Petro: Jiwe Lililokuwa Kikwazo na Likaja Kufanyika Mwamba
Yesu aliwauliza wanafunzi wake, “Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?” Petro alijibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Yesu akajibu akamwambia, “Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”[1] Hii ilikuwa ni moja ya siku zilizowahi kung’ara sana katika maisha ya Petro.
Muda mfupi baadaye, Yesu akawaambia wanafunzi wake kwamba atakufa huko Yerusalemu. Wakati Petro alipoanza kumkemea Yesu, alimjibu akamwambia, “Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu.”[2] Neno “kikwazo” lina maana ya “jiwe lililo kizuizi.” Kwa mara ya kwanza Yesu alimwita Petro “mwamba,” lakini mara hii anamwita “jiwe lililo kizuizi.” Hakuna wakati ambao Petro aliwahi kujikuta yuko gizani katika maisha yake kama siku hii.[3]
Kisa cha Petro kinazidi kumweka gizani zaidi siku ambayo Yesu alikuja kukamatwa usiku. Baada ya kuwa ameahidi kwamba hatamwacha Bwana wake, Petro alimkana Bwana wake na kukimbia kwa ajili ya hofu. “Mwamba” ulishindwa wakati wa saa ya majaribu.
Baada ya anguko hilo, mtu anayesoma vitabu vya Injli anaweza akahisi kwamba Petro hatakaa aweze kuchukua jukumu lolote la Kanisa. Kwa mshangao wetu, Petro anakuwa kiongozi katika kanisa la mwanzo. Ni nini kilicholeta hata hayo mabadiliko ya ghafla na haraka kiasi hicho? Jibu ni Pentekoste.
Baada ya kufufuka kwake, Yesu alitoa ahadi hii kwa wanafunzi wake, “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”[4] Ahadi hii ilitimia katika kitabu cha Matendo 2. Wanafunzi wakajazwa nguu za Roho Mtakatifu wakaanza kuhubiri. Kupitia nguvu za Roho Mtakatifu, zaidi ya watu 3000 waliamini katika Pentekoste ya kwanza.
Petro alibadilishwa na nguvu ya Pentekoste. “Jiwe lililokuwa kizuizi” limegeuka kuwa “Mwamba” ambaye aliliongoza Kanisa katika nyakati zake muhimu sana za mwanzo. Simoni Petro alihubiri kwenye eneo lote la Dola ya Kirumi, aliandika barua mbili za Agano Jipya, na hatimaye alisulubiwa kwa sababu ya imani yake.
Ni nini kilileta mabadiliko haya? Kupitia uwezo wa kubadilisha wa Roho Mtakatifu, mtu mmoja mvuvi Mgalilaya akawa kiongozi katika karne ya kwanza. Petro alijifunza kwamba kuwa mtakatifu inamaanisha kuishi ndani ya ukamilifu wote wa Roho Mtakatifu.
► Waombe wanafunzi wako watoe ushuhuda wa jinsi gani Roho Mtakatifu ameweza kuleta mabadiliko katika maisha yao. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu anakupa nguvu kwa ajili ya huduma, ushindi dhidi ya maovu, na furaha katika maisha yako ya Ukristo?
Petro hakuwa mwanafunzi peke yake aliyebadilishwa wakati wa Pentekoste. Kila mwanafunzi alibadilishwa na Roho Mtakatifu. Hata Thomaso wa mashaka alifanyika kuwa mmishenari mwaminifu sana. “Mwana wa ngurumo” akawa “Mtume wa Upendo.” Wafuasi wa Yesu walibadilishwa kutoka wanafunzi wenye hofu hadi kuwa jeshi lenye nguvu kwa ajili ya Injili. Kitabu cha Matendo kinaonyesha matokeo ya Roho Mtakatifu dhidi ya hawa waamini wa kwanza. Kanisa la kwanza lilikuwa na ufanisi sana siyo kwa sababu ya karama zisizokuwa za kawaida za mitume, bali ni kwa sababu ya karama zisizokuwa za kawaida za Roho Mtakatifu. Wanafunzi walijifunza kwamba maisha matakatifu yako ndani ya ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
Ahadi Iliyoahidiwa ya Roho Mtakatifu
Kwa hakika, hili lilikuwa ni jambo moja la kushangaza sana ambalo wanafunzi walikuwa hawajawahi kulisikia kutoka kwa Yesu: “Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke.”[1] Hawa wanafunzi walikuwa wameacha vyote wakamfuata Yesu. Hebu fikiria mshtuko wao wakati Yesu aliposema, “Kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.”
Kwenye Chakula cha Mwisho, Yesu alielezea jinsi Roho Mtakatifu atakavyowahudumia waamini. Roho Mtakatifu:
Atakuwa Msaidizi (Yohana 14:16-17)
Atakuwa Mwalimu (Yohana 14:26)
Atakuwa shuhuda wa Mwana (Yohana 15:26)
Atauthibitishia ulimwengu (Yohana 16:7-11)
Atasema kweli yote (Yohana 16:13-15)
Baada ya kufufuka, Yesu alirudia ahadi yake ya kutuma Roho Mtakatifu:
"Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, 'ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache… Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.'"[2]
Huduma ya Yesu hapa duniani haikuishia tu msalabani, au kwenye kaburi, au hata kwenye kupaa kwake mbinguni. Huduma ya Yesu ilikamilishwa wakati wa Pentekoste. Alama ya utambulisho wa huduma ya Yesu ilikuwa kwamba, “atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.”[3] Karama za Roho Mtakatifu zilikuwa ni kilele cha huduma ya Yesu hapa duniani.
Kupokelewa kwa Roho Mtakatifu
Kwenye kitabu cha Matendo, Roho amelipa nguvu Kanisa kwa ajili ya huduma. Wakati wa Pentekoste, ahadi ya kupelekewa Msaidizi ilitimia. Baada ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliendelea kuwepo katika kanisa. Alama zilizoambatana na ujio wa Roho Mtakatifu zilithibitisha huduma yake kwa waamini.
Kwanza, “kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu.”[4] Hii inaonyesha ujio wa nguvu ya Roho Mtakatifu. Katika Matendo, tunaona nguvu za Roho Mtakatifu zikitenda kazi kupitia kwa waamini. Baada ya Pentekoste, kanisa lilihudumu kwa nguvu mpya na ufanisi mkubwa. Roho Mtakatifu amekuwa akitenda kazi duniani hata kabla ya Pentekoste.[5] Lakini baada ya Pentekoste, nguvu ya Roho imekuwepo wakati wote katika huduma za kanisa.
Pili, “kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja.”[6] Katika maandiko, siku zote moto unawakilisha usafi. Alama ya Roho Mtakatifu ilikuwa usafi wa moyo. Petro alitoa ushuhuda wake kwenye Baraza la Yerusalemu kuhusu kazi ya Mungu miongoni mwa Mataifa:
"Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi, wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa Imani."[7]
Tatu, wale waliokuwa katika chumba cha juu “wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.”[8] Hii iliwawezesha wanafunzi kushuhudia kwenye mataifa yote. Kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu, wanafunzi waliweza kutekeleza Agizo Kuu la Kristo. Katika Babeli, Mungu aliihukumu dhambi yao kwa kuwachanganya katika lugha zao wasiweze kuelewana. Wakati wa Pentekoste, Mungu aliruhusu kila msikiaji kuisikia injili “katika lugha yake mwenyewe.” Wakati wa Pentekoste, Mungu alianza kugeuza mtawanyiko wa athari za dhambi lugha zilizojitokeza wakati wa Pentekoste ziliwakilisha ahadi ya Mungu kwamba Injili itawafikia watu wa mataifa yote kupitia nguvu za Roho mtakatifu afanyaye kazi kupitia Kanisa.
Wakati wa Pentekoste, mwishowe wanafunzi walikuja kutambua kile Yesu alichokuwa amemaanisha aliposema, “Yawafaa ninyi mimi niondoke.” Roho Mtakatifu hakuwa mbadala wa “pili bora” kwa Yesu Kristo. Wakati Yesu aliyefanyika mwili asingeweza kuwa mahali popote kwa wakati mmoja tu, Roho Mtakatifu yuko mahali popote kwa wakati mmoja. Roho Mtakatifu aliwawezesha wanafunzi kutekeleza Agizo Kuu la Yesu. Roho Mtakatifu huwawezesha Wakristo kuishi maisha matakatifu yanayoweza kuwa ushuhuda kwa ulimwengu wote.
Utakatifu katika kanisa la mwanzo: Maisha katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu
Kitabu cha Matendo kinaonyesha kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya kila mwamini. Kwa sababu ya nguvu ya Roho Mtakatifu, Wakristo walikuwa na nguvu ya kushuhudia,[9] ujasiri mbele ya upinzani,[10] ushindi dhidi ya dhambi za kujitakia,[11] na karama za roho kwa ajili ya huduma.[12] Waamini wa mwanzo walikuwa watakatifu kwa sababu waliishi katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
Kitabu cha Matendo kinaonyesha kanisa la mwanzo likitimiza wito wa Yesu wa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi, wito wake wa “mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu,” na ahadi yake kwamba “kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo (wewe) utafanya.” Hii ilifanyika kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Kitabu cha Matendo kinaonyesha uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha ya waamini hawa wa mwanzo.
Nguvu kwa ajili ya Huduma
Kama vile Yesu alivyokuwa “amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alipokabiliana na Shetani,[13] Petro alikuwa “amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alipokabiliana na mamlaka za Kiyahudi.[14] Luka anaelezea maisha ya Petro kwa maneno yale yale aliyotumia kuelezea maisha ya Yesu. Kazi ya Roho Mtakatifu inayoonekana katika maisha ya Yesu Kristo duniani yalikuwa sasa ni heshima kwa waamini wote.
Katika siku ya Pentekoste, waamini zaidi waliongezeka kwenye kanisa kuliko wakati mwingine wowote wa huduma ya Yesu hapa duniani. Kupitia Nguvu ya Roho Mtakatifu, mitume walihudumu kwa nguvu na mamlaka. Miujiza ya uponyaji ilidhihirisha nguvu za Mungu kwa ulimwengu usioamini. Watu walikuwa “wamejazwa kwa mshangao na kustajaabu,” na watu wote “wakawakusanyikia.”[15] Kwa jinsi mitume walivyokuwa wakihudumu katika ukamilifu wa Nguvu ya Roho Mtakatifu, huduma zao zilionekana kujaa nguvu ya kimungu. Kupitia Nguvu ya Roho Mtakatifu, mitume waliweza kutekeleza Agizo la Yesu la “kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi.”[16]
Ujasiri wa Kiroho
Wanafunzi walikuwa wajasiri katika kutangaza Injili
Nguvu ya kubadilisha ya Roho Mtakatifu inaonekana wazi katika kitabu chote cha Matendo ya mitume. Mitume ambao kwa miezi michache iliyopita walikuwa wamekimbia katika tukio la kukamatwa kwa Yesu, sasa wanahubiri kwa ujasiri mkubwa.
Muda mfupi baada ya Pentekoste, wakuu wa dini waliwakamata Petro na Yohana. Ni wiki chache tu zimepita, Petro alikuwa amemkana Kristo. Sasa, “Petro, akiwa amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alihubiri kwa ujasiri mkubwa. Wakuu wa dini “walishangaa” kwa maneno ya hawa “watu wa kawaida ambao walikuwa hawana elimu yeyote.”[18]
Kupitia ujazo wa Roho Mtakatifu, mitume walikuwa wajasiri katika kuhubiri kwa nguvu na upako. Kutoka kundi la watu waoga, wavuvi, watoza ushuru, na wafanyakazi wa kawaida, wanafunzi sasa wamekuwa ni watu ambao “wameupindua ulimwengu.”[19]
Wanafunzi walikuwa wajasiri mbele ya mateso
Walipokabiliwa na upinzani, mitume hawakuomba kwa ajili ya kuachiwa kutoka kwenye mateso, bali kwa ajili ya ujasiri wa kumhubiri Kristo bila kujali mateso. “Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote…” Mungu alijibu maombi yao. “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”[20]
Alama isiyokuwa na dosari yeyote ya kazi ya Roho Mtakatfu kwa kanisa ilikuwa ni ile ya ujasiri wa kuitangaza Injili mbele ya upinzani. Hadi mwisho wa karne ya kwanza, Injili ilikuwa imeenea kutoka watu 120 kutokea chumba cha juu hadi kwenye majiji yote ya Dola ya Kirumi.
Maisha ya Ushindi
Katika kila kizazi, Wakristo wamekabiliwa na jaribu la kuwa ”Wakristo wa Jumapili,” – watu ambao wanahudhuria makanisani lakini maisha yao hayaonyeshi mabadiliko ya ndani na mwisho unaoeleweka. Kanisa la mwanzo lilibadilika katika kila eneo la maisha kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu.
Katika Agano la Kale, tunaona juhudi za watu waliotaka kushikamana na agano, lakini wakijikuta hawawezi kufanya hivyo kwa sababu mioyo yao ilikuwa imegawanyika. Mtunga Zaburi aliwaelezea watu wa Israeli kwamba: “Mioyo yao haikuwa thabiti kwake. Wala hawakuwa waaminifu katika Agano lake.” [21]
Kupitia Ezekieli, Mungu aliahidi siku ambayo watu wake wangebadilishwa.
"Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda."[22]
Kabla ya Pentekoste, mitume walifuata mwelekeo uliokuwa unafanana na ule wa wana wa Israeli. Walikuwa wanataka kumfuata Kristo, lakini wakishindwa siku zote. Walikuwa na mashaka; walipigania nafasi; walikimbia kwa hofu. Wakati wa Pentekoste, ahadi ya Ezekieli ilitimia. Mitume walipewa uwezo na Roho Mtakatifu wa kuishi maisha ya ushindi. Badala ya kuwa na moyo wenye kutii nusu nusu, walitembea katika kutii kwa furaha sheria ya Mungu. Kupitia Roho Mtakatifu, maisha ya ushindi yakawa ni jambo la kawaida kwa watu wa Mungu.
Mwongozo wa Huduma
Kabla ya Pentekoste, tamaa na hofu vilitawala maisha ya mitume. Juhudi zao za kumtumikia Yesu zilikwamishwa na kushindwa kwao wenyewe. Baada ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwaongoza mitume kwenye huduma zilizokuwa na ufanisi.
Roho Mtakatifu aliliongoza Kanisa katika maamuzi magumu yaliyoathiri mahusiano kati ya Wayahudi na mataifa waliogeukia Ukristo.[23] Roho Mtakatifu aliongoza uchaguzi wa viongozi wa Kanisa.[24] Roho Mtakatifu alimwongoza Paulo katika safari yake ya Makedonia.[25] Roho Mtakatifu alimwongoza Paulo katika safari yake ya kurejea Yerusalemu mbali na hatari iliyokuweko ya kukamatwa.[26]
Huduma za kanisa la mwanzo ziliongozwa na Roho Mtakatifu.
Umoja
Labda ushahidi muhimu sana unaoweza kukumbukwa wa kazi za Roho Mtakatifu kwa Kanisa la mwanzo ni umoja miongoni mwa waamini wake. Katika maombi yake ya Mchungaji Mkuu pale mlimani, Yesu aliombea umoja wa Kanisa. Aliomba:
"…ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi." [27]
Ombi la Yesu lilijibiwa wakati wa Pentekoste. Matendo 2:42 inaonyesha umoja huu katika maisha ya Kanisa: uwajibikaji katika mafundisho ya mitume, ushirika, usherehekeaji wa Chakula cha Meza ya Bwana, na maombi. Ushirika huu ulionekana kwa kanisa kuwajibika kwa mtu na mtu mwingine. Luka alitoa ushahidi kwamba, “Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji;” kwa sababu Wakristo walijali mahitaji ya kila mmoja wao.[28]
Mara sita, Luka anatumia neno “kwa moyo mmoja” kuelezea umoja wa Kanisa. Hii haimaanishi kwamba Wakristo walikubaliana kwa kila jambo. Masuala magumu yalitishia kuligawa Kanisa. Wayahudi na mataifa waliogeukia Ukristo hawakukubaliana kuhusu Sheria za Musa![29] Paulo na Barnaba hawakukubaliana kuhusiana na Yohana Marko. [30]
Lakini pamoja na tofauti zao, Kanisa liliunganishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Jinsi waamini walivyofuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, Kanisa lilifungwa pamoja “kwa moyo mmoja.”
Kama mimi na wewe tungeweza kuwaona wale mitume siku chache kabla ya Yesu kukamatwa, kamwe tusingeweza kufikiria kama watu hawa wangeweza kuja kuwa na ufanisi mkubwa kiasi hicho katika huduma. Walikuwa na hofu, wivu wa wenyewe kwa wenyewe, na wenye mashaka yaliyopitiliza. Miezi michache baadaye, watu hawa wamebadilika kabisa. Ni nini kilichotokea?
Kabla ya Pentekoste, Mitume walijaribu kuishi maisha yanayomfanania Kristo kwa nguvu zao wenyewe, na mara kwa mara walishindwa. Baada ya Pentekoste, mitume waliishi chini ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Hii ndiyo siri ya maisha ya utakatifu na huduma yenye ufanisi.
[5] Mifano ya kazi za Roho Mtakatifu katika Agano la Kale: Mwanzo 1:2; Mwanzo 6:3; Kutoka 31:3; Hesabu 11:25-29; Waamuzi 3:10; 6:34; 13:25; 1 Samweli 10:6-10; 2 Mambo ya Nyakati 28:12; Nehemia 9:20; Isaya 63:10-14; Zakaria 4:6-9.
[17]“Hatujazwi Nguvu ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kufanya kazi yeyote maalumu, lakini tu ni kumruhusu Mungu afanye kazi kupitia sisi.”
- Oswald Chambers
Utakatifu katika kanisa la mwanzo: Maisha katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu
Kitabu cha Matendo kinaonyesha kazi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya kila mwamini. Kwa sababu ya nguvu ya Roho Mtakatifu, Wakristo walikuwa na nguvu ya kushuhudia,[1] ujasiri mbele ya upinzani,[2] ushindi dhidi ya dhambi za kujitakia,[3] na karama za roho kwa ajili ya huduma.[4] Waamini wa mwanzo walikuwa watakatifu kwa sababu waliishi katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
Kitabu cha Matendo kinaonyesha kanisa la mwanzo likitimiza wito wa Yesu wa kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi, wito wake wa “mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu,” na ahadi yake kwamba “kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo (wewe) utafanya.” Hii ilifanyika kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Kitabu cha Matendo kinaonyesha uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha ya waamini hawa wa mwanzo.
Nguvu kwa ajili ya Huduma
Kama vile Yesu alivyokuwa “amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alipokabiliana na Shetani,[5] Petro alikuwa “amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alipokabiliana na mamlaka za Kiyahudi.[6] Luka anaelezea maisha ya Petro kwa maneno yale yale aliyotumia kuelezea maisha ya Yesu. Kazi ya Roho Mtakatifu inayoonekana katika maisha ya Yesu Kristo duniani yalikuwa sasa ni heshima kwa waamini wote.
Katika siku ya Pentekoste, waamini zaidi waliongezeka kwenye kanisa kuliko wakati mwingine wowote wa huduma ya Yesu hapa duniani. Kupitia Nguvu ya Roho Mtakatifu, mitume walihudumu kwa nguvu na mamlaka. Miujiza ya uponyaji ilidhihirisha nguvu za Mungu kwa ulimwengu usioamini. Watu walikuwa “wamejazwa kwa mshangao na kustajaabu,” na watu wote “wakawakusanyikia.”[7] Kwa jinsi mitume walivyokuwa wakihudumu katika ukamilifu wa Nguvu ya Roho Mtakatifu, huduma zao zilionekana kujaa nguvu ya kimungu. Kupitia Nguvu ya Roho Mtakatifu, mitume waliweza kutekeleza Agizo la Yesu la “kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi.”[8]
Ujasiri wa Kiroho
Wanafunzi walikuwa wajasiri katika kutangaza Injili
Nguvu ya kubadilisha ya Roho Mtakatifu inaonekana wazi katika kitabu chote cha Matendo ya mitume. Mitume ambao kwa miezi michache iliyopita walikuwa wamekimbia katika tukio la kukamatwa kwa Yesu, sasa wanahubiri kwa ujasiri mkubwa.
Muda mfupi baada ya Pentekoste, wakuu wa dini waliwakamata Petro na Yohana. Ni wiki chache tu zimepita, Petro alikuwa amemkana Kristo. Sasa, “Petro, akiwa amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu” alihubiri kwa ujasiri mkubwa. Wakuu wa dini “walishangaa” kwa maneno ya hawa “watu wa kawaida ambao walikuwa hawana elimu yeyote.”[9]
Kupitia ujazo wa Roho Mtakatifu, mitume walikuwa wajasiri katika kuhubiri kwa nguvu na upako. Kutoka kundi la watu waoga, wavuvi, watoza ushuru, na wafanyakazi wa kawaida, wanafunzi sasa wamekuwa ni watu ambao “wameupindua ulimwengu.”[10]
Wanafunzi walikuwa wajasiri mbele ya mateso
Walipokabiliwa na upinzani, mitume hawakuomba kwa ajili ya kuachiwa kutoka kwenye mateso, bali kwa ajili ya ujasiri wa kumhubiri Kristo bila kujali mateso. “Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote…” Mungu alijibu maombi yao. “Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”[11]
Alama isiyokuwa na dosari yeyote ya kazi ya Roho Mtakatfu kwa kanisa ilikuwa ni ile ya ujasiri wa kuitangaza Injili mbele ya upinzani. Hadi mwisho wa karne ya kwanza, Injili ilikuwa imeenea kutoka watu 120 kutokea chumba cha juu hadi kwenye majiji yote ya Dola ya Kirumi.
Maisha ya Ushindi
Katika kila kizazi, Wakristo wamekabiliwa na jaribu la kuwa ”Wakristo wa Jumapili,” – watu ambao wanahudhuria makanisani lakini maisha yao hayaonyeshi mabadiliko ya ndani na mwisho unaoeleweka. Kanisa la mwanzo lilibadilika katika kila eneo la maisha kwa Nguvu ya Roho Mtakatifu.
Katika Agano la Kale, tunaona juhudi za watu waliotaka kushikamana na agano, lakini wakijikuta hawawezi kufanya hivyo kwa sababu mioyo yao ilikuwa imegawanyika. Mtunga Zaburi aliwaelezea watu wa Israeli kwamba: “Mioyo yao haikuwa thabiti kwake. Wala hawakuwa waaminifu katika Agano lake.” [12]
Kupitia Ezekieli, Mungu aliahidi siku ambayo watu wake wangebadilishwa.
"Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda."[13]
Kabla ya Pentekoste, mitume walifuata mwelekeo uliokuwa unafanana na ule wa wana wa Israeli. Walikuwa wanataka kumfuata Kristo, lakini wakishindwa siku zote. Walikuwa na mashaka; walipigania nafasi; walikimbia kwa hofu. Wakati wa Pentekoste, ahadi ya Ezekieli ilitimia. Mitume walipewa uwezo na Roho Mtakatifu wa kuishi maisha ya ushindi. Badala ya kuwa na moyo wenye kutii nusu nusu, walitembea katika kutii kwa furaha sheria ya Mungu. Kupitia Roho Mtakatifu, maisha ya ushindi yakawa ni jambo la kawaida kwa watu wa Mungu.
Mwongozo wa Huduma
Kabla ya Pentekoste, tamaa na hofu vilitawala maisha ya mitume. Juhudi zao za kumtumikia Yesu zilikwamishwa na kushindwa kwao wenyewe. Baada ya Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwaongoza mitume kwenye huduma zilizokuwa na ufanisi.
Roho Mtakatifu aliliongoza Kanisa katika maamuzi magumu yaliyoathiri mahusiano kati ya Wayahudi na mataifa waliogeukia Ukristo.[14] Roho Mtakatifu aliongoza uchaguzi wa viongozi wa Kanisa.[15] Roho Mtakatifu alimwongoza Paulo katika safari yake ya Makedonia.[16] Roho Mtakatifu alimwongoza Paulo katika safari yake ya kurejea Yerusalemu mbali na hatari iliyokuweko ya kukamatwa.[17] Huduma za kanisa la mwanzo ziliongozwa na Roho Mtakatifu.
Umoja
Labda ushahidi muhimu sana unaoweza kukumbukwa wa kazi za Roho Mtakatifu kwa Kanisa la mwanzo ni umoja miongoni mwa waamini wake. Katika maombi yake ya Mchungaji Mkuu pale mlimani, Yesu aliombea umoja wa Kanisa. Aliomba:
"…ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi."[18]
Ombi la Yesu lilijibiwa wakati wa Pentekoste. Matendo 2:42 inaonyesha umoja huu katika maisha ya Kanisa: uwajibikaji katika mafundisho ya mitume, ushirika, usherehekeaji wa Chakula cha Meza ya Bwana, na maombi. Ushirika huu ulionekana kwa kanisa kuwajibika kwa mtu na mtu mwingine. Luka alitoa ushahidi kwamba, “Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji;” kwa sababu Wakristo walijali mahitaji ya kila mmoja wao.[19]
Mara sita, Luka anatumia neno “kwa moyo mmoja” kuelezea umoja wa Kanisa. Hii haimaanishi kwamba Wakristo walikubaliana kwa kila jambo. Masuala magumu yalitishia kuligawa Kanisa. Wayahudi na mataifa waliogeukia Ukristo hawakukubaliana kuhusu Sheria za Musa![20] Paulo na Barnaba hawakukubaliana kuhusiana na Yohana Marko.[21] Lakini pamoja na tofauti zao, Kanisa liliunganishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Jinsi waamini walivyofuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, Kanisa lilifungwa pamoja “kwa moyo mmoja.”
Kama mimi na wewe tungeweza kuwaona wale mitume siku chache kabla ya Yesu kukamatwa, kamwe tusingeweza kufikiria kama watu hawa wangeweza kuja kuwa na ufanisi mkubwa kiasi hicho katika huduma. Walikuwa na hofu, wivu wa wenyewe kwa wenyewe, na wenye mashaka yaliyopitiliza. Miezi michache baadaye, watu hawa wamebadilika kabisa. Ni nini kilichotokea?
Kabla ya Pentekoste, Mitume walijaribu kuishi maisha yanayomfanania Kristo kwa nguvu zao wenyewe, na mara kwa mara walishindwa. Baada ya Pentekoste, mitume waliishi chini ya uwezo wa Roho Mtakatifu. Hii ndiyo siri ya maisha ya utakatifu na huduma yenye ufanisi.
[22]“Hatujazwi Nguvu ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kufanya kazi yeyote maalumu, lakini tu ni kumruhusu Mungu afanye kazi kupitia sisi.”
- Oswald Chambers
Utakatifu leo:Tutakuwa watakatifu tu kama tutajazwa na Roho Mtakatifu
Wakristo wengi wamejaribu kuishi maisha ya utakatifu kupitia nguvu zao wenyewe – na wameshindwa. Kupitia nidhamu ya kibinafsi inawezekana kwa kipindi kifupi tu kudumisha ushindi dhidi ya dhambi za nje. Kwa nguvu zetu wenyewe, inawezekana kuwapenda jirani zetu kwa muda tu. Hata hivyo, kwa muda mfupi tutashindwa pamoja na kutumia nguvu zetu wenyewe.
Ni kwa nini tunapambana? Ni kwa sababu tunajaribu kuishi maisha ya utakatifu kwa nguvu zetu wenyewe. Inachosha sana kujaribu kuishi maisha ya Kikristo kwa nguvu zetu wenyewe. Tunapambana tukiwa na tabia za dhambi; tunapambana tukiwa hatuna upendo mkamilifu; tunapambana tukiwa na moyo uliogawanyika. Kwa ulinganifu, maisha katika Roho ni ushindi tosha kwa wingi wa maisha.
Mungu hajatupangia sisi tuishi maisha ya utakatifu kwa nguvu zetu wenyewe. Ametufanya sisi tuishi kwenye uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika Kanisa la mwanzo, maisha ya utakatifu yaliwezekana tu kwenye uwepo wa uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika Kanisa leo, maisha matakatifu yanawezekana tu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Tabia zile zilizoacha alama kwa kanisa la mwanzo, zitaacha alama pia kwa kanisa la leo kama tutaishi katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu. Kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu, tunaweza kuwa na moyo mtakatifu na mikono mitakatifu.
Nguvu katika huduma, ujasiri wa kiroho, ushindi dhidi ya dhambi, na umoja miongoni mwa waamini – yote yanatokana na uwepo wa Roho Mtakatifu. Tunapokuwa tumejazwa na Nguvu za Roho Mtakatifu, tunakuwa tumepewa uwezo wa kuishi maisha ya Kikristo ya utoshelevu ambayo Mungu amekusudia kwa watu wake.
Nyaraka za Paulo zinaonyesha kwamba kuwa mtakatifu ni kumfanania Kristo. Kuwa mtakatifu ni kufikiri, kuongea na kufanya kama ambavyo Kristo angefanya. Huuni mtizamo mzuri, lakini kwa haraka tunakuja kutambua kwamba kwa nguvu zetu wenyewe hatuna uwezo wa kufikiri, kuongea au kufanya kama ambavyo Kristo angefanya.
Baadhi ya Wakristo huvaa nembo ya YAN kwenye nguo zao. YAN inasimama badala ya “Yesu Atafanya Nini?” Inatukumbusha kwamba tumeitwa tuishi kama Kristo alivyoishi; sisi ni waigizaji wa mambo ya Kristo. Hata hivyo, ni rahisi zaidi kuvaa nembo ya YAN kuliko kuishi katika mfano halisi wa Yesu. Mbali na nguvu ya Roho Mtakatifu, hatuna uwezo wowote wa kufanya kwa mfululizo yale ambayo Yesu angeweza kufanya.[1]
Mimi kidogo nina urefu wa inchi 6 na uzito wa paundi 200. Mimi siyo mkimbiaji. Jaribu kufikiri umeniambia, “Ili uwe mchezaji mzuri ni lazima ucheze kama Michael Jordan. Kabla ya kutupa mpira wowote, ni lazima ujiulize, ‘Michael Jordan atafanya nini?’” Ushauri huu hautanisaidia mimi. Sina uwezo kama alio nao Michael Jordan.
Hata hivyo, jaribu kufikiria kwamba ningepewa zawadi za Michael Jordan alizo nazo. Fikiria kwamba ningeweza - kupitia roho ya Michael Jordan – kufanya kila kitu ambacho Michael Jordan anafanya. Sasa ingewezekana mimi kuiga mambo makubwa ya mcheza kikapu huyu.
YAN (Yesu Atafanya Nini?) haitatosha. Ndani yetu wenyewe, hatuna uwezo wa kumuiga Yesu. Hata hivyo, Roho Mtakatifu aliyeifanikisha huduma ya Yesu anapatikana kwetu leo. Kupitia ujazo wa Roho Mtakatifu, wewe na mimi tunaweza kumfanania Kristo. Huu ni mguso wa Roho Mtakatifu katika maisha ya mwamini.
Roho Mtakatifu alimpa Yesu nguvu kwa ajili ya maisha ya ushindi na huduma yenye matunda; Ujazo wa Roho Mtakatifu ilikuwa siri ya maisha ya ushindi na huduma zenye kuzaa matunda za mitume; ujazo wa Roho Mtakatifu ndiyo siri ya maisha ya ushindi na huduma zenye matunda leo.
Paulo aliandika, “Basi nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. ”[2] Kuna chaguzi mbili tu: Kutembea katika Roho au kutimiza tamaa za mwili. Hatuwezi kwa nguvu zetu wenyewe kushinda tamaa za mwili. Ndiyo, tunaweza kuwa washindi kwa siku au wiki moja, lakini njia pekee ya kupata ushindi wa muda mrefu juu ya tamaa za mwili ni kujitoa kwa Roho Mtakatifu.
Soma Warumi 8:1-17.
Katika muhtasari wake mkubwa wa maisha ya kujazwa Roho katika Warumi 8, Paulo alilinganisha njia mbili za kuishi - maisha kwa kufuata mambo ya mwili na maisha yanayoongozwa na Roho wa Mungu.
“Kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”
Katika Warumi 7, Paulo anaonyesha juhudi zake za huko nyuma jinsi alivyokuwa anatekeleza sheria za Mungu kwa juhudi zake mwenyewe. Juhudi hizo zilishindwa. Kwa nini? Kwa sababu “mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”[3]
Katika Warumi 8, Paulo anafurahia kwamba, “hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.” Tuko huru na hukumu ya adhabu siyo kwa sababu Mungu ameamua kupuuzia dhambi zetu; bali ni “Kwa sababusheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” Tuko huru na hukumu ya dhambi kwa sababu sasa tunaishi katika Roho.
Paulo anaonyesha kwamba kuna njia mbil za kuishi. Njia ya kwanza ni kuishi “katika mwili.” Hii ni akili ya kimwili tu. Akili ya kimwili ni “adui kwa Mungu.” Ni vigumu sana kwa mtu anayeishi katika mwili kumpendeza Mungu. Aina hii ya maisha ya kimwili mwisho wake ni kifo: ”Kwa kuwa kuiweka akili kwenye mambo ya mwili ni kifo.”
Njia ya pili ya kuishi ni pamoja na akili ambayo “imeshikamanishwa na Roho.” Mtu anayeishi kwa misingi ya Roho hufanikisha “mahitaji ya haki yanayotakiwa na sheria” Tuna “maisha” na “amani” kwa sababu “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.”
Katika Warumi 6, Paulo alifundisha kwamba ni lazima tuishi maisha yaliyo juu ya dhambi ya makusudi. “Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?”[4] Kwa nguvu zetu wenyewe, haiwezekani kuishi maisha yaliyo juu ya dhambi ya makusudi. Tumezaliwa kutegemea dhambi na kuwa mbali na Mungu. Tutawezaje kutimiza matakwa ya Warumi 6? Jibu linapatikana katika Warumi 8. Kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu “tunaweza kuyazika matendo yetu ya mwili.” Tunaweza kuishi maisha ya utakatifu kwa sababu Roho wa Mungu anafanya kazi ndani yetu.
Robert Coleman aliandika:
"Kuishi katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu ni kama upendeleo wa wafuasi wa Kristo leo kama wa wale mitume wa mwanzo ambao walikaa katika chumba cha juu…. Ukweli unaofunika wote, utakatifu aliokuwa nao Kristo wa Roho Mtakatifu ndiyo msingi wa Ukristo wa Agano Jipya."[5]
Nguvu ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu aliyeyatoa mapenzi yake yote kwa Mungu inafanya maisha ya utakatifu yawezekane. Pasipo Roho Mtakatifu, kumfafanania Kristo hakutawezekana. Roho Mtakatifu hufanya iwezekane kwa sisi kuishi maisha ya utakatifu.
Nabii Zakaria aliona maono ya kinara cha taa pamoja na miti miwili ya mizeituni. Bakuli lilikuwa la kugawa mafuta bila kikomo kwa ajili ya taa saba. Malaika alifafanua maana ya yale maono. Zerubabeli, mtawala wa Yuda, alikuwa amepewa jukumu la kulijenga upya hekalu. Kazi hii kubwa ilionekana kama ni mlima kwake. Mungu alimwahidi kwamba kazi hii ni lazima itamalizika aliposema, “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu.” Kupitia Roho wa Bwana, mlima utageuka kuwa nchi tambarare.[6]
Kwa njia ile ile, Wakristo leo ni lazima wawe na ujazo endelevu wa Roho Mtakatifu. Paulo aliwaagiza Wakristo wa Efeso “wajazwe Roho.”[7] Agizo hilo ni la wakati uliopo; hii inatakiwa iwe mfumo wa mara kwa mara wa maisha. Maisha yetu ya kila siku ni lazima yaongozwe na yeye. Tunazoeshwa furaha ya maisha ya utakatifu jinsi tunavyoendelea kuishi katika ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
“Roho Mtakatifu, naomba unijaze hadi nifurike. Siwezi nikaubeba ujazo mwingi sana, lakini ninaweza nikajazwa kwa kiwango changu kinachonitosha.”- Imenukuliwa na Dr. David Bubb
Uzoefu wa Utakatifu: Sifa bainifu za Maisha ya Utakatifu
Fikiria kwamba ulikuwa na uwezo wa kuepuka aina zote za dhambi katika maisha yako. Fikiria kwamba ulikuwa huru na vitendo vyote vya dhambi na tabia zote za dhambi. Hakuna mtu yeyote anayeweza kukunyooshea kidole kwa lolote baya. Je, hii itatimiza kusudi la Mungu la maisha ya utakatifu?
Hapana! Utakatifu ni zaidi ya kuepuka dhambi. Utakatifu ni pamoja na kuzaa matunda. Utakatifu siyo njia mbaya au ya kisheria iliyo kinyume na maisha. Utakatifu ni uhusiano wa furaha na Mungu. Utakatifu unaonekana pale Roho Mtakatifu anapotengeneza matunda yake katika maisha yetu.
Tunda la Roho
► Soma Wagalatia 5:13-26.
Katika Wagalatia 5, Paulo anatoa ulinganifu wa maisha katika Roho na maisha katika mwili. Hadi kufikia hapa katika Wagalatia, Paulo amekuwa akiwaonya waamini wa Galatia kuhusu hatari iliyopo ya kuachana na uhuru wao katika Ukristo na kurejea kwenye utumwa wa mila na sheria za Kiyahudi. Wamekombolewa kutokana na juhudi zao za kuutafuta wokovu kupitia matendo yao mema, na kwamba hawapaswi kurejea tena kwenye utumwa huo.
Hata hivyo, Paulo anagundua uwepo wa hatari nyingine tena. Wakati mtu anapowekwa huru kutokana na dhambi, anaweza kujaribu kuutumia uhuru mpya uliopatikana ili kujihusisha na tamaa zake mwenyewe. Kwa hiyo Paulo anawaonya waamini wa Galatia, “Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.”
Paulo anafanya ulinganifu wa nia mbili za kuishi. Mfano mmoja wa maisha ni “kutimiza tamaa zote za mwili,” na mwingine ni “kutembea katika Roho.” Paulo anatoa mifano hii miwili ya ulinganifu kuonyesha “tunda” la kila kipengele katika maisha.
Kwanza, Paulo anaonyesha “kazi za mwili.” Haya ni matokeo ya asili ya mwanadamu ambayo hayako chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Kazi za mwili ni pamoja na:
Anahitimisha kwamba, “Ninawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya hapo mwanzo kwamba, watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”
Kisha Paulo anaonyesha “tunda la Roho.” Hili ni matokeo ya maisha mtu aliyoishi chini ya uongozi na nguvu ya Roho mtakatifu. Hili ni “tunda moja” na siyo mchanganyiko wa “matunda”. Katika 1 Wakorintho 12, Paulo anaorodhesha kundi la “karama” na anasema kila Mkristo atapewa kutoka katika karama hizo na “Roho, kama apendavyo yeye mwenyewe.” [1] Katika Wagalatia, hata hivyo, kuna tunda moja tu, linalokua kwa asili katika moyo wa kila mtu anayetembea katika Roho.
Tunda la Roho siyo orodha ya sifa tunazoweza kuzitengeneza kwa nguvu zetu wenyewe. Hili ni tunda ambalo kwa asili linakua wakati mtu anapokuwa amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Hivi ndivyo maisha ya utakatifu yanavyoonekana. Ni matokeo ya asili ya moyo mtakatifu.
Paulo aliorodhesha “kazi za mwili” kumi na tano. Anaorodhesha mambo tisa kuhusiana na tunda la Roho:
Tunda linalohusiana na Mungu: upendo, furaha, amani
Tunda linalohusiana na watu: uvumilivu, utu wema, fadhili
Tunda linalohusiana na tabia ya ndani: Uaminifu, upole, kiasi
Chanzo cha sifa hizi zote ni upendo. Upendo, “ndio kifungo cha ukamilifu.”[2] Upendo “hutimiza sheria” na hutoa mwanya wa hili tunda kukua na kustawi.
Kuenenda kwa Roho
Tunda la Roho ni ongezeko la asili la maisha tunapokuwa tumejazwa nguvu za Roho. Huu ni msisitizo wa msingi wa Paulo kwa Wagalatia alipokuwa akisema na watu waliojaribu “kukuza” hili tunda kwa nguvu zao za utii kwa sheria. Paulo anawataka waelewe kwamba hawawezi kulipata hili tunda; ni matokeo ya maisha ndani ya Roho.
Ukweli huu kila siku umekuwa wa uwiano kwa Paulo kwa kumbukumbu kwamba Roho Mtakatifu yuko kwa kumaanisha. Utakatifu siyo wa bahati mbaya; ni lazima “tuifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu.“[3] Katika Kolosai, inaonekana kwamba waamini wengi walidhania wanaweza kuendelea katika mfumo wao wa maisha ya zamani. Hapo, Paulo anasisitiza juhudi zinazohitajika ili kuweza kuishi maisha ya utakatifu. Kwa Wakolosai, Paulo anaandika kuhusu “kujivika” sifa za maisha matakatifu. Hii inaelekeza nidhamu endelevu inayohitajika kwenye utakatifu:
"Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu."[4]
Kwa jinsi hiyo hiyo, Paulo hataki Wakristo wa Galatia wafikirie tu kirahisi kwamba maisha matakatifu yanaweza kuendelea bila nidhamu binafsi na juhudi. Katika majibu yao kuhusu sheria, hawapaswi kuwa wazembe. Paulo anasema,[5]
“Enendeni kwa Roho.” Kutembea ni kitendo kinachohitaji juhudi.
“Kuongozwa na Roho.” Nikiongozwa, nitafuata. Kitendo kinachohitaji juhudi.
“Tukiishi kwa Roho.” Kuishi ni chaguo na hatua. Kitendo kinachohitaji juhudi.
“Kutembea hatua kwa hatua na Roho.” Hii ndiyo yenye nguvu kuliko vitenzi vinne hapa juu. Ni neno la kijeshi linaloashiria askari akitembea kwenye mstari. “Kutembea kwenye mstari na Roho” kunahitaji juhudi na nidhamu.
Kama Wakristo tuliojazwa na Roho, kamwe tusifikiri kwamba tumekua sana Kiroho kiasi kwamba hutuwezi kuangukuia kwenye “tamaa za mwili.”[6] Hata hivyo, kamwe tusimruhusu Shetani atushawishi kwamba hatuwezi kuwa huru kutokana na kujitawala dhidi ya tamaaza mwili kupitia nguvu za Roho Mtakatifu. Tunavyozidi kupiga “hatua za kutembea na Roho Mtakatifu” tunatengeneza tunda la Roho ndani ya maisha yetu.
► Baada ya kuwa tumejifunza kuhusu nguvu ya mguso wa Pentekoste kwa mitume wa mwanzo na baada ya kupitia kuhusu tunda ka Roho, jadili ni kwa jinsi gani maisha ya kujazwa Roho Mtakatifu yanaweza kuonekana leo. Ni kwa jinsi gani ujazo wa Roho Mtakatifu unagusa mitazamo yetu, kutembea na Kristo kila siku, na juhudi katika huduma?
Jonathani na Rosalind Goforth walikuwa wamishenari wa Kanisa la Kipresibiteri la Kanada kwa ajili ya China kuanzia mwaka 1888-1933. Bibi Goforth alijaribu kufuata mfano wa Yesu katika maisha yake, lakini mara kwa mara alishindwa. Baada ya miaka ishirini ya kujitahidi, Rosalind Goforth alijifunza kwamba siri ya ushindi wa maisha ya Ukristo ni Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu ambaye anatengeneza tabia ya Yesu katika maisha yetu. Bibi Goforth alitoa ushuhuda kwamba maisha yake baada ya muda huo aliweza kuyaweka katika neno moja, “Mapumziko.”
Kwa jinsi walivyoweza kuruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi kupitia wao, hawa akina Goforth walimwona Mungu akitenda kwao miujiza mikuu. Jonathani Goforth alijibidiisha kwa miezi kadhaa kujifunza lugha ya Kichina. Alipojaribu kuhubiri kwa Kichina, wasikilizaji wachache sana waliweza kumwelewa. Siku moja alipokuwa akihubiri, Ghafla alijikuta anaweza kuwasiliana kwa ufasaha, akitumia misamiati ambayo kamwe alikuwa hajawahi kuwa na ujuzi nayo. Baadaye alikuja kutambua kwamba kundi la wanafunzi kutoka Kanada walikuwa wameitumia siku hiyo kwa ajili ya kuiombea huduma yake. Kuanzia siku hiyo, Jonathan Goforth aliweza kuwa na uthibiti kamili wa lugha ya Kichina. Kile ambacho Goforth hakuweza kukifanya, Roho Mtakatifu alikifanya kwa ajili ya mtumishi wake aliyejisalimisha kwake.
Mungu aliwaongoza hawa akina Goforth ndani ya maeneo ya China ambayo kamwe yalikuwa hayajawahi kuguswa kwa Injili. Maelfu waliweza kubadilishwa kupitia huduma hii ya mtu na mkewe Goforth. Ufunguo wa mafanikio yao siyo uwezo wao mkubwa waliokuwa nao; bali ni katika kuishi ndani ya ukamilifu wa Roho Mtakatifu
Kwenye mazishi yake, Mchungaji wa kanisa la Kipresibiteri la Knox alitoa siri ya mafanikio ya Jonathani Goforth. “Alikuwa mtu aliyemuelewa Mungu – aliyejisalimisha kabisa kwake, na aliyejiweka wakfu kwake. Alikuwa amebatizwa kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Alijazwa Roho Mtakatifu kwa sababu ubinafsi ulishaondolewa katika nafsi yake.”[1]
Jonathani na Rosalind Goforth walielewa umuhimu wa kutembea katika Roho siku hadi siku. Walielewa maombi yaliyokuwa katika wimbo aliouandika Edwin Hatch: “Niwekee pumzi, Pumzi ya Mungu, hadi moyo wangu utakasike.” Wakati moyo wangu umetakaswa, nitakapokuwa mtu, ninataka kile Mungu anachotaka.
[1] Ilichukuliwa kutoka Wesley L. Duewel, Heroes of the Holy Life (Grand Rapids: Zondervan, 2002), 52-64.
Tafakuri ya Somo la 9
(1) Kuwa mtakatifu ni kuishi maisha yenye ukamilifu wa Roho Mtakatifu.
(2) Katika maisha yake duniani, Yesu alihudumu akiwa na Nguvu za Roho Mtakatifu. Yesu aliahidi nguvu hii kwa wafuasi wake. Kwa sababu ya ahadi hiyo, aliwahakikishia mitume wake kwamba, “Mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke.”
(3) Wakati mitume walipojazwa na Nguvu za Roho Mtakatifu wakati wa Pentekoste, maisha yao yalibadilishwa. Alama tatu zilidhihirisha utendaji huu mpya wa Roho Mtakatifu:
Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, inadhihirisha nguvu za ujio wa Roho Mtakatifu
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao kuliambatana na Roho Mtakatifu
Uwezo wa kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka kuliwavika mitume uwezo wa kwenda kushuhudia kwa mataifa yote.
(4) Jinsi kanisa la mwanzo lilivyoishi katika Nguvu za Roho Mtakatifu, walipata uzoefu huu:
Ongezeko la nguvu kwa ajili ya huduma
Ujasiri wa kuitangaza Injili
Ujasiri kwenye nyakati za mateso
Maisha ya ushindi
Uongozi kwa ajili ya huduma
Umoja mongoni mwa waamini
(5) Kama vile mitume walivyokuwa watakatifu tu kupita Roho Mtakatifu, nasi tutakuwa tu watakatifu katika nguvu za Roho Mtakatifu. Pasipokuwa na ujazo wa Nguvu za Roho Mtakatifu, hatutakuwa na uwezo wa kufuata mfano wa Yesu Kristo. Ni katika nguvu za Roho Mtakatifu peke yake tunapoweza kuishi maisha yanayofanana na ya Kristo.
(6) Tutakavyoendela kuishi ndani ya Roho Mtakatifu, maisha yetu yataonesha tunda la Roho kama zao la asili la maisha ya utakatifu.
Kazi ya Kufanya
(1) Andika barua kwa Mkristo mchanga anayekueleza kwamba, “Ninajijua mimi ni Mkristo, lakini ninaendelea kupambana na mitazamo ya kimwili na maeneo mengine ninayojua ni mdhaifu wakati wa kukabiliana na majaribu.” Msaidie Mkristo huyu mchanga kuelewa umuhimu wa kuwa mtu aliyejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu.
(2) Anza kikao kinachofuata cha darasa kwa kunukuu Wagalatia 5:22-25.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.