Christopher alikulia kwenye familia moja ya Kiasia-Kimarekani nchini Marekani. Tangu wakati alipokuwa bado kijana mpevu alikuwa anavutiwa zaidi na wanaume kuliko wanawake. Wazazi wake walishtuka na kuona aibu kutokana na shauku ya kijana wao. Akiwa kijana mdogo alikuwa kwenye mfululizo wa mahusiano na wanaume. Alikuwa anategemea kupata upendo wa kweli na uwajibikaji, lakini kila uhusiano hatimaye ulishindwa. Kwa uzembe alianza kuwa na mahusiano yasiyo ya maadili na wanaume wengi. Alianza kuwa na mahusiano mabovu na wanaume wengi. Kila kitu kilianza kubadilika kwa Christopher wakati mama yake alipookoka na kumpa upendo na kukubalika ambapo alikuwa hajawahi kupata hapo nyuma. Alianza kutambua kwamba utambulisho wake wa msingi ni wa mtu aliye kwenye sura ya Mungu. Alitubu na kuwasilisha vipengele vyake vyote vya maisha yake kwa Mungu. Alipata ukamilifu na kusudio lake kwenye uhusiano wake na Mungu.
Asili ya Kibinadamu Iliyoanguka na Matamanio ya Dhambi
Wakati Mungu alipomuumba Adamu na Hawa, aliwafanya watu walio wakamilifu katika maeneo yote, bila ya kasoro au mapungufu (Mwanzo 1:31). Asili zao zilitamani kile ambacho kilikuwa ni sahihi na kizuri. Fahamu zao na akili zao vyote vilifanya kazi kwa usahihi. Kisha Adamu akaamua kutokutii maagizo ya Mungu. Alipofanya hivyo, asili yake ya mwanadamu iliharibika (Warumi 8:20-23). Miili na akili za kibinadamu zilidhurika. Hata mtu mwenye afya njema sana na akili nyingi hudhuriwa na matokeo ya dhambi. Dhambi iliharibu kabisa kile ambacho kilikuwa kikamilifu hadi hapo Kristo atakaporudi (1 Wakorintho 15).
Kwa uharibifu ambao umeshafanyika kwenye asili yetu ya ubinadamu na miili yetu ya asili, tusitegemee kwamba matamanio yetu ya asili ya miili yetu siku zote yatakuwa sahihi. Ukweli ni kwamba tamaa zetu nyingi haziko sawa. Kwa kawaida watu hutamani yale mambo yaliyo mabaya. Yesu aliiona hali hiyo ya asili ya dhambi ya ubinadamu wakati alipoorodhesha aina zote za dhambi zinazotoka moyoni (Marko 7:21-22).
Katika somo hili tunazungumzia kuhusu masuala ya kujamiana. Kati ya matamanio yote ya binadamu, matamanio ya ngono yanaweza yakawa ndiyo yenye nguvu sana kuliko mengine yote.
Matamanio mabaya ya ngono huonekana ni jambo la kawaida kwa yule mtu anayejisikia. Anaweza akafikiri kwamba hapaswi kulaumiwa kwa ajili ya kuwa kwenye matamanio yake. Hata hivyo, kila mtu anapaswa ajizuie na mwelekeo wake wa asili kwa ajili ya kuweza kufanya yaliyo sahihi. Mtu anaweza kuwa na mwelekeo wa asili wa kusema uongo au kuiba, au kuwa mwenye vurugu, mvivu, au asiyekuwa na subira. Watu hawapaswi kuwajibika kwa wao kuzaliwa katika hali hiyo ya ukasoro, lakini watu wanakuwa ni wenye hatia wakati wanapoingia kwenye matamanio ya asili na kutenda dhambi.
Wakati mwingine unyanyasaji wa utotoni au hali zingine za kimazingira husababisha mtu apambane na misukumo ya ushoga au tamaa zingine mbaya za ngono. Hata hivyo, tamaa mbaya za ngono hazipaswi zionekane ni tofauti na matamanio mengine yanayosababisha mtu kutenda dhambi. Mtu anahitaji neema inayofanana kwa ajili ya ukombozi na utakaso kutoka kwa Mungu, kwa sababu zozote zile ambazo zilihusika.
Ukweli kwamba matamanio mabaya kwa watu wengine hujisikia ni jambo la kawaida hapaswi kuwa ni jambo la kushangaza. Dhambi kwa ujumla huonekana ni ya kawaida na ya asili kwa yule mtu ambaye ana uzoefu wa tamaa kwa ajili ya kutenda dhambi.
Sisi kwa asili ni watoto wa tabia ya hasira (Waefeso 2:3). Hii inamaanisha kwamba kwa asili sisi ni watu wa mwelekeo wa kutenda dhambi, na tunajileta wenyewe kwenye hukumu kwa kutenda dhambi ambazo ni za asili kwetu. Ukweli kwamba mtu amezaliwa akiwa na mwelekeo fulani wa dhambi haimaanishi kwamba inapaswa ifuatwe, hata kama itaonekana kwamba ni jambo la kawaida kwake.
► Kwa nini hatupaswi kutii tamaa zetu zote za asili?
Biblia inatupa maelezo kwamba sisi tumeitwa ili tufananishwe na mfano wa Kristo (Warumi 8:29). Tunapaswa tumvae Bwana wetu Yesu Kristo. Matamanio yetu ya kimwili hayapaswi yawe ndiyo msingi wa maisha, badala yake tunapaswa tuipeleke misukumo isiyokuwa sahihi kwenye mamlaka ya Mungu (Warumi 13:14).
► Je, inaonekanaje kupeleka misukumo yetu isiyokuwa sahihi kwenye mamlaka ya Mungu?
Matamanio yako ya ngono yanapaswa yapelekwe kwenye kusudio lako kuu, yaani, kumtukuza Mungu kwa kuonyesha sura ya Mungu. Maisha ya kumfuata Kristo ni maisha ambayo yanaendana na sura ya Mungu uliyo nayo.
Utambulisho wa Mwanadamu
Uelewa ulio sahihi wa Utambulisho wa Mwanadamu
Watu wengine huamini kimakosa kwamba asili yao ya kibinadamu inaweza ikaaminika katika kuwapeleka kwenye njia sahihi. Inaonekana kwao kuwa ni jambo lenye mantiki kwamba matamanio ambayo yanatoka kwenye asili yao wenyewe yanapaswa yawaongoze kwenye utoshelevu. Hawatambui kwamba asili yao haiwezi ikaaminika kwa sababu imeharibiwa na dhambi. Matamanio ya mtu binafsi hayatamwongoza kwenye utoshelevu kwa sababu matamanio yake hayo yamevurugwa. Wala matamanio ya asili ya mtu, mbali na Mungu, hayawezi kumwongoza kufanya mambo ambayo kimaadili ni sahihi.
Watu wanaamini kwamba wanapaswa kufuata matamanio na mihemuko yao wenyewe katika kutengeneza kusudi lao wenyewe kwa ajili ya maisha. Wanaamini ni muhimu kabisa kuwa na utambulisho binafsi ambao haujafafanuliwa au kuwekewa mipaka na mamlaka yeyote ile au matakwa ya kimaadili. Wanafikiri kwamba watu binafsi wanapaswa kuamua ni mambo gani yanayowafaa na yenye thamani kwa ajili yao wenyewe. Huwa hawataki taasisi au masharti ambayo yanaweka ukomo wa tabia zao. Asili potofu ya mwanadamu inafanyika kuwa ndiyo kipimo cha maadili badala ya Neno la Mungu.
Kwa kuwa kujamiiana ndiyo sehemu yenye nguvu sana ya asili ya mwanadamu, watu wengi huchukulia matamanio ya ngono kuwa ndiyo kiini cha utambulisho wao. Wanafikiri kwamba ni lazima wafuate matamanio yao ya ngono ili wajione kwamba wao ndiyo wenyewe. Watu hufikiri kwamba kujamiiana siyo kile tu wanachotaka au kufanya, bali kwamba wao ni nani. Wanafanya hivyo kuwa ndiyo utambulisho wao.
Tofauti na jinsi ulimwengu unavyofikiri, Biblia inatueleza kwamba sisi tumeumbwa katika sura ya Mungu, na tumeundwa kwa kusudi la kuwa na uhusiano na Mungu. Huu ndiyo utambulisho wetu wa kweli kama wanadamu.
Hakuna kitu chochote katika uwepo wetu duniani ambacho kinaweza kutupa ukomo wa utambulisho wetu wa kweli. Sifa za kuwepo kwetu duniani kwa kawaida ndizo hali tulizo nazo hapa duniani kwa sasa. Hazitufanyi tuwe sisi ni nani. Ukabila wetu, hadhi ya kijamii, au hadhi ya kiuchumi siyo utambulisho wetu, bali ndiyo hali yetu. Mtu anaweza akawa daktari, nyota wa kuonyesha burudani, au kiongozi wa kitaifa, lakini mtu huyo anasimama mbele za Mungu kama kiumbe wa Mungu aliyeumbwa katika sura ya Mungu, na kwamba utambulisho huo ndio ulio muhimu na wa maana zaidi.
Ujinsia wetu ni sehemu yenye nguvu sana ya hali yetu. Tunayo mielekeo ya ngono, matamanio, na mambo ya kukatisha tamaa. Lakini mambo hayo yote siyo utambulisho wetu; ni sehemu tu ya hali zetu.
Tumezaliwa na asili ya dhambi kwa sababu dhambi ya Adamu ilimtenganisha mwanadamu na Mungu (Warumi 5:18). Lakini hata utendaji wetu wa dhambi siyo utambulisho wetu; ni hali yetu, na inaweza ikabadilishwa kwa neema na nguvu za Mungu (Warumi 5:19).
► Kuna tofauti gani kati ya utambulisho wa mtu na hali ya mtu?
Utambulisho wa Binadamu na Maadili Binafsi
Utambulisho ni muhimu kwa sababu mtu huweka maadili yake juu ya utambulisho wake. Maadili ni kanuni ambayo inatambulisha tabia kama ni njema au na mbaya. Kama mtu atakuwa anafikiri kwamba ujinsia wake ndiyo utambulisho wake, basi ataamini kuwa ni sawa kufuata mielekeo yake ya kijinsia.
Wakati mwingine mtu husema, “Nilizaliwa hivi; ni jambo la kawaida kwa mimi kufanya hivi, siyo vibaya kwangu.” Lakini Biblia inafundisha kwamba wote kabisa tulizaliwa katika hali ya dhambi (Warumi 5:12, Waefeso 2:3). Siyo jambo sahihi kwetu sisi kufuata asili yetu ya dhambi kwa sababu tu inaonekana kwamba ni asili yetu.
Asili yetu ya dhambi si utambulisho wetu. Asili yetu ya dhambi si sisi ni nani. Asili yetu ya dhambi ni hali yetu. Ujinsia wetu siyo utambulisho wetu. Badala yake, watu walioumbwa katika sura ya Mungu ndiyo utambulisho wetu. Kama tutaukiri ukweli huu, tutatambua kwamba Mungu huamua ni jambo gani lililo jema na lililo mbaya, na kwamba sisi tunawajibika kwake. Utambulisho wetu unatusaidia sisi kuelewa kiwango kilicho sahihi cha tabia takatifu.
► Je, ni kwa jinsi gani uelewa wa mtu kuhusiana na utambulisho wake unavyogusa maadili yake?
Uelewa Sahihi wa Jinsi
Sisi tunafahamu ukweli kwamba wanadamu na wanyama wengi wametenganishwa kwenye dume na jike. Tunaweza tukahisia kwamba Mungu ni mwanamume au mwanamke, lakini hilo litakuwa ni makosa. Mungu ni kiumbe ambaye yuko kwenye asili iliyo kubwa kuliko jinsi, ambaye alikuwa yupo kabla ya jinsi kuwepo. Jinsi zote mbili za wanadamu zilitokana na sura ya Mungu (Mwanzo 1:27). Jinsi zote mbili za wanadamu ni udhihirisho wa sura ya Mungu.
Sura ya Mungu siyo tu kitu ambacho kimejumuishwa kama sehemu ya asili ya mwanadamu. Sura ya Mungu siyo tu silika fulani tulizopewa sisi kama vile uwezo wa kupenda, kuthamini uzuri, na uelewa wa mema na mabaya. Asili yote ya mwanadamu ni kielelezo cha sura ya Mungu.
Hakuna kitu chochote isipokuwa sura ya Mungu ambacho kinaweza kuchukuliwa maanani kwamba ndicho kiini cha uwepo wetu. Kimsingi sisi ni viumbe tulio katika sura ya Mungu. Hakuna maelezo ya kina kuhusiana na hali yetu ya kibinadamu yanayoweza kukubalika yawe ndiyo utambulisho wetu wa msingi au msingi thabiti wa maadili yetu.
Chaguo la Mungu la jinsi kwa ajili ya kila mtu ni sehemu ya mpango wake wa jinsi ambavyo mtu huyo atakavyoweza kuonyesha sura ya Mungu. Baadhi ya watu wanakataa kukubaliana na jinsi ambayo Mungu aliwapa. Wanaweza hata kujaribu kuishi kama mtu wa jinsi iliyo tofauti na jinsi yake. Baadhi ya watu hujaribu hata kubadilisha miili yao kwa njia ya upasuaji. Huu ni uharibifu mkubwa na kusikitisha wa uumbaji wa Mungu, kwa sababu kusema kweli mtu hawezi akabadilisha jinsi kwa kuubadilisha mwili wa asili. Kila mtu ni mwanamume au mwanamke kwenye maeneo yote ya asili ya mtu – na siyo tu kimwili. Mungu anatutaka sisi tumtukuze yeye na tuakisi sura yake tukiwa kwenye jinsi aliyotupa kila mmoja wetu.
Kiwango cha Mungu kuhusu Maadili
► Mwanafunzi anapaswa asome Waebrania 13:4 kwa ajili ya kikundi.
Aya hii inatueleza kwamba ndoa inapaswa iheshimike katika kiwango cha hali ya juu sana. Dhambi ya kufanya ngono ni kuivunjia heshima ndoa. Mungu atahukumu uasherati.
► Mwanafunzi anapaswa asome 1 Wakorintho 6:18 kwa ajili ya kikundi.
Dhambi za kingono zinajumuisha mawazo ya tamaa, uasherati, uzinzi, kujamiana na wanandugu, ubakaji, unyanyasaji wa kingono kwa watoto, shughuli za ushoga, na matumizi ya picha au video za ngono.
Mawazo yenye tamaa: Kupenda kuwazia mawazo ya tamaa na mtu yeyote ambaye siyo mwenzi wako.
Uasherati: Kufanya ngono kunakohusisha watu ambao hawajaolewa.
Uzinzi: Kufanya ngono kunakohusisha mtu ambaye tayari yuko kwenye ndoa na mtu mwingine.
Kujamiiana na wanandugu: Kufanya ngono na mtu wa karibu wa familia ambaye siyo mwenzi wako.
Vitendo vya ubakaji: Unyanyasaji wa kijinsia, kulazimishwa mtu kufanya ngono kwa nguvu bila ya hiari yake.
Unyanyasaji wa kingono kwa watoto: Kufanya ngono kunakohusisha mtu ambaye bado hajafikia umri wa mtu mzima wa kuweza kuamua kufanya kwa hiari tendo la ndoa na/au ambaye bado hajaweza kuwa na matamanio ya kufanya ngono.
Shughuli za ushoga: Kufanya ngono kunakohusisha watu wenye jinsi moja.
Matumizi ya picha za au video vya ngono: Kuandika, matumizi ya picha na video zenye maudhui ya kuamsha hisia za kufanya ngono kwa kuonyesha watu wakiwa uchi au wakifanya tendo la ngono.
Yote haya kwa pamoja ni ukiukwaji wa uhusiano wa ndoa.
Kumbuka—kila njaa inayotuvutia katika mwili ni unyonyaji wa hitaji ambalo linaweza kutimizwa vyema na Mungu. Muktadha pekee wa kimungu katika kujamiiana ni kujamiiana kwa watu walioko kwenye ndoa. Ngono haramu ni… tamu mara moja, lakini ni kitu kitakachotia sumu katika hamu yetu ya kiroho hadi tutamani kile ambacho mwisho wake kitatuangamiza sisi. Ngono haramu haitatufanyia jambo lolote zaidi ya kutubomolea usikivu wetu dhidi ya utakatifu, haki, na uwepo wa Mungu kwenye maisha yetu.[1]
Katika vifungu vingi, kitabu cha Mithali kinaonya kwamba uasherati huharibu maisha ya mtu na husababisha kifo (Kwa mfano: Mithali 2:16-19 na Mithali 6:24-29, 32-33).
Robertson McQuilkin anaandika kwamba:
[Makusudi ya Mungu kwa ajili ya kujamiiana kwa mwanadamu] kiakili yanakiukwa kwa kiasi kikubwa sana kuliko hata ambavyo lingetendeka tendo lenyewe. Mungu hakumuumba tu mwanamume na mwanamke; aliwaumba kwa ajili ya kila mmoja kuwa mwandani wa mwingine, kuwa katika dhamana ya maisha ya ndoa, na umoja unaofanania asili yake yeye mwenyewe. Ili kusudi hili la juu liweze kukamilishwa, hali ya kuwa mwandani ni lazima iwe ya kipekee na kujitoa kwa kudumu au vinginevyo haitakuwa umoja. Uaminifu ni wa muhimu zaidi katika akili. Mwandani ulio wa kipekee, kujitoa kwa kudumu, na uaminifu wa mmoja kwa mwingine unakiukwa kwanza kutokea kwenye akili.[2]
► Wanafunzi wanapaswa wasome 1 Wakorintho 6:9-11, 15-20 and Mathayo 5:27-30 kwa ajili ya kikundi.
Kila jamii ina mitazamo ya kitamaduni ya uhusiano kati ya wanaume na wanawake. Mitazamo hii ya kitamaduni ni ya viwango vya chini sana kuliko viwango vya maadili ya kibiblia. Tamaduni nyingi zina desturi nyingi tu kwa ajili ya kudumisha jamii yenye utaratibu. Wanavumilia dhambi ya kujamiiana kama inasimamiwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia matokeo mabaya au kashfa. Kiwango cha kibiblia kuhusu maadili ni tofauti.
Kwa masikitiko, baadhi ya makanisa hufuata maadili ya tamaduni za jamii zao badala ya maadili yaliyoko kwenye Biblia. Wanawaadhibu watu ambao dhambi zao zimekuwa za dhahiri na za uzembe, lakini wanawavumilia watu ambao wanafanya dhambi zinazofanana na hizo na walio waangalifu zaidi katika kuficha dhambi yao au wanaodhibiti matokeo yake.
Aya hizi zinatueleza kwamba watu ambao wanatenda dhambi hizi siyo waumini na hawataingia mbinguni. Baadhi ya waumini wa Korintho walikuwa wametenda dhambi hizi katika siku za nyuma lakini walikuwa wamekombolewa dhidi ya hizo dhambi.
Fundisho lolote la kiimani linalofumbia macho dhambi hizi kwa mtu ambaye alishakiri kwamba ameokoka ni fundisho potofu. Kama mtu atajinadi kwamba ni mfuasi wa Kristo na bado anaendelea kufanya dhambi ya uzinzi, kwa mujibu wa maandiko, kanisa linatakiwa limwondoe mtu huyo katika kanisa na wasimchukulie kama mtu aliyeamini (1 Wakorintho 5:11-13).
Viongozi wa makanisa wanapaswa waweke mfano mzuri wa tabia. Wakati kanisa linaporuhusu viongozi wa kuongoza ibada wavae mavazi yasiyo na staha au wanaporuhusu aina za ngoma za hisia za mahaba kanisani, wanamaanisha kwamba tamaa mbaya za kingono ni za kawaida. Wanamaanisha kwamba dhambi ya kingono si jambo kubwa.
Mifumo ya uvaaji kwenye jamii inadokeza kwamba mtu anakuwa hajavaa vizuri kama atakuwa hajaonyesha maumbile yake ya kimwili ili kuleta mvuto wa kufanya ngono. Washirika wa kanisa wakati mwingine huangukia katika kosa hili, hasa kwenye matukio maalumu. Wanafikiri hawajavaa vizuri isipokuwa kama wanafuata mitindo ya jamii yao. Kanisa ni lazima lifundishwe kwamba kufanya hivyo ni makosa. Mtu aliyeokoka hapaswi kabisa kusababisha matamanio mabaya kwa watu wengine. Katika 1 Timotheo 2:9-10 tunaelezwa kwamba watu waliookoka wanapaswa kuvaa na kutenda kwa namna ambayo mtu yeyote atakayekuwa anawaangalia atajua kwamba wanaishi maisha ya uangalifu, yenye usafi na wasiokuwa tayari kutenda dhambi au kuwashawishi watu wengine kutenda dhambi.
[1]Gary Thomas, Sacred Marriage (Grand Rapids, MI: Zondervan, 2000), 210.
[2]Robertson McQuilkin, An Introduction to Biblical Ethics, 2nd ed. (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, Inc., 1995), 216.
Ponografia
Maana yake ni kuandika, kutumia matumizi ya picha na video zenye maudhui ya kuamsha hisia za kufanya ngono kwa kuonyesha watu wakiwa uchi au wakifanya tendo la ngono.
Mtandao unaifanya hivi kupatikana kwa urahisi duniani kote. Wachungaji na viongozi wa zamani hawakukutana na majaribu haya kwa sababu mitandao ilikuwa bado haijakuwepo wakati wa ujana wao. Wanaweza hata wasielewe yale ambayo kizazi kipya kinapitia. Lakini watu ni lazima wafundishwe kutumia kanuni za Kibiblia kwenye kuchagua mambo ya burudani.
Ponografia ni mbaya kwa sababu imekusudiwa kumfanya mtu awaze matendo ya uasherati, uzinzi, na aina nyingi upotovu wa kingono. Ni kivutio kwa mtu ambaye ana matamanio ya kutenda dhambi. Ponografia hualika na kumwezesha mtu kushiriki matendo yasiyokuwa ya kimaadili ambayo Mungu anayashutumu. Yesu alisema kwamba kuchagua kufikiria mambo haya ni dhambi (Mathayo 5:28).
Ponografia pia ni mbaya kwa sababu inashusha thamani ya watu na mahusiano. Inapunguza tendo la kujamiiana kuwa shughuli ya ubinafsi. Inawatendea watu kama vitu vya kutumia kwa ajili kujifurahisha binafsi badala ya kuwathamini watu kama walioumbwa kwa sura ya Mungu, na walioundwa kwa mahusiano yenye afya.
Ponografia inaleta uraibu. Ponografia, kwa ujumla kama dhambi, ni utumwa (Yohana 8:24, 2 Petro 2:19). Mtu anayetumia ponografia anajisikia sana kuwa na hitaji kubwa kwa ajili yake. Hawezi kufikiria kuishi bila hiyo. Inaonekana kwake kwamba maisha yatakuwa matupu na yasiyokuwa na hamu bila ya kupata mambo ya kufikirika anayoyapata kutoka kwenye Ponografia. Kama uraibu mwingine wowote ulivyo, tamaa inakuwa ya kuteketeza, na mtumiaji huanza kudhabihu vitu vingine vizuri katika maisha yake.
Ponografia inakua hatua kwa hatua. Mtumiaji anaanza kuhitaji vifaa ambavyo ni vya wazi zaidi na vimepotoshwa. Ataanza kufurahishwa na mawazo ambayo hapo mwanzoni yangemchukiza na kumletea hofu.
[1]Ponografia ina madhara. Mtumiaji anakuwa na uwezo mdogo wa kufurahia tendo la uhusiano wa kawaida. Tamaa zake zinakuwa siyo za asili kiasi kwamba haziwezi kutoshelezwa tena. Anakuwa wa kupuuzia mateso ya wengine na yuko tayari wengine wateseke kwa ajili ya starehe yake.
Baadhi ya Madhara ya Ponografia
Kufikiria vitendo vinavyoonyeshwa kwenye ponografia huathiri akili na miili ya watumiaji kana kwamba kimwili walikuwa wanafanya vitendo hivyo wao wenyewe.
Ponografia huwakilisha hali zisizo za kweli zinazosababisha ubongo kuwa na majibu ya furaha yenye nguvu zaidi kuliko ambavyo ingeweza ikawa kwenye tendo halisi la asili la kujamiiana.[2] Ubongo hujitengeneza ili kuendana na kiwango hiki cha juu kisicho cha kawaida cha kemikali za kufurahisha. Kwa sababu hiyo ubongo huendelea kudai kiasi kikubwa zaidi cha ponografia na ponografia iliyopotoka zaidi ili mtazamaji aendelee kupata raha. Mabadiliko ya kemikali kwenye ubongo yanaweza hatimaye kumfanya mtu kushindwa kabisa kuwa na au kufurahia uzoefu wa kawaida wa kingono katika maisha halisi. Sehemu ya ubongo inayotuwezesha kufanya maamuzi pia huharibika kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha kemikali ya raha.
Mungu alikusudia uzoefu wa kingono kuwa wa kuunganisha katika mahusiano. Homoni inayotolewa kwenye ubongo wakati wa tendo la ndoa huunganisha kihisia washiriki, na kuimarisha uhusiano wao. Hili ni zawadi nzuri ndani ya ndoa. Hata hivyo, kutazama ponografia humunganisha kihisia mtazamaji na ponografia yenyewe.
Hatia na aibu ya kutumia ponografia huwatenga watu, kuwazuia wasiweze kuunganishwa tena na watu wengine kwenye mahusiano yenye nguvu. Pia huharibu uaminifu ulioko kwenye uhusiano wa ndoa.
Kwa kuwa husababisha uwiano usiokuwa sawa kwenye ubongo, utumiaji wa ponografia unaweza kusababisha mfadhaiko wa akili kwa mtazamaji.
Mambo yanayoonyeshwa kwenye ponografia wakati mwingine husababisha vurugu na unyanyasaji katika maisha halisi ya mahusiano ya ndoa.
Wachungaji na wazazi wanapaswa kuwaonya vijana wao juu ya hatari ya kushiriki ponografia. Wazazi hawapaswi kuwapa watoto ufikiaji usiozuilika kwenye mtandao wakati wanapokuwa hawajakomaa kuweza kuzuia majaribu. Mtu yeyote anayepambana na jaribu la kuzuia matumizi ya ponografia anapaswa mara kwa mara atoe taarifa ya ushindi au kushindwa, kwa mtu wa kimungu na anayeaminika. Uchunguzi wa mara kwa mara utakaofanywa na muumini aliyekomaa unaweza ukasaidia sana kudumisha kujitolea kwa usafi na kupata uthabiti wa ushindi.
► Je, ni mazoea gani unayopaswa kupendekeza kwa watu wengine ili kuwasaidia katika kuwazuia kutokana na hali hii yenye kuzoesha tabia mbaya kutokana na ponografia? Je, kanisa linawezaje kusaidia?
"Shetani anataka ‘kuiba, kuua na kuharibu’ (Yohana 10:10) furaha yako ya kingono, na ponografia ni silaha yake kuu. Ponografia inaahidi kukuridhisha kingono, lakini kwa kweli inakupokonya uwezo wa kufurahia jambo halisi."
- The Freedom Fight
[2]Taarifa yote iliyoko kwenye kifungu hiki na vifungu vinne vinavyofuata vimenukuliwa kutoka mtandaoni https://thefreedomfight.org, chanzo cha Biblia kilichopendekezwa kwa ajili ya wale wanaotaka kuwekwa huru na kutolewa kwenye kifungo cha matumizi ya ponografia..
Udhalilishaji wa Watoto / Ubakaji
Udhalilishaji wa watoto/ubakaji ni kufanya tendo la kujamiiana kwa makusudi. Ni upotofu wa ngono unaofanywa kinyume na matakwa ya mtu. Ni tendo la uovu kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na:
Linapingana na makusudi ya mungu yaliyo mema kwa ajili ya kujamiiana ndani ya ndoa ya ahadi (Waebrania 13:4).
Linaiba hali ya mtoto ya kutokuwa na hatia – kwa kuwa sasa mtoto anajikuta amekuwa na uzoefu wa mambo ambayo bado hakutakiwa kuyajua.
Linamnyang’anya mtoto ubikira wake (1 Wathesalonike 4:3-7).
Linampa mtoto hisia ya uwongo ya kuwa ana hatia; mtoto anajikuta yuko kwenye tendo baya, lakini hana uwezo au haruhusiwi kufanya chaguo halisi.
Linasababisha mtoto kufanya maamuzi yanayohusu kujamiiana ambayo bado hana ukomavu nayo wa kuyafanya.
Hufanya watoto kuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kuchagua tabia zisizokuwa na maadili kwa siku za baadaye kwa sababu wanajihisi wachafu na wasio na thamani (Mathayo 18:6).
Linaongeza jaribu kwa mtoto la kujihusisha katika tabia na au shughuli zilizo chafu kwa siku za baadaye.
Linawadhulumu wale ambao wako kwenye mazingira hatarishi na ambao hawawezi kujitetea wenyewe.
Linamjeruhi mtu aliyefanywa kwa sura ya Mungu, ambaye ana thamani isiyokuwa na kikomo (Mwanzo 1:27).
Udhalilishahi au ubakaji wa mtoto wakati mwingine hufanyika ndani ya familia na miongoni mwa marafiki. Inawezekana kusiwepo na kushukiwa kuwepo kwa hali hiyo kwa sababu wanafamilia na marafiki wanaofanya hayo wanaaminika, na mtoto anakuwa anaogopa kumwambia mtu yeyote kuhusu kile ambacho kimetendeka kwake.
Ubakaji ni kulazimishwa mtu kimwili (aidha mtoto au mtu mzima) kufanya tendo la ngono pasipokuwepo na ridhaa yake. Ubakaji ni uovu kwa sababu nyingi zinazofanana kwamba udhalilishaji wa mtoto ni uovu (Kumbukumbu la Torati 22:25-27).
Aina nyingine ya unyanyasaji wa kijinsia ni usafirishaji wa watu kwa ajili ya biashara ya ngono. Duniani kote, watoto na vijana wanatekwa nyara na watu wasiojulikana, au kuuzwa na wanafamilia na wanaenda kutumika kwa ajili ya kufanya ukahaba au kwa ajili ya kutengeneza ponografia. Familia zilizo katika hali ya umaskini wakati mwingine zinashindwa kuwalinda watoto wao kutokana na biashara hii chafu kwa kuwa wanajihisi kutamani sana kupata fedha. Mtu fulani anapata faida, lakini watoto siyo tu kwamba wanaumizwa kimwili lakini pia wanadhurika vibaya sana kiakili na kihisia. Huu ni ugandamizaji wa dhambi kwa watu maskini na walioko hatarini na kwamba Mungu lazima atahukumu (Mithali 14:31).
Dhambi hizi zilizo kinyume cha watoto zinavunja moyo wa Mungu (Mathayo 18:10-14, Zaburi 146:7-9). Wale wote wanaotenda dhambi hizi hawataponyoka pasipo kupata adhabu ya Mungu (1 Wathesalonike 4:6, Ezekieli 7:8-9). Watu waliookoka wanapaswa kushiriki upendo na huruma ya moyo wa Mungu na kufanya kazi ya kutetea, kuokoa, na kuwaponya wale wote ambao wameingizwa kwenye utumwa (Mithali 24:11-12, Ayubu 29:12-16, Zaburi 72:12-14).
Ngono - Binafsi
Kupiga punyeto ni kitendo kinachohamasisha viungo vya uzazi vya mtu kwa ajili ya kuamsha hisia na furaha ya ngono au kuondoa fadhaa ya ngono.
Biblia haina hukumu mahususi ya hatia kuhusu kupiga punyeto kama ni ukosefu wa maadili. Walakini, ngono binafsi inaweza kuwa chanzo cha kusababisha mawazo ya kutamani, matumizi ya ponografia, na uasherati, ambayo yote ni matendo ya dhambi (Mathayo 5:27-28, Mathayo 15:19-20).
Kupiga punyeto pia siyo tendo la busara kwa sababu ni lenye kuzoesha tabia mbaya inayomtawala mtu: jinsi unavyoendelea kufanya ndivyo unavyojihisi kwamba unapaswa kuendelea kufanya.
Kupiga punyeto kwa kulazimishwa wakati mwingine huelekeza kwenye suala la ndani zaidi, kama vile matatizo ya hisia au uhusiano, au unyanyasaji wa kijinsia.
► Wanafunzi wanapaswa wasome 1 Wakorintho 6:12-13, 18-20 na 1 Wathesalonike 4:1-8 kwa ajili ya kikundi.
Mungu alipanga umoja wa kimwili katika ndoa kwa ajili ya kusaidia kumuunganisha mwanamume na mwanamke kihisia na kiroho (1 Wakorintho 6:16-20, Malaki 2:15).
Watu wengi…wanadhania kwamba kupiga punyeto kunaweza kukasaidia kushughulikia hali ya kuwa kapera hadi pale watakapokuwa wameanza kuoa. Wanashindwa kuelewa hata hivyo, kwamba hilo zoezi linapofanyika kuwa ni la mazoea, linaweza likatishia uzuri na ufanyaji wa ngono ya ndoa katika siku zijazo.
Ngono ya kibinafsi huleta uzoefu wa kufanya ngono ambao unakuwa umekosa kusudi muhimu la ngono: kuunganishwa kwa watu wawili kuwa mwili mmoja, kimwili na kihisia… Kupiga punyeto hakupaswi kutumike kama ni mbadala kwa ajili ya shughuli za ngono zenye afya, na za kawaida ndani ya ndoa.[1]
Je, mtu ambaye hajaoa anapaswa kufanya nini kama kitendo cha kupiga punyeto ni tatizo katika maisha yake?
Hata kama mtu anapiga punyeto kwa madhumuni ya kupunguza tu msukumo wa kufanya ngono, bado ni vyema kuachana na jambo hilo, kwa sababu ya majaribu yaliyopo kwa sasa, na kwa sababu ngono ya kibinafsi haikamilishi makusudi ya Mungu kwa ajili ya kujamiiana.
Kama kuna aina nyingine yeyote ya uasherati katika maisha yao, lazima waungame na kuziacha dhambi hizo. Wanapaswa mara kwa mara na kila mara watoe hesabu ya kushinda na kushindwa kwao kwa mshauri mzee mcha Mungu ambaye atawaombea na kuwapa ushauri.
Ikiwa kupiga punyeto ni matokeo ya hisia au matatizo ya kimahusiano au unyanyasi wa kijinsia wa ngono uliopita, kupata ushauri kutoka kwa mshauri wa Kikristo mtaalamu mwenye taaluma hiyo ni jambo la kufaa sana.
[1]Dr. Tim Clinton and Dr. Diane Langberg, The Quick-Reference Guide to Counseling Women, (Grand Rapids, MI: Baker Books, 2011), 185.
Biblia inasemaje kuhusu Matendo ya Ushoga
Mungu alipanga ndoa iwe ni uhusiano wa kudumu, na wa kujitolea kati ya mwanamume na mwanamke. Mungu aliona kwamba Adamu alikuwa anahitaji kuwa na msaidizi (Mwanzo 2:18). Neno msaidizi linamaanisha mtu anayefanana na mwingine, kuwa msaidizi kwa kuwa tofauti katika njia za kusaidia. Mungu alimuumba mwanamke na siyo mwanamume mwingine awe msaidizi wa Adamu (Mwanzo 2:22). Hitimisho la simulizi ya uumbaji inatoa kanuni ya ujumla ya ndoa kwa wanadamu wote katika ndoa, mwanamume na mwanamke watakuwa kitu kimoja kwa namna ya pekee ya kufanana (Mwanzo 2:24).
Yesu alizungumza kuhusu mpango wa Mungu wa ndoa (Mathayo 19:4-6). Alirejea kifungu kutoka katika kitabu cha Mwanzo na kusema kwamba mwanamume na mwanamke hukutana na kuwa kitu kimoja katika uhusiano wa kipekee na wa kudumu.
Mtume Paulo alitoa kauli nyingi kuhusu ndoa. Alisema kuwa ndoa ni kielelezo kinachotufundisha sisi kuhusu uhusiano kati ya Kristo na Kanisa (Waefeso 5:22-33). Kwenye kifungu chote cha Waefeso, alitoa kauli kuhusu uhusiano kati ya wanaume na wake zao. Alinukuu kauli kutoka vitabu vya Mwanzo na Mathayo kuhusu uhusiano maalumu kuhusu mwanamume na mke wake (Waefeso 5:31). Ni jambo lililo wazi kutokana na kifungu kwamba ndoa ni uhusiano kati ya mwanamume na mwanamke.
Kitabu cha Mambo ya Walawi kinatoa matumizi ya kina sana kuhusu sheria ya Mungu kwa Waisraeli. Inasema kwamba kwa mwanamume kulala na mwanamume mwingine kama ilivyo kwa mwanamke ni machukizo (Mambo ya Walawi 18:22). Adhabu ya kitendo cha ushoga kwa washiriki wote wawili kilikuwa ni kifo, kwa sababu wote kwa pamoja walifanya machukizo (Mambo ya Walawi 20:13).
Wakati mwingine watu husema kwamba Mambo ya Walawi hayawahusu watu wa kizazi cha sasa. Ni ukweli kwamba baadhi ya maagizo katika Mambo ya Walawi yalikuwa na umuhimu wa sherehe za kiyahudi. Hata hivyo, maamrisho yaliyoko kwenye Mambo ya Walawi 18-20 yanakataza upotofu mwingine wa kijinsia kama vile kufanya ngono na jamaa wa karibu, kufanya ngono na wanyama, na kufanya umalaya na mtoto wa kike wa kumzaa. Maagizo mengine katika sura hizi yanakataza kuwatoa watoto kama dhabihu, kuiba, kuabudu sanamu, kuwatendea vibaya walemavu viziwi na vipofu, kuwakandamiza watu maskini, kutowatendea mema wageni, na kuwa na mizania za uongo. Ni dhahiri kwamba maagizo haya ni matumizi ya viwango vya Mungu vya maadili na haki ambavyo vinatumika kwa watu wote, mahali popote, na kwa wakati wowote.
► Mwanafunzi anapaswa asome Warumi 1:18-32 kwa ajili ya kikundi.
Kifungu hiki kinaanza na taarifa kwamba hukumu ya Mungu inakuja juu ya watu wote ambao kwa kujua wanamwasi Mungu kwa makusudi. Kifungu kinasema kwamba baada ya watu kukataa ujuzi wa Mungu mmoja wa kweli, aliye Muumbaji, walianza kuwa waabudu sanamu, wakiabudu vitu vilivyoumbwa na yeye. Kukataa kwao ukweli kulisababisha dhambi ya ngono, hata kusababisha kufikia katika kiwango cha kufanya ushoga. Kifungu kinaelezea kwamba ngono kati ya watu wawili wa asilia moja ni kinyume cha asili. Baadhi ya watu wamesema kwamba kifungu kinarejea ubakaji wa ulawiti, lakini kifungu kinasema kwamba watu kwa pamoja walifanya makosa na kupokea hukumu kwa ajili yake, kwa hiyo kinarejea utendaji wa hiari wa pamoja. Kifungu kinaenda mbali zaidi kuorodhesha aina nyingi za dhambi na kuelezea mtazamo wa uasi dhidi ya Mungu.
Mtume Paulo aliorodhesha shughuli za ushoga pamoja na dhambi nyingine ambazo Mungu anazihesabia kuwa ni hatia (1 Wakorintho 6:9-10, 1 Timotheo 1:9-10).
Majukumu ya Kanisa
Baadhi ya makanisa yamejitahidi sana kutafuta njia ya kuonyesha upendo kwa watu ambao wako kwenye dhambi ya zinaa. Baadhi ya makanisa yamehalalisha aina mbalimbali za dhambi za kingono kama za kawaida, za asili, na zisizoepukika.
► Je, majukumu ya kanisa ni yapi kuhusiana na masuala ya maadili ya ngono?
Kufundisha na Kupenda Haki
Wakati mwingine kanisa linaonekana kutohusika na aina mbalimbali za uasherati wakifikiri kwamba hazina madhara na upotofu wake ni mdogo. Kwa mfano, wanaweza kudhania kwamba vijana wengi ambao hawajafunga ndoa watafanya ngono badala ya kuwafundisha jinsi ya kushinda dhidi ya jaribu. Watu waliookoka ni lazima washikilie kiwango cha Mungu cha maisha ya utakatifu na waiache ngono iwe ni akiba ya baadaye kwa ajili ya ndoa.
Ujumbe wa kanisa unapaswa kuwa sawa na maelezo ya Biblia. Mungu atawahukumu wale wote walio na shughuli za kujamiiana nje ya ndoa (Waebrania 13:4). Waumini hawapaswi kuvutiwa na mtu aliye kwenye matendo machafu ya ngono. Wafuasi wa Kristo hawapaswi kufanya mambo ya mizaha kwenye suala la uasherati. Dunia inafundisha kwamba dhambi ya zinaa inapaswa kusimamiwa kwa uangalifu ili kuepuka mimba na magonjwa, lakini ujumbe wa kanisa ndiyo ulio wa umuhimu zaidi. Kanisa linapaswa lifundishe kwamba dhambi ya zinaa hupelekea kwenye majuto, familia kuporomoka, majaribu kuzidi, kutotosheka, na kuwa mwenye hatia.
Kushirikisha Injili
Kanisa linapaswa liwapende watu wote wenye dhambi na kutoa neema na msamaha wa Kristo.
Siyo dhambi kupata majaribu; hata Kristo mwenyewe alijaribiwa, lakini hakutenda dhambi (Waebrania 4:15). Kanisa halipaswi kumfanya mtu ajihisi kwamba amehukumiwa na kuonekana asiyefaa kwa sababu ya majaribu, hata yale majaribu potofu ya ngono. Matamanio mabaya hayafanani kati ya mtu na mtu, lakini kila mtu amezaliwa na asili yake ya dhambi pamoja na kasoro za kiroho zinazosababisha matamanio mabaya.
Mchungaji anaweza kujihisi kwamba hajafundishwa mahususi kwa ajili ya kumsaidia mtu mwenye matamanio mabaya, lakini anaweza kutoa ushauri na kumsaidia huyo mtu mwenye tatizo kama hili kama mtu mwingine yeyote mwenye dhambi. (Sehemu mbili zinazofuata za somo hili zinatoa ushauri mahususi zaidi za ushauri kwa ajili ya kusaidia waumini kuwa washindi dhidi ya majaribu ya uasherati.)
► Je ni kwa jinsi gani kanisa linatakiwa lihusike wakati mshirika wa kanisa anapokuwa ametenda dhambi ya uasherati?
Kumrejesha Mwenye Dhambi
Wagalatia 6:1 inasema kwamba kanisa ni lazima lijaribu kumrejesha mshirika ambaye ametenda dhambi. Hiyo haina maana kwamba mtu huyo ataendelea na nafasi yake ya huduma au kurudishwa haraka katika nafsi yeyote ya utumishi baada ya kuwa amefanya dhambi na kuthibitishwa. Urejesho inamaanisha kwamba ni mtu kurejeshwa tena kwenye ushirika na utunzaji wa kanisa. Kama mshirika ametubu kweli, anasemehewa na Mungu na kanisa. Kanisa linapaswa kutoa uwajibikaji wa kiroho kumsaidia mtu huyo aweze kuimarisha ushindi na kuwa tena mwenye nguvu za kiroho. Kama muumini aliyerejeshwa tena akiendelea kuishi katika kuwajibika, anaweza hatua kwa hatua akajenga tena kwa upya uaminifu na imani kwa familia yake.
Ikiwa msichana ambaye hajaolewa akipata mimba, kanisa halipaswi kumtenga kutoka kwenye ushirika na uangalizi wa kanisa bila ya kujaribu kumfanyia urejeshwaji wa kiroho. Kama atatubu na kurejea kwenye uwajibikaji wa kiroho, huyo msichana amesameheka. Dhambi yake siyo mbaya kuliko dhambi ya yule mwanamume aliyehusika kumpa mimba. Wakati mwingine anatendewa kwa ukali kwa sababu tu matokeo ya dhambi yake yanaonekana sana hadharani.
Katika maeneo mengine, kanisa linamtendea mtoto tofauti kabisa kwa kuwa alizaliwa nje ya ndoa, lakini hili ni kosa kwa sababu siyo kosa la mtoto. Kanisa kumpenda na kumkubali mtoto haimaanishi kuwa linahalalisha dhambi.
Kulinda watu walio katika Mazingira Hatarishi.
Katika jamii kadhaa, wazazi ambao huona aibu kwa ajili ya mimba ya mtoto wao ambaye mimba yake haijatokana na ndoa wanashawishika kumuua mtoto ambaye bado yuko tumboni ili kutunza hadhi ya familia yao. Lakini kamwe hakuna sababu ya maana kwa ajili ya kufanya mauaji (Kutoka 20:13). Kila mtoto ambaye hajazaliwa ameumbwa katika sura ya Mungu (Mwanzo 9:6, Zaburi 139:13-14). Mtoto wa Msichana huyo ni lazima alindwe, apendwe na atunzwe.
Kutoa Njia Mbadala kwa Umaskini
Kanisa ni familia ya watu wa imani. Haitoshi kwa kanisa kuhukumu dhambi. Kanisa ni lazima lichukue hatua ya kuwatunza washirika wake. Kwa mfano, mtu anayesaidiwa kifedha kutokana na shughuli za dhambi anaweza akahitaji msaada ili aweze kutengeneza usaidizi mwingine mbadala utakaomsaidia kifedha.
Kwa mfano, wasichana kadhaa walikuwa wanahudhuria kwenye kanisa kubwa na walikuwa wakiimba kwenye kwaya ya kanisa. Familia zao zilikuwa maskini. Wasichana hawa walikuwa kwenye mahusiano machafu na wanaume kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu katika familia zao. Je, kanisa lifanye nini katika mazingira kama hayo?
► Je, kanisa lako linapaswa kufanya nini ili kuwasaidia watu kuachana na mifumo ya maisha ya dhambi.
Msaada kwa wale Wanaostahimili Majaribu
Tumeshajadili mada nyingi zilizo ngumu kwenye somo hili. Kuna uwezekano kwamba watu wengi wanaosoma somo hili watakuwa wametatizika na baadhi ya masuala haya. Baadhi ya wasomaji ni viongozi wa makanisa ambao wanahitajika kujua jinsi ya kutoa ushauri kwa washirika wao wanaokabiliwa na majaribu.
Haijalishi ni aina gani ya majaribu yaliyoko, kuna baadhi ya tabia na mifumo ya mawazo ambayo inaweza kumsaidia mwamini kuwa mshindi.
Mfuasi wa Kristo anaweza kusaidiwa na mambo yafuatayo:
1. Kujikabidhi kabisa kuwa kwenye uhusiano wako na Kristo (Mathayo 16:24-27). Majaribu ya dhambi ya uasherati, kama yalivyo majaribu mengine yote, ni mashambulizi ya Shetani dhidi ya nafsi yako (1 Petro 2:11). Lengo lake ni ili aibe na kuchinja na kuharibu (Yohana 10:10). Unapaswa ukimbie kwa ajili ya kuokoa maisha yako (2 Timotheo 2:22).
2. Kuwa na uhakika kwamba Yesu anakujali (Zaburi 139:1-3, 1 Petro 5:6-10). Anajali kuhusu imani yako, mahitaji yako ya kimwili, na usafi wako. Katika hali yake ya ubinadamu, alistahimili kwa ushindi majaribu yote ya kimwili na kiakili tunayokabiliana nayo sisi, na anayo neema tunayoihitaji kwa ajili ya kutuwezesha kuwa washindi (Waebrania 4:14-16).
3. Kutokuuamini uongo wa Shetani (Yohana 8:44). Shetani anaweza kukuambia, “Yesu hajali, vinginevyo angeondoa hamu ya ngono ambayo inakukatisha sana tamaa.” Katika 1 Petro 5:7-8 tunaambiwa kwamba Yesu anajali na shetani ndiye anayetaka kutuharibu sisi. Shetani anaweza kwa makosa akakushutumu wewe kuwa ni mwenye dhambi kwa sababu ya kuwa mtu mwenye matamanio ya ngono (Ufunuo 12:10).
4. Kumwangalia Yesu peke yake na kumtukuza kwa jinsi alivyo (Zaburi 105:3-4). Shetani atakuwa anapendelea kuiharibu imani yako na uhusiano wako na Mungu kupitia jaribu hili (Yohana 10:10). Lakini kusudi la Yesu katika jaribu hili ni kwamba imani yako iweze kuimarishwa, na kwamba utakuwa mtu bora zaidi wa kumtukuza yeye (1 Petro 1:5-9). Unapoelekeza mwelekeo wako kwa kumwabudu Yesu, atakuwa pale ulipo wakati huo kwa ajili ya kukusaidia wewe (Zaburi 46:1).
5. Kulitafakari Neno la Mungu (Zaburi 119:9). Kusoma, kusikiliza, na kulitafakari Neno la Mungu kutakusaidia wewe kusimama kwa ushindi katika wakati wa majaribu. Yesu alipojaribiwa, alitumia maandiko katika kushinda (Mathayo 4). Ni lazima tufanye vivyo hivyo.
6. Kumshukuru Mungu hata katika matamanio yako ya ngono, wakati unapokuwa unaomba nguvu za kulishinda jaribu (2 Wakorintho 12:7-9). Unaweza kumshukuru Mungu kwa ajili ya matamanio yako ya asili uliyo nayo, kwa sababu ni sehemu ya mpango wa Mungu wa ubinadamu wako na yanakulazimisha kumtegemea Yesu na kutafuta nguvu zake. Udhaifu wako unakupa fursa ya kukomaa katika kutembea kwako pamoja na yeye.
7. Kuweka wazi wa maisha yako mbele ya mtu mmoja mwenye busara na mcha Mungu (Wagalatia 6:2). Kuwa muwazi na mwaminifu kwa mtu mwingine (wa jinsia yako) ambaye amekutangulia mbali kwenye safari ya imani kutakuwa ni msaada sana kwako. Watakuwa na uwezo wa kuomba kwa ajili yako na kukushauri. Kuzungumza nao kuhusu mapambano yako kutakusaidia wewe kudumisha usafi na kuendelea kutiwa moyo katika imani yako.
8. Kutumikia watu wengine na kuweka mwelekeo wako kwa ajili ya mahitaji yao (Wafilipi 2:3-5). Pambana na kuhusika kwako kwa wingi kuhusu mahitaji na matamanio yako mwenyewe kwa kuwatumikia watu wengine.
9. Kuoa au kuolewa na mtu sahihi katika wakati wa Mungu (Mithali 5:15, 18-19). (Masomo yajayo yanajadili jinsi ya kufanya chaguo lililo zuri kwa ajili ya ndoa).
► Je, katika haya ni mawazo gani yaliyo mapya kwako? Je, ni mawazo gani ambayo umeona ni ya msaada sana katika maisha yako?
► Je, ni tabia gani nyingine au mifumo ya mawazo ambayo imekuwa ni ya msaada kwako?
Usafi wa Maadili kabla ya Ndoa
Vijana hukabiliana na majaribu mazito kabla ya kuoa. Ni muhimu kwao kukumbuka kwamba wanahitaji kuwa na msaidizi wa maisha atakayeweza kuwa mwaminifu.[1] Hawapaswi kufikiria kuwa na uhusiano na mtu ambaye anataka kujiridhisha kwa muda tu bila ya ndoa. Hawapaswi kuwa na uhusiano na mtu ambaye siyo mtu aliyeokoka/mwamini aliyejitoa kabisa (1 Wakorintho 7:39). Wanapaswa tu kufikiria mtu ambaye atakuwa mwenzi mwaminifu na mzazi mzuri kwenye ndoa.
Kijana ambaye anataka awe na ndoa nzuri anapaswa awe mtu mwaminifu, aliyejitoa kuwa mfuasi wa Kristo ili kwamba aina ya mtu aliye sahihi kwake aweze kuvutiwa naye (Mithali 3:4-8). Mtu hudhihirisha tabia yake njema kwa tabia iliyo sahihi na uvaaji wenye heshima (1 Timotheo 2:9-10). Watu wanaofanya mambo ya uzembe na watu wa jinsia tofauti wanamaanisha kwamba wako tayari kuwa na mahusiano yenye msingi wake kwenye matamanio ya uovu (1 Wathesalonike 4:1-7). Mtu anayevaa katika njia inayosababisha matamanio ya uovu hutaka amshawishi mtu mwingine apate furaha naye ambayo haina ahadi (Mithali 7).
Mungu amewapa dhamana wazazi, wachungaji, na viongozi wengine wa Kikristo kutoa mwongozo katika tabia, mavazi, na chaguzi zinazohusiana na mahusiano. Vijana wanapojikabidhi kwa viongozi hawa katika kumtii Mungu, watakuwa na baraka tele za Mungu na watalindwa dhidi ya madhara mengi na majaribu.
► Wanafunzi wanapaswa wasome 1 Petro 5:5 na Waebrania 13:17 kwa ajili ya kikundi.
Ni jukumu la watoto na vijana kujikabidhi kwa ajili ya hekima na uongozi wa wazazi wao na mamlaka za kiroho. Ni wajibu wa hawa viongozi kuwasaidia vijana kuishi maisha ya ushindi dhidi ya majaribu.
► Wanafunzi wanapaswa wasome Warumi 13:14 na 1 Wakorintho 10:13 kwa ajili ya kikundi.
Mungu hapendi kuona na au haruhusu watu waliookoka wawe kwenye mazingira ya majaribu juu ya kiwango cha kiwango cha kushindwa kujizuia au kuepuka endapo wako tayari kufanya hivyo. Vijana wana wajibu wa kuyakimbia majaribu (2 Timotheo 2:22). Hata hivyo, wazazi wanapaswa wawazuie vijana wao katika kujihusisha na majaribu yasiyokuwa ya lazima kwa kadri itakavyowezekana. Kuna njia tatu ambazo wazazi hufanya haya:
1. Kwa kutoa maelekezo mahususi. Hii ni kuhusiana na yale ambayo watoto wanapaswa aidha wafanye au wasifanye, ni nani wawe naye, na waende wapi (Waefeso 6:1-4). Wazazi hawatakiwi kuwaruhusu watoto wao kuwa kwenye maeneo au hali ambazo ukomavu wao hautoshi kuwazuia dhidi ya majaribu. Kwa mfano, kijana na msichana watakuwa pamoja kwenye maeneo yaliyojificha au ya siri, kuna uwezekano mkubwa wakavutiwa kuingia kwenye tabia ya uovu.
2. Kwa kuwafanya watoto wao wawajibike wanapokuwa kwenye mazingira yenye majaribu. Wazazi wanapaswa waombe wakiwa kwa pamoja na vijana wao na wawaulize maswali kuhusiana na maisha yao. Matokeo mazuri ya uwajibikaji itategemea uimara wa uhusiano uliopo kati ya mzazi na mtoto. Kama mtoto hawezi kumwamini mzazi wake kwamba ni mwenye upendo, anayemkubali, na wa msaada kwake, mtoto hatataka kukiri kushindwa kwa jambo lolote.
3. Kwa kuwapa vijana ushauri wa kibiblia. Wazazi wanapaswa wawasaidie vijana wao wajifunze jinsi ya kutafakari mazingira kwa kutumia kanuni za kibiblia kwenye akili zao (Mithali 4:1-9, Mithali 7:1, 4-5). Wanapaswa wazungumze na vijana wao kuhusu hatari wanazokuwa wanaziona dhidi yao. Wanapaswa wawasaidie vijana wao katika kufanya maamuzi mbalimbali ambayo watataka kuyafanya. Wanaweza kuwasaidia vijana wao kutafakari mbele ya muda kuhusu ni jinsi gani wataweza kuepukana na majaribu na ni nini kifanyike wakati watakapokuwa katika majaribu.
Kanisa ni lazima lijitofautishe na utamaduni wao wakati linapokuwa linatetea maadili ya kibiblia. Tamaduni nyingi hazizingatii dhambi ya ngono kuwa ni jambo zito. Wanawategemea vijana ambao bado hawajaoa wawe katika mahusiano ya ngono kabla ya ndoa.
Kanisa kamwe halipaswi liwe na dhana kwamba dhambi ya ngono ni jambo la kawaida kwa vijana. Mungu anasema kwamba mwasherati hatakuwa na urithi katika ufalme wa Kristo (Waefeso 5:5).
► Je, ni kwa jinsi gani kanisa linaweza kusaidia vijana ambao wanapambana na majaribu ya dunia?
► Wanafunzi wanapaswa wasome Waefeso 5:3-7 na Waebrania 13:4 kwa ajili ya kikundi.
Kipindi cha muda ambao uhusiano unakuwa upo kabla ya ndoa (yaani uchumba) siyo kipindi ambacho mahusiano ya ngono yanapaswa kuanza. Badala yake, ni kipindi cha muda ambacho mwanamume na mwanamke wanahakikisha kwamba wanashirikishana vipaumbele vya kiroho na kibiblia. Ni muda ambao wanakuza ufahamu wa kila mmoja kumjua mwenzake kunakowasaidia kukuza kuaminiana kwa kila mmoja kiasi cha kuwawezesha kuingia kwenye ahadi ya kudumu kwa kila mmoja. Kama hawatakuwa na uwezo wa kufikia kila mmoja kuwa mwaminifu kwa tabia ya mwingine, watapaswa wasitishe huo uhusiano na siyo kuendelea kuoana.
Watu kwenye jamii nyingine huchelewesha ndoa kwa sababu katika tamaduni zao wanategemea ndoa iwe na uwigo mpana wa maandalizi na sherehe ya gharama. Mara nyingi, wenzi huishi kwa miaka mingi na wakawa na watoto huku wakiwa bado wanachelewesha kufanyika kwa ndoa. Kwa baadhi ya wenzi, gharama za harusi zinawaathiri kifedha kwa muda mrefu baadaye kwa sababu walitumia kila kitu walichokuwa nacho kwa ajili ya tukio la harusi na inawezekana hata wakaingia kwenye kukopa fedha. Kanisa linapaswa liwe ni jamii ya watu wenye imani ambao wanafanya aina nyingine ya harusi iliyo tofauti na hizo. Ndoa ya Kikristo ni kwa ajili ya mwanamume na mwanamke ambao kila mmoja amejikabidhi kwa mwenzake na kwa Mungu na hawapaswi kutegemea kutumia gharama kubwa ambazo zitachelewesha kufanyika kwa harusi au ambazo zitaumiza wanandoa hapo baadaye.
► Je, kuna njia gani ambazo ndoa ya Kikristo inapaswa iwe tofauti na ndoa za kitamaduni kwenye jamii?
Kuwafundisha Watoto Kusudi na Maagizo ya Mungu kuhusiana na Ngono
Watoto huwa wanaona na kusikia marejeo mengi kuhusu ngono. Wanasikia maoni mbalimbali kutoka kwa watu kuhusu ni lipi jema au baya. Watoto mwishowe huwa wanakuwa na hisia za ngono, matamanio, na majaribu, kwa hiyo ni muhimu sana kwa wazazi wa Kikristo kuwaeleza Mungu anasema nini kuhusu ngono. Watoto hawapaswi wajue undani kuhusiana na tendo la ngono, kwa sababu hawajakomaa ya kutosha kuweza kuolewa, na kwamba ujuzi wake utawafanya wapatwe na majaribu yasiyokuwa ya lazima.
Watoto wanahitajika wajue mpango wa Mungu na wajibu wao wa kumtii yeye. Wanahitajika wajue kwamba watajakutana na majaribu huko baadaye. Wanahitajika waandaliwe kumtii Mungu na kutawala matamanio yao wenyewe ya kufanya ngono hadi hapo watakapokuwa wameoa au kuolewa.
Fundisho linalofuata ni muhimu kwa ajili ya kufundishia watoto kuhusu mtazamo wa ngono bila ya kuzungumzia kwa undani na kwa kina kuhusu tendo la ndoa. Limeandikwa katika njia rahisi ya kueleweka, jinsi utakavyoweza kuzungumza na watoto.
Kuzungumza na mtoto
► Soma Mwanzo 2:7, 18-24 ukiwa na mtoto.
Kifungu hiki kinatueleza kwamba Mungu aliumba mwanamume wa kwanza na mwanamke wa kwanza na akaweka ndani yao uhusiano mahususi/wa kipekee.
Mungu aliitengeneza ndoa kama uhusiano maalumu kati ya mwanamume na mwanamke. Watu wawili waliooana wanakuwa na upendo maalumu kwa ajili ya kila mmoja. Sehemu ya uhusiano wao ni furaha maalumu wanayokuwa nayo wakati wanapokutanisha miili yao pamoja kwa siri katika tendo linaloitwa kujamiiana. Mungu aliitengeneza kujamiiana ili kumpa mume na mke furaha na wakati mwingi kumfanya mwanamke apate mtoto.
Kwa kuwa tendo la ndoa linaleta furaha maalumu, mwanamume na mwanamke wanakuwa na matamanio ya asili ya kuona na kuushika mwili wa mwingine na kila mmoja hufurahia usikivu wa mwenzake.
Ndani ya Biblia, Mungu anatuambia kwamba ngono ni nzuri na sahihi kwa ajili ya mume na mke. Lakini Mungu pia anatueleza kwamba ngono ni mbaya sana kwa watu ambao hawajawahi kuoa au kuolewa. Mungu ametupa maamrisho kuhusiana na tendo la ngono yumkini kwa sababu kuu nne:
(1) Furaha ya tendo la ndoa imetengenezwa kwa ajili ya ndoa.
Mungu ameifanya ngono kuwa sehemu maalumu ya uhusiano wa ndoa. Ingawaje inawezekana kwa kila mwanamume au mwanamke yeyote kuwa na furaha ya pamoja kwa njia hii, furaha hiyo ni ya kipekee zaidi katika ndoa, kwa sababu kila mtu amepewa mtu wake peke yake. Kwa watu ambao bado hawajawa katika ndoa, ngono haina maana hiyo, na hawawezi kuwa na uhusiano kamili ambao Mungu aliukusudia. Kwa hiyo, mtu ambaye bado ni mdogo sana kuweza kuolewa hapaswi kufanya tendo la kujamiiana. Watu hawapaswi kujamiiana hadi wawe wameweka ahadi ya ndoa na kufanya sherehe ya ndoa ya hadharani. Mtu anapaswa kufanya ngono na mwenzi wake tu.
(2) Tamaa za ngono zina nguvu sana.
Siyo kosa kuwa na matamanio ya kujamiiana, kwa sababu Mungu ndiye aliyeyaweka matamanio hayo. Lakini ni makosa kuongeza kwa makusudi matamanio ya kufanya jambo ambalo Mungu hapendi. Kwa sababu hiyo:
Isipokuwa tu katika ndoa, mtu hatakiwi kufanya mambo ambayo yatasababisha matamanio ya kujamiiana kuwa na nguvu zaidi, kama vile kwa makusudi kutazama au kufikiria mwili wa mtu mwingine kwa makusudi.
Isipokuwa tu katika ndoa, mtu hatakiwi kumgusa mtu mwingine kwa namna yeyote ile ambayo itaongeza hamu yake ya kutaka kufanya ngono.
Mtu hatakiwi kuchagua kuwa na fikra za kufanya mambo mabaya.
Mtu hatakiwi kuangalia picha au video ili kufurahia kuona watu wakifanya mambo mabaya.
Mtu hatakiwi kuvaa kwa njia ambayo itaweza kuwafanya watu wengine kutaka kufanya mambo mabaya au kujenga fikira za kufanya mambo mabaya.
Mtu hatakiwi kufanya au kuongea mambo ambayo yanaonekana kana kwamba anataka kufanya mambo mabaya.
(3) Matamanio yetu hayawezi kutuongoza sisi.
Wanyama wanadhibitiwa na hisia na matamanio yao. Sisi siyo wanyama; ni watu tulioumbwa kwa sura ya Mungu. Kwa sababu hiyo, ni lazima tufikirie kile tunachotakiwa kufanya, na hatimaye tufanye maamuzi sahihi. Hatupaswi tutawaliwe na hisia au na matamanio yetu. Wakati mwingine ni sawa kufanya kile tunachokitaka, wakati mwingine haipaswi iwe hivyo. Matamanio yetu hayawezi kutuambia ni lini ngono ni sahihi. Badala ya kuzitii hisia zetu, tunapaswa tufuate maelekezo ya Mungu kutoka katika Biblia kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
(4) Kujamiiana wakati mwingine husababisha kuwa na watoto.
Mungu amepanga kwamba watoto wapatikane kutoka katika mahusiano ya upendo. Amepanga kwamba watoto watahitaji miaka mingi ili wakulie katika familia ambayo inawapenda na kuwatunza. Mtoto mdogo ambaye mama na baba hawajaoana kwa kawaida huwa hana baba na mama kwa pamoja ili kumtunza hadi pale atakapokuwa mtu mzima.
Kwa kutambua hizi kweli nne zilizoorodheshwa hapa juu, watu ambao wanataka wampendeze Mungu na wawe na maisha bora watafuata maelekezo ya Mungu. Maelekezo hayo yatatengeneza tabia za uangalifu za kuwasaidia kupinga jaribio la kutokumtii Mungu.
Maombi kwa ajili ya Mtoto
Mpendwa Mungu,
Asante kwa kunifanya mimi niwe (mvulana au msichana). Asante kwa ajili ya mpango wako maalumu na mzuri kwa ajili ya ndoa. Naomba unisaidie kukupenda na kukutii wewe katika maisha yangu yote. Unaona kila kitu ninachokifanya, na unajua kila kitu ninachofikiria. Nakuomba unisaidie mimi ili siku zote niweze kutii maelekezo yako kwa maisha yangu yote. Ninachotaka mimi ni mawazo na matendo yangu yaweze kukupendeza wewe. Nisaidie ili na mimi niweze kuwasaidia marafiki zangu waweze kukutii wewe kwa kuwa kielelezo kizuri kwao. Kwa wakati unaofaa, ninapokuwa mtu mzima. Nisaidie kuwa (mume au mke) unayetaka mimi niwe. Nakupenda, Mungu!
Ameni
Maombi
Baba wa Mbinguni,
Asante kwa kutufanya sisi tuwe katika sura yako, ukiyapa maisha yetu kusudi na maana.
Asante kwa ajili ya kuunda jinsia ili kutusaidia sisi kuakisi sura yako.
Asante kwa ajili ya muundo wako mzuri na makusudi kwa ajili ya kujamiiana kwa wanadamu katika ndoa.
Tunatubu njia zetu ambazo kwazo tumeliasi Neno lako. Naomba utuoshe, utusamehe, na ututakase katika Jina la Yesu (1 Wakorintho 6:11). Utuweke huru kutoka katika utumwa wa dhambi (Warumi 6:6-7). Kwa sasa tunaikabidhi miili yetu kwako, tukijiachilia kabisa kufanya yale yaliyo mema na sahihi machoni pako (Warumi 6:13-14).
Tuwezesha sisi jinsi ya kujifunza tabia za kufikiri na mwenendo wa haki (1 Timotheo 4:7, Zaburi 23:3). Tunakusihi mawazo na matendo yetu yawe ya kukupendeza wewe machoni pako (Zaburi 19:14). Asante kwa ajili ya ahadi yako ya ushindi kwetu katika kila wakati wa majaribu (1 Wakorintho 10:13).
Ameni
Kazi za kufanya
(1) Soma Wagalatia 5:16-6:9 wakati ukiwa unatafakari mada zilizojadiliwa kwenye somo hili. Jibu maswali yafuatayo kwa kuandika:
Je, kuna tofauti gani kati ya matamanio ya mwili (5:16) na matendo ya mwili (5:19)?
Je, ni mambo gani mawili yaliyoahidiwa kwa wale wanaotenda matendo ya mwili (5:19-21, 6:7-8)?
Je, ni kwa jinsi gani mtu aliyeokoka/mwamini atakavyoweza kuwa na nguvu za kutotii matamanio ya mwili (5:16, 22-23, 25)?
Je, ni kweli zipi baadhi ambazo waumini wanapaswa kukumbuka wakati wa majaribu ambazo zitaweza kuwasaidia kushinda? (Taja angalao nne kutoka katika kifungu hiki).
Je, ni mambo gani ambayo watu waliookoka/waumini wameagizwa kufanya katika kifungu hiki? (Taja angalao nne kutoka katika kifungu hiki).
Je, ni nini wajibu wa watu waliookoka/waumini mmoja kwa mwingine (6:1-2, 6)?
(2) Soma Warumi 6:1-23. Jibu maswali yafuatayo:
Je, ni mambo gani ambayo kifungu hiki kinasema kwamba ni ya ukweli kuhusu kila mtu aliyeokoka/mwamini? (Orodhesha mambo 6-8)
Je, ni maamuzi gani ambayo watu waliookoka/waumini ni lazima wayafanye kwa ajili ya ukweli kwa sababu ya ukweli juu yao? (Orodhesha mambo 6-8)
Je, kwa nini mtu aliyeokoka/mwamini anatarajia kuwa mshindi kwenye majaribu ya kutenda dhambi? (Andika kifungu kimoja.)
(3) Soma Warumi 8:1-14. Andika maombi kulingana na kweli zilizoko katika kifungu hiki.
(4) Tafakari kwa kichwa Warumi 6:11-14 na Wakolosai 3:5-7. Mwanzoni mwa kuanza kwa kipindi cha darasa kinachofuata, andika au rudia kusema yale uliyokariri kutoka kichwani.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.