Hadi kufikia mwishoni mwa somo hili, mwanafunzi atapaswa:
(1) Kuelezea sifa na tabia za upendo wa kweli.
(2) Kufafanua inamaanisha nini kumpenda mtu bila masharti.
(3) Kuelezea umuhimu wa kuthibitisha upendo kwa lugha ya msingi ya upendo ya mtu.
(4) Kutumia maneno ya kuthibitisha katika kuonyesha upendo na uthamini kwa ajili ya sifa binafsi za mwanafamilia, sifa bainishi za tabia na sifa bainishi za nafsi ya mtu.
Yusufu alichanganyikiwa kwa kuwa mke wake hakuwa na furaha. Hakujua ni kitu gani alikuwa anahitaji kutoka kwake. Yusufu alifanya kazi kwa bidii sana na kuweza kuwapa mke na watoto wake nyumba na chakula na kila kitu cha muhimu kilichohitajika katika maisha. Alimruhusu mke wake aweze kununua kitu chochote anachokihitaji. Mke wake hakuwa na wasiwasi kuhusiana na jambo lolote. Je, ni nini cha zaidi ambacho mke anaweza akawa anahitaji? Yusufu alijisikia kwamba mke wake alikuwa hathamini kazi yake anayoifanya.
Hana hakuwa na furaha kwa sababu alikuwa anamtaka Yusufu amwonyeshe upendo wake kwake kwa kufikiria juu ya mambo mahususi kwa ajili yake. Zawadi yake aliyoipenda sana kutoka kwa Yusufu ni kinyago cha mti kilichokuwa kimetengenezwa kwa ajili yake na Yusufu na kilikuwa kimeandikwa jina lake na Yusufu kutoka kwenye duka lake. Badala ya Yusufu kumwambia Hana kwamba anunue chochote alichokihitaji, alitamani Yusufu wakati mwingine amnunulie maua.
Yusufu na Hana walikuwa wakiongelea kuhusu hisia zao na wakaanza kila mmoja kuelewa mahitaji ya mwenzake.
Upendo wa Kweli ni nini?
► Je, inamaanisha nini kumpenda mtu kwa kweli?
► Mwanafunzi anapaswa asome 1 Wakorintho 13:4-8 kwa ajili ya kikundi. Kutokana na kifungu hiki, orodhesha sifa na matendo ya upendo. Orodhesha mambo ambayo upendo hauko hivyo na upendo haufanyi hivyo.
Inaweza ikaonekana kutoka katika kifungu hiki kwamba upendo unajulikana kwa kile ambacho sicho zaidi ya kile ambacho ndicho. Lakini maelezo ya kile ambacho upendo haufanani nacho yanatufundisha sisi kuhusu upendo unafanania nini. Kama upendo hauna kiburi, basi ni nini? Ni kinyume chake. Upendo ni unyenyekevu.
► Sasa andika kinyume cha kila kimoja cha mambo ambayo siyo ya kweli kuhusu upendo, kama ilivyoelezwa kwenye 1 Wakorintho 13:4-8 na kuandikwa kwenye Jedwali la hapo juu.
Upendo Unavyofanania
Unachokifanya Upendo
Upendo wa Kweli:
Siyo jambo la hisia tu (ingawa hisia mara nyingi huambatana na upendo)
Unatolewa kwa kufanya uchaguzi, na siyo kwa sababu ya mahitaji
Siyo wa masharti; hautegemei matendo ya mtu mwingine
Ni wa kukusudia, siyo wa bahati mbaya
Unagharimu kitu.
Hutafuta ni kitu gani kizuri sana kwa ajili ya mtu mwingine
Hujidhihirisha wenyewe kwa njia ya utoaji
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee…” (Yohana 3:16). Upendo wa kweli hujidhihirisha wenyewe kwa njia ya utoaji. Hii si lazima iwe kutoa zawadi inayoonekana au ya mali. Wakati mwingine zawadi inaweza ikawa ni maneno mazuri ya upendo; Wakati mwingine zawadi ni muda wako unaoutoa: Kuwa pamoja na mtu na kuwa unapatikana kwa ajili yake. Wakati mwingine upendo hutolewa kupitia matendo ya huduma au mguso wa upendo. Mungu Baba alitupenda sana sisi kiasi kwamba alitoa kile kizuri kuliko vyote alivyokuwa navyo, Mwanawe wa pekee, ili kwamba tuweze kufanyika watoto wake. Tanapokuwa tunawapenda watu wengine kwa ukweli kabisa, ni lazima tutatoa.
Upendo wa kweli hauna masharti. Siyo tegemezi kwenye tabia au kustahili kwa mtu anayetakiwa kupendwa. Haisemi kwamba, “Kama utafanya hivi na kunipendezesha mimi katika njia hii, basi nitakupenda; lakini kama utafanya vile na kunichukiza, sitaweza kukupenda.”
Upendo wa masharti unasema, “Kama tabia yako itanifurahisha mimi, nitakuzawadia udhihirisho wa upendo utakaokuwa na maana kwako. Lakini kama hutafanya vile ninavyotaka, nitazuia udhihirisho wangu wa upendo.”
Upendo halisi hauna masharti. Utajidhihirisha wenyewe bila kujali kwamba mpokeaji atafanya kitu au hatafanya. Upendo utajieleza wenyewe hata wakati ambapo mpokeaji hana uwezo wa kutoa majibu ya huo upendo; wakati akiwa hana chochote cha kutoa kama mrejesho wake.
Ni muhimu kutambua kwamba kumpenda mtu bila masharti haina maana lazima tumpe kile anachotaka. Haimaanishi kwamba tunawaondolea matokeo ya tabia zao mbaya. Inamaanisha kuwa tunajaribu kila wakati kufanya kile kilicho bora kwao. Ni vigumu sana kumwona mtu unayempenda akiwa anateseka, lakini ikiwa anatenda mabaya, uzoefu wa mateso anayopitia mara nyingi ni kitu pekee kinachoweza kuwafanya kubadilika kutoka katika tabia zao mbaya za uharibifu. Wakati mwingine kile kilicho bora kwa wapendwa wetu ni kuwa waruhusiwe kupambana. Kwa nyakati nyingine, inakuwa ni jambo jema kwetu kuwasaidia kutoka katika mapambano yao. Mara nyingi tunahitaji ushauri wa kimungu na msaada wa Roho Mtakatifu katika kujua tufanye nini katika hali hizi zote.
► Je, ni kitu gani kitakachoweza kutuchochea sisi kuwapenda watu wengine kwa upendo usiokuwa na masharti?
► Mwanafunzi anapaswa asome Warumi 5:8 kwa ajili ya kikundi.
Watu wengi wanahisi kwamba upendo wa Mungu msingi wake ni kwenye utendaji wao. Kwa sababu hiyo, huwa hawaelewi ni kwa nini wawe na upendo usiokuwa na masharti kwa watu wengine. Lakini katika Warumi 5:8 tunaambiwa kwamba Mungu tayari alikuwa ameshatupenda hata wakati ambapo tulikuwa maadui zake. Alitupa Mkombozi wakati tulipokuwa wenye dhambi. Upendo wa Mungu kwa watu wote ni usiokuwa na masharti. Upendo wake hauna misingi yake kwenye tabia yako au utendaji wako. Mungu anakupenda kwa jinsi ulivyo kama mtu, uliyeumbwa kwa sura yake.
Anapenda tuwapende watu wengine kwa njia ile ile ambayo anatupenda nayo sisi (Yohana 15:12, Waefeso 5:2, 1 Yohana 4:11). Sababu ya msingi ambayo inatupasa sisi tuwapende watu wengine bila ya masharti ni kwamba Mungu ametuita sisi tufanye hivyo (Mathayo 5:43-48, 1 Petro 4:8).
Unaweza ukawa unatoa bila ya upendo,
lakini ni jambo lisilowezekana kabisa
ukapenda bila ya kutoa.
Upendo ni lazima ukugharimu kitu fulani.
Watu hujisikia Kupendwa kwa njia Tofauti
Mungu anapenda mchanganyiko wa aina mbalimbali za watu. Huwapa watu kuwa wa mwonekano wa kipekee. Hakuna katika watu wawili wakatokea kuwa na njia zilizo sawa za kufikiria na kuwasilisha hisia zao. Kwa sababu ya tofauti zilizo kwenye mwonekano wao, watu walioko kwenye familia zetu wana mahitaji yaliyo tofauti na sisi. Tofauti zetu tulizo nazo kila siku zinaathiri mahusiano ya familia.
Mojawapo ya njia ambazo watu binafsi hutofautiana ni jinsi wanavyodhihirisha upendo na katika kile ambacho kinawafanya wajisikie wanapendwa, wanathaminiwa, na salama katika mahusiano yao na watu wengine.
Kuna njia nyingi za kuonyesha upendo, na pia kuna njia nyingi za kuwafanya watu wajihisi kwamba wanapendwa. Gary Chapman anaorodhesha aina tano za jumla kuhusu udhihirisho wa upendo.[1] Anaziita Lugha Tano za Upendo. Kila moja ya njia hizi za kuonyesha upendo ni utaratibu wote wa tabia, na siyo tu matendo ya mtu binafsi.
Ingawa kila mtu anahitaji kupendwa katika njia zote tano, inaonekana kuwa watu binafsi hujihisi kwamba wanaopendwa zaidi na aina moja ya udhihirishwaji kuliko wanavyojisikia kwenye aina nyingine za udhihirisho. Udhihirisho nyingine za upendo hazimaanishi jambo lolote kubwa la maana kwao.
Lugha Tano za Upendo
Watu huonyesha upendo kupitia:
1. Maneno ya uthibitisho
2. Muda ulio bora
3. Zawadi
4. Matendo ya Huduma
5. Mguso wa kimwili
Hata hivyo, watu hutambua na kupokea upendo kwenye hizo njia tano.
Lugha ya Msingi ya Upendo
Watu wengi kwa kawaida hutambua na kudhihirisha upendo kimsingi katika njia moja au mbili ya njia hizo tano. Kama wanafamilia hawataonyesha udhihirisho wa upendo wao kwa ajili ya mwanandoa au mtoto katika lugha ya msingi ya upendo ya mtu huyo, mwanandoa au mtoto huyo huenda asijisikie kama anapendwa, ingawaje wanakuwa wanaonyeshwa upendo kwa njia nyingine.
Mwanamke maalumu kimsingi anaweza kudhihirisha upendo wake kwa kutoa muda wake kwa mtu mwingine ambaye anampenda. Atajaribu kuwa pamoja naye kwa mazungumzo na kuwa kwenye mawasiliano na wale anaowapenda. Atatumia muda wake kwa ajili ya kufanya kazi za pamoja. Vivyo hivyo, kwa kuwa hiyo ndiyo njia ya msingi ya yeye kuonyesha upendo, ndiyo njia ambayo yeye hutambua kwa wepesi zaidi upendo wa watu wengine walio nao kwa ajili yake. Anajisikia anayependwa zaidi sana wakati mtu mwingine anapojitolea muda wake kwa ajili yake. Endapo mume wake atamnunulia zawadi au akamfanyia jambo lolote jema, haiwi na maana kubwa sana kwake kulikoni angeutumia muda wake akiwa pamoja na yeye.
Mwanamume fulani kimsingi anaweza kuonyesha upendo kupitia mguso wa kimwili. Atamkumbatia mke na watoto wake na kuwa mwenye furaha wakati wao wanapokuwa wanamkumbatia yeye na kutaka kuwa karibu na yeye. Anaweza akawa anawakumbatia marafiki zake au angalao kuwapiga kidogo kwenye mabega yao au akawasukuma au akavurumishana nao kwa upendo. Anaweza akathamini kazi ngumu ya mke wake aifanyayo kwa ajili ya familia yao, lakini kazi anayofanya sicho kitu kinachomfanya ajisikie kwamba anapendwa na mke wake. Huwa anajisikia anayependwa wakati anapoketi karibu naye na kumpa fursa aweze kuweka mikono yake juu yake kumzunguka, au wakati mke anapomgusa maeneo mbalimbali ya mwili wake kwa njia ya upendo.
Gari linakuwa na tanki la mafuta. \Wakati tanki likiwa liko tupu, gari linakuwa halina uwezo wa kufanya kazi. Wakati mtu anapoupokea upendo katika njia anayoitambua na anahitaji upendo, husababisha mhemuko wa mafuta. Wakati tanki la mhemuko wa mtu linapokuwa limejaa, anakuwa na uhakika kamili na nguvu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali. Anakuwa na uwezo zaidi wa kushirikiana na watu wengine. Anakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua migogoro. Anajisikia kuhamasika katika kukuza na kufanikisha malengo.
Wakati mtu anapokuwa hajapokea upendo kwa njia ambayo anaitaka mwenyewe, anakosa mhemuko utokanao na mafuta. Ni nadra sana mtu kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kukamilisha au kuendeleza jambo endapo atajisikia kwamba hapendwi.
Ikiwa mara kwa mara hatutawaonyesha wanafamilia wetu upendo katika lugha ya msingi ya upendo, hawataweza kutambua ni kwa jinsi gani sisi tunawapenda. Huu ndiyo ukweli, bila kujali ni kiasi gani tunachojisikia nacho kwamba tunawapenda. Tunapaswa tuwasilishe upendo wetu kwao katika njia ambayo wanaielewa.
Kama tutakuwa tunamuumiza mtu mwingine kwenye lugha yake ya msingi ya upendo, hali hiyo ni mbaya zaidi. Kwa mfano, kama maneno ya uthibitisho ndiyo nia muhimu zaidi ya kuonyesha upendo kwa mtoto wetu, maneno yetu ya kukosoa yatakuwa yanamuumiza mtoto zaidi sana kuliko ikiwa angekuwa na lugha tofauti ya msingi ya upendo.
[1]Mawazo mengi kwenye sehemu hii yana msingi wake kutoka katika kazi ya
Gary Chapman, The Five Love Languages: How to Express Heartfelt Commitment to Your Mate, (Northfield Publishing, Chicago, 1995)
Kukua Kupitia Upendo Wetu wa Mtu mmoja kwa Mwingine
Kwenye Somo la 1, tulijifunza kuhusu jinsi ambavyo Mungu aliwaumba watu wote kwa ajili ya uhusiano na yeye mwenyewe pamoja na watu wengine. Mdhihirisho wa upendo ni sehemu muhimu sana kwenye kila aina ya uhusiano. Ni muhimu kwetu kuelewa njia ambazo wanandoa wetu, watoto wetu, na wanafamilia walioshikamana nasi wanavyojisikia kupendwa sana. Elimu hii inatuwezesha sisi kudhihirisha upendo wetu kwa ajili yao katika njia ambazo ni za maana zaidi kwao kibinafsi.
Ndoa ni mara chache sana watu wanategemea iwe jinsi itakavyokuwa. Mara nyingi watu huwa wanakatishwa tamaa na tofauti kati yao wao wenyewe na wenzi wao. Inapotokea kuwa ni suala la kudhihirisha upendo, inaweza ikaonekana kwamba hali itakayokuwa nzuri ni ile ya watu wote kuweza kuwa na lugha ya msingi inayofanana ya upendo. Kutokuelewana kwingi na kufadhaika kungeweza kuepukika endapo wangekuwa katika usawa mmoja wa aina hii. Hata hivyo, tofauti kama hizo zinaweza kuimarisha kama wanandoa wenyewe watakuwa wamejikabidhi kabisa kwenye ndoa yao na kuendelea kukua katika upendo wao kwa ajili ya kila mmoja.
[1]Mchakato wa kila mmoja kujaribu kumwelewa mwenzake, kuzoeana na mwenzake, na kuonyesha kujali katika njia zenye maana humkuza kila mtu na hufanyika ni onyesha la ajabu la upendo wa kweli. Tunapokuwa tunawahudumia wanafamilia wetu kwa kudhihirisha upendo kwao katika njia ambazo wanajisikia kwamba wanapendwa, huwa tunakua katika uelewa wetu na tabia.
Linapokuja suala la kudhihirisha upendo kwa wanandoa wetu na wanafamilia wengine, ni muhimu sana kutambua kwamba hatuwezi tukadhihirisha upendo peke yake kwa njia zetu wenyewe, au tukadhihirisha upendo wakati tu tunapojisikia. Upendo ni uchaguzi na kujitolea kabisa, kwa kuchochewa na thamani ya uhusiano. Katika masuala fulani, tutapaswa tujifunze njia mpya za kuonyesha upendo. Yawezekana hatukukulia kwenye familia iliyokuwa ikidhihirisha upendo kwa njia fulani, lakini mwanafamilia leo anahitaji kupendwa hivyo kwa jinsi ile. Kwenye hali kama hizi, kudhihirisha upendo kwa njia isiyokuwa ya kuzoeleka kunaweza kuonekana ni kujihisi jambo la kushangaza au lisilofaa kwetu tangu mwanzo, lakini tunaweza tukajifunza. Ni muhimu kwamba kamwe tusitende kama ni jukumu lisilokuwa la kupendeza au kwamba ni usumbufu kudhihirisha upendo wetu. Ikiwa itaonekana kwamba tunatenda nje ya uwajibikaji, udhihirisho wetu wa upendo hautawasilisha upendo wa kweli.
► Wanafunzi wanapaswa wasome Warumi 12:9-10, 16 na 1 Petro 3:7-8 kwa ajili ya kikundi. Kutokana na maandiko haya, taja sababu kadhaa ambazo itatupasa tujali kuhusu njia ambazo familia zetu zinajisikia kuwa zimependwa zaidi sana.
Ni jambo muhimu kukumbuka kwamba upendo ni tendo la kujidhabihu binafsi katika kutafuta jambo zuri zaidi kutoka kwa mtu mwingine
Sisi tumezaliwa na asili ya ndani ya ubinafsi. Upendo wa kweli kwa watu wengine hauji kwa njia ya kawaida kwa yeyote kati yetu. Upendo wa kweli hufanyika ni kitu kinachowezekana kutokana na kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu (Warumi 5:5). Kama watu tuliookoka, tunapaswa tujifunze jinsi ya kushikamana na njia ya Yesu ya kufikiri, kama ambavyo Paulo anaelezea katika Wafilipi 2. Tutakapokuwa tunafanya hivyo, tutafanya yafuatayo:
Hatutachochewa na tamaa za binafsi (Aya ya 3).
Hatutakuwa na mtazamo uliokithiri wa kujiangalia umuhimu wetu tu (Aya ya 3)
Tutakuwa tunawafikiria watu wengine kuwa ni wa maana zaidi kuliko sisi wenyewe (Aya ya 3)
Tutakuwa waangalifu katika kuangalia maslahi ya watu wengine (Aya ya 4)
Ni lazima tuweke ahadi ya kukua katika upendo wetu kwa ajili ya wanafamilia wetu. Tunapaswa tujifunze kugundua mahitaji yao na kuangalia njia ambazo zitaweza kuwatimizia mahitaji yao. Lengo letu liwe ni kuwaonyesha upendo wetu kwa ajili yao katika njia ambazo watajisikia wenye kupendwa zaidi.
Sisi kama wazazi tunapaswa pia tuwafundishe watoto wetu kuwajali ndugu na dada zao, wazazi, mababu na mabibi zao katika njia hizi. Watu wetu wanahitaji kujifunza kupenda na kutumikia familia zao. Wanaweza wakajifunza jinsi ya kudhihirisha upendo kwa ajili ya familia zao kwa njia zenye maana zaidi. Ni lazima tufundishe kwa mifano. Tunapaswa pia tuchukue muda wa kuelezea dhana hizi kwao na kuwaongoza katika kuzifanyia matumizi katika mahusiano yao.
► Je, kuna njia gani ambazo wazazi wanaweza kuwasaidia nazo watoto wao kujifunza huu upendo wa kujitoa binafsi kwa ajili ya watu wengine, wakianzia na familia zao wenyewe?
“Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
- 1 Wathesalonike 3:12
Upendo wa Lugha ya 1: Maneno ya Uthibitisho
Watu ambao lugha yao ya msingi ni maneno ya kuthibitisha hujisikia wenye kupendwa zaidi wakati watu wengine wanatumia maneno ya kudhihirisha kuwathamini kwa uaminifu kwa ajili yao. Kama lugha ya msingi ya upendo kwa mwanamke ni maneno ya udhihirisho, mume wake anaweza akadhihirisha upendo wake wakati anapokuwa anaongea naye au anapoongea kuhusu yeye. Anaweza akamwandikia taarifa ndogo, akimwambia baadhi ya sababu mahususi za yeye kumthamini. Anaweza kuzungumza na mtu mwingine yeyote kuhusiana na tabia ya mke wake au kazi yake jinsi ilivyo nzuri. Wakati mke wake atakapokuja kusikia kuhusu maneno yake, atajisikia kupendwa na kuthaminika.
Tunaweza tukawauliza marafiki zetu kwa ajili ya ushauri kwa njia ambayo kwamba inathibitisha thamani yao. Kwa mfano:
“Wewe unaongeza mtazamo mzuri kila wakati, kwa hiyo nataka nipate mawazo yako juu ya jambo hili…”
“Wewe ni mzoefu katika jambo hili, kwa hiyo ningependa nipate ushauri wako…”
“Wewe unajua mengi sana kuhusu ____ kisha ninafanya, kwa hiyo kama una ushauri au mapendekezo yako kwa ajili yangu, nitafurahiwa kama nitayasikia.”
Maneno yote ya uthibitisho yanapaswa yazungumzwe kwa uaminifu. Vinginevyo, yatakuwa hayana maana au yenye kujeruhi. Maneno ya uthibitisho ambayo hayana uaminifu yanadhoofisha mahusiano. Yanakuwa hayako kwenye msingi wa ukweli, kwa hiyo msikilizaji wake hawezi akaamini uhamasishaji wa msemaji.
Maneno ya uaminifu ya uthibitisho ni ya kweli kwa ajili ya ukweli. Siyo ya bandia au yaliyotiwa chumvi nyingi. Kwa kuwa uthibitishaji ni udhihirisho wa kutoka ndani ya moyo. Kinachokuwa kimesemwa ni kile ambacho msemaji kwa ukweli anajisikia nacho na anakiamini.
Maneno ya uthibitisho yanaweza yakamhamasisha msikilizaji kuendelea kukua na kuwa na maendeleo ya baadaye, lakini kamwe hapaswi kuwa mtu wa hila. Hatupaswi tujaribu kuwadhibiti watu wengine kwa maneno ya uthibitisho.
► Mwanafunzi anapaswa asome Waefeso 4:29 kwa ajili ya kikundi. Je, ni maelezo gani yametolewa hapa kwa ajili ya mambo ambayo hayapaswi kusemwa? Je, maneno yetu yanapaswa yakamilishe nini? Je, baadhi ya maneno yanaweza kuwa yanafaa kwenye hali moja na yakawa hafai kwenye hali nyingine?
Kile tunachowaambia watu wengine lazima kila wakati kiwe kinachofaa na chenye neema. Mambo ambayo tunayasema yanapaswa yampe Mungu fursa za kufanya kazi ndani ya maisha ya wale ambao tunazungumza nao. Tunachosema kinapaswa kiwe kinachojenga, na siyo kinachobomoa. Kinapaswa kiweze kukuza afya na uponyaji, na kamwe kisiwe kitakachoharibifu.
Mada za Uthibitisho
Kuna aina tofauti za maneno ya uthibitisho. Siyo maneno yote ya uthibitisho yanakuwa na thamani inayolingana au umuhimu. Maneno ya thamani ya juu ya uthibitisho yanahitaji mawazo mapana na yenye nguvu nyingi kutoka kwa mtu anayewapa; inawezekana hata ikawa ni kujisikia vibaya kuyasema wakati mwingine; lakini maneno haya yanaunganisha upendo katika kiwango chenye nguvu, na njia zenye maana zaidi.
Kusifia Mwonekano
Kusifia mwonekano wa mtu kunaweza kuwa njia mojawapo ya kutoa uthibitisho, hasa kama unaonyesha kuthamini kwa ajili ya juhudi zao au njia ambazo wanazitumia katika kudhihirisha nafsi ya mtu. Hata hivyo, kusifia mwonekano wa mtu ni uthibitisho ulio dhaifu, hasa wakati inapokuwa kwamba haihusiani na asili ya mtu.
Watu wa kipekee wenye mvuto ambao mara nyingi wamekuwa wakisifiwa huwa wanafikia kutokuwa na uhakika kuhusiana na mwonekano wao, kwa sababu wanaanza kujihisi kwamba thamani yao ndipo inapotegemea, na wanafikiri inapaswa iwe kamilifu.
Thamani ya mtu haiamuliwi na mvuto wake wa nje. Aidha, kuna mipaka katika kile ambacho mtu anaweza kufanya ili kuboresha mvuto wao wa kimwili. Kwa sababu ya mambo haya, aina hii ya uthibitisho haipaswi kutumika kupita kiasi.
Kupongeza Mafanikio na Huduma
Njia nyingine ya kumpongeza mtu kwa maneno ni kupongeza kwa mafanikio na utendaji wake. Mtu anayekuwa anazungumza huchukua muda mwingi wa kudhihirisha shukrani kwa yale ambayo mtu mwingine ameyafanya, badala ya kuchukulia matendo yake kama ya kawaida.
Mifano:
Mke anampongeza mume wake kwa kutimiza lengo gumu alilokuwa akilifanyia kazi.
Mume anaona na kumshukuru mke wake kwa kile alichokifanya katika kumsaidia yeye kwenye mradi aliokuwa akiufanyia kazi.
Wanafamilia wakimpongeza mpishi aliyetengeneza mlo mzuri kwa ajili ya wao kufurahia.
Wakati unapokuwa unapongeza utendaji au mafanikio, jaribu sana kuepuka kumfanya mtu huyo afikiri kwamba upendo wako unategemea utendaji wake mtu huyo. Kwa mfano, kumwambia mwanao kwamba unajivunia yeye kwa sababu alipata matokeo mazuri kwenye mtihani kunaweza kukamfanya ajisikie kwamba utampenda kwa kiasi kidogo sana ikiwa atapata matokeo hafifu. Njia moja ya kuthibitisha thamani ya mtu ni kusema, “Nina furaha kwamba uliweza kufanya vizuri kwenye mtihani wako. Ninajivunia wewe kwa kuchukua jukumu la kujifunza na ukafanya vizuri kadri ulivyojitahidi.” Lakini hata iwe unafanyaje, usiache kupongeza mafanikio ambayo ni muhimu kwao.
Kutambua Tabia na Juhudi
Ni jambo zuri zaidi kuthibitisha tabia ya mtu na juhudi ambazo zimefanywa na yeye katika kumfanikisha badala ya kuthibitisha utendaji wake mzuri tu.
Kwa mfano: Mwanariadha mtoto anapaswa apongezwe zaidi kwa jitihada zake na tabia yake nzuri kuliko kushinda mchezo. Watu wachache ndiyo wanaoweza kufanikiwa katika utendaji, lakini mtu anaweza kuchagua kuonyesha tabia njema na tabia ndiyo muhimu zaidi.
Kumpongeza mtu kwa jinsi Alivyo
Uthibitisho ulio bora zaidi ni ule wa kutambua tabia za mtu: sifa za kibinafsi, sifa bainishi za tabia, na sifa bainishi za nafsi binafsi ya mtu. Aina hii ya uthibitisho una nguvu zaidi kuliko uthibitisho wa mafanikio kwa sababu una misingi yake kwenye thamani ya mtu mwenyewe, na siyo katika hali zinazobadilika.
Mifano:
“Watoto wanakuwa na mvuto wako! Wewe ni mzuri sana katika kuelezea mambo kwao, na una subira sana kwa maswali yao.”
“Ninakuamini, kwa sababu nimekuja kukuona kwamba wewe ni mtu mwaminifu.”
Kuhusishana kwa karibu kwenye aina hii ya uthibitisho, ni utambuzi wa jinsi Mungu anavyofanya kazi ndani ya maisha ya mtu, kwa kuwezesha kuwa na njia fulani au kufanya jambo fulani.
Mifano:
“Ninapenda kuona jinsi Mungu anavyokutumia katika maisha ya vijana unaowaongoza. Mmoja wao aliniambia kwamba anataka aishi ka ajili ya Yesu kwa sababu ya kukuangalia maisha yako!”
“Ninaamini kwamba Mungu anakwenda kukusaidia wewe katika changamoto ya hili jukumu ulilokabidhiwa. Nitakuwa nikikuombea!”
Mdhihirisho wa furaha na shukrani kwa ajili ya uwepo wa mtu na uhusiano ni baadhi ya maneno yenye nguvu ya uthibitisho, Vinaonyesha thamani ya mtu.
Mifano:
“Mikusanyiko ya kifamilia huwa ni ya kipekee zaidi wakati ukiwa pale.”
“Ninapenda kuwa na wewe.”
“Wewe ni wa thamani sana kwangu, na ninakupenda!”
Taarifa Muhimu Kuhusiana na Maneno na Uthibitisho.
1. Kamwe usilaumu au kudhihaki tabia za mtu za kimwili. Watu hubeba pamoja nao tabia za mwilini katika maisha yao yote. Kamwe usitake kumpa mtu jina la utani lenye msingi wake katika tabia zake za mwilini, haswa anapokuwa ana kasoro za kimwili.
2. Uthibitishaji wa uwezo, sifa, na tabia njema humpa motisha msikilizaji kuendelea na kukua ndani yake. Kuonyesha dosari husaidia mara chache sana.
3. Kutoa ushauri kunaweza kuwa na maana kwamba kuna kosa kwa msikilizaji. Kama unataka kutoa ushauri kwa mtu, toa uthibitisho wenye nguvu ukiambatana na huo ushauri.
4. Mapendekezo yanayotolewa kwa njia ya malalamiko hayaleti motisha. Kwa mfano, kusema kwamba kazi hiyo inapaswa kuwa imefanywa tayari, au kuonyesha aibu kutokana na kushindwa kwa mtu kuitekeleza, huwa haisaidii. Kauli hizi humfanya mtu ajisikie kama tayari ameshindwa; kama ataendelea kufanya kazi hiyo baadaye, bado atajisikia kwamba ameshindwa.
Maneno ya Kuumiza
Mtu ambaye anahitaji sana maneno ya uthibitisho huwa anakuwa ameumizwa zaidi na maneno kinzani yanayotolewa. Kukosolewa kimsingi kunaumiza sana na kunamfanya anayekosolewa kuwa na mashaka kuhusu thamani yake kama mtu. Kutokuwa na subira, na maneno ya hasira husababisha madhara ya mhemuko ambako mtu anayefanyia hayo anaweza kamwe asipone tena kabisa. Hii wakati mwingine ni kweli wakati msemaji anapokuwa haelewi maumivu yanayosababishwa na maneno yake na kamwe hataomba msamaha.
Kama na maneno yenye nguvu ya uthibitisho yanavyohusiana na thamani ya mtu, ni vivyo hivyo ilivyo mbaya zaidi, kwamba kauli zenye kuumiza ni shambulio la binafsi. Kwa mfano, “Natamani nisingekutana nawe kamwe.”
Kauli mbaya zaidi zifuatazo ni zile ambazo zinatangaza jambo fulani kuhusiana na tabia muhimu ya mtu: “Wewe ni____.” Kauli zinazoleta madhara kuhusu tabia ni pamoja na “Wewe kila wakati____” au “Wewe kamwe ____.” Kauli hizo zinadokeza kuwa mtu huyo hana uwezekano tena wa kuimarika kwa sababu ya dosari muhimu zisizoweza kubadilika.
Ikiwa mtu atakuwa amejeruhiwa – hasa ikiwa ameumizwa katika sehemu yake ya msingi ya lugha ya upendo – kwa kawaida atajaribu kujiondoa kutoka katika kuendelea kupata majeraha zaidi. Watu wanaotumia maneno yaliyo hasi kwa kawaida siyo watu wakarimu kwa maneno chanya, kwa hiyo msikilizaji anakuwa anayo matumaini madogo sana kwamba anaweza akapata tiba iliyo nzuri zaidi kwa kubadilisha tabia yake. Hatakuwa ametiwa moyo wa kuboresha tabia yake ili aweze kuvuna upendo.
Wakati mwingine watu walio wa hasira husema mambo ya kuumiza kwa sababu lengo lao ni kutaka kuumiza mtu mwingine, Nyakati nyingine, msemaji huwa anakuwa ana nia njema, lakini bado maneno yake yatakuwa ni yenye kuumiza. Watu wengine hutumia maneno hasi kutaka kumlazimisha mtu fulani awe na tabia nzuri, lakini hilo nalo kamwe haliwezi kufanya kazi.
► Mwanafunzi anapaswa asome Wakolosai 3:8 kwa ajili ya kikundi. Watu waliookoka hawapaswi kuendelea kutenda dhambi dhidi ya Mungu na dhidi ya watu wengine katika njia kama hizi.
Kwa ajili ya majadiliano ya Kikundi
► Kwa maneno yako mwenyewe, elezea kuhusu upendo wa kweli. Je, kwa nini ni lazima Roho Mtakatifu atusaidie kuwa na uwezo wa kuwapenda watu wengine kama inavyotupasa?
► Fafanua inamaanisha nini kumpenda mtu bila masharti. Kuna umuhimu gani wa upendo wa Mungu kwako usiokuwa na masharti?
► Je, kwa nini ni muhimu hasa kudhihirisha upendo kwa mwenzi wako au mtoto kwa lugha yao ya msingi ya upendo?
► Je, ni kwa jinsi gani kupokea maneno ya kuthibitisha kumekuwa na manufaa kwako?
► Je, ni kwa jinsi gani umeonyesha upendo wako kwa ajili ya wanafamilia wako kwa maneno ya uthibitisho katika wiki hii.
Maombi
Baba wa Mbinguni,
Asante kwa kunifundisha mimi kuhusu upendo wa kweli usiokuwa na masharti. Asante kwa kuuelezea katika Neno lako na kwa kuudhihirisha kupitia upendo wako kwangu.
Nisaidie nijifunze jinsi ya kupenda na kuitumikia familia yangu kama Kristo naye alivyonipenda na kunitumikia mimi. Nipe uwezo wa kuzingatia ustawi wa mwenzi wangu wa ndoa, watoto, ndugu zangu na wazazi.
Asante kwa kunikumbusha umuhimu wa maneno ninayoyasema. Ninasikitika kwa maneno ambayo nilishawahi kuyasema na ambayo yamekuwa ni ya kuumiza watu wengine na kukuvunjia wewe heshima. Naomba unisaidie katika kukumbuka kwamba maneno yangu ni lazima yawe yenye kuthibitisha, ya kujenga, na ya kuponya.
Ameni
Kazi za Kufanya
(1) Zungumza na wanandoa walio katika ndoa yenye nguvu, ukiwauliza maswali ya kujifunza kutokana na maisha yao. Utakapokuwa umemaliza mazungumzo, andika aya mbili kuhusu maarifa waliyoshiriki na chochote ambacho unataka ukitumie wewe kwenye ndoa yako mwenyewe.
Hapa kuna mawazo kuhusiana na maswali utakayouliza:
Je, kuna tofauti gani kati ya nafsi zenu binafsi ambazo zimeathiri uhusiano wenu?
Je, ni kwa jinsi gani kila mmoja wenu amekua kutokana na hizi tofauti?
Je, ni kwa jinsi gani umelazimika kurekebisha matarajio yako, mtazamo wako na tabia yako ili uweze kuheshimu na kutumika kwa kila mmoja?
Je, ni njia gani za kivitendo unazotumia kuonyesha upendo wenu kwa kila mmoja?
Je, mwenzi wako hufanya nini au kusema mambo gani ambayo yanakusaidia wewe kujua kwamba unapendwa?
Je, ni kwa jinsi gani uhusiano wako na mwenzi wako umeathiri uhusiano wako na Mungu?
(2) Katika Mithali 31:10-31 mwandishi amejumuisha maneno mengi ya uthibitisho kwa ajili ya mke wake. Maelezo ya tabia na maneno yake yanatuambia kuhusu tabia yake. Je, yeye anamthibitisha mke wake kwa mambo ya aina gani? Angalia kifungu kwa ajili ya mambo haya:
Mwonekano wake
Mafanikio yake na huduma
Tabia na juhudi yake
Yeye ni nani kama mwanadamu?
Yeye ni nani kama mwamini?
Je, tunaweza kujifunza mambo gani kutokana na yale yaliyowekewa msisitizo katika kifungu hiki?
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.