► Taja neno katika lugha yako ambalo lina maana zaidi ya moja. Mtu anapotumia neno hilo, ni kwa namna gani utafahamu maana anayomaanisha?
Moja kati ya Nyanja muhimu ya tafsiri ya Biblia ni muktadha wa kifungu ambacho unakisoma. Katika somo hili tutajifunza muktadha wa kihistoria-kiutamaduni na mazingira ya muktadha wa kifungu cha nadiko.[1]
[1]Nyenzo nyingi katika somo hili zinatoka katika sura ya 6-7 ya J. Scott Duvall na J. Daniel Hays, Grasping God’s Word (Grand Rapids: Zondervan, 2012).
Muktadha wa kihistoria-kiutamaduni
► Soma 2 Timotheo 4:6-22.
Paulo anamwandikia Timotheo, “Jitahidi kuja kabla ya wakati wa baridi” (2 Timotheo 4:21). Sikiliza ombi la Paulo katika mwanga wa historia ifuatayo:
Paulo yupo gerezani kule Rumi. Muda mfupi tu atauawa kwa ajili ya imani yake.
Timotheo anahudumu Efeso, mamia ya kilometa toka Rumi.
Kusafiri baharini ni hatari hasa wakati wa baridi. Kwa Timotheo kufika Rumi kabla ya baridi, anatakiwa aanze safari mara tu baada ya kupokea barua.
Muktadha wa kihistoria unaongeza katika sisi kutambua hisia nyuma ya ombi la Paulo. Paulo anasema zaidi ya, “Tafadhali nitembelee ukipata nafasi.” Anamuomba mwanae wa kiroho, “Ninataka kukuona tena kabla ya sijafa. Endapo ukingojea hadi wakati wa baridi, usafiri hautawezekana. Tafadhali uje kabla haujachelewa.” Barua ina ujumbe ule ule hata kama haufahamu kabisa muktadha wa kihistoria, lakini Muktadha wa kihistoria unaonesha ukumbwa wa ombi la Paulo.
Muktadha wa kihistoria na kiutamaduni ni muhimu kwa sababu Mungu hakutoa Biblia katika lugha moja ambayo kila mtu duniani anaelewa. Matamko mawili kuhusiana na maandiko ni muhimu:
1. Kanuni za maandiko ni kweli kwa kila mtu wa kila mahali nyakati zote.
2. Kanuni a maandiko zilitolewa kwa watu mahususi katika mahali mahususi kwa wakati mahususi.
Tofauti za kihistoria-kiutamaduni ambazo zinatenga ulimwengu wetu na ulimwengu wa kale
3
Daraja
Kanuni zinazofundishwa katika andiko
4
Ramani
Mahusiano na Agano Jipya (kwa ajili ya vifungu vya Agano la Kale)
5
Mji wetu
Matumizi ya kanuni katika ulimwengu wetu
Kwa kadiri tunavyoelewa vizuri muktadha wa kihistoria na kiutamaduni wa maandiko, ndivyo tutaelewa vizuri kanuni za msingi za Biblia.
Tunapojifunza muktadha wa kihistoria-kiutamaduni, tunaisoma biblia katika “mji wao” ili uelewa ujumbe kwa wapokeaji wa kwanza. Kisha tutaangalia “mto” – Tofauti za kihistoria-kiutamaduni ambazo zinatenga ulimwengu wetu na ulimwengu wa kale. Jinsi tunavyoelewa vizuri ulimwengu wa Biblia, ndivyo tutakavyosikia vizuri zaidi neno la Mungu akiongea katika ulimwengu wetu leo.
Kusoma maandiko katika muktadha wake wa asili ni muhimu kwa sababu ndio msingi muhimu wa kanuni za kutafsiri Biblia: Tafsiri yeyote sahihi ya andiko la Biblia ni lazima liwe sawasawa na ujumbe wa asili wa andiko. Sitakiwi kutafsiri maana ambayo itakinzana na ujumbe wa asili wa andiko.
Muktadha wa kihistoria-kiutamaduni ni nini? Muktadha wa kihistoria-kiutamaduni ni kitu chochote nje ya andiko ambacho kinatusaidia sisi kuelewa andiko lenyewe. Hii inajumuisha majibu ya maswali kama vile:
Maisha ya Waisraeli kule jangwani yalikuwaje (Muktadha kwa ajili ya Kutoka—Kumbukumbu la Torati)?
Utamaduni wa Palestina ulikuwaje wakati wa karne ya kwanza (Muktadha kwa ajili ya Injili)?
Waalimu wa uongo walikuwa ni nani ambao wanamsababishia Paulo kuchanganyikiwa katika Wagalatia na Wafilipi?
Baadhi ya maswali ya kuuliza unapojifunza muktadha wa kihistoria-kiutamaduni yanajumuisha:
(1) Tunafahamu nini kuhusiana na mwandishi wa Biblia?
Kwa sababu Mungu alizungumza kupitia waandishi wa kibinadamu, ufahamu wa waandishi utatusaidia kuelewa vema neno la Mungu.
Unaposoma nyaraka za Paulo, kumbuka maisha yake kabla ya kubadilishwa. Anapoelezea “alivyoutumainia mwili,” (Wafilipi 3:4-6) fahamu kwamba mafarisayo waliheshimika sana kutokana na umakini wao wa kutii sheria. Tunapokumbuka unafiki wao na walivyokataa kumkubali Yesu, tukumbuke pia upendo wao kwa kila taarifa katika sheria ya Mungu.
Kwa upande mwingine, Paulo anapojielezea mwenyewe kwamba “wa kwanza” wa wenye dhambi, (1 Timotheo 1:15) kumbuka kwamba Paulo alilitesa kanisa na aliwatoa wakristo ili wauawe. Huyu ni yule mtu ambaye ameishi na kumbukumbu ya maisha yake ya awali kabla ya kukutana na Kristo akiwa njiani kuelekea Dameski.
Tunaposoma Kutoka, tunatakiwa kujifunza kuhusu heshima na upendeleo aliokuwa nao Musa katika ikulu ya Farao. Tunapofikiri kuhusiana na maisha ya anasa katika ikulu, kile ambacho Waebrania 11:25 anasema kuhusu Musa sasa kinakuwa na maana sana “…akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo.” Tunapoona fursa za kielimu na kiutamaduni alizozifurahia kijana Musa, tunaona kwamba Mungu anamuaandaa mtumishi wake huyu kuongoza taifa kubwa.
(2) Tunafahamu nini kuhusiana na wapokeaji wa Biblia?
Pamoja na kujifunza kuhusu mwandishi wa Biblia, tunapaswa pia kujifunza kwa kadiri tunavyoweza kuhusu wapokeaji wa kwanza.
Nyingi kati ya nyenzo katika Mambo ya Nyakati ya 1 na 2 zimerudiwa kutoka Samweli na Wafalme. Kwa nini? Mambo ya Nyakati iliandikwa baada ya Waisraeli kurudi kutoka uhamishoni. Wafalme inaonesha ni kwa nini Mungu aliruhusu Israeli kupata hukumu; Mambo ya Nyakati inaonesha kwamba Mungu bado anawajali watu wake.
Yeremia anahubiri nyakati zinazozunguka uharibifu wa Yerusalemu. Tunaposoma ujumbe wake wa hukumu, tunapaswa kukumbuka kwamba hukumu iliyotamkwa iko karibu kutokea. Hata hivyo, katika Yeremia tunasoma pia ahadi ya Mungu, “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho” (Yeremia 29:11). Ahadi hii inakuja wakati watu wako karibu kuchukuliwa kwenda utumwani katika nchi ya ugeni. Mpango wa Mungu kwa watu wake unajumuisha hukumu ambayo itawaleta katika toba.
Waraka wa 1 Yohana ulielekezwa kwa Wakristo wanaopitia mafundisho potofu: kwamba ni roho tu ndiyo nzuri; mwili na kila kitu kinachoonekana ni viovu. Waalimu wa uongo walisema kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili; alionekana tu kuwa kama mwanadamu. Yohana anawakumbusha wasomaji wake kwamba Yesu alikuwa na mwili wa nyama unaoonekana. “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa” (1 Yohana 1:1).
Waalimu wa uongo walisema pia wokovu unapatikana kupitia maarifa ya siri ambayo yanafunuliwa kwa watu wachache tu. Yohana anaonesha kwamba ni lazima tutii ili tuwe na maarifa ya kweli ya Mungu; “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake” (1 Yohana 2:3). Maarifa yanayoleta uzima wa milele yanahusisha upendo “Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu” (1 Yohana 3:14).
(3) Tunafahamu nini kuhusiana na mazingira ya kihistoria ya kitabu?
Hebu fikiria muhubiri anatangaza, “Leo nitahubiri namna ambayo mkristo anaweza kupata mke. Waamuzi 21:20-21 inatuambia kwamba tunatakiwa kwenda katika kijiji jirani na kungoja katika vichaka. Mmoja wapo wa wanawake vijana wanapokuja kutoka kijijini, mkamate na umbebe hadi nyumbani kwako. Hiki ndicho kielelezo cha kibiblia cha kuchagua mke.” Ni lazima utilie shaka matumizi ya mhubiri juu ya matumizi ya maandiko!
Kitu gani hakiko sawa katika matumizi ya muhubiri? Waamuzi Inasema kwamba wanaume wa kabila la Benjamini walipata wake zao kwa namna hii wakati fulani. Hata inasema pia walifanya hivi kwa sababu ambayo ilikuwa nzuri – kulitunza kabila moja la Israeli. Hata hivyo, muhubiri anapuuza muktadha wa kihistoria. Habari hii inakuja mwishoni mwa kitabu cha Waamuzi, kitabu kinachoonesha anguko la Israeli kutoka katika mpango wa Mungu hadi kwenye machafuko. Badala ya kuonesha mpango wa Mungu kwa ndoa, habari inaonesha kile ambacho kilitokea pale watu wa Mungu walipoasi.
Wakati mwignine tunafahamu kiasi kidogo kuhusiana na mwandishi na wapokeaji wake, lakini tunafahamu kuhusiana na mazingira ya kihistoria. Hatufahamu kuhusiana na mwandishi wa kitabu cha Ruthu, lakini tunafahamu matukio yaliyotokea katika siku ambazo waamuzi walitawala (Ruthu 1:1). Huu ulikuwa ni wakati wa machafuko ya kijamii katika Israeli (Waamuzi 21:25). Ikikinzanana ukosefu wa uaminifu kwa Mungu uliooneshwa na Israeli, kitabu cha Ruthu inaleta umakini katika uaminifu wa Ruth, mjane wa kimoabu.
Habari inatueleza namna Boazi alivyomuoa Ruth kwa hiari ili kuwainulia uzao watoto wa Naomi waliokufa. Kama mkombozi wa ukoo, Boazi alitoa sadaka urithi wake mwenyewe ili kumtunza Naomi. Katika kufanya hivyo, Boazi akapata nafasi katika ukoo wa Daudi (Mathayo 1:6, 16).
Muktadha wa kihistoria ni muhimu unapotafsiri kitabu cha Yona:
Ninawi ilikuwa mji mkuu wa Ashuru adui mkubwa na hatari wa Israeli.
Karibu na wakati ambapo Yona alikuwa anahubiri Ninawi, Amosi na Hosea walikuwa wanaonya kwamba hukumu ya Mungu ingekuja juu ya Israeli kupitia mikono ya waashuru.
Kwa mtazamo wa kibinadamu, Yona kukataa kuhubiri Ashuru kunaeleweka. Kitabu cha Yona inaonesha mtazamo wa Mungu, ambaye anawapenda watu wote bila kupendelea.
(4) Tunafahamu nini Kuhusiana na Mazingira ya kiutamaduni ya Kitabu?
Muktadha wa kihistoria-kiutamaduni wa andiko pia unaagazia mila za kitamaduni za ulimwengu wa Biblia. Tunapata uelewa mpya wa mifano ya Yesu tunaposoma katika mwanga wa mazingira ya mila za Palestina katika karne ya kwanza:
Mfano wa Msamaria mwema (Luka 10:30-35) ulikuwa ni mshangao kwa wapokeaji wa Kiyahudi. Wasikilizaji wa Yesu wasingeshangaa kuhusiana na viongozi wa dini kushindwa kumsaidia msafiri aliyekuwa amejeruhiwa. Hata hivyo, walitegemea ambaye angemsaidia angekuwa rabi au farisayo. Kinyume chake, Yesu anamuonesha Msamaria aliyedharauliwa kama kielelezo cha upendo.
Katika mfano wa mwana mpotevu (Luka 15:11-32), tunapaswa tukumbuke kwamba wababa wa kiyahudi walikuwa wana heshima sana. Wasikilizaji walitegemea kwamba baba angekataa kumrejeza mtoto wake aliyerudi, au pengine angeruhusu awe mtumishi. Kinyume chake, baba aliachilia mbali habari za heshima yake katika furaha ya kurudi mwanae aliyepota. Kitendo hiki kinashangaza sana kiasi kwamba baadhi ya watu wa utamaduni wa mashariki wanauita mfano huu “Mfano wa baba anayekimbia.” Katika namna ile ile, Baba yetu wa mbinguni hatusubiri hadi sisi tujirekebishe ndipo tupokee msamaha; kinyume chake, anamtafuta mwenye dhambi aliyeasi. Hii ni picha ya upendo usio na kipimo wa Baba yetu.
Nyaraka za Paulo zinatakiwa kusomwa katika mwanga wa hali ya utamaduni ya karne ya kwanza. Waefeso 5:21–6:9 ilikuwa ya kushtusha kwa wasomaji wa Paulo. Agizo la Paulo la wanawake kutii waume zao lilikuwa ni la kawaida; Agizo lake kwamba waume wafuate kielelzo cha Yesu cha upendo wa kujitoa kilikuwa ni kigeni kwa wasikilizaji wa Kirumi. Watoto walitegemewa kuwatii wazazi wao, lakini hakuna hata mmoja katika ulimwengu wa Kirumi ambaye angemwambia baba asiwachokoze watoto wake.
Paulo anapowaambia Wafilipi kuishi kana kwamba wenyeji wao uko mbinguni, (Wafilipi 3:20) alikuwa anauandikia mji ambao ulikuwa na haki na upendeleo maalumu wa kiraia kwa raia wa dola ya Rumi. Kwa sababu mji ulianzishwa kama eneo la kupumzikia wanajeshi waliostaafu, wenyeji wa Filipi walijali sana uraia wao. Paulo anawakumbusha kwamba wao wenyeji wao uko mbinguni, na si katika miji ya duniani. Kwa kufahamu muktadha wa kihistoria-kiutamaduni kunatupa sisi uelewa mzuri wa Wafilipi.
Kugundua Muktadha wa Kihistoria-Kiutamaduni
Kama tulivyoona, kujifunza kwetu muktadha wa kihistoria-kiutamaduni wa kifungu unaanza kwa kuuliza maswali. Ni kwa namna gani tutagundua majibu ya maswali yetu? Nyongeza ya kozi inatoa baadhi ya vyanzo ambavyo vinaweza kutupatia majibu ya maswali yetu. Tunashauri pia kutumia kozi za utangulizi wa Agano la Kale na Agano Jipya ambazo zinatolewa na Shepherds Global Classroom. Kozi hizi zitakupa historia ya nyuma ya kila kitabu katika Biblia.
[1]Picha: “Interpreting the Bible” imechorwa na Anna Boggs, inapatikana katika https://www.flickr.com/photos/sgc-library/52377290578, licensed under CC BY 2.0. Concept from J. Scott Duvall and J. Daniel Hays, Grasping God’s Word (Grand Rapids: Zondervan, 2012)
Muktadha wa Kibiblia
Kitu kingine cha kukiangalia kwa makini kwa ajili ya kutafsiri Biblia ni muktadha unaozunguka. Ni muhimu kuuliza, “Ni kwa namna gani mstari, kifungu, sura, na kitabu kinakaa vema katika Biblia nzima?”
Hebu fikiri umepata kipande cha karatasi chenye ujumbe mfupi wa sentensi moja iliyonyofoka kutoka katika barua nzima. Karatasi inasoma, “Ndio, 7 ni sawa.” Sentensi hii inamaanisha nini?
Pengine mwandishi alikuwa na miadi na mtu mwingine. Anathibitisha kwamba saa 7:00 mchana ni sawa kwa kikao.
Pengine mke wa mwandishi ametuma ujumbe akiuliza, “ni watu wangapi ninatakiwa kuwaalika kwa ajili ya chakula cha jioni ijumaa jioni?” Anajibu, “saba (watu) ni sawa.”
Pengine mwandishi ametoa ofa ya kuuza kitabu kwa $8.00. mtu mmoja anamuuliza, “Je, utapunguza bei hadi $7.00?” Mwandishi anajibu, “Sawa, $7 ni sawa.”
Tutaelewa maana ya sentensi husika kama tu tutafahamu muktadha. Tunasoma sentensi katika muktadha wa kifungu chote. Tunasoma sentensi katika muktadha wa barua yote. Kwa upana zaidi, tunaweza kusoma barua katika muktadha wa mfululizo wa barua kati ya watu hawa wawili.
Maandiko yanafanya kazi kwa namna hiyo hiyo. Mstari husika ni lazima usomwe katika muktadha wa mistari inayozunguka, sura, na kitabu. Muktadha unakipanua kifungu kutoka katika muktadha wa karibu hadi kwenye Biblia nzima.
Ili kuelewa mstari husika, ni lazima tuangalie muktadha unaozunguka. Zaburi 1:3 inatupa ahadi nzuri kwa mtu ambaye hupendezwa na sheria za Bwana. Atakuwa kama mti unaopata maji vizuri na kuzaa matunda. “kila alitendalo litafanikiwa.” Baadhi ya watu wamechukulia hii kama ahadi ya baraka za mali na mafanikio kwa kila mwamini.
Hata hivyo, unaposoma Zaburi yote ya 1, umakini si katika mafanikio ya mali bali mafanikio ya rohoni kwa wale ambao wanatembea katika sheria za Bwana. Zaburi inahitimisha na ahadi; Mungu “anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea” (Zaburi 1:6). Ukinzani ni kati ya njia inayofahamika (ikiangaliwa na kuthibitishwa) na Mungu na njia ambayo inaelekea upotevuni.
Kwa kufuata Zaburi zingine zote na Biblia nzima, ujumbe umethibitishwa. Mafanikio ya mwamini hayapatikani katika umiliki wa mali, bali katika uthibitisho wa Mungu. Haya ndiyo mafanikio ya kweli.
Kusoma kifungu katika muktadha, fuata hatua hizi tatu:
1. Tambua namna kitabu kilivyogawanywa katika vifungu. Muktadha wa karibu wa mstari unaosoma ni upi?
2. Fupisha mawazo makuu ya kifungu katika sentensi moja au mbili. Hii itakusaidia kuuelewa ujumbe wa sehemu yote.
3. Soma kitabu chote na uliza, “Ni kwa namna gani kifungu ninachojifunza kinakaa vema katika ujumbe wa kitabu?”
Biblia nzima > kitabu chote > kifungu au sura > mstari
Biblia > Nyaraka za Paulo > Warumi > Warumi 12-15 > Warumi 12:1-2
Warumi 12:1-2 inatutaka sisi kujitoa kwa Mungu.
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Hii inaanzisha sehemu (Warumi 12-15) ambayo inaonesha ni kwa namna gani kujitoa huku kutaonekana katika maisha ya kila siku ya mkristo. Kutembea kutoka muktadha wa karibu, Warumi 12-15 inafuata sura 11 za mafundisho yenye maelekezo ambayo yanaonesha namna tulivyopatanishwa na Mungu.
Zaidi ya muktadha wa Warumi, kila waraka wa Paulo unaonesha kujali kwake kuhusiana na utendaji wa kivitendo wa imani yetu ya Kikristo. Mwisho, Warumi 12:1-2 inaingia katika ujumbe wa Biblia yote wa kumtii Mungu na kujitoa kwa Mungu. Kwa mfano, Lugha ya Warumi 12:1-2 inaonesha lugha ya dhabihu katika Mambo ya Walawi. Jinsi tutakavyoelewa muktadha mpana vema wa Biblia, ndiyo maneno ya Paulo yanavyokuwa na nguvu.
Zamu Yako
► Soma kila mistari ifuatayo na kisha soma muktadha wake wa karibu. Jadili ni kwa namna gani muktadha unaathiri uelewa wako wa mstari.
1. Soma Mathayo 18:20. Hii inamaanisha nini?
2. Sasa soma Mathayo 18:15-20. Je, hii inaathiriri maana ya 18:20?
1. Soma Warumi 8:28. Hii inaahidi nini?
2. Sasa soma Warumi 8:28-30. Ni ahadi gani njema katika 8:28?
1. Soma Ufunuo 3:20. Nani anaalikwa?
2. Sasa soma Ufunuo 3:14-21. Mwaliko unamlenga nani?
Makosa Yaliyozoeleka Katika Kujifunza Muktadha
Kwa kuhitimisha somo hili, tutaangalia baadhi ya makosa yaliyozoeleka ambayo watafsiri wanafanya wanapojifunza muktadha wa maandiko.
Kutumia Taarifa Zisizo Sahihi
Mwanafunzi alitoa mawasilisho yake katika Mathayo 19:23-24. Alisema wakati wa Yesu, kwamba lango moja la kuingia Yerusalemu liliitwa “tundu ya sindano.” Lango hili lilikuwa finyu sana kiasi kwamba mzigo wa ngamia ilibidi uondolewe ili kwamba mnyama asukumwe kwa kulazimishwa kupita kupitia lango.
Yapo matatizo mawili katika mawasilisho ya mwanafunzi:
1. Hakuna ushahidi wa kibilia unaoonesha lango hili wakati wa Yesu. “Tundu ya sindano” ilimaanisha vile vile inavyomaanisha leo, tundu la sindano ya kushonea.
2. Kwa sababu taarifa ya historia yake haikuwa sahihi, mwanafunzi alifikia hitimisho lisilosahihi kuhusiana na andiko. Mawasilisho yake yalionesha kwamba tuondoe kila kitu kinachozidi katika maisha yetu ili tuweze kupenya katika ufalme wa Mbinguni.
Hata hivyo, Yesu hakua anafundisha kwamba ni vigumu kwa tajiri na mwenye mamlaka kuingia ufalme wa Mungu; alikuwa anafundisha kwamba haiwezekani! Wanafunzi walishtushwa na hili hadi wakauliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”
Yesu hakujibu, “Ni vigumu ila ukijaribu kwa bidi unaweza kupenya.” Alijibu kwa kutumia habari njema ya injili: “Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.” Katika kujifunza muktadha, usiache taarifa zisizo sahihi zikukoseshe.
Kuweka Muktadha kuwa Kipaumbele kuliko Ujumbe
Hatari ya pili ni kuruhusu kujifunza muktadha kuwa muhimu kuliko ujumbe wa andiko. Paulo aliwakumbusha wakristo wa Korintho kwamba taarifa zisizo sahihi zinaweza kusababisha kiburi, lakini upendo huwanufaisha wengine (1 Wakorintho 8:1).[1] Ni rahisi kufurahishwa na taarifa za muktadha kiasi ambacho tunasahau ujumbe wa andiko tunalojifunza.
Mtu anaweza akajifunza kila kitu kuhusiana na utamaduni wa Wasamaria na kusahau kusudi la mfano wa msamaria mwema: “Enenda... ukafanye vivyo hivyo” (Luka 10:37). Katika jambo hili, ufahamu wetu hautakuwa na matumizi. Jifunze ili kupata ujumbe wa andiko; usizikwe katika kujifunza kwa ajili yako mwenyewe. Jifunze ili kufundisha na kuhubiri kwa ufanisi, si kwa ajili ya kujivuna kwa ajili ya ufahamu wako mkubwa!
[1]Paulo hayuko kinyume cha maarifa; aliandika waraka ili kutoa maelekezo mazuri kwa kanisa changa. Hata hivyo, “maarifa” yenye kiburi cha Wakorintho yanachopelekea uharibifu, na sio kujenga.
(1) Tafsiri sahihi inahitaji kujifunza muktadha wa kila kifungu mahususi cha Biblia.
(2) Muktadha wa kihistoria-kiutamaduni unazingatia mazingira ya kitamaduni ya Biblia. Uliza:
Tunafahamu nini kuhusiana na mwandishi wa Biblia?
Tunafahamu nini kuhusiana na wapokeaji wa Biblia?
Tunafahamu nini kuhusiana na mazingira ya kihistoria ya kitabu?
Tunafahamu nini kuhusiana na mazingira ya kiutamaduni ya kitabu?
(3) Muktadha wa Biblia unaagazia ni kwa namna gani mstari unakaa vizuri katika andiko lote.
Somo la 5 Zoezi
Katika Somo la 1, ulichagua kifungu cha maandiko ambayo utayasoma wakati wote wa kozi hii. Jifunze muktadha wa kihistoria-kiutamaduni na muktadha wa Biblia wa andiko ulilolichagua. Andaa ukurasa wa nakili ambapo utajibu maswali mengi kwa kadiri inavyowezekana kutoka katika majadiliano ya somo hili kuhusianana Muktadha.
Uliza:
Mwandishi ni nani?
Aliandika lini?
Historia yake ya nyuma ni ipi?
Wapokeaji wake ni nani?
Walikuwa na matatizo gani?
Ni mazingira gani yanayozunguka kifungu?
Ni matukio gani ya kihistoria ambayo yalitokea wakati wa kitabu hiki?
Ni vitu gani katika utamaduni ambavyo yanasaidia kuelezea kitabu?
Soma sura zinazozunguka kifungu ili kutambua muktadha wa Biblia wa kifungu.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.