Je, ni sheria gani tunaizungumzia?
Maagizo mengi ya Agano la Kale yanaonekana kama hayataweza kutumika kwa watu wa wakati huu. Hapa kuna mifano:
- 
	
Usimwache mwanamke mchawi kuishi (Kutoka 22:18)
 - 
	
Kila miaka saba, mwisho wake, fanya maachilio (Kumbukumbu la Torati 15:1-2).
 - 
	
Siku saba mfanyie sikukuu Bwana pasaka katika Yerusalemu (Kumbukumbu la Torati 16:1-6).
 
Baadhi ya wanazuoni huzigawa sheria za Agano la Kale katika makundi matatu: sheria za ibada, sheria za kiraia, na, sheria za maadili
Sheria za ibada zilihusika na utoaji wa dhabihu, eneo la kuabudia, na taratibu za kuabudu. Wakristo wa wakati huu hawafuati sheria za ibada za kiyahudi kwa sababu utaratibu huo umetimilika katika kazi iliyofanywa na Kristo (Wakolosai 2:17, Waebrania 10:1).
Sheria za kiraia zilikuwa ni kwa ajili ya taifa la Israeli. Walitoa sheria kwa ajili ya shughuli za biashara, kulinda haki za binadamu, kutoa kanuni za utekelezaji wa sheria, na kulinda utambulisho wa kidini wa Israeli. Haiwezekani kwa Mkristo wa leo kufuata sheria za kiraia za wayahudi kwa sababu sheria hizo siyo sheria za taifa lao. Kwa mfano, nyakati za agano la Kale, wakati mtu alipotakiwa kuuawa kwa ajili ya kuabudu miungu, hilo halikufanyika kwa uamuzi wa mtu mmoja. Hakimu alisikiliza shauri lililokuwepo, kisha hukumu iliungwa mkono na watu (Kumbukumbu la Torati 17:6-12).
► Je kwa nini haiwezekani kwa Mkristo kutimiza sheria za kiraia za waisraeli wa kale katika hali zilivyokuwa mwanzoni?
Sheria za maadili zilitambua matendo kadhaa kwamba yalikuwa ni sahihi au ni mabaya kwa nyakati zote. Kwa mfano, Amri Kuu za Mungu zilizuia ibada za sanamu, kumkufuru Mungu, uzinzi na wizi (Kutoka 20:5, 7, 14, 15).
Ingawa wakristo hawafanyi kama zilivyokuwa mwanzoni, yaani matendo maalumu yalioamriwa kwenye sheria za ibada na sheria za kiraia. Walakini, sheria hizo bado zina umuhimu kwa sababu zinadhihirisha asili ya Mungu, ambazo kamwe hazibadiliki. Ingawaje hatuwaui watu wenye kufuata ibada za sanamu au wazinzi, sheria hizo zinatuonyesha kwamba dhambi hizo ni machukizo kwa Mungu. Ingawaje hatuachi ngano shambani kwa ajili ya maskini, tunajua kwamba ni lazima tuwajali maskini kwa vitendo. Ingawaje hatuwapeleki tena wanyama kwenye maeneo ya ibada kabla hatujawaua, tunajua kwamba kila kitu ni mali ya Mungu, na tunatakiwa tutoe sadaka kwa vile vitu tulivyo navyo. Kwa hiyo, ingawaje hatuyafanyi kwa vitendo matendo ya zamani, tunapaswa tutafute matendo mapya ambayo yataweza kukamilisha kanuni hizo.
Sababu nyingine ya umhiumu wa sheria za ibada na sheria za kiraia ni kuwa zinatoa kanuni za maadili za kutumiwa katika njia maalumu. Kukataa hizo kanuni ingekuwa ni sawa na kuzikataa sheria za maadili. Kwa mfano, hatuhitaji kuwa na chuma za kuzunguka dari ya nyumba kama nyumba yetu haijakusudiwa kuwa na watu juu ya dari (Kumbukumbu la Torati 22:8). Lakini sheria hii ya zamani inatuambia kwamba tunapaswa tuzifanye nyumba na maeneo ya ardhi zetu visiwe na vitu vya hatari kwa watu.
► Je, kuna utaratibu gani wa wakati huu wa sasa ambao tunapaswa tufanye ili kukamilisha kanuni iliyopo katika Kumbukumbu la Torati 22:8?
Kwa hiyo, ni sheria gani ambayo Paulo anazungumzia katika kitabu cha Warumi? Ni mapenzi ya Mungu kwa wanadamu, yaliyoelezwa kwenye amri zake (Agano la Kale na Agano Jipya). Ingawaje baadhi ya amri hazikamilishwi katika hali yake ya mwanzoni iliyotakiwa, mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kimsingi yanafanana. Ukiukwaji wa sheria ya Mungu ni dhambi (1 Yohane 3:4).