanisa lipo kwa ajili ya Mungu, kuabudu kwa kanisa kunapaswa kuwe katika kumlenga Mungu. Wakati kuabudu kunapofanyika kwa kuwalenga viongozi wa kibinadamu au watendaji, inakuwa ni ya kibinadamu, ambayo ni ibada ya sanamu. Kuabudu kubaya kunafanyika kimwili, kwa kuwatukuza baadhi ya watu na kuvutiwa na tamaa za mwili. Kuabudu kuliko kubaya kunaweza hata kufikia kuwa ni ibada za kishetani kwa sababu wanaokuwa katika kuabudu wanajiachilia wenyewe kuwa katika hisia na roho zisizotoka kwa Mungu.

Kanisa Moja la Ulimwengu wote

► Mwanafunzi atapaswa kusoma Waefeso 4:1-6. Je, kuna jambo gani la muhimu ambalo kifungu hiki kinataka kuonesha kuhusu kanisa?

Paulo aliwataka waumini wawe katika umoja. Sababu za kuwa katika umoja ni kwamba kuna kanisa moja tu, kama na ambavyo Mungu ni mmoja na injili ni moja tu. Wakristo wote wa kweli wako katika mwili mmoja. Kuna ukristo mmoja na kanisa moja kwa sababu kuna Mungu mmoja.

Ukweli kwamba kuna kanisa moja la ulimwenguni kote kunawekewa msisitizo katika 1 Wakorintho 12:13, wakati Paulo aliposema kwamba watu wote wa Mataifa wanaoamini wawe mwili mmoja.

Ukiri wa imani ni kanuni ya imani za msingi za Ukristo. Ukiri wa imani ya Ukristo wa kwanza ulioitwa “Imani ya Mitume” ulihusisha taarifa iliyokuwa inasema “Ninaamini katika kanisa moja la katholiko.” Neno katholiko katika kanuni ya imani halina maana ya kurejea Kanisa Katoliki. Ilimaanisha “mahali pote” au “mzima.” Ukiri wa imani ulikuwa unasema kwamba kuna kanisa moja tu linalowakilishwa na Wakristo kila mahali.

► Mwanafunzi atapaswa kusoma Waefeso 2:20.

Kanisa limejengwa juu ya msingi mmoja: huduma na ukweli vilivyofunuliwa na mitume na manabii; na huduma, ujumbe, upatanisho, na maisha endelevu ya Yesu Kristo. Kuna msingi mmoja na kanisa moja.

Kuna dini moja iliyoko katika nchi ya China inayoitwa Mwangaza wa Mashariki, (Eastern Lightning). Wanaamini kwamba kazi ya Yesu ilishakwisha, na kwamba Mungu amemtuma masihi mpya wa wakati huu wa sasa. Huyu masihi ni mwanamke wa Kichina ambaye anafundisha mafundisho mapya ya imani.

► Je, utakuwa na jibu gani la kumjibu mtu aliyetoka katika dini ya Mwangaza wa Mashariki?

Umoja wa kanisa la ulimwengu haimaanishi kwamba shirika moja ndilo kanisa lote. Hakuna shirika moja linaloweza kufikia ukaribu wa kukamilisha kusudi la Mungu kwa ajili ya kanisa kila mahali ulimwenguni. Yesu aliwaambia mitume wake wasitegemee kwamba Wakristo wote watakuwa kwenye shirika moja (Marko 9:38-39).

Kanisa Katoliki linadai kuwa ndilo kanisa lote la Mungu. Wamomoni na Mashahidi wa Yehova wanadai jambo linalofanana na hilo.

► Je, utasema nini kwa mtu ambaye anadai kwamba shirika lake ndilo kanisa lote la Mungu hapa ulimwenguni?

Uwajibikaji wa Kanisa la mahali kwa Kanisa Moja

Kanisa la mtaa halipaswi na au halitakiwi kujiona kwamba liko huru kutengeneza mafundisho ya imani kwa ajili yake lenyewe. Kwenye eneo moja, Paulo alitoa maelekezo, kisha akasema ilifanyika kwa njia hiyo katika makanisa yote ya Mungu (1 Wakorintho 11:16). Aliliambia kanisa kwamba wanapaswa wawakubali baadhi ya wahudumu wa huduma kwa sababu wanawakilisha makanisa mengine (2 Wakorintho 8:23-24). Alikuwa anamaanisha wazi kwamba itakuwa ni makosa kwa kanisa kuamua kushikamana na mafundisho ya imani yanayotofautiana na makanisa mengine yote.

Kanisa la Wakorintho lilikuwa limebarikiwa kuwa na karama za kiroho. Walianza kujifikiria wenyewe kama walio huru, wasiokuwa na hitaji la kumsikiliza mtu mwingine yeyote. Paulo alifanya masahihisho ya fikra zao na utendaji wao na akawakumbusha kwamba wao hawakuwa chanzo cha asili cha Neno la Mungu; lilikuja kwao kutoka kwa watu wengine na halikuwa limekuja kwao kwa ajili yao pekee (1 Wakorintho 14:36). Aliendelea kusema kwamba wale waliokuwa katika kanisa lao ambao walikuwa na ufahamu wa kiroho wangetambua maelekezo ya Paulo kwamba yamevuviwa na Mungu.

Kanisa la mahali linapaswa lijiongoze na liwe na uwezo wa kujiendesha lenyewe; lakini linahitaji liwe na uhusiano na kanisa la ulimwengu kwa ajili ya kuimarisha mafundisho ya imani, vianzo vya mafundisho, na mtazamo wa ulimwengu wa umisheni.

Wakati wa leo kuna makanisa mengi na mchanganyiko mbalimbali wa mafundisho ya kiimani, ingawaje wanadai kwamba yanafuatana na Biblia. Kwa kanisa kuwajibika kwa ajili ya kanisa la ulimwengu haimaanishi kwamba ni lazima lijitahidi kufanana na makanisa mengine yote yanayolizunguka. Kinachohitajika hapa ni kushikamana na mafundisho yote ya imani kwa ajili ya Ukristo ambayo yalikuwa ni muhimu wakati wa kuanza kwa kanisa la Agano Jipya. Ni lazima kanisa pia liwe sehemu ya jumuiya ya makanisa ambayo yanawajibika kwa ajili ya kila mmoja na mwenzake.

Kwa ajili ya kuwa na uthabiti wa mafundisho ya imani, Kanisa la mtaa linapaswa lizingatie mambo matatu:

1. Kuwa na imani kwamba Biblia ndiyo mamlaka iliyo kamili.

2. Mafundisho ya imani yaliyokuwa muhimu katika historia ya Ukristo.

3. Kuwa na ushirika na jumuiya ya makanisa yaliyo na teolojia nzuri inayokubalika.

Katika somo hili tunajifunza kipengele cha pili kutoka katika vipengele vitatu vilivyooanishwa katika orodha ya hapa juu. Tutazungumzia kuhusu jumuiya za makanisa kwenye somo lingine.

Kanisa la mtaa halipaswi kujiona kwamba liko huru kukubaliana na mafundisho yeyote ya imani yaliyo kinyume na mafundisho ya imani ya Ukristo ambayo yalikuwa ni muhimu wakati wa kanisa la kwanza. Mafundisho hayo yameelezwa kwenye ukiri au unaweza kusema matamko ya Imani ya mwanzoni. Imani ya Mitume, Imani ya Nikea, na imani ya Kalsedonia zinaelezea mafundisho ya imani ambayo yalikuwa ni muhimu kwa Ukristo tangu mwanzo. Hii ni pamoja na imani ya mafundisho ya Utatu Mtakatifu wa Mungu, uungu wa Kristo na kuhusu Roho Mtakatifu. Endapo kuna kanisa linalokataa mafundisho haya ya mwanzo ya imani, halipaswi kujiita lenyewe kuwa ni la Kikristo, kwa sababu hilo litakuwa ni dini tofauti.

Imani ya Nikea

Nina mwamini Mungu mmoja, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.

Na katika Bwana mmoja, Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu, Mwana pekee wa milele wa Baba; Yu Mungu kutoka Mungu, Yu nuru kutoka nuru, Yu Mungu kweli kutoka Mungu kweli; Mwana wa milele asiyeumbwa, mwenye uungu mmoja na Baba: Kwa yeye huyu vitu vyote viliumbwa. Aliyeshuka mbinguni kwa ajili yetu wanadamu na kwa wokovu wetu; akatwaa mwili kwa uweza wa Roho Mtakatifu katika Bikira Mariamu, akawa mwanadamu; Akasulubiwa kwa ajili yetu zamani za Pontio Pilato; Aliteswa, akazikwa. Siku ya tatu akafufuka kama yanenavyo Maandiko Matakatifu: Akapaa mbinguni; ameketi mkono wa kuume wa Baba; Naye atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Na ufalme wake hauna mwisho.

Na nina mwamini Roho Mtakatifu Bwana mtoa uzima, atokaye katika Baba na Mwana; anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana; aliyenena kwa vinywa vya manabii. Na nina aamini kanisa moja, takatifu, (katholiko) la Kikristo la ulimwengu wote na la kimitume. Nina kiri ubatizo mmoja na ondoleo la dhambi. Nina tazamia ufufuo wa wafu na uzima wa ulimwengu ujao. Amen.

Je, itakuwaje kama mtu ataamua kutokukubaliana na mojawapo ya maelezo yaliyoko kwenye Imani ya Nikea? Kwa kuwa imani hizi zimeshikiliwa na kanisa tangu mwanzo, kama ataamua kukataa mojawapo ya hizi, atakuwa anajinadi kuwa ana uelewa wa kweli ambao kanisa halikuwahi kuwa nao kwa miaka 2000. Kama kanisa au mtu binafsi hawezi kushikamana na imani zilizoko kwenye Imani ya Mitume, Imani ya Nikea, na Imani ya Kalsedonia, imani yake haistahili kuaminika. Imani zote zilizoko hapa zinaunga mkono injili. Ikiwa mtu anakataa mojawapo ya mafundisho haya, anaweza kuwa anaichanganya injili.

► Je, utasema nini kwa mtu anayesema kwamba yeye ni Mkristo lakini hakubaliani na maelezo yaliyoko kwenye Imani ya Nikea?

Taarifa Saba kwa Muhtasari

1. Kanisa la mahali ni kundi la waumini ambao wamejitoa kuwa pamoja kuwa kanisa katika eneo waliko.

2. Kanisa linadhihirisha asili ya Mungu kwa ulimwengu.

3. Maisha ya Roho ni maisha na umoja wa kanisa.

4. Uanachama wa kanisa una msingi wake kwenye uhusiano na Mungu na kujitoa kwa ajili ya kundi la waumini.

5. Kuna kanisa moja tu la ulimwengu wote linalofuata Ukristo wa aina moja kwa sababu kanisa ni kuhusiana na Mungu mmoja.

6. Hakuna shirika lolote la kibinadamu ambalo linaweza kuwa ni kanisa lote la Mungu katika ulimwengu.

7. Kanisa la mahali ni lazima lishikamane na imani zote muhimu na za kihistoria za kanisa la ulimwengu wote.

Kazi za kufanya Somo la 1

1. Kariri taarifa Saba kwa Muhtasari kwa ajili ya somo la 1. Andika aya moja inayoelezea maana na umuhimu wa kila kipengele katika hizi Taarifa Saba kwa Muhtasari (jumla aya saba) kwa mtu ambaye siyo wa darasa lako. Wakilisha kwa kiongozi wako wa darasa kabla ya kuanza kwa kipindi cha darasa kinachofuata. Kuwa tayari kushirikisha aya moja kwa kikundi kama kiongozi wa darasa atakutaka ufanye hivyo wakati wa majadiliano. Andika taarifa hizi kutoka kwenye ufahamu wako bila ya kuangalia mahali popote mwanzoni mwa kipindi cha darasa kinachofuata.

2. Wakati wa kozi hii, utahitajika kufundisha somo, au sehemu ya somo, kwa mtu binafsi au kikundi ambacho siyo sehemu ya darasa lako. Unaweza kuchagua maudhui ya kufundisha. Itakupasa ufanye hivyo mara tatu, kwa kutumia mafundisho tofauti. Fanya mpangilio wako mwenyewe wa nafasi za kufundisha na toa taarifa kwa kiongozi wa darasa baada ya kuwa umemaliza kufundisha.

Next Lesson