Angalizo kwa kiongozi wa darasa: Tunza muda darasani kwa ajili ya kufanyia kazi shughuli katika somo hili, hata kama kitahitajika kipindi zaidi ya kimoja cha darasa.
Katika kozi hii, tumeangalia hatua za kutafsiri Biblia: Uchunguzi, Tafsiri, na Matumizi. Tumejifunza juu ya kuepuka makosa yaliyozoeleka katika kutafsiri Biblia. Tumejifunza kanuni muhimu kwa ajili ya kujifunza maandiko. Tumefanyia mazoezi kila hatua. Katika somo hili, kwanza tutapitia tena mchakato wote. Kisha darasa zima kwa Pamoja litajifunza vifungu toka Agano la Kale na Jipya kwa kutumia mchakato huu. Pia uatafanyia mazoezi stadi kibinafsi. Kisha utakamilisha mradi wa kozi uliouanza katika Somo la 1.
Tofauti za kihistoria-kiutamaduni ambazo zinatenga ulimwengu wetu na ulimwengu wa kale
3
Daraja
Kanuni zinazofundishwa katika andiko
4
Ramani
Mahusiano na Agano Jipya (kwa ajili ya vifungu vya Agano la Kale)
5
Mji wetu
Matumizi ya kanuni katika ulimwengu wetu
Sehemu inayofuata ya somo hili linarudia tena mchakato wote wa kutafsiri Biblia. Wakati wa kila hatua ya mchakato wa tafsiri, watafsiri wanatakiwa kuuliza maswali ambayo yatawaongoza katika mahitimisho sahihi. Maswali haya yana msingi katika kanuni za kutafsiri.
Maswali yanayotakiwa kuulizwa kwenye kila hatua katika mchakato yameorodheshwa. Mifano inaonesha namna ya kutumia maswali na kwa nini ni ya muhimu kwa ajili ya tafsiri sahihi.
Mkusanyiko wa maswali yanatakiwa kuchukuliwa kama boksi ya vifaa kwa ajili ya tafsiri. Kama ambavyo mjenzi hatahitaji kutumia kila kifaa katika mradi wa jengo fulani, sio kila swali hapa litatumika kwa kila kifungu. Swali linaweza kuchukuliwa kuwa halihitajiki endapo majibu yake yanaonekana hayawezi kuwa halisi au endapo yanaonekana kutochangia chochote.
[1]Picha: “Interpreting the Bible” Imechorwa na Anna Boggs, inapatikana katika https://www.flickr.com/photos/sgc-library/52377290578, licensed under CC BY 2.0. Concept from J. Scott Duvall na J. Daniel Hays, Grasping God’s Word (Grand Rapids: Zondervan, 2012)
Uchunguzi: Kuelewa Muktadha wa Kihistoria-Kiutamaduni
Mtume Paulo mwandishi wa 1 Timotheo, alikuwa mlezi wa Timotheo. Hili lilkuwa ni agizo ambalo Paulo alikuwa anamuelekeza Timotheo, ambaye alikuwa mchungaji kijana.
Kuelewa mambo haya kunatusaidia sisi kutambua kwamba maelekezo ya Paulo hayawezi kutumika kwa kila mkristo.
Wapokeaji wa Kwanza
Walikuwa ni nani?
Walikuwa na tabia gani?
Filemoni alikuwa ni mwamini binafsi aliyeandikiwa.
Waebrania iliandikwa kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa wanateswa.
Mazingira
Ni wakati gani katika historia ya wokovu andiko hili liliandikwa?
2 Mambo ya Nyakati 7:14: “Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
“Watu wangu” linarejelea taifa mahususi ambalo lilikuwa watu wa Mungu. Ahadi “kuiponya nchi yao” si lazima iwe na matumizi ya moja kwa moja kwa katika kanisa.
Mazingira ya utamaduni yalikuwa nini? Kama inawezekana, tumia kamusi ya Biblia kusoma utamaduni wa asili. Hii itakusaidia kulinganisha/kukinzanisha utamaduni wao na wetu.
2 Wakorintho 13:12: “Salimianeni kwa busu takatifu.”
Kusalimiana kwa busu takatifu ulikuwa ni utamaduni wa kawaida baina ya wakristo wa wakati ule.
Yapi yalikuwa ni matukio yanayotokea kwa sasa?
Hali ndani ya kanisa ilikuwaje? (Vifungu vya Agano Jipya pekee)
Uchunguzi: Kuelewa Muktadha wa Uandishi
Angalia tabia za aina ya fasihi ya kitabu na kifungu.
N aina gani ya fasihi ya kitabu/kifungu hiki?
Nini ni tabia za aina hii ya fasihi?
Zaburi 124:4-5:
Aina ya Fasihi: Ushairi
Tabia: Usambamba
Ufunuo 12:3:
Aina ya Fasihi: Fasihi ya kiapokaliptiki
Tabia: Wanyama ni Alama
Uchunguzi: Kuelewa Kusudi Kuu la Kitabu
Kusudi la uandishi lilikuwa nini? Tafuta kile ambacho mwandishi anasisitiza au ambacho mwandishi ameonesha wasiwasi, kutoa maelezo, au changamoto kwa wasomaji.
1 Wakorintho 7:1: “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika…”
1 Wakorintho iliandikwa ili kujibu barua ambayo kanisa la Korintho lilimwandikia Paulo, likimuuliza maswali.
Ni nini kinaonekana kuwa tatizo/mahitaji ya wapokeaji?
1 Wakorintho 1:10: “Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.”
Mgawanyiko imejadiliwa mara kwa mara katika barua.
Mwandishi alikuwa akiwaambia nini wapokeaji? Maagizo yeyote yanayotolewa baada ya Uchunguzi wa mwandishi ni dalili za wazi za kile ambacho mwandishi alitarajia. Yanaonyesha jinsi tunavyopaswa kutumia kifungu.
Uchunguzi: Kutambua Mwanzo na Mwisho wa Kifungu
Mara nyingi, lakini si mara zote, mgawanyo wa sura utaashiria mwisho au mwanzo wa kifungu. Mara kwa mara, sura nzima inaweza kuunda kifungu kimoja. Wakati mwingine, migawanyo ya sura huwekwa kimakosa na haipaswi kutumiwa kama mgawanyiko wa vifungu. Tazama mabadiliko ya mada, ambayo kwa kawaida yana alama zinazoonesha mpito. Ukijaribu kuweka mambo mengi sana katika kifungu, kifungu hakitakuwa na mada moja kuu. Ikiwa hutajumuisha vya kutosha katika kifungu, kifungu hakitakuwa na mawazo kamili.
Ni mistari gani inayijumuishwa katika kifungu?
2 Wakorintho 7:1: “Kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi wangu…”
Sehemu hii ya kifungu inapatikana mwishoni mwa sura ya mwisho, 2 Wakorintho 6:14-18.
Isaya 52:13-15 iko katika kifungu kile kile kama Isaya 53.
Uchunguzi: Kuelewa Nanma Kifungu Kinahusiana na Kitabu
Je, ni simulizi ambayo inaingia katika wazo kuu kubwa?
Waamuzi 17:5: “Basi mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya miungu, naye akafanya naivera, na kinyago, akamweka wakfu mmoja miongoni mwa wanawe, akawa kuhani wake.”
Mtu mmoja alikuwa na sanamu yake na kuhani wake. Mstari hu una mistari inayozunguka simulizi ya Waamuzi 17-18 inaelezea wazo la jumla la Waamuzi, “…kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe” (Waamuzi 17:6, Waamuzi 21:25).
Je, kinatoa theolojia kwa ajili ya matumizi ya baadae?
Je, ni matumizi ya kifungu kilichipita katika kitabu?
Waefeso 4-6 kimsingi ni matumizi ya vitendo ya theolojia inayofundishwa katika Waefeso 1-3. Katika Waefeso 4:1 neno “Kwa hiyo” linaonyesha daraja kutoka kufundisha theolojia hadi kufundisha matumizi ya vitendo.
Waefeso 4:1: “Kwa hiyo nawasihi...mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa…”
Uchunguzi: Angalia Muundo wa Kifungu
Je, baadhi ya nyenzo ni maandalizi ya kifungu kikuu?
Marko 2:2: “…Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni….”
Taarifa hizi zinamuandaa msomaji kusikiliza kuhusiana na mtu aliyeshushwa toka darini.
Ni maneno gani yanatumika kuunganisha mawazo kimpangilio?
Kujirudia kwa matumizi ya ndipo katika Mathayo 24.
Je, swali au tatizo limewasilishwa?
Warumi 6:1: “Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?”
Ni maneno gani yaliyotumika kuunganisha mawazo kimantiki?
Kujirudia kwa matumizi ya Kwa katika Warumi 6 kuonesha mfuatano wa kimantiki.
Je, ulinganifu au ukinzani umetumika?
Warumi 6:19-20: “…Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa…”
Ukinzani baina ya utumwa wa kale (kwa uchafu na uasi) na utumwa wa sasa (kwa haki).
Maneno haya yote ni maneno yanayoonesha hitimisho.
Je, kuna orodha yeyote?
1 Timotheo 4:12: “…bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”
Ni vielelezo au lugha gani za picha ambazo zimetumia?
Warumi 6 inatumia kusulubiswa kama tamathali ya semi.
Je, njia ya kufikia lengo umeelezwa?
Warumi 8:13: “…kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.”
“kwa Roho” – njia
“mkiyafisha matendo ya mwili” – Lengo
“mtaishi” – Lengo kuu
Je, kuna sababu za matamko yaliyotolewa au madai?
Kujirudia kwa matumizi ya Kwa yanapelekea katika mafafanuzi ya matamko katika Warumi 6.
Je, kuna kilele au sehemu kuu? Hili ni swali mahususi kwa ajili ya simulizi
Katika mfano uliotolewa katika Mathayo 21:33-41, mistari ya 38-39 ni kilele.
Je, chanzo na matokeo vimeelezewa?
Wagalatia 5:16: “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.”
Chanzo: “Enendeni kwa Roho”
Matokeo: “hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.”
Je, sehemu hii inakaa kama ufupisho wa kile kilichopita au kinachofuata?
Waamuzi 2:11-23 inafupisha kitabu cha Waamuzi.
Waefeso 5:1 inafupisha Waefeso 4:25-32.
Je, sehemu hii inanukuu au inarejea andiko lingine? Waandishi wa Agano Jipya mara nyingi wametumia nukuu au vielelezo kutoka Agano la Kale.
Warumi 12:1: “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
Katika mtari huu, dhabihu ni neno la picha ambalo linarejelea kitu katika Agano la Kale.
Uchunguzi: Chunguza na Jifunze Maneno Muhimu
Ni maneno gani muhimu katika kifungu?
Maneno muhimu kutoka katika 1 Wakorintho 2:14-15:
Mwanadamu wa tabia ya asili
Mtu wa rohoni
Maneno muhimu kutoka katika Warumi 8:
Mwili
Roho
Yanamanisha nini katika muktadha huu? Jifunze kila neno kwa kila moja.
Uchunguzi: Chunguza Kila Tamko
Lina maana gani? Rudia kwa maneno yako kile ambacho tamko linasema.
Kwa nini limejumuishwa, na kwa nini limewekwa hapa? Fikiria ingekuwaje endapo tamko hilo lisingekuwa hapo.
Tafsiri: Fupisha Ujumbe
Kwa kuwa sasa umechunguza kwa makini taarifa za kina na mstari au andiko, fupisha ujumbe wa mwandishi kwa wapokeaji wa kwanza. Ufupisho wa mstari unaweza kuwa wa sentensi moja. Ufupisho wa kifungu unaweza kuwa sentensi kadhaa au hata vifungu kadhaa.
Lengo la hatua hii ni kutaja kile ambacho mwandishi anakisema kwa wasomaji wake wa kwanza. Huu sio wakati wa kuwa na mawazo na ubunifu wako. Unaweza kuwa mbunifu wakati unatengeneza njia za kuwasilisha ujumbe katika mahubiri au mafundisho, lakini kwa sasa unajaribu kutafuta maana ya andiko. Maana inatakiwa kutoka katika maandiko na sio katika mawazo yako.
Ni nini mwandishi anajaribu kukisema kwa wapokeaji waliokusudiwa?
1 Wakorintho 1:10-13 inaweza kufupishwa namna hii: “Tafadhali pataneni katika mafundisho yenu na ushirika na msigawanyike na kuwa makundi. Nimesikia kutoka katika nyumba ya Kloe kwamba mnabishana. Mnachagua kuwafuta viongozi mbalimbali, lakini ni Kristo tu ndiye alikufa kwa ajili yenu.”
Angalia ufupisho wako. Fikiria maswali yafuatayo Pamoja na nyezo ambazo zimepatikana kutoka katika Uchunguzi ulioufanya:
Je, nimezingatia vya kutosha hali ya mazingira ya awali ya uandishi?
Ni nini kinaonekana kuwa nia na makusudi ya mwandishi kuandika kifungu hiki?
Je, tafsiri yangu ya kifungu inalingana na dhana kuu ya kitabu?
Je, tafsiri yangu inakipa kifungu jukumu lake sahihi katika kitabu?
Je, msisitizo wa muundo wa kifungu unaendana na muhtasari wangu?
Je, maana ya kila tamko ndani ya kifungu linaunga mkono muhtasari wangu?
Je, ninatafsiri ipasavyo matumizi ya mwandishi ya maneno muhimu?
Tafsiri: Taja Kanuni
Katika kifungu, tafuta kanuni moja inayotumika nyakati zote na watu wote. (Kifungu kinaweza kufundisha kanuni kadhaa, lakini kwa sababu ya kufanyia mazoezi, chagua moja.) Itaje katika sentensi moja.
Moja kati ya kanuni zinazopatikana katika Waefeso 4:25: “Sema kweli katika mawasiliano yote.”
Kisha angalia ili kuhakikisha kwamba kanuni yako inaonesha kwa usahihi ujumbe wa asili wa andiko:
Kanuni hii imefundishwa kwa uwazi katika andiko?
Kanuni hii inapatana na maandiko mengine?
Kanuni hii ni kweli kwa nyakati zote kwa watu wote?
Husianisha kanuni na kweli nyingine:
Ni kweli gani inayohusiana ambayo imefunuliwa kwingineko katika maandiko?
Ni kwa namna gani kweli hii inaongezeka katika ufahamu wetu?
Je, tafsiri yangu inaweza kusahihishwa kwa kuzingatia maandiko kwa ujumla wake?
Je, kweli hii inonekana kupingana na vifungu vingine? Kama ni hivyo, je, vinaweza kupatanishwa?
Matumizi: Tengeneza Matumizi Kwa ajili ya leo
Kanuni ambazo umezipata zinaweza kutumika kwa namna tofauti tofauti. Fanya matumizi moja mahususi katika ulimwengu wa leo.
Ni katika mazingira gani mahususi ya wakati wa leo ambapo ukweli huu unaweza kutumika?
Je, ni lini, wapi, na kwa nani taarifa hizo zinafaa?
Ni kwa namna gani ukweli unaweza kutumika katika kitendo na wazo?
Kama nikikichukua kifungu kwa umakini sana, kitaniletea mabadiliko gani katika Maisha yangu?
Muulize Roho Mtakatifu kukuongoza katika kuliishi neno la Mungu anayeishi katika Maisha yako.
Kufanyia Mazoezi Kutafsiri ya Nyaraka
Tunapotafsiri nyaraka za Agano Jipya, tunaanza kwa kuchunguza kwa kadiri inavyowezekana kuhusina na waraka, tunaendelea kuchunguza waraka ili kupata ujumbe wake, na tunamaliza kwa kutumia kanuni katika ulimwengu wetu. Safari hii ya tafsiri inatuchukua sisi kutoka ulimwengu wa wapokeaji wa kwanza hadi kwenye ulimwengu wa msomaji wa leo.
Kufanyia Mazoezi Pamoja
► Pamoja kama darasa, fanyia kazi mchakato wa tafsiri kwa ajili ya 1 Yohana 2:15-17. Kama nyongeza ya maswali na mchakato wa tafsiri ulioelezewa hapo juu, kumbuka kujifunza yaliyomo katika nyaraka kama aina ya fasihi (ona Somo la 6).
Kufanyia Mazoezi Peke Yako
► Kila mwanafunzi achukue mojawapo ya vifungu hivi na kufanyia mazoezi mchakato wa tafsiri. Kisha wanafunzi washirikishe hitimisho zao kwa wanakikundi katika kundi.
Warumi 13:8-10
Waefeso 6:18-20
2 Timotheo 4:6-8
Yakobo 3:13-18
1 Petro 2:9-10
Kufanyia Mazoezi ya Kutafsiri Sheria za Agano la Kale
Tunapotafsiri sheria za Agano la Kale, kwanza tunatakiwa kuelewa ilimaanisha nini kwa wapokeaji wa kwanza. Lazima tutazame kwa makini utofauti kati ya mazingira yao na yetu, hasa hasa utofauti wowote ambao unahusiana na ukweli kwamba tunaishi katika Agano Jipya. Katika sheria za Agano la Kale, tunatakiwa kutambua kanuni ambazo zitatendewa kazi na watu wote wa nyakati zote. Kisha tunaweza kuzitumia kanuni hizi katika maisha yetu.
Kufanyia Mazoezi Pamoja
► Pamoja kama darasa, fanyia kazi mchakato wa tafsiri kwa ajili ya Hesabu 15:37-41. Kama nyongeza ya maswali na mchakato wa tafsiri ulioelezewa hapo juu, kumbuka kujifunza yaliyomo katika sheria za Agano la Kale kama aina ya fasihi na tumia maswali katika Somo la 6.
Kufanyia Mazoezi Peke Yako
► Kila mwanafunzi achukue mojawapo ya vifungu hivi katika mchakato wa tafsiri. Kisha wanafunzi washirikishe hitimisho zao kwa wanakikundi katika kundi.
Mambo ya Walawi 19:9-10
Kutoka 20:4-6
Kutoka 22:10-13
Kumbukumbu la Torati 14:1-2
Somo la 10 Zoezi
Katika Somo la 1, ulichagua mojawapo ya vifungu hivi vya maandiko.
Kumbukumbu la Torati 6:1-9
Yoshua 1:1-9
Mathayo 6:25-34
Waefeso 3:14-21
Wakolosai 3:1-16
Sasa kwa kuwa umefanyia kazi kila hatua ya safari ya tafsiri, fanya usomaji yakinifu wa kifungu ulichokichagua. Ukimaliza, andaa somo kutoka mojawapo kati ya mfumo huu:
1. Kama umekuwa ukisoma kozi katika kundi, utatakiwa kushirikisha ujifunzaji wako katika mawasilisho. (1) Onesha uchunguzi wako, (2) Fundisha kanuni kutoka katika andiko, na (3) Onesha namna ya kutumia andiko katika maisha ya mwamini leo.
2. Kama umekuwa unasoma peke yako, andika andiko lenye kurasa 5-6 ambapo utaelezea (1) Uchunguzi wako, (2) Kanuni kutoka katika andiko, na (3) Onesha namna ya kutumia andiko katika Maisha ya mwamini leo.
Print Course
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.