Siyo jambo la siri kwamba wanaume na wanawake wanatofautina kwa njia nyingi! Wanaume wengi hujitahidi kujieleza kuhusu mihemuko yao, wakati wanawake wengi huona kwamba kuonyesha udhihirisho wa mihemuko ni sehemu ya mawasiliano ya kweli. Wanaume hupenda kujitolea kwenye mambo yenye hatari zaidi, wakati wanawake kwa kawaida wanapenda kuhusika na mambo ya usalama. Wanaume kwa asili yao huvutiwa sana na uzuri wa maumbile ya mwanamke, wakati wanawake wengi kwa asili yao wanavutiwa na urafiki wa mihemuko. Tofauti nyingi zaidi zinaweza kuorodheshwa.
Kando na tofauti hizi zilizopo kati ya jinsia hizi, mke na mume wanazo tofauti nyingi kwenye mambo ya utu. Yawezekana mmoja akawa anafurahia kuwa na watu wengine, lakini wengine wakawa wanafurahia kukaa wapweke. Kuna mambo madogo wanayopendelea, kama vile ni kwa jinsi gani kiasi cha mwanga kiwepo kwenye nyumba au joto la chumbani liwe kiasi gani. Ndoa nyingi zinatatizwa na kutoelewana kuhusu jinsi fedha zitakavyoweza kutumika. Tofauti hizi hazimaanishi ni lazima ziwe tofauti za tabia; zinaweza tu kuwa ni tofauti za nafsi ya mtu binafsi na maoni.
Kwa kuwa ndoa inamwunganisha mwanamume na mwanamke, wakati mwingine watu hufikiri kwamba tofauti zilizopo zinapaswa zifikie mwisho. Mtu anaweza akafikiri kwamba tofauti alizo nazo mwenzi wake ni kasoro zinazopaswa kurekebishwa. Kila mwenzi atakuwa anafanya bidii au jitihada za kujaribu kubadilisha maoni, tabia na mambo ambayo mwenzake anayapendelea.
Ni kweli kwamba kila mtu anapaswa aweze kukua na au kujiendeleza kwa sababu ya uhusiano. Hata hivyo, wakati mwingine majaribio yetu ya kutaka kumbadilisha mtu yanatokea kuonekana kuwa ni shambulio la mambo binafsi ya mtu. Katika ndoa zenye nguvu/afya, kila mwenzi husitawisha nidhamu ya kumpenda, kumheshimu, kumthamini, na kumhudumia mwenzake.
► Je, kuna tofauti gani nyingine kati ya mwanamume na mwanamke? Je, kuna tofauti gani nyingine kwenye nafsi ya mtu binafsi ambazo watu wengine wanapaswa wazikubali?
Kuchagua Kutumikia
Kwenye kitabu chake, Ndoa takatifu (Sacred Marriage), Gary Thomas anasema,
Ndoa iliyo nzuri siyo kitu unachokitafuta, bali ni kitu ambacho unapaswa ukifanyie kazi. Inahitajika jitihada kubwa. Ni lazima uusulubishe ubinafsi wako. Wakati mwingine ni lazima ukabiliane, na nyakati nyingine utapaswa kukiri. Zoezi la msamaha ni muhimu. Haikataliwi kwamba ni kazi ngumu, lakini hatimaye ni kazi inayolipa. Hatimaye, inatengeneza uhusiano ulio katika uzuri, uaminifu, na kusaidiana kwa faida ya kila mmoja.[1]
Thomas anamnukuu Otto Piper:
Ikiwa ndoa…ni tukio la kukatisha tamaa kwa watu wengi, sababu inaweza ikapatikana kwenye [kutojali] kwa imani yao. Watu hawapendi kuambiwa ukweli kwamba baraka za Mungu zinaweza tu zikapatikana na zikafurahiwa wakati zinapokuwa zinatafutwa kwa kung’ang’ania (Mathayo 7:7; Luka 11:9). Kwa hiyo, ndoa kwa pamoja ni zawadi na jukumu ambalo linapaswa likamilishwe.[2]
Mara nyingi ndoa hushindwa kustawi kwa sababu tu waume na wake wanafikiria mahitaji yao wenyewe tu badala ya kujaribu kutimiza mahitaji ya kila mmoja wao.
Sisi hatuwezi kukidhi kabisa kwa ukamilifu wote mahitaji ya wengine. Baba yetu wa mbinguni peke yake ndiye mwenye uwezo kamili wa kututosheleza katika mambo tunayohitaji na matamanio yetu, na ndiyo sababu Yesu alikuja. Kusudi lake ni ili atukomboe sisi, atujaze na Roho wake - Roho Mtakatifu – na atulete kwenye uhusiano wa kina na unaotosheleza pamoja na “Abba, Father” (Warumi 8:14-15; Wagalatia 4:6).
Hata hivyo, mojawapo ya kusudi la Mungu katika ndoa ni kwamba iwe ni mahali pa kujifundishia utumishi; aina ile ya utumishi unaofanana tunaouona ndani ya Yesu (Yohana 13:14). Mungu anataka akuze ndani ya kila mume na mke moyo wa unyenyekevu wa mtumishi ambaye anawajibika kwa ajili ya watu wengine (Wafilipi 2:3-8).
Baadhi ya ndoa zilizo nzuri, na zenye furaha zipo kwa sababu mwenzi mmoja alichagua kusahau kabisa ubinafsi na kumhudumia mwenzake kupitia hali ngumu isivyo kawaida ya magonjwa, kushindwa, misiba, au mambo ya kuhuzunisha. Baadhi ya waume hutoa ushuhuda kwamba maisha yao yangewezekana yakawa yameharibika kabisa kama wake zao wangekuwa hawaombi kwa ajili yao, kuwasamehe, kuwawajibisha kwa wema, na kuwapenda bila masharti yeyote katika vipindi ambavyo vilikuwa hata havifai kupendwa kabisa. Wake wengine hushuhudia kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya uvumilivu wa waume zao ambao uliwawezesha kushinda mihemuko ya uharibifu iliyokuwa ikisababishwa na baba mnyanyasaji au kiwewe kingine. Kwa kuwa tunaishi katika dunia iliyoanguka na ya watenda dhambi, ambako viumbe vyote vinaugulia (Warumi 8:22), kila mtu aliyeko kwenye ndoa amebeba vidonda na makovu. Lakini neema ya Mungu inaweza ikatuwezesha sisi kuwa watu tunaojali na kuwatunza watu wengine na kuganga vidonda/majeraha yao!
Kila mmoja wetu alizaliwa akiwa katika hali ya ubinafsi. Kwa asili tunajali zaidi mahitaji yetu wenyewe kuliko mahitaji ya wengine, Neema ya Mungu yenye kuokoa na kutakasa inaweza ikatubadilisha sisi kupitia Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu hadi tutakapokuwa watu tunaoweza kutanguliza mahitaji ya watu wengine kwanza kuliko mahitaji yetu. Ndoa huwa zinastawi wakati kila mwana ndoa anapokuwa makini kwenye mahitaji na matamanio ya mwenzi wake.
► Je, inamaanisha nini kuchagua kutumika?
[1]Gary Thomas, Sacred Marriage, Grand Rapids: Zondervan, 2000), 133.
Mungu alipanga wanaume na wanawake wawe na mahitaji na matamanio tofauti. Hii inamaanisha kwamba mwanamume hapaswi kuhisia kwamba mwanamke atakuwa na furaha kwa mambo yanayofanana na yale yanayompatia yeye kuwa na furaha. Mwanamke hapaswi kuhisia kwamba mwanamume wake anataka atendewe kama vile na yeye anavyotaka atendewe. Ni wazi kwamba, baadhi ya njia za kupenda na kuheshimu zinapaswa ziwe sawa kwa wote, lakini bado wanaume na wanawake kila mmoja anakuwa na mahitaji fulani ya kipekee.
Kama tutaelewa mahitaji maalumu ya wanaume na wanawake, tunaweza pia tukaelewa jinsi ya kutimiza mahitaji ya mwenzi mwingine. Inasikitisha kwamba mabishano na mijadala mingi kati ya waume na wake hayatatui matatizo kwa sababu kila mtu anashindwa kuelewa mahitaji ya mwingine. Kila mmoja anaweza akawa na hasira na mwenye chuki kwa sababu mwenzake haelewi.
Watu wote wanahitaji kupendwa na kuheshimiwa, lakini kuna tofauti kati ya mwanamume na mwanamke. Hitaji la msingi la mwanamke ni upendo, na hitaji la msingi la mwanamume ni heshima.[1]
► Je, umechunguzaje kwa makini tofauti hii iliyopo kati ya mahitaji ya wanaume na wanawake?
[1]Kitabu kiitwacho Love and Respect cha Dr. Emerson Eggerich kimekuwa ni cha msaada sana katika sehemu hii.
Jinsi Mume atakavyoonyesha Upendo kwa Mke wake
Waefeso 5:25, 28 inasema kwamba, “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake… Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe….”
Mume anapaswa kumwambia mke wake mara kwa mara kwamba anampenda, hapaswi kudhania kwamba anajua kwamba anampenda. Anapaswa pia amwonyeshe upendo wake zaidi sana kuliko maneno tu.
Ni lazima aonyeshe upendo kwa njia ambazo ni muhimu kwa wake. Mume hapaswi afikirie kwamba mke wake ana hisia za kwamba anapendwa kwa sababu tu anamwonyesha upendo katika njia anazoziona kwake kwamba ni muhimu. Mahitaji ya mke wake ni tofauti na mahitaji yake.
Mke huwa anataka kujua kwamba mume wake anamlinda kimwili na kimhemuko. Mume anapaswa kushughulikia migogoro yoyote inayosababishwa na majirani. Mume anapaswa ahakikishe kwamba makazi yao ni sehemu salama ya kuishi. Atapaswa azungumze upande wake wa kumtetea anapokuwa anakosolewa na watu wengine kwa mambo yasiyostahili, hata kama ikiwa ni wanaukoo. Hapaswi kumpiga mkewe au kumdhuru kimwili kwa njia yeyote ile kama njia ya kumfanya akutii wewe. Anapaswa afanye kila linalowezekana kuhakikisha anatoa mahitaji ya familia yake. Kama mwanamume ni mzembe katika mambo ya fedha, mke wake atakuwa na hisia kwamba hajali kuhusu mahitaji ya familia yake.
Dondoo za Kifedha kwa ajili ya Waume
Matatizo ya kifedha ni mojawapo ya sababu kuu za vianzo vya migogoro ndani ya ndoa. Waume wanapaswa wafanye yafuatayo:
Kataa kufanya jambo lolote lisilokuwa la uaminifu au la kifisadi kwa ajili ya kujipatia faida; kumbuka kwamba uko chini ya mamlaka ya Mungu.
Toa fungu lako la kumi kwenye kanisa kwa sababu unamwamini Mungu pia kutoa kwa ajili yako.
Tafuta chaguo lililo bora zaidi la ajira lakini uwe tayari kufanya kazi ambayo yaweza isiwe ya kupendeza kwa sasa.
Aidha kama umeajiriwa au laa, tafuta kazi ya kufanya kila siku ili iweze kukusaidia wewe mwenyewe na watu wengine.
Usipende kutumia fedha iliyo kwa ajili ya kesho kwa kukopa fedha leo.
Unapotumia fedha kwa ajili ya jambo la furaha, wahusishe mke na watoto wako.
Weka akiba kwa ajili ya mambo ya kawaida ya kila wakati kama vile kodi kwa ajili ya nyumba uliyopangisha kuishi.
Wekeza fedha kwa ajili ya kuendeleza hali yako kuliko kutumia fedha kwa ajili ya mambo ya starehe.
(2) Mume humpenda mke wake kwa kujiwekea akiba kwa ajili yake.
Mume anapaswa kujiweka yeye mwenyewe katika hali ya usafi wa kimaadili na kujipatia furaha kutoka kwa mke wake, “Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe siku zote; Na kwa upendo wake ushangilie daima (Mithali 5:19). Kama mwanamume anakuwa na uhusiano usiofaa au wa kimaadili na wanawake wengine, au anatumia burudani chafu, mke hujisikia kwamba hapendwi.
(3) Mume humpenda mke wake kwa kujaribu kumwelewa.
Mume hawezi kufanikiwa kumwelewa mke wake kila wakati, lakini atapaswa achukue muda wa kumsikiliza na kumchunguza. Maandiko yanawaambia waume kwamba, “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili…na kama warithi pamoja wa neema ya uzima…” (1 Petro 3:7).
Ikiwa mwanamume atafanyia mzaha hisia na maoni ya mke wake, mke atajisikia kwamba hapendwi. Atamtaka mume wake ajaribu kumwelewa wasiwasi wake hata kama kauli zake hazionekani kuwa na mantiki kwake.
Kwa kuwa Mungu alimfanya mwanamume kuwa kichwa cha nyumba (Waefeso 5:23), mume ana jukumu ka kuiongoza nyumba yake (1 Timotheo 3:4-5). Hata hivyo, mume na mke wanapaswa kuwa na muda wao kwa ajili ya majadiliano hadi pale watakapokuwa wamekubaliana kwenye maamuzi mengi. Mume hapaswi kuwa mwepesi wa kuamua mambo kwa haraka bila ya kupata hisia na maoni ya mke wake.
Kama hawawezi kukubaliana kwenye jambo lolote, mume anaweza akahitajika kufanya maamuzi, lakini anapaswa ajisikie kusikitika kwa sababu wameshindwa kwa pamoja kufikia kwenye kukubaliana. Kwa kawaida kukosekana kwa umoja ni onyo kwa mume. Wanawake mara nyingi wana hekima na utambuzi ambao wanaume wanahitaji katika kufanya maamuzi mazuri.
► Mwanafunzi anapaswa asome Waefeso 4:2-3, 15-16 kwa ajili ya kikundi. Je, ni kwa jinsi Aya hizi zinatumika kwenye uhusiano kati ya mume na mke?
Wake walio wengi huhisi kwamba waume zao hawathamini kazi wanazozifanya. Mume anapaswa aonyeshe kuwa na shukrani kwa mke wake, Anapaswa atambue juhudi ambazo mke wake anazifanya kwa ajili ya familia yake. Kamwe hapaswi kumkosoa hadharani au mbele ya watu wengine.[3] Anapaswa asifie tabia yake, uzuri wake, na uwezo wake. Kwa kadri ile atakayojaliwa, mume anapaswa amsaidie aweze kuvaa vizuri. Mke hajisikii kupendwa wakati anapojiona kwamba mume wake hamjali kuhusiana na mwonekano wake.
Mume anapomkosoa mke wake anaweza akasababisha mke wake akafikiri kwamba yeye hafai kama mtu na akamkatisha tamaa. Paulo anawaambia waumini, “Wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote (Tito 3:2).
Ikiwa ukosoaji uwe ni wa lazima, mume ni lazima awe mwangalifu sana kuthibitisha kwamba uthamini wake kwa mke wake ni mkubwa zaidi kuliko ukosoaji wake. Anapaswa kuepuka kutaja mifano ya wanawake ambao anawajua ni bora kuliko mke wake katika sifa nyingi za tabia.
(5) Mume anampenda mke wake kwa kutenga muda wake kwa ajili ya uhusiano.
Ili kushiriki maisha pamoja kunahitaji kuwepo na muda wa mazungumzo. Mahusiano huimarishwa kwa maneno (Mithali 16:24, Mithali 20:5). Wanandoa wanapaswa wazungumzie juu ya mambo ambayo yamesheheni kwenye siku zao. Wanapaswa wazungumzie kuhusu urafiki wao, hisia zao, matamanio yao, na mambo ambayo wanapaswa wahusike/wawajibike nayo. Mke hujisikia kupendwa wakati mume wake anapopata muda wa kuzungumza naye na kumsikiliza. Mume anapokuwa amerejea nyumbani kutoka kazini anaweza akajisikia kuchoka na hajisikii kuongea au kusikia kuhusu matatizo ya nyumbani, lakini mume hapaswi kudharau kusikiliza. Kama mume anataka urafiki wa kimwili lakini hawezi kumfikisha kwenye urafiki wa mhemuko, mke anajisikia kama anayetumiwa tu lakini hapendwi.
(6) Mume anampenda mke wake kwa kumvumilia katika madhaifu yake.
1 Petro 3:7 inafundisha, “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu….” Wanawake wengi hawana nguvu za mwili walizo nazo wanaume wengi. Kadhalika, wanawake wengi ni wahanga wa mihemuko ya maumivu na kuhuzunishwa kuliko wanaume. Mwanamume anapaswa kumfariji na kumtia moyo mke wake. Anatakiwa ajifunze jinsi ya kumwondolea msongo wa mawazo. Anapaswa kujiepusha na kudai kujamiiana wakati akiwa amechoka, akiwa kwenye msongo wa mawazo au kwenye hofu.
(7) Mume anampenda mke wake kwa kumpatia mahitaji yake.
Kama vile ambavyo mwanamume anavyotaka awe na zana bora zaidi za kazi yake na mahali pazuri pa kufanyia kazi yake, anapaswa pia aandae mazingira mazuri kwa ajili ya mke wake. Atapaswa kuhakikisha kwamba nyumbani kumekarabatiwa vyema na kujazwa vitu ambavyo anavihitaji.
Matokeo wakati Waume wanapokuwa Wanawapenda Wake zao.
Waume wengi huja kuona kwamba wanapokuwa wameonyesha upendo kwa wake zao, wake zao huitikia kwa furaha na ushirikiano. Wanawake hujisikia furaha wakati waume zao wanapowajibika kwa ajili yao na kuwaonyesha upendo kwa jinsi orodha inavyoonekana. Wanaume hupata mambo mengi kutoka kwenye ndoa zao wanapokuwa wameonyesha upendo kwa wake zao (Waefeso 5:28).
Hata hivyo, wanaume huwa hawana uhakika wa matokeo. Mwanamume hatakiwi kuonyesha upendo kwa kusudi tu la kupata kitu anachokitaka. Anapaswa aonyeshe upendo ili aweze kumpendeza Mungu na atimize mahitaji ya mke wake kuliko kuhangaika na mahitaji yake mwenyewe.
Baadhi ya wanawake wameathirika kimhemuko kama matokeo ya mambo ya nyuma yaliyopita, na wanaweza wasiwe na mwitikio wa haraka wa upendo wa waume zao. Mazoea haya ya kuonyesha upendo siyo mbinu za kujaribu kwa siku chache kama majaribio. Mume anapaswa kuendelea kuonyesha upendo bila kukoma kupitia njia hizi kwa sababu ya upendo alio nao ndani ya moyo wake kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya mke wake. Kristo analipenda Kanisa kwa aina hii ya uaminifu na kwa kujitolea kama dhabihu binafsi.
[1]Kuna maandiko mengi ambayo yanahusiana na ukweli huu ikiwa ni pamoja na Waefeso 5:28-31, Wakolosai 3:19 (ulinzi wa mihemuko), 1 Timotheo 5:8 (utoaji wa kimwili), Nehemia 4:13-14 (ulinzi wa kimwili), na 1 Timotheo 2:14 (ulinzi wa kiroho).
[3]Katika muktadha wa ndoa, hii ni matumizi ya maagizo ya Mungu kwetu katika Waefeso 4:29-32; 5:25-29 na Mathayo 7:12.
Jinsi Mke Anavyoonyesha Heshima kwa Mume Wake
Waefeso 5:33 inaagizwa, “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.”
Mwanamume anahitaji heshima. Wanaume wengi wako radhi kupewa heshima na watu wengine kuliko kupendwa nao. Mungu aliwaumba wanaume ili kulinda, kuwa msaada, na kuongoza familia zao. Nafasi ya baba na mume inahitaji kuheshimiwa hata kabla hajafanya jambo lolote la kuweza kumletea heshima. Mke anapaswa aonyeshe heshima kwa mume wake hata kama matendo yake ni mabaya. Anampasa amtendee kama mtu, aliyeumbwa kwa sura ya Mungu, ambaye ni muhimu sana hata pale ambapo hatumii mamlaka yake kwa usahihi (Waefeso 5:23). Hii haimaanishi kwamba hawezi kumweleza kwamba hakubaliani na matendo au maamuzi yake mabaya, lakini hapaswi kumtendea hivyo kwa kumkosea heshima.
Wakati mke anapomheshimu mume wake kwa kujitiisha kwa uhuru chini ya mamlaka yake, anaonyesha upendo wake kwa ajili ya Yesu (Waefeso 5:22, 31-33). Baadhi ya wake hufikiri kwamba wanawapenda waume zao hata wakati ambapo wanakuwa wakishindwa kuwaheshimu – wakiwalaumu kwa mabaya huko nje kwa watu wengine, wakiendesha mambo ya siri, na wakitumia maneno yenye kuumiza. Wanapaswa waelewe kwamba hakuna kiwango chochote cha upendo kinachoweza kuwa ni fidia kwa ukosefu wa heshima.
Wanawake wengi wana mwelekeo wenye nguvu wa kuwa mama wa mtoto mchanga. Wana uwezo wa asili na matamanio ya asili ya kujali mahitaji ya watoto wachanga, Jaribu kufikiria jinsi mwanamke atakavyokuwa anajisikia ikitokea mtu kusema, “Huna uwezo wa kumtunza mtoto mchanga.” Vivyo hivyo, wanaume nao wana mwelekeo wenye nguvu wa kulinda, kulisha, na kuongoza. Wakati mke wa mtu anapomweleza kwamba hana uwezo wa kufanya mambo hayo, mume hujihisi kwamba atakuwa ni mwanamume aliyeshindwa.
Mke anapaswa aelewe kwamba kutakuwepo na wanaume wengine ambao wana haiba yenye nguvu, wanaopata fedha nyingi, au wanaoshikilia nyadhifa mbalimbali za juu kuliko mume wake. Hapaswi amfanye mume wake kama mtu aliyeshindwa kwa kumlinganisha na wengine. Kama tunavyojifunza kutoka katika kitabu cha Waefeso 5:21-33, mke ni mtu mmoja pamoja na mumewe. Inapotokea mke akamshutumu mume wake au akamlinganisha na wengine, kwa pamoja anajisambaratisha yeye na mwenzake kwa pamoja na kuharibu uhusiano wao.
► Mwanafunzi anapaswa asome Mithali 31:11-12, 26 kwa ajili ya kikundi. Je, Aya hizi zinatufundisha nini kuhusu jinsi ambavyo mke mcha Mungu anavyomtendea mume wake kwa tabia na maneno?
(1) Mke humheshimu mumewe kwa maneno ya uthibitisho.
Mke anapaswa awe na uthibitisho wa uwezo wa mumewe. Heshima itaonekana kuwa dhahiri katika maneno ya uthibitisho ambayo mke huzungumza na mumewe. Maneno yana mguso mkubwa kwa wanaume wengi. Aidha yatajenga au yatabomoa (Mithali 14:1). Aidha yana uwezo wa kutia moyo au kudhoofisha. Aidha yataimarisha matumaini yake na kujiamini kwake au yatasambaratisha moyo wake kabisa (Mithali 18:21). Mwanamume hawezi akawa na mafanikio kwenye kila biashara au akawa na uwezo wa kushikilia nyadhifa mbalimbali, lakini mke wake anapaswa athibitishe jitihada zake za kuutengeneza mji wake na utoaji wa ulinzi kwa familia yake. Hapaswi kwa namna yeyote ile kujaribu kumvunja moyo mumewe kwa maneno yake anapokuwa na mawazo ya kutenda jambo fulani au anapokuwa anakabiliana na changamoto mpya.
► Wanafunzi wanapaswa wasome Mithali 15:4 na Mithali 16:24 kwa ajili ya kikundi.
(2) Mke humheshimu mume wake kupitia kujisalimisha kwake (1 Petro 3:5).
Kujisalimisha kwa mke hakumaanishi kwamba yeye ni mtu wa chini sana kuliko mumewe (kwa cheo, uwezo n.k.) Badala yake ni kumaanisha kwamba majukumu yao ni tofauti. Hata katika Utatu Mtakatifu wa Mungu tunaona kwamba Mwana ananyenyekea kwa Baba ingawa Mwana siyo wa chini sana kuliko Baba kwa asili au nguvu au sifa yake yeyote.
Kwa baadhi ya wake kanuni hii siyo rahisi kwao, hasa ikiwa waume zao hawaishi kufuatana na Neno la Mungu, au kama hawana upendo kwao. Baadhi ya wanawake wanajihisi kwamba wana uwezo wa kufanya maamuzi yaliyo bora zaidi kwa ajili yao wenyewe, au kwa familia zao kuliko ambavyo waume zao wangeweza kufanya. Wakati mwingine mwanamke anakuwa yuko sahihi katika jambo hili, na mwanamume katika makosa. Hata hivyo, endapo mke atanyenyekea kwa mumewe pale tu anapokuwa anakubaliana na yeye, anapoka mamlaka ya mumewe na haina maana kwamba anajinyenyekesha au anajisalimisha kwa ukweli. Kujisalimisha maana yake ni kuruhusu mwingine aweze kufanya maamuzi.
Petro anawaambia wanawake walioolewa ifuatavyo:
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. (1 Petro 3:1, 3-4).
Kuna hali mbalimbali zenye matatizo. Wake wengi huuliza maswali. “Je, kama ataniambia nifanye jambo hili_______ kuna ulazima wa mimi kulifanya?” Somo hili haliwezi kuzungumzia kwa mapana hali mbalimbali kubwa za matatizo zilizopo. Hata hivyo, tatizo la kutokujisalimisha kwa mke haliko kwa sababu ya mume kutaka mambo fulani ambayo mke hapaswi kuyafanya. Mke anaweza asitake kujisalimisha/kuwa mtiifu kwa mume wake kwa sababu anafikiri kwamba mume wake atakuwa mtu wa kutofikiri endapo atafanya hivyo. Inawezekana mume hana upendo wala fadhila. Mke hatapenda kusalimisha uhuru wake wa kufanya maamuzi yake mwenyewe. Mke anaweza akawa ana tabia ya ukaidi. Mke hutumia mifano ya matendo au makosa yasiyokuwa na fadhila ya mume wake kama kisingizio cha kukataa mamlaka yake kwa ujumla. Hali hii ni ya kutotaka kutii maagizo ya Neno la Mungu.
Biblia inatuambia kwamba mke mcha Mungu na mtiifu anaweza kumvuta mume wake kwa Bwana. Hatuna uhakikisho kwamba mume anaweza kuokoka kwa sababu ya mke mwema, lakini upo uwezekano mdogo sana wa mume kuweza kuokoka endapo mke wake aliye Mkristo ni mkaidi. Mke anaweza kupata wingi wa kukubalika kwa mume wake kwa kuwa mwenye heshima, lakini hiyo siyo sababu ya msingi ya kufanya hivyo. Anapaswa amheshimu mume wake kwa kuwa anawiwa amheshimu na kwa sababu anataka kumpendeza Mungu.
Mithali 12:4 inasema, “Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.” Ikiwa mke anamtendea mume wake pasipokuwepo na heshima mbele ya marafiki zake, anaiondoa heshima aliyo nayo mumewe ambayo kamwe hatakaa aweze kuirejesha tena. Wanaume huvutiwa na wanaume wengine ambao wako na wanawake wao waliojisalimisha kwao kwa unyenyekevu na utiifu. Wanaume huwahurumia wanaume wenzao ambao wana wake wasiokuwa na heshima.
(3) Mke humheshimu mume wake kwa kuwa makini na mahitaji yake (Mithali 31:15, 21, 25, 27).
Wakati mke anapojifunza kwa undani mambo ya pekee kuhusu jinsi ya kuandaa chakula na kuitunza nyumba yake kwa njia ambayo inamfurahisha mume wake, mume hujisikia kuheshimika. Ikiwa mke atakataa kubadilisha tabia zake kwa ajili yake, mume hujisikia kwamba yeye sio muhimu kwa mke wake.
Ikiwa mke atakuwa anawajibika na shughuli nyingi za kazi au marafiki au kanisa au mambo ya burudani na hana muda wa kutosha kumsikiliza na au kuzungumza na mumewe au kushughulikia mahitaji yake kama inavyostahili, mume hujisikia kwamba yeye sio muhimu kwa mke wake.
Mwanzo 2:18 inafundisha, “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.’”
(4) Mke humheshimu mume wake kwa kumridhisha kimapenzi.
Kuridhika kutokana na tendo la kujamiiana kunaonekana kuwa ni muhimu zaidi kwa wanaume kuliko ilivyo kwa baadhi ya wanawake. Mwanamke anaweza asijisikie kujihusisha na tendo la kujamiiana mara nyingi labda iwe hisia zaka na matamanio yake vimeelekezwa kwake, ambayo ni mara chache kuliko ambavyo mwanamume atakuwa amehitaji. Hii inamaanisha kwamba mara nyingi mwanamume anaweza kuwa haridhiki wakati mke wake anapokuwa haelewi au hashughuliki na hitaji lake. Mke anaweza hata kudharau matamanio ya mume wake ya kutaka kujamiiana naye kwa sababu tu ya unyanyasi alioupitia au kuuona wakati wa nyuma uliopita. Mume anapaswa ajaribu kuwa mvumilivu na kumwelewa mke wake. Lakini mke anapaswa aelewe kwamba ni vyema kwake wakati wote atimize hitaji la mumewe la kujamiiana hata katika nyakati ambazo yeye mwenyewe hajisikii kuwa na uhitaji huo. Kama mwanamume ni mwaminifu na anayewajibika kikamilifu kwa ajili ya mke wake, na hana mahusiano mengine mabaya na wanawake wengine, anaweza kujisikia kukasirishwa sana wakati mke wake anapokuwa hajali kuhusu hitaji lake. Uaminifu wa mume kwenye ahadi ya ndoa yake kamwe hakuhitajiki kutegemea kuridhika kwake kimwili, lakini umakini wa mke wake kwenye mahitaji yake ya kujamiiana kunaweza kupunguza mapambano yake dhidi ya majaribu.
Wimbo wa Sulemani unasema: “Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake… Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani, Tufanye maskani katika vijiji… Huko nitakupa pambaja zangu. (Wimbo wa Suleman i2:16; Wimbo wa Sulemani 7:11-12, mkazo umeongezwa; ona pia 1 Wakorintho 7:3-5).
Matokeo ya Kutotii kwa mujibu wa Maagizo ya Mungu
Maelezo yaliyoko kwenye aya hizi hayatumiki kwenye kila mgogoro ulioko kwenye ndoa lakini ni ya kawaida yaliyozoeleka. Maelezo haya yanaonyesha mizunguko ya asili ya tabia – na -athari – ambayo inatokea wakati wanandoa wanapojibu hisia zao pasipo kiroho, badala ya: (1) Kutambua ni nini wanachokihisi, (2) Kukumbuka ukweli wa Mungu na kile anachotaka kwa ajili yao, na (3) Kumtegemea Roho Mtakatifu awasaidie kujibu kwa njia za Kibiblia.
Ikiwa mke hatembei katika Roho na haruhusu upendo wa Mungu ufanye kazi kupitia kwake anaweza kuwa na mwitikio wa asilia tu am bao unaweza kuleta athari kubwa kwenye ndoa yake. Kama mke hatajisikia kwamba anapendwa, hajisikii kuwa salama. Ataanza yeye mwenyewe kujidai na kutaka kuzuia mamlaka ya mumewe kwa sababu hamwamini katika kumjali yeye. Wakati mke anapokuwa akifanya haya, mume anajihisi kama asiyepewa heshima. Akijaribu kutetea mamlaka yake kwa dhati na kudai heshima, mke hujisikia na hata zaidi kwamba mume hana upendo kwake.
Ikiwa mwanamume hatembei katika Roho ili kuruhusu upendo wa Mungu ufanye kazi kupitia yake, anaweza akashindwa kuwa na tabia ambayo itaimarisha ndoa yake. Wakati mwanamume anapojihisi na kujiona kwamba anavunjiwa heshima yake, hujisikia kuumizwa na kuwa na hasira. Anaweza akasema mambo ya kuumiza kwa mke wake. Kama atakuwa anajaribu kudhibiti hisia zake, anaweza akaamua kunyamaza kimya. Hatapenda kuwa karibu na mke wake au kufungua moyo wake kwake, kwa sababu anahisi kwamba yeye siyo wa kushirikiana naye. Anapokuwa akifanya hayo, mke wake anakuwa haelewi ni kwa nini. Labda alimtendea pasipokuwa na heshima kwa kuwa alikuwa anajaribu kumfanya atambue kwamba hakuwa na furaha na kwamba inampasa kubadilika. Anapokuwa na hasira na kujiondoa kwake, mke anafikiri kwamba mume anadhihirisha kwamba hana cha kujali tena katika hisia zake. Anaweza akajisikia hata na zaidi kwamba anavunjiwa heshima.
Mtu huwa katika hatari zaidi ya kuingia kwenye majaribu wakati uhusiano wa ndoa umeporomoka. Mke hushawishika kuwa mpinzani zaidi kwa uongozi wa mume wake. Anadiriki hata kumzungumza kuhusu habari za mumewe kwa watu wengine wasiohusika kwa kumvunjia heshima. Anaweza akaingia kwenye jaribu la kuwa kwenye uangalifu wa mwanamume mwingine wa nje anayeonekana kumthamini zaidi. Mwanamume anashawishika kukaa mbali na mke wake kwa sababu ya kukerwa na tabia yake. Anaweza akashawishika kufurahia kuwa kwenye uangalifu wa mwanamke mwingine anayemthamini mbali na mkewe.
Kila mtu anawajibika kwa Mungu kwa ajili ya uchaguzi. Mungu hawezi akasemehe dhambi ya mtu kwa sababu ya kile ambacho kimefanywa na mwenzi wake. Mungu anaahidi kututia nguvu ya kutusaidia kuishi kama inavyotupasa. Kusudi la taarifa hii siyo kwa ajili ya mtu kudai ni kitu gani kinachohitajika kutoka kwa mwenzi wake au kumlaumu mwenzi kwa kosa la mtu mwingine. Kusudi ni ili mtu aweze kutambua kwamba anao wajibu wa kumpendeza Mungu na kumpa mwenzi wake mahitaji yake anayohitaji.
Malengo Mabaya
Wakati mwingine mtu hutafuta njia ya kuyafanya maisha yake yawe marahisi. Mume anataka kurahisisha maisha yake kwa kutaka mke wake abadilike. Vivyo hivyo, mke naye anaweza akafikiri kwamba maisha yake yatakuwa bora zaidi kama mume wake atabadilika. Mtu anamuuliza mshauri, au mchungaji au marafiki jinsi ya kuweza kumbadilisha mtu mwingine. Kumbadilisha mwenzi wa mtu mwingine siyo lengo lililo sahihi. Mtu ambaye anajaribu kuyafanya maisha yake yawe marahisi kwa kutumia mbinu za mahusiano hazichochewi na upendo kwa ajili ya Mungu au mtu mwingine.
Wakati mwingine mtu hujaribu kwa miaka kusahihisha makosa ya mtu mwingine. Hawaachi kukosoa makosa yanayofanana. Ingawaje kila mmoja anakuwa ana makosa ya ukweli, kila mwanandoa hatimaye ni lazima amkubali mwenza wake kwa makosa yake. Makosa yanaweza yakawa kasoro za mwonekano, kasoro za tabia, au kasoro za kiroho (Zikiwemo hata dhambi). Uhusiano haupaswi utegemee nia ya mtu mwingine ili ubadilike. Anaweza akajihisi kwamba hawezi kubadilika. Iwe ni kwa sababu yeyote ile kwamba habadiliki, kila mwenza anapaswa kuonyesha upendo na heshima, kila mmoja akimthamini mwingine hata katika makosa yake.
Hitimisho
Mungu aliitengeneza asili za wanaume na wanawake, na aliitengeneza ndoa kukidhi mahitaji ya mwanadamu. Hata hivyo, tunaishi katika ulimwengu wa ambamo ndoa na familia zimeharibiwa kwa kiasi kikubwa sana na dhambi. Kila mmoja wetu kwa nafsi yake ameharibiwa na dhambi zetu sisi wenyewe na dhambi za watu wengine ambazo zimetuathiri. Hatuwezi tukazizoea ndoa kama Mungu alivyokuwa amekusudia bila ya neema ambayo inatubadilisha sisi na inatusaidia sisi kuonyesha neema hiyo kwa watu wengine. Tunahitajika tuwe na Roho wa Mungu wa kututakasa ili tuwe na malengo yaliyo masafi, upendo wenye nguvu, na unyenyekevu ambao unahudumia.
Kwa ajili ya Majadiliano ya Kikundi
► Je, kuna maudhui gani kwenye somo hili ambayo ni mapya kwako? Je, ni kwa jinsi gani umepanga kubadilisha misimamo yako na tabia zako?
► Je, ni jambo gani ambalo kanisa linaweza kufanya ili liweze kuimarisha ndoa?
Maombi
Baba wa Mbinguni,
Asante kwa kutengeneza uhusiano wa ndoa ili kukidhi mahitaji mengi sana maalumu. Asante kwa kutupa sisi maelekezo yako kwa ajili ya ndoa.
Tusaidie tuwe na upendo na uelewa wa kujali kama inavyopaswa tuwe. Tusaidie tuwe na familia ambazo zinadhihirisha upendo wako kwa dunia.
Asante kwa ajili ya neema yako ambayo sisi inatusaidia sisi kuwa na upendo kama vile na wewe unavyofanya.
Ameni
Kazi za Kufanya
(1) Fanya kukariri 1 Wakorintho 13:4-8. Mwanzoni mwa kuanza kwa kipindi cha darasa kinachofuata, andika au rudia kusema yale uliyokariri kutoka kichwani.
(2) Andika maneno yasiyopungua kurasa mbili ukielezea mahitaji ya mume na mke. Toa mfano wa tabia ya mwanandoa ambayo inasaidia katika kukidhi mahitaji hayo. Tumia Maandiko katika kusaidia kila moja ya mahitaji unayojadili.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.