Fikria kwamba wewe ni mtu wa umri wa miaka 75 unayeishi katika taifa la watu wanaoabudu sanamu mara ghafla unasikia sauti ya Mungu ikiongea. Utajibuje?
Mungu akamwambia Ibrahimu, “Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;”[1] “Acha kila kitu na unifuate!” Mungu hakuwambia Ibrahimu aende wapi. Alisema tu, “nifuate.”
Ibrahim alimwamini Mungu na akamfuata kutoka nchi ya Uru hadi Harani, na kutoka Harani hadi Kaanani. Ibrahimu alitembea zaidi maili 1,000 kwa ajili ya kutii amri ya Mungu.
Ibrahimu aliziamini ahadi ambazo zilionekana kama ni jambo lisilowezekana kabisa. Aliamini kwamba Mungu atampa mtoto, ingawaje Sara alikuwa ameshapitiliza umri wake wa kuweza kupata mtoto. Aliamini kwamba Mungu ataenda kumpa nchi ya ahadi, ingawaje hakuwa na ardhi yeyote aliyokuwa ameimiliki katika nchi ya Kaanani. Aliamini kwamba Mungu atamfanya awe Taifa kubwa, ingawaje hakuwa na watoto.” Ibrahimu, mtu aliyetoka katika jamii ya kipagani, aliitwa rafiki wa Mungu.[3] Alitembea na Mungu.
► Waulize watu watatu katika darasa lako watoe ushuhuda wa jinsi walivyotembea na Mungu hadi sasa. Kutembea na Mungu kulianza lini? Umejifunza masomo gani wakati huo?
[2]Sala kwa ajili ya Utakatifu “Bwana, Ninaachilia mipango na makusudi yangu mwenyewe, Matamanio na mategemeo yangu yote, Na ninakubaliana na mapenzi yako kwa maisha yangu. Ninatoa kwako maisha yangu, na kila kinachohusiana nami kabisa navitoa kwako viwe vyako daima. Nijaze na unizingire kwa Roho wako Mtakatifu, Nitumie sawasawa na mapenzi yako, nitume popote unapotaka, Yatimize mapenzi yako yote ndani ya maisha yangu, kwa gharama yeyote, sasa na hata milele.”
- Betty Stam (Mfiadini China)
Utakatifu katika vitabu vitano vya kwanza vya biblia- Kutembea na Mungu
Watu watakatifu hutembea na Mungu; wanautumia muda wao na Mungu. Wanapokuwa wanatembea na Mungu, wanakua na kufana na yeye. Kuwa matakatifu ina maana ya kujenga uhusiano wa ndani sana na Mungu.
Mungu alitembea na Adamu na Hawa katika Bustani ya Eden. Baada ya dhambi kuvunja mahusiano wao na Mungu, Adamu na Hawa walijificha kutoka uso wa Mungu. Dhambi ikawatenganisha na Mungu.
Dhambi huvunja mahusiano na Mungu; huvunja mahusiano kati ya wanadamu; Adamu alimlaumu Hawa. Adamu na Hawa walishirikiana katika dhambi, lakini dhambi pia ikawaharibia mahusiano yao wenyewe. Malengo ya Mungu ni kwa watoto wake kutembea kwa amani pamoja naye na watu wengine. Malengo ya Shetani ni kuharibu mahusiano yetu na Mungu pamoja na watu wengine.
Dhambi iliharibu mahusiano kati ya Mungu na wanadamu, lakini Mungu alitafuta njia mbadala ya kurejesha uhusiano huo. Dhabihu zilitumika kudumisha mahusiano na Mungu mtakatifu. Hatuwezi kuwa watakatifu kwa juhudi za wanadamu; tunakuwa watakatifu kupitia mahusiano na Mungu mtakatifu.
Katika Agano la Kale lote, tunaona mifano halisi ya watu waliotembea na Mungu. Hawatembei tena na Mungu katika ile bustani nzuri. Kwa sababu ya dhambi, wanadamu sasa wanatembea na Mungu katika ulimwengu wa Dhambi wa giza. Lakini bado hata katika ulimwengu wa dhambi, inawezekana kutembea na Mungu. Huu ni utakatifu.
Kutembea na Mungu kunahitaji nidhamu-binafsi
Kutembea kwa ukaribu na Mungu kunahitaji nidhamu binafsi ya kuweza kusema hapana kwa matamanio ya dhambi. Kwenye nyakati za giza kabla ya Mafuriko, Henoko “alitembea na Mungu.”[1] Henoko alijiweka katika nidhamu mwenyewe ya kusema “Hapana” kwenye majaribu.
Henoko alizungukwa na majaribu yale yale kama majirani zake, lakini mahusiano yake na Mungu yalidhibiti mwitikio wake kwenye mambo ya dhambi. Watu wengine husema, “Raha hii ni nzuri sana, acha niifurahie.” Henoko alisema, “Raha hii inaonekana ni nzuri katika mwili, lakini inaonekana ni uovu kwa Mungu wangu. Sitajeruhi mahusiano yangu na Mungu kwa sababu ya tamaa za kimwili.”
“Hatupati” utakatifu kwa kuwa na nidhamu-binafsi. Ni kwa neema ya Mungu pekee inayotufanya tuwe watakatifu. Tumeokolewa kwa neema, na tunafanywa watakatifu kwa neema. Hata hivyo, haimaanishi kwamba nidhamu-bianafsi siyo muhimu.
Dallas Willard aliandika, “neema haipingwi na juhudi, neema hupingwa na tunavyopata.”[2] Kutembea kunahusisha juhudi, lakini hata juhudi hiyo huja kama matokeo ya neema ya Mungu. Juhudi zetu haziwezi kutupatia neema ya Mungu; juhudi zetu ni mwitikio wa furaha ya neemayake. Kama watoto wa Mungu hatuupati upendeleo wa Mungu kwa juhudi zetu wenyewe, bali tunatambua hitaji la nidhamu-binafsi.
Kutembea na Mungu kunahitaji utii
Mungu alimwita Ibrahhimu kwenda mahali ambapo hajawahi kupaona, “Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru...”[3] Ibrahimu alitembea na Mungu katika maisha ya utii. Maisha ya utakatifu ni moyo wenye kutii:
"Kwa Imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako."[4]
Mungu hakuwa amempa Ibrahimu ramani ya nchi ya Kaanani. Hakumpa Ibrahimu maelezo yeyote ya safari anayotakiwa kwenda. Alimtaka tu Ibrahimu aondoke-na akatii. Kutembea na Mungu kunahitaji utii. Maisha ya utakatifu yanahitaji utii.
Kutembea na Mungu kunahitaji Imani inayokua
Wakati Ibrahimu alipoondoka nyumbani hakukuwa na ushahidi wowote wa ahadi za Mungu. Ibrahimu alitembea na Mungu katika maisha ya utakatifu. Tunapokuwa tunatembea na Mungu, tunajifunza kumwamini kabisa. Imani yetu inaongezeka kila tunapoutumia muda wetu na yeye. Hii ilikuwa ni muhimu sana kwa Ibrahimu kwa sababu alikabiliwa na jaribu kubwa zito kuliko lile la kuondoka nyumbani kwake.
Akiwa kule Kaanani, Mungu alimwita Ibrahimu na kumtaka amtoe mwanae Isaka awe dhabihu. Mungu alishamwahidi Ibrahimu kwamba atamfanya awe baba wa mataifa yote. Baada ya miaka mingi, Ibrahimu na Sara wakapata mtoto. Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake awe dhabihu ya kuteketezwa. Mwandishi wa Waebrania anasema, “Kwa Imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu.”[6]
Kwa kuwa Ibrahimu alitembea na Mungu, alimtegemea Mungu. Ibrahimu alikuwa akitembea na Mungu, kwa hiyo aliweza kumwamini Mungu hata pale alipokuwa hajaelewa kwa ukamilifu maagizo ya Mungu. Ibrahimu alitembea na Mungu katika mahusiano ya kukua kwa imani yake.
Kutembea na Mungu kunahitaji kwamba tumwamini yeye. Tunapotembea na Yesu, tunamwamini yeye hata pale tunapokuwa katika maeneo magumu. Tunamruhusu Mungu afanye lile analoliona kwamba ni jema katika maisha yetu.
Kanuni hii inaonekana katika maandiko yote. Katika majaribu yasiyofikirika, Ayubu alijifunza kwamba anaweza kumwamini Mungu. Akiwa uhamishoni, Yeremia alileta ahadi za Mungu za kuleta mema katika maeneo ya mateso makali.[7] Akiwa kwenye maumivu makali yaliyofanyika miiba kwenye mwili wake, Paulo anajifunza neema ya Mungu, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.”[8]
Historia ya Ibrahimu na taarifa za watu wengine wa Mungu kupitia historia zao zinatufundisha kwamba kutembea na Mungu kunahusisha utii kamili katika maagizo yake na uaminifu kabisa katika amri zake. Kadri tunavyotembea naye, imani yetu kwake inakua zaidi.
Kutembea na Mungu ni mahusiano yaliyojitenga
Sura ya kutembea ni ya kawaida sana katika maandiko. Kwa masikitiko, Israeli mara nyingi ilitembea na dhambi badala ya kutembea na Mungu. Wafalme wengi wa Israeli “walitembea katika dhambi.” Walijenga mahusiano na dhambi. “Abiya alifanya dhambi zote ambazo baba yake alifanya kabla yake.”[9] Wafalme wengine “walitembea katika njia za baba” zao kuliko kutembea na Mungu. Walijenga mahusiano na dhambi; hawakutembea na Mungu.
Kutembea na Mungu ni mahusiano yaliyojitenga. Mungu ni Mungu mwenye wivu.[11] Huwezi kutembea kwa wakati mmoja na Mungu na wakati huohuo na dhambi. Mtunga Zaburi aliuliza, “Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?” Ni nini mahitaji ya kuishi katika uwepo wa Mungu?
"Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake."[12]
Malaki sema, “Mmemchokesha Bwana kwa maneno yenu,” Waisraeli wakauliza, “Tumemchokesha kwa maneno gani?” Malaki akajibu, “Kwa kuwa mwasema, Kila atendaye mabaya ni mwema machoni pa Bwana, naye huwafurahia watu hao,”[13] Wana wa Israeli walitaka kuwa marafiki wa Mungu wakati wakiwa wanaendeleana dhambi za makusudi. Badala yake Malaki aliwaonya kwamba siku ya hukumu inakuja, inawaka kama tanuru. Katika siku hiyo, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi.[14] Mungu mtakatifu hawezi kuacha kushughulikia dhambi.
Mungu aliwashutumu wana wa Israeli kwa kutenda dhambi za mataifa badala ya kuishi maisha ya utii kwa amri za Mungu, “kwa maana hamuendi katika amri zangu, wala hamkuzishika hukumu zangu, bali mmetenda mambo kama hukumu za mataifa wanaowazunguka.”[15] Wana wa Israeli hawakuweza kutembea na Mungu wakati walikuwa wanatembea katika dhambi. Wana wa Israeli hawakuweza kutembea katika njia za Bwana na wakati huo huo katika njia za dhambi. Ingawaje walikuwa ni taifa lililokuwa limeteuliwa na Mungu, Mungu aliwaadhibu kwa dhambi zao. Haingewezekana kutembea na Mungu na huku wanatembea na dhambi.
Utakatifu katika matendo: Kutembea na Mungu ni mahusiano endelevu
Tunapokuwa tunatembea na Mungu, tunakua katika mahusiano yetu na yeye. Katika Kumbukumbu la Torati 6, Musa alitoa picha ya nini maana ya kutembea na Mungu. Alisema kwamba watu wa Israeli wanapaswa kuwafundisha watoto wao sheria. Ni Wakati gani? Wakati wote:
"Nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo."[1]
Mtu anayetembea na Mungu anadumisha uhusiano usiokatika kati yake na Mungu. Hakuna tofauti kati ya “maisha ya kawaida” na “maisha ya kanisani”. Watu watakatifu siyo “Wakristo wa Jumapili tu” ambao wanamtumika Mungu wawapo kanisani tu. Watu watakatifu hutamani kuwa na mahusiano na Mungu yanayoendelea na yanayokua.
Wakati wana wa Israeli waliposhindwa kutunza ukuaji wa kila siku wa mahusiano yao na Mungu, waligeukia kwenye miungu mingine. Wakati mfalme Sulemani alipofanya uzembe katika mahusiano yake na Mungu, alijikuta amevutwa kwenye miungu ya uongo ya wake zake.
Hata Kanisa la mwanzo lilikutana na hatari hii. Kanisa la Efeso lilianzishwa na Paulo kwa uamsho wa kuvutia sana. Mtume Yohana alitumika kama mchungaji wao kwa muda. Mariamu, mama wa Yesu, aliishi Efeso. Walikuwa watu waliotangulia kupata ufahamu wa ukweli kuhusu Injili. Lakini katika kizazi kimoja tu, Yohana akaja na onyo hili:
"Nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza."[2]
Ni nini kilichotokea? Kwa sababu walishindwa kutunza hisia zao za upendo wa zamani, na kwa sababu walishindwa kuendelea kukua katika mahusiano yao na Mungu, upendo wao ukawa baridi.
Tunayaona haya katika mahusiano ya wanadamu. Je, unaweza kumfikiria mwanamume aliyemwoa mwanamke mzuri sana, anatundika cheti cha ndoa ukutani, lakini hana muda wa kushirikana naye? Je, ndoa yao hii ina afya? Hapana! Inachukua zaidi ya kuwa na cheti cha ndoa ili kuijenga ndoa yenye afya. Ndoa yenye afya hukua hatua kwa hatua kwa miaka wakati watu hawa wawili wakiendelea kukua katika upendo na mwenzake.
Kwa njia hiyo hiyo, tunaitwa tuendelee kukua katika upendo kwa ajili ya Mungu. Kutembea na Mungu ina maana ya kuendelea kuutumia muda pamoja na yeye. Kutembea na Mungu ina maana yakuendelea kukua katika mahusiano na yeye. Hii ndiyo maana ya kuwa mtakatifu.
Kutembea ni kitendo endelevu. Kinaashiria uhusiano unaoendelea na kukua. Mtu mtakatifu anaendelea kukua katika mahusiano yake na Mungu. Kipindi cha kujisalimisha kwa Yesu siyo mwisho wa njia. Maisha ya utakatifu yanahusisha kuendelea kutembea na Mungu. Kutembea kwetu na Mungu kunaanzia pale tunapozaliwa na kuendelea mpaka kumwona Mungu uso kwa oso. Maisha ya utakatifu ni mahusiano endelevu.
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwamba maisha ya kiroho yanategemea kabisa kudumisha mahusiano na yeye mwenyewe:
"Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote."[3]
Baadhi ya Wakristo huufikiria uhusiano wao na Mungu kama “Sala ya mwenye dhambi” ikifuatiwa na maisha yaliyobadilishwa kidogo sana. Picha ya Kibiblia ya mahusiano na Mungu iko tofauti. Maisha ya Kikristo yameunganishwa na mzabibu.[4] Maisha yetu ya kiroho yameimarishwa kupitia mahusiano yetu ya kila siku na mzabibu. Ikimaanisha kwamba, tawi lililotenganishwa na mzabibu halichukui muda kufa. Mkristo aliyetenganishwa na mzabibu hufa haraka sana.
Kutembea na Mungu kunatuhitaji tutumie muda wetu na yeye. Haiwezekani ukatembea na mtu ambaye hujatumia muda na yeye. Watakatifu hutumia muda wao na Mungu. Mara nyingine wanasalimisha nafasi za biashara na starehe ili tu waweze kuutumia muda wao na Mungu. Wanaelewa kwamba hakuna jambo la muhimu kama mahusiano yao na Mungu. Kama Mariamu alivyoketi kwenye miguu ya Yesu, kadhalika watu watakatifu wanajua kwamba “jambo moja muhimu” ni muda wao pamoja na Mungu.[5]
Watu watakatifu huupa kipaumbele muda wao na Mungu. Wanajua kwamba maombi na maandiko ni muhimu sana kuliko shughuli nyingine zozote-hata kuliko huduma. Hukumbuka kwamba Yesu mara nyingi “alikuwa akiamka mapema sana” kwa ajili ya kumuomba Baba yake, kwa hiyo walijenga tabia ya kutumia muda wao ili kuwa naye katika maombi.
Watu watakatifu wanaelewa kwamba kutembea na Mungu inamaanisha kufuata maelekezo. Wako makini na uongozi wake. Hawaulizi tu kwamba, “Je, shughuli hii ni dhambi?” bali wanauliza “Je, jambo hili litanisogeza karibu na Mungu?” Wanataka wampendezeshe Mungu katika kila uamuzi, kwa sababu wana mioyo mitakatifu na wako makini kuwa mbali na dhambi. Wanaelewa kwamba kuwa na mahusiano na Mungu kunahitaji kutenganishwa na chochote cha kumchukiza yeye.
► Ni njia gani za kivitendozinazohitajika kukuza uhusiano wa ndani na Mzabibu?
► Kuna changamoto tatu zinazozuia mahusiano yetu na Mungu. Ni zipi?
Baba yake na Frances Havergal[1] (1836-1879) alikuwa mtumishi katika Kanisa la Uingereza.[2] Akiwa na umri wa miaka 14, Frances aliyatoa maisha yake kwa Kristo. Katika maisha yake yote, Frances aliwekeza nia ya kutembea karibu na Yesu. Aliandika, “Oh, nifanye niwe chombo kilichotakaswa na kilicho tayari kutumiwa na Bwana! Kuna nyakati nyingine ninausikia sana upendo kwa ajili yake kwamba sina maneno ya kuweza kuulezea… lakini bado nahitaji kuwa karibu. Siyo tu kuijua Imani, lakini kuwa pamoja naye ndiyo itakalowezesha hili.” Kwa kutembea na Mungu, alikuwa karibu sana na yeye.
Mwaka 1873, Havergal alishuhudia kwamba “ametakaswa na dhambi zake zote na kufanywa mtakatifu kutokana na utakaso endelevu wa Roho wa Mungu.” Hakuna kilichoweza kumzuia katika kutembea kwake na Mungu. Maombi yake ya kujitoa kwa ajili ya Mungu ndio ukawa wimbo wake, “Chukua maisha yangu na uniweke wakfu Bwana, kwa ajili yako wewe.”
Havergal alisalimisha kila kitu kwa Mungu. Hii ndio maana ya kutembea na Mungu. Ni kuwa karibu sana na yeye kiasi kwamba kila kitu ni mali yake. Baada ya kitambo kirefu cha maisha ya kutembea na Mungu, maneno ya mwisho ya Harvegal yalikuwa, “Uzuri, utukufu wa kuwa karibu na malango ya mbinguni! Pumziko la Baraka!” Kaka yake aliandika kwamba uso wake, “ulikuwa na furaha sana, kana kwamba alikuwa anazungumza na yeye (Yesu).”
Dada Havergal alitembea na Mungu; alikuwa mtu mtakatifu. Kutembea na Mungu siyo kwa watu walioishi katika nyakati za Biblia tu. Unaweza kutembea na Yesu leo; unaweza kuwa mtakatifu.
[1] Image: "Frances Ridley Havergal", Christmas Sunshine with Love and Light for the New Year (1886), retrieved from https://commons.wikimedia.org/wiki/File:Frances_Ridley_Havergal.jpg, public domain.
[2] Kisa hiki cha Frances Havergal kimenukuliwa kutoka Wesley L. Duewel, Heroes of the Holy Life (Grand Rapids: Zondervan, 2002), 80-89.
Tafakuri ya Somo la 2
(1) Kuwa mtakatifu ina maana ya kudumisha mahusiano na Mungu. Utakatifu ni kutembea na Mungu.
(2) Kutembea na Mungu kunahitaji nidhamu ya kibinafsi ya kusema “hapana: kwa ajili ya tamaa mbaya.
(3) Nidhamu ya binafsi haikatai nguvu ya neema. Tunaokolewa kwa neema, tunafanywa watakatifu kwa neema.
(4) Kutembea na Mungu kunahitaji uaminifu kamili katika amri za Mungu. Hatuwezi kutembea na Mungu pamoja dhambi kwa wakati mmoja.
(5) Kutembea na Mungu kunahitaji utii kamili kwenye ahadi za Mungu.
(6) Kutembea na Mungu inamaanisha kujenga uthabiti wa kila siku wa mahusiano na Mungu.
(7) Maisha ya utakatifu yanahitaji mahusiano ya kila siku na mzabibu. Maisha yetu ya kiroho yanategemea kabisa uhusiano wetu na Mungu.
Kazi ya Kufanya
(1) Fikiria kwamba Mwamini mpya Mkristo anakuambia, “Nataka niwe na mahusiano ya ndani sana na Mungu. Nampenda Mungu, lakini ni vigumu kwangu kukua kwenye mahusiano na yeye. Siwezi kumwona Mungu kwa sababu inaonekana anakaa mbali sana. Nifanye nini?" Andika ukurasa mmoja juu ya jinsi utakavyoweza kumsaidia huyu mwamini mpya kuelewa jinsi ya kukua katika mahusiano yake na Mungu. Kwenye kipindi cha darasa kinachofuata, kila mwanafunzi asome majibu yake na kuwepo na muda wakuyajadili haya majibu.
(2) Anza kikao kinachofuata cha darasa kwa kunukuu 1 Yohana 1:6-7.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.