Tamaduni kuu tatu ziliutengeneza ulimwengu uliokuwa umepokea injili kwenye karne ya kwanza. Mungu aliuandaa ulimwengu uwe katika hali ya kupokea injili itakayokuwa ya mafanikio makubwa sana.
Utamaduni wa Wayunani
Iskanda Mkuu aliitawala dunia ya ujima na akatengeneza himaya yake. Kwa makusudi alieneza utamaduni wa Kiyunani, kwa sababu aliamini ulikuwa ni wa juu na bora zaidi kuliko tamaduni nyingine zote na kwa sababu ingesaidia katika kuunganisha himaya yake. Alimtaka kila mtu azungumze lugha ya Kiyunani na kuishi katika mila za Kiyunani. Hali hii ilifanya maandalizi kwa ajili ya Injili kwa sababu wamishenari waliweza kuhubiri injili kwa kutumia lugha ya Kiyunani katika himaya yake yote.
Mawazo ya Wayunani yaliwafanya watu wajione kama watu huru binafsi badala ya kundi la kikabila au familia. Kwa hiyo, walikuwa wazi zaidi katika kufanya maamuzi binafsi kuhusiana na mambo ya dini. Watu walijitambua kwamba ilikuwa rahisi kwao kubadilisha dini yao.
Wayunani walijiona wenyewe kama ndio raia wa dunia hii, badala ya raia tu wa nchi yao ndogo. Walitambua kwamba kuna ukweli unaotumika kwa watu wote, badala ya kila kikundi cha watu kuwa na ukweli wao wenyewe. Hali hii iliwafanya watambue kwamba ukweli unaweza kuja kwao kutoka mahali pengine popote na siyo lazima kutoka kwenye utamaduni wao wenyewe.
Wanafalsafa wa Kiyunani walijaribu kujibu maswali kuhusu maana ya maisha na ulimwengu. Waliamini kwamba majibu yapo ambayo yanaweza kuelezea kuhusu maisha kwa kila mtu.
Wanafalsafa wa Kiyunani walijaribu kutumia akili kuonesha kwamba dini za zamani zilikuwa potofu. Pia walisababisha watu kutoridhika na hadithi za miungu. Miungu ilikuwa ni maelezo ya kibinadamu yaliyotiwa chumvi mno kwa makosa ya kibinadamu, ukosefu wa maadili na matendo ya uovu.
Wanafalsafa wa Kiyunani walipendekeza maelezomapya kuhusiana na maisha na ukweli. Kila falsafa mpya ilifanyiwa mdahalo, na hakuna falsafa iliyofanikiwa katika kujibu maswali yote kwa ukamilifu. Waligundua na kujadili maswali muhimu tu lakini hawakuweza kujibu yote.
Falsafa haiwezi kukidhi mahitaji ya kiroho ya kibinadamu.
Ukristo unajibu maswali yote yanayoulizwa na falsafa na pia hutosheleza mahitaji ya kiroho.
► Je, Ni kwa jinsi gani utamaduni wa Kiyunani uliweza kuibadilisha dunia na kuandaa kuenea kwa injili?
Utamaduni wa Kirumi
Himaya ya Kirumi ilianza baada ya kuanguka kwa himaya ya Kiyunani katika maeneo au nchi mbalimbali chini ya himaya moja. Warumi walishinda na kutawala mataifa mengi, lakini utamaduni uliokuwa ukitumika zaidi ni ule wa Kiyunani.
Ushindi wa Warumi ulisababisha watu wengi kupoteza imani yao kwa miungu yao mingi iliyokuwa haina uwezo wa kuwasaidia. Watu walikuwa na ari zaidi ya kusikia kuhusu Mungu mwenye nguvu, wa ulimwengu wote.
Warumi waliamini katika miungu mingi na walikuwa na hadithi nyingi kama zilivyokuwa mithiolojia (hadithi zinazoelezea asili ya watu na matukio) za Wayunani. Warumi wengi waliokuwa wanazuoni kwa uhakika hawakukubaliana na miungu lakini waliitumikia dini kama sehemu ya utamaduni wao.
Sheria ya Kirumi ilileta dhana zilizo wazi zaidi kuhusu haki. Mahakama za Kirumi zilizingatia ushahidi katika njia nzuri zaidi. Hii ilisaidia katika kuweka msingi wa mafundisho ya imani kuhusiana na mtu kuwa na hatia na kupewa haki.
Umiliki wa Warumi ulimaliza vita ndogo ndogo kati ya mataifa, wakileta kitu kilichoitwa Pax Rumina, yaani Amani ya Warumi. Hali hii ilifanya kuwepo na usafiri wa amani, na wamisionari waliweza kuvuka mipaka ya nchi mbalimbali bila matatizo.
► Je, ni kwa jinsi gani utamaduni wa Kirumi uliweza kuibadilisha dunia na kuandaa kuenea kwa injili?
Utamaduni wa Kiyahudi
Wayahudi walikuwa wameenea kwenye ulimwengu wote wa maendeleo, na kila mahali walianzisha masinagogi na kufundisha imani yao. Mitume Waligundua kwamba “Musa anahubiriwa katika kila mji” (Matendo 15:21). Uaminifu wa Wayahudi kwa dini yao ya Israeli, ulikuwa na ushawishi katika Rumi.
Dhana ya Uyahudi ya Mungu mwenye mamlaka na mtakatifu iliheshimika zaidi kuliko mithiolojia za Wayunani za miungu ya upotovu na isiyokuwa na maadili. Hali ya juu ya maadili ya dini ya Uyahudi ilikuwa ni kivutio kwenye dunia ya machafuko ya kimaadili. Ukristo ulishirikishwa maadili haya, ukayakuza, na kuhubiri uwezo wa neema ya kubadilisha mwenye dhambi na kumfanya aishi maisha matakatifu.
Dhana ya Uyahudi ya kusudi la Mungu katika historia na matazamio ya Masihi yalileta matumaini kwa ajili ya baadaye. Matumaini hayo yalikuwa ni Mungu kuingilia kati, na siyo suluhisho za kibinadamu. Ukristo ulitanagaza kwamba Masihi ameshafika na kwamba enzi mpya imeshaanza.
► Je, ni kwa jinsi gani utamaduni wa Kiyahudi uliweza kuibadilisha dunia na kuandaa kuenea kwa injili?
Kifungu cha kujifunza – Warumi Sehemu ya 7
Katika kifungu hiki, mtume nanaelezea ni kwa nini anaandika hii barua. Anataka kuwatembelea, kisha apokee msaada kutoka kwao ili aweze kuanza safari yake ya kwenda Hispania. Hili kusudi la barua linaongoza muundo wake kwa sababu Paulo alieleza injili ni nini, kwa nini kila mtu anaihitaji, kwa nini wajumbe wa injili ni muhimu, na kwa nini alikuwa na sifa za kwenda katika safari hiyo. Alionesha kwamba umisheni wa dunia nzima siku zote ulikuwa ni mpango wa Mungu.
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Warumi 15:8-33 kwa ajili ya kikundi.
Maelezo ya Aya-kwa-Aya
(15:8) Yesu alikamilisha ahadi za kimasihi zilizokuwa zimetolewa kwa mababu wa Kiyahudi na kujidhihirisha kupitia taifa la Kiyahudi na dini.
(15:9-12) Kupitia nukuu kadhaa za Agano la Kale, mtume anaonesha kwamba siku zote Mungu alikusudia injili iende kwa Wamataifa. Katika Maandiko Paulo ananukuu Manabii walikuwa wametabiri kwamba:
Watu wa Mataifa watakuwa watu wa kumwabudu Mungu
Masihi atatawala juu ya watu wa Mataifa.
Watu wa Mataifa watamtumainia Masihi.
(15:13-14) Mtume anatoa maombi ya baraka kwa kanisa la Rumi na kusema kwamba anaamini kwamba washiriki wake wameimarika kiroho. Kwenye aya zinazofuata, atawaita kwa ajili ya kazi ya umishenari. Hata kanisa lililobarikiwa kuwa na nguvu za kiroho litakuwa halijakamilika kama halina maono na kuhusika na kazi ya umishenari.
► Je, kunatokea nini kama kanisa halina nia ya kusaidia kazi ya umishenari kwa ajili ya maeneo yaliyo mbali?
(15:15-16) Mtume anawaambia kuhusu wito maalumu anaopaswa waubebe kwa ajili ya injili kwa Wamataifa. Mungu amempa karama maalumu za kiroho kwa ajili ya kazi hii. Matamanio yake ni kwamba makanisa yanayotokana na Wamataifa yawe matakatifu na ya kweli, yanayompendeza Mungu.
(15:17-19) Mungu alishampa mafanikio katika huduma yake. Wamataifa wengi wamekuwa watiifu kwa Neno la Mungu. Mojawapo ya matokeo muhimu sana ya huduma ni kwamba watu wanatubu na kuishi katika kumtii Mungu. Hakuna alama nyingine ya mafanikio kama hiyo. Anasema kwamba huduma yake imeambatana na miujiza ya Mungu. Alisambaza injili kwenye maeneo yote makuu ya nchi.
(15:20-22) Jaribio lake lilikuwa ni kuhubiri mahali ambapo injili haijawahi kuhubiriwa tena kabla. Hatua kwa hatua alikamilisha maeneo yote ya nchi. Kipaumbele hicho kilikuwa ndiyo sababu hakuweza kusafiri kwenda Rumi, kwa sababu injili alikuwa tayari imeshahubiriwa huko.
(15:23-24) Alikuwa ameshahubiri injili kwenye kila eneo lililokuwa karibu naye. Alitaka kanisa la Rumi limsadie afanye ziara ya umishenari nje yao aingie Hispania. Safari hiyo itampa nafasi ya kuhubiri na kufanya ushirika pale Rumi, na pia asaidiwe kufika katika mikoa ambayo alikuwa bado hajawahi kuihubiria injili.
► Elezea ni kwa jinsi gani kila Mkristo na kila kanisa lina deni la kuunga mkono upelekaji au uenezaji wa injili. (Kama itahitajika, ona kumbukumbu iliyoko katika Warumi 1:15, kwenye somo la kwanza.)
(15:25-29) Kwa kuanzia, atafunga safari ya kwenda Yerusalemu ili akachukue sadaka kutoka kanisa la watu Wamataifa na kwenye kanisa la Wayahudi. Sadaka hii ilikuwa ni muhimu sana. Kwa kuituma hiyo sadaka, Wamataifa walikuwa wanakiri dhamana waliyo nayo kwa Wayahudi kwa sababu Wayahudi waliogeukia Ukristo ndio waliowaletea injili. Kwa kuipokea ile sadaka, Wayahudi wanakiri kwamba Wamataifa walikuwa sawa na wao katika kanisa moja. Hakutakuwepo na mgawanyo wa dini za Kikristo. Ndiyo maana Paulo aliwataka waombe kwamba waamini wa Kiyahudi wapokee sadaka zao.
(15:30-33) Aliwataka waombe kwamba aokolewe kutoka katika hatari ya wale Wayahudi wasioamini katika Yerusalemu, ili kwamba aweze kufika Rumi. Maombi yake yalijibiwa, ingawaje siyo katika njia aliyokuwa ameichagua. Paulo aliwasili Rumi kama mfungwa baada ya kukamatwa huko Yerusalemu na kuwekwa mahabusu na watawala wa Kiyahudi, akachukuliwa na gavana wa Kirumi, na mwishowe akapelekwa Rumi kwa mashtaka. (Taarifa hii iko katika kitabu cha Matendo, kuanzia 21:26 hadi mwisho wa kitabu cha Matendo.) Hatujui tena baada ya hapo kama Paulo alikuja kufanya safari ya kwenda Hispania.
► Ni kwa jinsi gani tunaona utoaji wa Mungu kwenye matukio ya maisha ya Paulo, hata kama safari yake ya kwenda Hispania haikufanyika tena kama alivyokuwa amepanga?
Kifungu cha kujifunza – Warumi Sehemu ya 8
Muhtasari wa sura ya 16
Kuna salamu nyingi kwa majina yao katika waraka huu kuliko kwenye maeneo mengine yote aliyoandika Paulo. Inawezekana ikawa hivyo kwa kuwa alikuwa hajawahi kukaa Rumi, anawataja watu wote aliokuwa amezoeana nao waliokuwepo pale kwa ajili ya kusaidia kuanza uhusiano wake na kanisa.
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Warumi 16 kwa ajili ya kikundi.
Maelezo ya Aya-kwa-Aya
(16:1-2) Fibi yumkini alikuwa miongoni mwa wale waliobeba barua hii. Paulo aliwaambia wamsaidie dada huyu katika huduma yake kwa sababu alikutana na mahitaji ya watu wengi. Mtu mzuri wa kuweza kumsaidia ni yule ambaye tayari amefanyika kuwa ni baraka kwa watu wengine.
(16:3-4) Priska na Akila walidiriki kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya Paulo. (Ona Mdo 18:1-3, 24-26 kwa historia zaidi kuhusiana nao).
(16:7, 11, 21) Jamaa za Paulo zimetajwa katika aya hizi.
(16:13) Mwanamke anayetajwa hapa inawezekana labda siyo mama yake na Paulo. Inawezekana Rufo alikuwa mtoto wa Simoni wa Krete ambaye alibeba msalaba wa Yesu, kwa sababu katika Marko 15:21 jina lake limetajwa kama aliyekuja kujulikana kwa kanisa baadaye.
(16:17-18) Kuna watu ambao wanajaribu kuwatenga wenzao kutoka kwenye misingi ya ukweli ya kanisa ili waweze kujenga mambo yao wenyewe ya watu kuwafuata wao. Watu hawa hawamtumikii Kristo, bali matamanio yao wenyewe. Ujumbe wao ni tofauti kabisa na mafundisho sahihi ya imani kuhusiana na wokovu. (Ona 3 Yohane 1:9-10 na 2 Petro 2:1-3.)
(16:19) Tunapaswa tujifunze kwa kiasi kikubwa kadri inavyowezekana kuhusu ukweli. Hatupaswi tujue mengi kuhusiana na mambo ya uovu. Watu ambao wanajifunza kuhusu mambo ya uovu wanakabiliwa na hatari ya mvuto wa uharibifu na upotoshaji wa kufikiri kwao.
(16:20) Kanisa ni lazima mwishowe litashinda dhidi ya Shetani kupitia kazi ya Kristo (Mwanzo 3:15).
(16:22) Tertio hakuwa mwandishi wa waraka huu, bali ni mtu aliyeandika yale ambayo Paulo alikuwa anamzungumzia yeye ili ayaandike.
(16:25-27) Aya hizi zinarejea kwenye mada muhimu za barua hii. Angalia maneno “injili yangu” na “kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo.” Anaelezea tena kwamba injili ni ufunuo wa sasa wa ile siri iliyositirika na ujumbe wa mitume. Anamalizia na kurejea mara ya mwisho kuhusu mambo ya umisheni, akiwakumbusha wote kwamba ujumbe ni kwa ajili ya mataifa yote. Lengo la kazi ya umisheni ni sawa na kama Yesu alivyoagiza katika Agizo Kuu (Mathayo 28:19-20): kuwaleta watu kwenye utii kwa Kristo. Hii inamalizia barua kama ilivyoanza, kama 1:5 anasema: kwamba sababu ya huduma ni kuwaleta Wamataifa wote kwenye kumtii Mungu.
Uwasilishaji wa Injili kutoka kwa Warumi
Injili inaweza kufafanuliwa kwa kutumia aya pekee kutoka katika kitabu cha Warumi. Uwasilishaji huu wa injili mara nyingine unaitwa “Barabara ya Kirumi.”
Sentensi ya kwanza ya ufafanuzi kwa kila kitu kinachorejewa ni muhimu sana kukikumbuka.
Warumi 3:23
“kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”
Kila mtu ametenda dhambi kwa kufanya mambo ambayo wanajua ni makosa. Aya hii inaonyesha kwamba kuna tatizo kubwa la ukweli ambalo watu wanalo. Hawajamtii Mungu; kwa makusudi kabisa wamekataa kumtii Mungu. Hakuna hata mtu mmoja ambaye hahusiki. Hakuna mtu ambaye anaweza kukubalika na Mungu kwa misingi ya kwamba siku zote amekuwa akitenda yaliyo sahihi.
Kwa msisitizo wa ziada kuhusiana na jambo hili, unaweza kutumia Warumi 3:10 (Hakuna mwenye haki hata mmoja”) na 5:12 (“na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”).
Warumi 6:23
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Wenye dhambi wamevuna kifo cha milele, lakini Mungu anatoa uzima wa milele kama zawadi kupitia kwa Yesu.
Aya hii inaonyesha ni kwa nini dhambi ni mbaya sana, adhabu ya dhambi imepitishwa kwa kila mtu. Ni kifo cha milele, hukumu ya Mungu ambayo kila mwenye dhambi anastahili.
Tofauti na kifo ambacho tumeshakipata, Mungu anatoa karama ya maisha, jambo ambalo tulikuwa hatujastahili.
Warumi 5:8
“Bali Mungu aonesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.”
Karama ya Mungu ilitolewa kwa kifo cha Yesu Kristo kwa ajili yetu.
Mungu hakuwa tayari kutuachilia tupokee hukumu tuliyokuwa tumestahili. Kwa kuwa anatupenda, alitoa njia mbadala ya kupokea rehema. Yesu alikufa kama dhabihu ili tuweze kusamehewa. Mungu hakungojea tufanye jambo fulani ili tustahili wokovu – ilikuja kwetu wakati bado tuko wenye dhambi. Wokovu hautolewi kwa watu wazuri, bali kwa wenye dhambi.
Warumi 10:9
“ukimkiri Yesu … na kuamini … utaokoka.”
Hitaji peke yake kwa ajili ya wokovu ni kwa mwenye dhambi kukiri kwamba ni mwenye dhambi na kuamini ahadi ya Mungu ya msamaha.
Vipi kuhusu kutubu? Kama mtu atakiri kwamba amefanya makosa na anataka kusamehewa, anaonyesha kwamba anataka kwa hiari yake mwenyewe kuondokana na dhambi zake.
Warumi 10:13
“Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.”
Utoaji wa wokovu ni kwa kila mtu. Hakuna mtu hata mmoja aliyetengwa. Hakuna sifa nyingine zinazohitajika.
Warumi 5:1
“Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu.”
Kuamini ahadi ya Mungu kunatufanya tuwe marafiki wa Mungu, na hatuendelei kuhesabiwa wenye hatia tena.
Kuwa na amani na Mungu ni kumaanisha kwamba sisi siyo maadui wake tena; tumepatanishwa. Dhambi ambayo imetutenganisha na Mungu inaondolewa na kutupwa. Kuhesabiwa haki inamaanisha kuhesabiwa kwamba huna hatia tena. Kuhesabiwa haki kwa imani inamaanisha kwamba kumwamini Mungu na ahadi zake ndicho kitu peke yake kinachohitajika kwa ajili ya msamaha wetu.
Warumi 8:1
“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.”
Kwakuwa tumeunganishwa kwa Kristo, hatuko tena kwenye hukumu ya dhambi tulizozitenda.
Kristo aliishi maisha yasiyokuwa na dhambi na akakamilisha mahitaji yote ya haki kwa njia ya kifo chake juu ya msalaba. Kwa imani tunajitambulisha naye na pamoja naye tunakubaliwa na Mungu Baba. Mungu anatuchukulia kama ambao kamwe hatujawahi kufanya dhambi.
Hitimisho
Elezea kwamba mwenye dhambi anaweza akaokoka kwa kumwomba Mungu, akikiri kwamba ni mwenye dhambi, na akiomba msamaha kwenye msingi wa dhabihu ya Yesu kwa ajili yake.
Kwa Kujifunza na Kutendea kazi
Njia bora zaidi ya kujifunza na kufanya mazoezi ya njia hii kwanza ni kuweka alama ya kila aya iyakayotumika katika Warumi kwa kuzungushia au kupiga mstari chini yake. Kisha, weka namba pembeni ya kila aya ukionyesha mtiririko wa matumizi yake. kwa mfano, pembeni mwa mastari ambao ndio utakaoanza kutumika kwanza, weka namba 1.
Kisha fanya zoezi la kuwasilisha injili. Soma kila aya na toa maelezo yanayoendana nayo. Hakikisha kuingiza dhana ambazo ziko kwenye sentensi ya kwanza baada ya kila aya (hapo juu). Kisha, ongezea maelezo mengine yeyote yatakayohitajika, kwa kutumia sentensi nyingine kama zitaonekana zina msaada. Siyo lazima kutumia maneno yale yale yaliyotumika au yaliyotolewa katika somo hili.
Fanya mazoezi hadi ujione kwamba unaweza kufanya mwenyewe bila ya kuangalia mahali pengine popote isipokuwa Biblia yako.
Maswali ya Mapitio Somo la 12
(1) Elezea jinsi tamaduni kuu tatu zilivyotayarisha ulimwengu kwa ajili ya kuenea injili katika karne ya kwanza.
(2) Je, mtu anaoneshaje kuwa Mungu wakati wote alipanga injili iende kwa Wamataifa?
(3) Je, ni kwa nini sadaka ya kanisa ilikuwa muhimu sana Yerusalemu?
(4) Je, Paulo alifikaje Rumi?
Print Course
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.