Angalizo kwa kiongozi wa darasa: Tunakushauri kufundisha somo hili katika vipindi viwili kwa sababu ya kiasi cha nyenzo kinachotakiwa kufunduishwa. Wanafunzi watakuwa na zoezi baada ya kipindi cha pili.
Kufahamu aina za Fasihi kunatusaidia sisi kutafsiri maandiko.
Biblia inapotuambia kwamba Daudi alichunga kondoo (1 Samweli 16:11), tunafahamu kwamba inaongea kuhusiana na kondoo wa kawaida, kwa sababu alikuwa mchungaji. Wakati kitabu cha Ufunuo kinasema Yohana aliona joka kubwa (Ufunuo 12:3) au kitu kama simba au dubu, tunafahamu kwa hakika, wanyama hao waliwakilisha vitu vingine kwa sababu kitabu cha Ufunuo kina alama nyingi.
Wakati 1 Wafalme 5:6 inatuambia kwamba Sulemani alileta miti ili kutumia kwa ajili ya ujenzi wa hekalu huko Yerusalemu, tunafahamu kwamba alileta miti halisi. Wakati Zaburi 1:3 inasema mwenye haki ni kama mti ulipandwa kando ya mto, tunafahamu kwamba alikuwa anafanya ulinganifu. Wakati Isaya 55:12 inasema kwamba miti itapiga makofi, inamaanisha kutakuwa na furaha hata asili pia inaonekana kufurahia.
Kuelewa aina ya fasihi ni muhimu katika kutafsiri Biblia. Kitabu cha ushairi (Zaburi) kitawasilisha tofauti na waraka (Warumi). Kuelewa tofauti kutatusaidia sisi kutafsiri kila kitabu kama mwandishi alivyokusudia. Hapa ni utangulizi wa aina kubwa za fasihi katika maandiko.
Aina ya Fasihi: Historia
Sehemu kubwa ya Biblia ni historia: Pentatuki, vitabu vya historia, Injili, na Matendo ya Mitume, na sehemu zingine fupi fupi ni historia ya kweli na ya uhakika ya watu halisi na matukio halisi.
(Biblia pia ina vielelezo vya kufikirika vilivyotolewa na manabii na mifano aliyotoa Yesu. Tutajadili tafsiri ya hivi katika sehemu inayofuata kwa sababu ni tofauti na tafsiri ya simulizi za kihistoria.)
Maswali ya Kuuliza Unaposoma Historia
Unatakiwa kuuliza maswali wakati unasoma simulizi ya historia ya Biblia:
(1) Habari ni nini?
Unaposoma simulizi, tunaangalia Muundo wa habari. Kwa mfano, Injili ya Luka inafuatilia huduma ya Yesu kule Galilaya; kisha inaangazia safari ya Yesu kwenda Yerusalemu na kujikita katika mafundisho yake kuhusiana na uanafunzi; Luka anahitimisha kwa kujikita katika kifo na ufufuo huko Yerusalemu. Katika Matendo ya Mitume, Luka anaonesha kukua kwa huduma ya kanisa. Tena, anafuata Muundo wa kijiografia. Injili inahubiriwa Yerusalemu; kisha inachukuliwa hadi Yudea yote na Samaria; na mwisho, Injili inaenda mwisho wa dunia kupitia huduma ya Paul kule Rumi.
(2) Watu katika habari ni nani?
Tunaposoma kuhusiana na watu wa kihistoria katika Biblia, tunajifunza kuhusiana na nguvu tunazoweza kuzitengeneza na udhaifu tunaotakiwa kuuepuka. Tunauliza maswali kama, “Nini kilimfanya Nehemia kuwa kiongozi mwenye ufanisi?” na “Nini kilikuwa ni tofauti kati ya kushindwa kwa Sauli na kufanikiwa kwa Daudi?” Tunalinganisha njia ya uinjilisti ya Petro na Paulo. Katika historia ya Biblia, tunapata picha ya watu.
(3) Je, simulizi hii ya kihistoria inatoa mfano gani wa kufuata?
Tunaposoma historia, tunapaswa kuuliza endapo matendo yanayooneshwa ni mifano kwa sisi kufuata. Simulizi ya kihistoria inaweza kutoa kielelezo cha kile ambacho Mungu anatarajia kutoka kwa watu wake. Kwa upande mwingine, inaweza kutoa historia muhimu ambayo haitoi kielelezo cha kufuata.
Unakumbuka mfano uliotolewa kuhusiana na muhubiri aliyetumia Waamuzi 21 kuhubiri juu ya namna ya kupata mke? Katika mfano ule, muhubiri alishindwa kuuliza, “Je, Waamuzi anaagiza Agizo hili au ni namna tu kuelezea kitendo?” Waamuzi 21 inaelezea matendo ya Waisrael; haiagizi kufuata tabia.
Unaposoma historia, tunatakiwa kuuliza, “Je, huu ni mfano wa kufuata?” au “Je, haya ni maelezeo ya habari?” Katika hali nyingi, jibu ni rahisi; hakuna anayeweza kufikiri kwamba Waamuzi 21 inatuagiza sisi kuteka mke! Hata hivyo, hali nyingi haziko wazi. Kitabu cha Matendo ya Mitume mahususi kabisa ni kigumu. Je, kanisa litegee Mungu kufanya Miujiza ambayo ilifanyika katika siku za kanisa la kwanza? Je waamini walijazwa na Roho Mtakatifu watanena kwa lugha mpya?
Ni kwa namna gani sasa tutaweza kuamua endapo kifungu kinatupa sisi kielelezo cha kufuata? Kama hatutajibu swali hili kwa usahihi, hatutasoma kwa usahihi vitabu vya kihistoria kama vile Waamuzi na Matendo ya Mitume. Kama hatutajibu swali hili kwa usahihi, tutasisitiza au kupuuza taarifa za kibiblia kwa kutegemea upendeleo wetu. Kumbuka kanuni hii: kama kifungu cha historia kinatupa sisi kielelezo cha kufuata, tunategemea kupata maelekezo ya wazi au mifano iliyorudiwa katika vifungu vingine.
Kwa mfano, Matendo ya Mitume inaonesha kwamba wakristo wa kwanza walikuwa na shahuku kuhusiana na uinjilisti. Tunafahamu kwamba huu ni mfano kwetu sisi kuufuata kwa sababu Mathayo 28:19-20 inatuagiza sisi kufanya wanafunzi. Matendo ya Mitume inaonesha kazi za Roho Mtakatifu katika kanisa. Tunafahamu kwamba hii inatakiwa kuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kanisa kwa sababu Yesu aliahidi kwamba Roho Mtakatifu atatia nguvu huduma ya wafuasi wake (Matendo ya Mitume 1:8). Kama tutashindwa kuhubiri au kuonesha nguvu ya Roho Mtakatifu katika huduma zetu, hatuishi sawasawa na kielelezo cha Matendo ya Mitume. Habari hizi ni kielelezo kwa kanisa.
Matendo ya Mitume pia inatueleza kwamba wakristo walikuwa na vitu vyote shirika na waliabudu katika nyumba za binafsi. Je, haya ni maagizo kutoka katika maandiko? Hapana. Utaratibu wa kuwa na vitu vyote shirika ulikuwa wa hiari, si lazima, kama Petro alivyomwambia Anania (Matendo ya Mitume 5:3-4). Vivyo hivyo, maandiko hayatuagizi sisi kuabudu katika nyumba binafsi.[1]
Kwa sababu matendo haya hayajaagizwa katika maandiko, tunaweza kuhitimisha kwamba ni sehemu ya historia ya kanisa lakini si lazima kwamba ni kielelezo kwa sisi kufuata. Matendo ya Mitume inaelezea kipindi fulani katika historia; haiagizi matendo haya kwa nyakati zote.
(4) Je, ni kanuni gani zinazofundishwa katika simulizi ya kihistoria?
Kutokana na Paulo, historia ya Biblia inatolewa kwa ajili ya maelekezo (1 Wakorintho 10:11). Inaonesha namna Mungu anavyofanya kazi katika historia na kile kinachompendeza au kisichompendeza Mungu. Kama wasomaji, tunatakiwa kutafuta kanuni kutoka katika simulizi za kihistoria.
Mara chache sana habari inasema, “Waisraeli walimlalamikia Mungu na wanaadhibiwa. Hautakiwi kumlalamikia Mungu.” Badala yake, tunaambiwa kwamba Waisraeli walimlalamikia Mungu na tunaona madhara ya dhambi yao, na tunapaswa kuelewa kanuni inayofundishwa. Badala ya maagizo ya moja kwa moja, historia inatupa kielelezo chanya ili kufuata na kielelezo hasi ili kuepuka. Katika kitabu cha Yoshua, tunaona utii kwa maagizo ya Mungu ulileta ushindi; katika kitabu cha Waamuzi, tunaona kwamba uasi kunaleta machafuko.
Kitabu cha Matendo ya Mitume
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatoa habari ya kihistoria ya kile kilichotokea baada ya maisha ya Yesu hapa duniani. Kwa wasomaji wa Agano Jipya, Matendo ya Mitume Inatoa muktadha kwa nyaraka zilizoandikwa kwa makanisa.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonesha kwamba kanisa, likiwezeshwa na Roho Mtakatifu, lisingeweza kuzuiwa katika utume wake wa kueneza Injili. Kanisa lilipitia mambo ya kimafundisho, migawanyiko ya ndani, changamoto katika uongozi, unafiki, upinzani wa kipepo, mateso kutoka kwa jamii, na majanga katika safari. Hata hivyo, kanisa lilitembea kifua mbele kwa furaha likishinda. Kwa sababu Roho Mtakatifu alilitia nguvu kanisa, watu binafsi na jamii zilibadilishwa na Injili.
Lengo la Luka kuandika Matendo ya Mitume lilikuwa ni kulipa kanisa ujasiri wa kuendelea kuutimiza utume wake wa kuufikia ulimwengu kwa Injili. Kusudi lake linaonekana katika kitabu chote katika dondoo zifuatazo. Dondoo nyingine za nyongeza zinaweza kuongezwa.
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kupeleka Injili hadi mwisho wa dunia (Matendo ya Mitume 1:8).
Roho aliwatia nguvu wanafunzi kuhubiri Injili siku ya Pentekoste, na watu 3,000 waliamini (Matendo ya Mitume 2:41).
Watu walikuwa wakiongezeka katika kanisa kila siku (Matendo ya Mitume 2:47).
Kiongozi wa kidini Gamalieli alisema kwamba kazi ya Mungu haiwezi kuzuiwa (Matendo ya Mitume 5:39).
Waamini walioteswa waliondoka Yerusalemu na kueneza Injili (Matendo ya Mitume 8:1, 4).
Kiongozi wa mateso alibadilishwa na akawa muinjilisti mkubwa (Matendo ya Mitume 9:13-22).
Paulo na wengine walifanya safari za kimisheni katika ulimwengu uliojulikana wa wakati ule (Matendo ya Mitume 13-21).
Paulo aliwahubiria watawala (Matendo ya Mitume 24-26).
Paulo alihubiri Rumi, mji mkuu wa dola (Matendo ya Mitume 28).
Matumizi ya Kitabu cha Matendo ya Mitume
Wakati mwingine msomaji anaweza kufikiri kwamba kitabu cha Matendo ya Mitume kinatueleza sisi ni kwa namna gani tufanye kazi ya kimisheni, kubatiza, kupanda kanisa, na uzoefu wa Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume inanakili namna ambavyo kanisa la kwanza lilifanya hayo mambo yote; hata hivyo, mwandishi hakukusudia kitabu cha Matendo ya Mitume kiwe kitabu cha maelekezo kwa huduma.
Hatupaswi kufikiri kwamba tunapaswa kufanya kwa namna ile ile ambayo kanisa la kwanza walifanya katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini tunaweza kujifunza mengi kutokana na vile tumeona kanisa lilivyokabiliana na changamoto.
Matendo ya Mitume inatuonesha sisi kwamba kanisa linatakiwa kuendelea kufika mbali na injili, mara zote likue na kupambana na matatizo yote kwa nguvu na hekima ya Roho Mtakatifu, likitengeneza Muundo kutokana na uhitaaji ili kutatua matatizo kwa vitendo.
[1]Baadhi ya wakristo duniani leo wanaona kwamba kuabudu nyumbani ni salama zaidi kuliko kukusanyika katika sehemu za umma. Hii ni kulingana na mazingira, na si Agizo kuu.
Aina ya Fasihi: Sheria za Agano la Kale
Thamani ya Sheria za Agano la Kale
Baadhi ya Wakristo wanafikiri kwamba Agano la Kale linamatumizi machache kwa waamini wa leo ispokuwa tu zile sehemu ambazo zinaelezea kanuni za Kikristo. Wanafikiri kwamba Sheria za Agano la Kale hazina matumizi kwa waamini wa leo.
Mtume Paulo aliandika mara nyingi kuhusu mabadiliko ya matumizi ya sheria za Agano la Kale kwa mwamini. Alisema kwamba kifo cha Kristo kiliondoa hukumu ya sheria na kwamba hatupaswi kuwahukumu waamini ambao hawafuati taratibu za sheria ya Agano la Kale (Wakolosai 2:14-17). Alisema kwamba mitume hawaishi tena chini ya matakwa ya kisheria za Kiyahudi (Wagalatia 2:14-16). Alikataa mchungaji mmataifa kutahiriwa (Wagalatia 2:3). Alisema kwamba kila mmoja anatakiwa kufuata dhamiri yake kuhusiana na chakula cha kiyahudi na siku na kwamba waamini hawapaswi kuhukumiana kuhusiana na matakwa haya (Warumi 14). Alisema kwamba mwamini aliifia sheria na kwamba tunamtumikia Mungu katika namna ambayo inatimiza makusudi ya sheria lakini si matakwa ya sheria kimahususi (Warumi 7:4, 6). Muhimu zaidi, alisema kwamba hakuna atakayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria (Warumi 3:20).
Biblia pia iantoa matamko kuhusiana na sheria za Agano la Kale likionesha kwamba bado zina umuhimu kwa mwamini. Kwa sababu sheria za Agano la Kale zilikuwa ni maelelezeo ya asili ya Mungu, mtu anayempenda Mungu atapenda na sheria zake (Ona Zaburi 1:2, Zaburi 119:7, 16, 70). Paulo alisema kwamba sheria ni takatifu, yenye haki, na nzuri (Warumi 7:12). Alisema pia, “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki” (2 Timotheo 3:16). Wakati anatamka tamko hili, neno maandiko kimsingi lilirejelea Agano la Kale. Paulo alimwambia Timotheo kwamba maandiko yanamfanya yeye mwenye hekima kwa ajili ya wokovu (2 Timotheo 3:15). Matamko haya yanatuambia kwamba kama waamini hatupaswi kuiacha sehemu yeyote ya Agano la Kale. Hata kama hatuokolewi kwa kufuata sheria za Mungu, tunataka kuelewa kusudi lake kwetu ili kwamba tuweze kumpendeza Yeye (2 Wakorintho 5:9-10).
Mgawanyo wa Sheria za Agano la Kale
Ili kutusaidia kuelewa kwa namna gani waamini wanatakiwa kuzitumia Sheria za Agano la Kale leo, tumechunguza na kuona aina baadhi ya makundi ya sheria.
Sheria za Kiibada zilikuwa ni kuhusu dhabihu, taratibu za kidini, vyakula, na siku maalumu. Paulo anasema kwamba sheria hizi zilitimilizwa ndani ya Kristo (Wakolosai 2:16-17). Kitabu cha Waebrania kinatoa matumizi ya kina ya maana ya ibaada za Agano la Kale. Kwa mfano, karibu vitu vyote katika hekalu husafishwa kwa damu, ikiwakilisha damu ya Yesu ambayo itasafisha Waamini (Waebrania 9:14, 21-24).
Sheria za Kiraia zilitolewa kwa Taifa la Israeli. Sheria za kiraia hazijaanzishwa na mtu mmoja mmoja, bali zilianzishwa na mamlaka zilizochaguliwa. Kwa mfano, watu waliofanya uchawi waliuawa (Kutoka 22:18), lakini kesi na adhabu zilifanywa na mamlaka iliyowekwa, na si na raia mmoja mmoja. Kumbukumbu la Torati 17:2-12 inelezea mchakato wa serikali ya mji kusikiliza mashahidi na kutoa hukumu ya haki; mahakama ya juu ilikuwepo kwa ajili ya kezi zilizokuwa ngumu zaidi.
Sheria za nchi zinaweza kuwa tofauti leo, na waamini mmoja mmoja hapaswi kuchukua wajibu binafsi kwa kutimiliza sheria za kiraia za Israeli ya kale. Hata hivyo, sheria hizo zinatufundisha sisi kuhusiana na haki ya Mungu na haki ambayo anaitarajia kutoka kwa watu wake. Kwa mfano, sharia ilitolewa katika Kutoka 22:18 inatuambia kwamba si sahihi kwa mtu kufanya uchawi. Sheria zingine za kiraia zinatueleza kwamba Mungu anataka taifa kuwalinda masikini na kupinga mambo yasiyo ya haki kwa watu wote (Kumbukumbu la Torati 24:14-15, 17-22).
Mtafsiri wa Biblia anajaribu kwanza kuelewa kanuni ya sheria mahususi za kiraia za Agano la Kale, kisha anazingatia namna ambavyo mwamini anatakiwa kutendea kazi kanuni hiyo. Tunatakiwa kuuliza, “Mungu alikuwa anajali nini? Kusudi la Mungu lilikuwa nini? Sheria hii inafunua nini kuhusiana na maadili ya Mungu?” Kisha tunaangalia matumizi ya wakati huu ya ambayo yatampendeza Mungu.
Sheria za Kimaadili zilitaja matakwa ya kudumu ya Mungu kwa ajili ya kuishi vema. Sheria za kimaadili zinazungumzia uaminifu, mambo ya kijinsi, kuabudu sanamu, na mambo mengine (Kutoka 20:4-5, 13-16). Sheria nyingi za kimaadili zimerudiwa tena katika Agano Jipya. Sheria za kimaadili ni msingi wa sheria za kiraia za nchi nyingi leo, ingawaje sheria za nchi hazifuati sheria za Mungu kwa usahihi. Sheria za Mungu kwa ajili ya watu wake zinaenda mbali zaidi ya kile ambacho jamii inahitaji.
Mgawanyo wetu wa makundi ya sheria si kamilifu. Vifungu katika Agano la Kale wakati mwingine inajumuisha makundi yote matatu ya sheria na sheria ambazo ni ngumu kuziweka katika makundi. Hata kama sio kamilifu, mfumo wa mgawanyo huu unatusaidia sisi kuelewa sheria za Agano la Kale ambazo zinatenda kazi kwa waamini wa Agano Jipya.
Unapojifunza sheria za Agano la Kale, zingatia muktadha mpana wa sheria unayojifunza. Kuwa makini na mazingira yanayozunguka simulizi. Ni kwa jinsi gani sheria inakaa vema katika muktadha?
Kisha uliza:
(1) Andiko hili lilimaanisha nini kwa wapokeaji wa kwanza?
Ili kuelewa namna Israeli walitafsiri sheria, uliza maswali kama vile:
Je, kuna muunganiko kati ya sheria na mazingira yanayozunguka mistari?
Je, sheria ni mwitikio wa hali mahususi inayohusiana na historia ya Israeli?
Je, sheria inahusiana na mfumo wa haki wa Agano la Kale?
(2) Ni tofauti gani iliyopo baina ya wapokeaji wa Biblia na ulimwengu wetu?
Zipo tofauti nyingi kati ya ulimwengu wetu na wa Agano la Kale kuliko kati ya ulimwengu wetu na ule wa Agano Jipya. Kwa mfano:
Hatutembelei tena hekalu moja; Roho Mtakatifu anakaa ndani ya kila mwamini.
Hatumwendei Mungu kwa dhabihu, Yesu Kristo alikufa mara moja kwa zote (Waebrania 10:10).
Neno la Mungu si sheria kwa nchi zetu. Tunaishi chini ya serilaki za kidunia.
(3) Ni kanuni gani zinazofundishwa katika andiko hili?
Tendo mahususi linalotakiwa na sheria za Agano la Kale linaweza lisihitajike leo. Tunatakiwa kutafuta kanuni ya kudumu inayofundishwa na sheria. Hili ni Daraja ambalo linaleta andiko kutoka mazingira ya kale katika ulimwengu wa leo. Kanuni hii itakuwa na mahusiano kati ya wapokeaji wa Agano la Kale na wapokeaji wa leo.
Taja kanuni katika sentensi 1-2. Ili kuhakiki endapo kanuni ni ya kibibli, uliza maswali haya:
Je, kanuni inaoneshwa kwa uwazi na sheria?
Je, kanuni hii inaweza kutumiwa na watu wote katika nyakati zote na mahali pote?
Je, kanuni hii inakubaliana na maandiko mengine?
(4) Je, Agano jipya linachukua kanuni hizi kwa namna yeyote?
Kila mojawapo la maswali matatu yaliyopita yatumika katika tafsiri yeyote ya kifungu chochote cha maandiko. Swali hili la mwisho linatakiwa kuongezwa kwenye mchakato wa tafsiri wakati tunapojifunza maandiko ya Agano la Kale. Kama umepata kanuni ya kudumu ya kifungu cha Agano la Kale, kanuni hiyo itabakia na matokeo yale yale leo. Hata hivyo, Agano Jipya linaonesha kwamba matumizi yanatofautiana na nyakati za Agano la Kale.
Kwa mfano, Kutoka 20:14 inaagiza, “Usizini.” Katika mafundisho ya Yesu ya mlimani, Yesu anapanua hii ili kugusa mawazo, na si tu kitendo (Mathayo 5:28). Mafundisho ya Yesu hayaondoi kanuni ya Kutoka 20:14; yanapanua matumizi yake.
[1]Sehemu hii imetolewa kutoka J. Scott Duvall na J. Daniel Hays, Grasping God’s Word (Grand Rapids: Zondervan, 2012).
Aina ya Fasihi: Ushairi
Biblia ina ushairi mwingi. Ayubu, Zaburi, Mithali, na Wimbo ulio Bora karibu yote ni ushairi, na Mhubiri inajumuisha baadhi ya ushairi. Kuna ushairi pia katika manabii. Ushairi ni aina ya uandishi ambayo inaonesha hisia kali. Haikuundwa ili kuwasilisha taarifa za kina za kihistoria au kutengeneza majadiliano ya kimantiki. Katika ushairi, tunausikiliza moyo wa mshairi; mahususi kabisa tunakuwa makini na hisia zinazooneshwa katika ushairi.
Mara nyingi ushairi unatumia tamathali za semi, na ni maelezeo ambayo hayakusudiwi kuchukuliwa kama lugha ya kawaida.
Hapa ni mfano wa tamko la kiushairi kutoka katika Zaburi: “Kwa upote wa uta wako [Mungu]ukiwaelekezea mishale” (Zaburi 21:12). Tunagundua kwamba kwa kawaida Mungu hana uta ambao atautumia kupiga mishale ya kawaida. Mwandishi anasema kwamba Mungu anaweza kumshinda yeyote ambaye anachagua kuwa adui yake. Mwandishi anawaeleza waamini kuwa na ujasiri na ushindi wa Mungu.
Mara nyingi ushairi unafanya kusudi la kufikirika ukiwasilisha kweli ambao umetajwa wazi sehemu nyingine katika Biblia. Usitengeneze kanuni ya imani au kutendea kazi kutoka katika kifungu cha ushairi kama haijafundishwa kwa uwazi katika vifungu vingine.
Mashairi ya Kiebrania wakati mwingine yanatumia muundo wa sauti lakini hawatumii vina na mizani kama mashairi ya Kiswahili yanavyotumia. Kuelewa sifa za mashairi ya Kiebrania kutakusaidia wewe kuelewa vema na kutambua uzusi wake.
Sifa za Mashairi ya Kiebrania
Usambamba
Mara nyingi mashairi ya Kiebrania yana msingi katika usambamba. Sentensi mbili zilizo sambamba zinatumika pamoja; sentensi ya pili inaongeza maana zaidi kwa ile ya kwanza lakini si kila wakati inaongeza taarifa mpya.
Kuna aina tatu za usambamba:
Mstari unaosema kitu kile kile kwa namna mbili tofauti (Zaburi 25:4, Zaburi 103:10, Mithali 12:28).
Mstari unaoonesha utofauti baina ya vitu viwili (Zaburi 37:21, Mithali 10:1, 7).
Mstari unaotoa tamko kisha unaongeza taarifa zaidi katika sentensi inayofuata (Zaburi 14:2, Zaburi 23:1, Mithali 4:23).
Tunapotafsiri usambamba, tunauliza mstari wa pili unaongeza nini katika mstari wa kwanza. Je, unajenga mtari wa kwanza, je, unatoa ukinzani kwa mstari wa kwanza, au je unongeza taarifa mpya?
Tamathali za Semi
Wakati vitabu vyote vya Biblia vinajumuisha tamathali za semi, hizi ni maaluhusi sana katika mashairi. Tamathali za semi zinazopatikana katika mashairi ya Kiebrania zinajumuisha:
1. Ulinganifu wa vitu viwili ambavyo vinafanana kwa namna fulani: “BWANA ndiye mchungaji wangu” (Zaburi 23:1).
2. Kutumia mubaraga ili kusisitiza jambo. Daudi anaelezea uchungu wake namna hii: “Kila usiku nakieleza kitanda changu...kwa machozi yangu” (Zaburi 6:6).
3. Kukizungumzia kitu kana kwamba ni mwanadamu: “Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja” (Mithali 1:20).
4. Kumuelezea Mungu kwa kutumia sifa za mwanadamu: “Macho (ya Mungu)... yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu” (Zaburi 11:4).
Unapotafsiri tamathali za semi, uliza taswira inayoonesha ambayo tusingeielewa endapo katika maelezo ya kawaida. Kwa mfano, “BWANA ndiye mchungaji wangu” ni zaidi ya “Mungu ananijali mimi.” Inazungumzia kujali, lakini pia inazungumzia upendo, uongozi wake, ulinzi wake kutoka kwa adui zetu, na nidhamu wakati tunatanga mbali na kujali kwake.
Kitabu cha Zaburi
Aina za Zaburi
Zipo aina kadhaa za Zaburi. Zaburi za sifa zinamheshimu Mungu kwa sifa, baraka, na kuingilia kati kwakwe (Zaburi 23, 29). Zaburi kuhusiana na sharia za Mungu zinamsifu Mungu kwa hekima na haki yake (Zaburi 119). Zaburi za huzuni zinaonesha hisia kwa Mungu, zikimuuliza msaada wake, na mzaburi kujitoa kwa mapenzi ya Mungu (Zaburi 3, 13, 22). Zaburi kuhusiana na mfalme zinaelezea baraka ambazo zinakuja kwa taifa kupitia mfalme anayemcha Mungu, na Zaburi hizo pia zinaelekeza kwenye ufalme ujao wa kimasihi (Zaburi 21, 72). Zaburi za hasira zinamuita Mungu kuamua kwa haki watu waovu na kuwatetea watumishi wake (Zaburi 69:21-28, Zaburi 59). Aina nyingine ya Zaburi zinaweza kuorodheshwa.
Matumizi ya kitabu cha Zaburi
Agano Jipya linatueleza sisi zaidi kuhusiana na Zaburi. Zaburi zinaelezea ibaada yetu kwa Mungu (Waefeso 5:19). Pia ni zinatummika kwa mafundisho na kutia moyo (Wakolosai 3:16).
Si kila mtazamo unaooneshwa na Zaburi ni mfano wa mtazamo tunaotakiwa kuwa nao. Hata hivyo, tunajifunza kutoka kwa Zaburi kwamba kila mtazamo unatakiwa kujitiisha kwa Mungu. Katika maombi, unaweza kumuelezea Mungu hisia zozote ulizonazo. Zaburi zinatuonesha kwamba Mungu anaweza kufanya upya imani ya mwamini ambaye anasumbuka na kuvunjwa moyo, hofu, na hasira.
Aina ya Fasihi: Mashairi yenye Hekima
Ayubu, Mithali, Mhubiri, na sehemu za Zaburi na Yakobo zinawasilisha kundi linalojulikana kama Mshairi yenye hekima. Katika kitabu cha Mithali na Mhubiri, maelekezo yanaelekezwa kwa wasomaji Vijana ambao wanajifunza kanuni za maisha.
Kitabu cha Ayubu
Vifungu virefu katika Ayubu vinatoa maneno ya wazungumzaji mbalimbali wa kibinadamu, wakiwemo Ayubu mwenyewe. Wazungumzaji wanaonesha mawazo tofauti tofauti. Mtafsiri wa Biblia hatakiwi kuchukulia maelezo kutoka katika mazungumzo ya wanadamu na kuyafundisha kama kanuni za kibiblia. Kitabu cha Ayubu kinachanganua kwa undani maelezo hayo na maneno na mtazamo wa Mungu. Katika Ayubu 38-42 Mungu anajibu mazungumzo, na Ayubu 1-2 pia inaonesha mtazamo wa Mungu.
Aina ya Fasihi: Mithali
Mithali ni Uchunguzi wa maisha ambao unatajwa kwa ufupi na kwa wazi. Zinataja kile ambacho mara nyingi kunatokea, lakini hazimaanishi kwamba hakutakuwa na mambo yasiyo ya kawaida/mambo ya kipekee.
Kwa juu juu, mithali ni rahisi kutafsiri. Hata hivyo, aina hii ya fasihi inaleta changamoto mahususi. Mithali inataja kanuni ya jumla kuhusiana na maisha, lakini kanuni hizi hazifanyi kazi katika kila mazingira. Kwa mfano, Mithali 21:17 inasema,
Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri.
Kama kanuni ya msingi, wale wanaopenda anasa kuliko kufanya kazi watakuwa masikini. Hii kanuni ya jumla ni kweli, lakini ina mambo mengi ya kipekee yasiyo ya kawaida. Baadhi ya matajiri wamerithi utajiri wao pasipo kufanya kazi. Wanatumia siku zao kunywa na kucheza, lakini ni matajiri. Watu wengine wanafanya kazi kwa bidii na wanabaki masikini. Mithali inafundisha kanuni ya jumla, lakini si kanuni kuu.
Kuna Mithali nyingi kwenye Biblia, si tu katika kitabu cha Mithali. Hapa ni mfano wa Mithali iliyosemwa na Yesu: “…wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga” (Mathayo 26:52). Wapo watu wakorofi ambao hawakufa kwa ghasia. Tena, Mithali ni kweli kwa sababu ni uchunguzi wa jumla, lakini yanaweza kuwepo mambo yasiyo ya kawaida au ya kipekee.
Tunapaswa kuuliza maswali haya tunapotafsiri mithali:
(1) Ni kanuni gani za jumla zinazofundishwa katika andiko hili?
Kanuni inayopatikana katika Mithali 21:17 ni thamani ya kufanya kazi kwa bidi na nidhamu. Mithali nyingi zinafupisha kanuni ambayo inaweza kutengenezwa katika kifungu kimoja cha maneno.
(2) Je, ni hali gani za zisizo za kawaida zinazoweza kutokea katika kanuni hii?
Kuhusiana na Mithali 21:17, tunaona mambo yasiyo ya kawaida katika maisha ya kila siku; inaonesha tu kwamba mtu mwenye busara anatakiwa kutambua kwamba kuna mambo yasiyo ya kawaida kwa kila kanuni ya jumla.
(3) Ni watu gani katika Biblia ni kielelezo cha kanuni hii?
Unapotafsiri mithali, ni msaada mkubwa sana kumtafuta muhusika katika Biblia ambaye anatoa kielelezo cha kanuni ya mithali. Kwa mfano, Mithali inasema, “Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu” (Mithali 11:2). Kiburi cha Sauli na unyenyekevu wa Daudi wa kukiri dhambi unaonesha namna mithali hii inafanya kazi katika maisha halisi.
Kitabu cha Mithali
Sehemu kubwa ya kitabu cha Mithali kiliandikwa na Sulemani. Kusudi lililotamkwa la kitabu ni kumsaidia mtu ambaye hajakua kupata hekima na kumsaidia mwenye hekima kuwa na hekima zaidi (Mithali 1:4-5).
Kitabu cha Mithali kinazungumza kuhusiana na aina tatu za watu. Mjinga amekua na kuwa mtu mzima lakini bado hajapata uzoefu na uelewa wa maisha. Mtu wa kawaida anatakiwa kupata hekima na kuepuka makossa ambayo yatamuharibu.
Mwenye hekima ni yule anaye elewa namna ya kuishi sawasawa na kanuni za Mungu. Ni lazima watu wamuhofu Mungu kama wanataka kuwa wenye hekima (Mithali 9:10). Wenye hekima huendelea kujifunza.
Mpumbavu amekataa hekiama (kanuni za Mungu) na amekataa kusikiliza. Anaonesha tabia mbaya na anateseka kwa kufanya maamuzi mabovu. Siyo kwamba mpumbavu hana akili, bali hayaelewi maisha kwa sababu amekataa maongozi ya Mungu.
Baadhi ya dhana kuu katika kitabu cha Mithali ni (1) hatari ya uvivu na thamani ya kazi (2) majanga yanayotokea kutokana na uasherati na uzinsi, na (3) maadili katika aina mbalimbali za mahusiano.
Kitabu cha Mhubiri
Kitabu cha Mhubiri kiliandikwa na Sulemani (Mhubiri 1:1).
Ujumbe wa Mhubiri: kama tu maisha haya yapo, hakuna haki au kusudi katika maisha au mfanikio yeyote makubwa.
Mhubiri anaelezea kwa nini maisha ya duniani hayawezi kuwapa watu utoshelevu au kusudi. Katika maisha haya:
Haki imepuuzwa.
Kila mtu anakufa na anasahaulika.
Waovu hufanikiwa.
Hekima ina nguvu lakini imedharauliwa.
Hekima na maarifa yanaongeza huzuni.
Mhubiri anatuonesha kwamba maisha ya mtu anayeishi maisha akiwa na mtazamo wa umilele atakuwa:
Mwenye furaha lakini akiwa makini na mambo ya maisha.
Kumbuka kwamba kifo kinakuja.
Atafurahia mambo mema lakini akikumbuka kuwa anawajibika kwa Mungu.
Hataruhusu lengo lolote la kidunia kuwa la muhimu zaidi.
Sulemani alifikia hitimisho hili: Kwa sababu kuna hukumu, mtumikie Mungu na ushike amri zake tangu ujana.
Aina ya Fasihi: Unabii wa Agano la Kale
Vitabu vya manabii wa Agano la Kale ni mkusanyiko ulioandikwa wa jumbe zilizo hubiriwa. Manabii 16 wana jumbe zilizorekodiwa katika maandiko. Ni Yeremia tu ndiye ana vitabu viwili. Baadhi ya manabii waliandika vitabu ambavyo haviko katika maandiko (1 Mambo ya Nyakati 29:29). Tunaelezwa kwamba wapo mamia ya manabii ambao hawakuandika chochote.
Manabii 16 walioandika walihudumu kati ya miaka ya 760-460 K.K. (Israeli ilianguka mwaka 722. Yuda ilianguka mwaka 587.) Katika kipindi hiki, kuinuka na kuangujka kwa dola mbali mbali za ulimwengu kulikuwa na mchango kwa Israeli kisiasa, kiuchumi, na kidini. Kuna wakati, wengi wa watu wa mataifa ya Yuda na Israeli walivunja agano lao na Mungu na kutumiakia miungu.
Manabii walikuwa watetezi wa agano la Mungu. Waliwakumbusha watu matakwa ya Mungu. Miaka kadhaa kabla, Mungu aliahidi Israeli kwamba Israeli wangepokea baraka au laana kwa kutegemea utii wao kwake (Mambo ya Walawi 26, Kumbukumbu la Torati 28-32). Manabii walitabiri kutimilika kwa ahadi hizo. Baraka zilizoahidiwa katika utii ni pamoja na uhai, afya, mafanikio, utele katika kilimo, uhuru, na usalama. Laana kwa kutotii ni pamoja na mauti, magonjwa, ukame, njaa, kuvunjika kwa familia na miji, kushindwa vitani, uhamisho toka nchini kwao, kupoteza uhuru, umasikini, na aibu.
Unabii ulikuwa ni mawasiliano ya ujumbe toka kwa Mungu. Unabii ulikuwa ni mahubiri, yakishughulikia jambo lililoppo na yalihitaji mwitikio wa haraka. Ujumbe wa manabii mara nyingi ulijumuisha na utabiri. Hata hivyo, nabii alikuwa mhubiri. Ujumbe wake ulikuwa wa kinabii ama alikuwa anatabiri au la.
Katika namna nyingi, hatujui ni kwa namna gani au lini utabiri uliokuwa ndani ya unabii ulitimilika. Ufahamu huo hauhitajiki sana kwa sisi kujifunza kutoka katika vifungu hivyo. Mara nyingi, utimilifu haukutokea ndani ya maisha ya nabii na wasikilizaji wake, lakini ujumbe huo ulihubiriwa kwa ajili matumizi na mwitikio wa haraka. Nabii alionesha ufalme wa Mungu unaokuja kama sababu ya watu kutubu na kumtii Mungu katika wakati uliopo (Habakuki 2:14).
Njia za manabii kuwasiliana na kuelezea mara nyingi zilikuwa si za kawaida na zenye lugha ya picha. Jumbe zao zilikuwa za kitamathali na mara nyingine zilijumuisha maonesho ya kawaida ya kimwili. Hata hivyo, hawakuhubiri kwamba watu wafanye jambo fulani jipya au lisilo la kawaida, bali kwamba wanatakiwa kutii sheria za Mungu zilizofunuliwa.
Mahubiri ya manabii, ambayo yalikuwa ni ili kuwaleta watu tena katika matakwa ya agano (mahusiano yao na Mungu), yanaweza kuhubiriwa leo na kuwaleta watu katika matakwa ya mahusiano yetu na Mungu.
Utabiri (hata wa yale matukio ambayo yatatokea mbeleni kabisa) yalikusudiwa kuwa na matokeo ya karibu. Watu waliitwa ili kutubu na kumtii Mungu. Kusudi hili linafanana na kusudi la mahubiri ya leo.
Baadhi ya utabiri ulikuwa na masharti. Wasikilizaji wangeepuka hukumu iliyotabiriwa kwa kutubu (Yeremia 18:7-11, Yeremia 26:13-19). Wasikilizaji wa Yona katika Ninawi waliepuka uharibifu hata kama ujumbe wa Yona haukutoa rehema (Yona 3:4-5, 9-10).
Utimilifu wa kusudi la Mungu hauna masharti; kwa mfano, katika Isaya 43:5-6 ahadi ya Mungu kwamba atawarejesha mateka tena kurudi Israeli kwa nguvu zake, lakini kifungu hakitoi masharti ambayo ni lazima kutimizwa na Israeli. bado, nafasi ya mtu katika matukuio haya yapo katika masharti ya uchaguzi wa mtu husika.
Vitabu vya unabii vina vifungu vya simulizi za kihistoria, lakini mara nyingi zikiwa katika muundo wa ushairi. Sio ngumu kutofautisha simulizi ya kihistoria ambayo ni lazima itafsiriwe kama lugha ya kawaida tofauti na vifungu vya ushairi ambavyo vinajumuisha alama.
Maneno Muhimu na Dhana katika Manabii
Ibada ya sanamu: Uvunjaji mkuu wa agano.
Uzinzi: Dhambi ambayo mara nyingi iliambatana na ibada ya sanamu na ilitumika kitamathali kurejelea ibada ya sanamu.
Mataifa: Inarejelea ulimwengu ambao haukuwepo katika agano la mahusiano na Mungu. Dhana mbili ndogo:
1. Mara nyingi mataifa walikuwa na chuki na Israeli.
2. Mungu alikusudia Israeli wamtukuze yeye kati ya mataifa.
Hekalu: Kituo kikuu cha uwepo wa Mungu. Dhana mbili ndogo:
1. Ibada ya kinafiki haikumuheshimu Mungu.
2. Maadui kuvamia kwa hekalu ilionesha kushindwa vibaya kwa Israeli na kupoteza uwepo wa Mungu.
Nchi/Urithi: Sehemu maalumu ambayo Mungu aliwaweka Waisraeli ili wabarikiwe.
Utumwa: Kutolewa katika sehemu aliyowapa Mungu, na kutumikishwa na mataifa mengine. Utumwa ulimaanisha kwamba Israeli wamepoteza Baraka za Mungu.
Mvua(na maneno yanayohusiana): Alama ya baraka endelevu za Mungu katika nchi ambazo aliwapa Waisraeli. Kukosekana kwa mvua kulizungumzia kutokukubalika na Mungu.
Mavuno (na maneno yanayohusiana): Baraka za Mungu zinahusiana na dhana ya mvua na nchi.
Siku ya Bwana: Hukumu ya ghafla ya Mungu ya mbeleni ambayo itawaharibu waovu. Israeli walifikiri kwamba hukumu ni kwa ajili ya mataifa na waliogopa sana kusikia kwamba watahukumiwa pia.
Farasi: Waliwakilisha nguvu ya kijeshi.
Kukombolewa kutoka Misri: Tukio la kihistoria ambalo liliwafanya Israeli kama taifa kumfanya Mungu mfalme wao. Kuabudu sanamu kulikuwa ni kukosa heshima kwa agano lililofanyika baada ya ukombozi.
Kutafsiri Fasihi ya Unabii
Fasihi ya unabii ni moja kati ya fasihi ngumu kutafsiri. Ili kutafsiri unabii kwa ufanisi, uliza maswali haya:
(1) Nabii alisema nini kwa ulimwengu wake?
Tofauti kabisa na mawazo ya watu wengi, fasihi ya unabii si kuhusu utabiri wa mbeleni pekee. Nabii alizungumza kwanza na ulimwengu wake.
Kwa mfano, Amosi aliandikwa kwa taifa la Israeli, ambalo lilikuwa linamuasi Mungu. Watu walikuwa wanafanikiwa na walifikiri wanaweza kupuuza sheria ya Mungu pasipo matokeo. Amosi alitangaza ujumbe wa hukumu: Israeli watahukumiwa kwa sababu wameacha haki na hukumu ya haki (Amosi 5:7).
(2) Watu wake waliitikiaje ujumbe wake?
Mwitikio wa Israeli kwa ujumbe wa Amosi unaonekana katika mwitikio wa Amazia, kuhani mkuu huko Betheli. Alimtaka Amosi kurudi Yuda na asihubiri tena katika ufalme wa kaskazini (Amosi 7:10-13).
(3) Ni kanuni gani kutoka katika ujumbe wa nabii inayozungumza katika ulimwengu wetu leo?
Kama ambavyo haki na hukumu ya haki ni viwango vya Mungu katika Israeli ya kale, Mungu anataka haki na hukumu ya haki kutoka kwa watu wake leo. Hatuwezi kumuabudu Mungu katika nyumba ya Mungu huku tukipuuza wito wake wa maisha ya haki (Amosi 5:22-24).
Maswali haya yataleta kweli ya unabii kutoka kwenye ulimwengu wa nabii hadi kwenye ulimwengu wetu. Kwa kuangalia ulimwengu wa nabii, tunahakikisha kwamba tafsiri yetu ina mizizi katika ujumbe wa asili.
Aina ya Fasihi: Fasihi ya Kiapokaliptiki
Maandiko ya kiapokaliptiki inajumuisha Danieli, Zekaria, Yoeli, Ufunuo, na vifungu kadhaa kutoka katika vitabu vingine vya Biblia.
Mwandishi wa kitabu cha apokaliptiki alipokea ujumbe katika maono au ndoto. Imejaa alama nyingi. Mara nyingi hutumia wanyama, au hata wanyama wa kutisha wa ajabu kama alama.
Badala ya kuelezea matukio katika mpangilio wa muda, maandishi yanaweza kuwa yanarudia rudia matukio/mazingira yale yale, maelezo ya tofauti yakitolewa katika kila maelezo.
Kanuni ya kawaida ya kutafsiri maandiko ni kuichukulia kawaida hadi pale inapoonekana kwamba mwandishi alikusudia kutumia lugha ya tamathali. Kwa habari ya fasihi ya kiapokaliptiki, mtafsiri anatakiwa kutambua kwamba mwandishi alikusudia taarifa zake nyingi kuwa za tamathali. Mifano ya maelezo ya tamathali zinaweza kuwa wale wanyama na mnyama wa kutisha katika maono ya Danieli.
Mifano ya alama za wanyama: Danieli 7:3-7, Ufunuo 12:3, Ufunuo 16:13, na Zekaria 6:1-3.
Maandiko ya kiapokaliptiki mara nyingi yanatoa changamoto ya kuitunza imani licha ya maovu na ukosefu wa haki katika ulimwengu wa sasa. Inaelezea mapambano makuu yakiwa na vita kali.
Maandiko ya Kiapokaliptiki katika Biblia yanaonesha ushindi mkuu wa Mungu, ambaye uhukumu maovu na kuzawadia mema. Kiini kikuu ni Mungu Mwenyezi ambaye anakuja kuwasaidia watu wake.
Ujumbe wa msingi wa maandiko ya kiapokaliptiki yanaweza kueleweka hata kama alama zote hazieleweki na hata kama mtafsiri hawezi kuweka mstari wa muda wa matukio ya kinabii.
Mifano ya vifungu vinavyoelezea vita kuu: Yoeli 2:9-11, Ufunuo 19:11-21, na Ufunuo 20:7-9.
Mifano ya vifungu vinavyofundisha ushindi wa mwisho na ufalme wa milele wa Mungu: Danieli 7:14, 27 na Zekaria 14:9.
Pamoja na vitabu vya kiapokaliptiki, sehemu nyingine za maandiko zinaweza kuwa za kiapokaliptiki kwa sababu zinazungumza kuhusu Mungu kuingilia kati kwa haraka wakati anahukumu nguvu ya uovu na kuwaokoa wenye haki. Si Maandiko haya yote yana tabia nyingine za maandiko ya kiapokaliptiki, kama vile alama za maono, wanyama. (Mifano ni Ezekieli 37-39, Isaya 24-27, Mathayo 24, Marko 13, Luka 21, 2 Wathesalonike 2, and 2 Petro 3.)
Matumizi ya Jumla ya Maandiko ya Kiapokaliptiki
Suluhisho kuu la uliwmengu huu si maendeleo ya kitamaduni au kijamii. Sio mageuzi ya kisiasa au mapinduzi. Suluhisho ni Mungu kuingilia kati. Kwa sasa anatupa imani, nguvu, na huruma kwa watu wake. Mbeleni atakuja kwa ghafla na kuubadilisha ulimwengu kikamilifu.
Waamini wanatakiwa kuwa wavumilivu katika imani. Uelewa uliokamilika wa sasa wa mpango wa Mungu au matukio katika ulimwengu si muhimu sana. Kuwa na imani haimaanishi kwamba watu wanaweza kubashiri matokeo fulani ya karibuni. Badala yake, watu wenye imani halisi wanamtii Mungu katika hali zote, kwa sababu wanafahamu kwamba mwishowe utii unathamani.
Aina ya Fasihi: Mfano
Mfano ni nyenzo ya kufundishia ambayo inalinganisha ukweli wa kiroho na vitu katika asili au hali halisi za maisha. Mfanano kati ya kiroho na kiasili unaoneshwa ili kwamba tuelewe vizuri kweli ya kiroho.
Kutoa mifano ilikuwa ni njia mojawapo aliyoipendelea Yesu kama njia yake ya kufundishia (Mathayo 13:34). Alitoa mifano 30 na anatumia mifanano ya tamathali.
Kupitia mifano, Yesu alifundisha maombi (Farisayo na Mtoza ushuru hekaruni, Luka 18:9-14), upendo kwa majirani zetu (msamaria mwema, Luka 10:29-37), asili ya ufalme wa Mungu (mifano katika Mathayo 13), na huruma za Mungu kwa wenye dhambi (mwana mpotevu, Luka 15:11-32).
Mifano ilimruhusu Yesu kuwakemea wasikilizaji wake bila kukabiliana nao moja kwa moja. Kwa sababu mifano ya Yesu iliyotolewa ilikuwa inavutia sana, ilifungua masikio ya wasikilizaji wa Yesu kwa maneno yake hadi pale ambapo walishtuka na kutambua “Ananiongelea mimi!” Nathani nabii alifanya vivyo hivyo alipomwambia Daudi mfano wa masikini mwenye kondoo mmoja (2 Samweli 12:1-10). Ni hadi Nathani aliposema, “Wewe ndiwe mtu huyo,” ndipo Daudi alitambua kwamba mfano ulikuwa unamuhusu yeye mwenyewe.
Kutafsiri Mfano
Mtafsiri anatakiwa kuwa makini na:
Ni kwa namna gani mfano ulitolewa?
Hitimisho la mfano lilikuwa ni nini?
Ni mwitikio gani au mabadiliko gani ya mtazamo ambayo mfano unatoa?
Wapokeaji wa kwanza walikuwa na mwitikio gani?
(1) Ni kwa namna gani mfano ulitolewa?
Mara nyingi Yesu alitoa mfano akiwa anajibu swali au mtazamo. Kufahamu mazingira ambayo mfano ulitolewa inamsaidia mtafsiri kuuelewa ujumbe.
Kama tafsiri yetu ya mfano haiendani moja kwa moja na mazungumzo au hali ambayo ilipelekea Yesu kuutoa mfano, tutakuwa tumekosa jambo muhimu.
Mifano ili Kujibu Swali. Wakati wa mazungumzo, mwanasheria alimuuliza Yesu, “jirani yangu ni nani?” Yesu angeweza kujibu, “Mwenye huhitaji katika njia yako ni jirani yako-na wajibu wako.” Badala yake, Yesu anatoa jibu lile lile kwa namna tofauti, kwa kutoa mfano wa msamaria mwema.
Agustino alikosea kutafsiri mfano kwa sababu alipuuza swali ambalo mfano ulikuwa unalijibu. Hii ndiyo tafsiri ambayo Agustino alitoa: Yesu (msamaria) alimwokoa Adamu (mtu) kutoka kwa Shetani (wanyang’anyi) na akampeleka kanisani (nyumba ya kulala wageni) kwa ajili ya ulinzi. Yesu alimlipa Paulo (mtunza nyumba ya wageni) dinari mbili (ahadi ya maisha ya sasa na yajayo) ya kushinda dhambi (vidonda). Tafsiri ya Agustino haikuwa sahihi kwa sababu haikuwa inahusiana na mazungumzo baina ya Yesu na mwanasheria.
Mfano ili kujibu mtazamo. Luka 15:1-3 inasema, “Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao. Akawaambia mfano huu, akisema”:
Mchungaji alikuwa na kondoo aliyepotea. Angalia furaha yake kondoo aliyepotea alipopatikana!
Mwanamke alipoteza shilingi moja. Angalia furaha yake alipoipata shilingi iliyopotea.
Baba aliyekuwa na mtoto mpotevu. Angalia furaha yake mtoto wake alipopatikana.
Kupitia mifano hii mitatu, Yesu alionesha, “Hautakiwi kupata mshituko kwamba ninakula na wenye dhambi. Angalia furaha kubwa mbinguni mwenye dhambi mmoja kitubu!”
Ni muhimu sana kukumbuka kwamba somo la msingi la mfano litahusiana moja kwa moja na swali ambalo limepelekea mfano kutolewa.
(2) Hitimisho la mfano lilikuwa ni nini? Ni mwitikio gani au mabadiliko gani ya mtazamo ambayo mfano unatoa?
Mara nyingi mfano unatoa dondoo kuu moja; ingawaje matumizi yanaweza kuwa mengi. Kila muhusika mkuu katika mfano anaweza kuwa anafundisha somo.
Tumekwisha kuangalia somo la msingi la mfano wa mwana mpotevu: Kuna furaha kubwa mbinguni mwenye dhambi mmoja akitubu. Dondoo hii kuu inajibu mazingira ambayo yalipelekea Yesu kutoa mfano: Mafarisayo hawakuwa tayari kuwasamehe wenye dhambi. Wahusika wote watatu, kila mmoja anafundisha somo moja ambalo linahusiana na dondoo kuu ya mfano moja kwa moja.
Muhusika
Somo
Mwana Mpotevu
Wenye Dhambi ambao wanamgeukia Mungu katika toba na wanaupata msamaha ulio tayari kwa ajili yao.
Baba Mwenye Upendo
Badala ya kutokuwa tayari kusamehe, Baba yetu wa mbinguni anafurahia msamaha.
Kaka Mkubwa
Mtu asiyesamehe hana upendo kama alio nao Baba.
Yesu alionesha ukinzani kati ya kutosamehe kwa kaka mkubwa na kusamehe kwa baba. Kusudi la Yesu lilikuwa kukemea kutosamehe kwa Mafarisayo. Aliwataka wao kutubu kutokana na mtazamo wao usio sahihi.
Mtu anayehubiri kutoka katika mfano huu anaweza kusisitiza upendo na msamaha wa baba kwa kusudi la kumtia moyo mwenye dhambi kutubu. Au anaweza kuhubiri kwamba waamini wanatakiwa kuwa na mtazamo wa Mungu wa kusamehe wasioamini.
(3) Wapokeaji wa kwanza walikuwa na mwitikio gani?
Ili kuelewa ni namna gani mfano ulikuwa na matokeo kwa wapokeaji wa kwanza, ni lazima tuelewe utamaduni wao. Mifano ya Yesu mara nyingi ilienda kinyume na utamaduni uliozoeleka. Hii iliwafanya wao kushangaa.
Kwa mfano, zingatia tena mfano wa mwana mpotevu. Wapokeaji wa Yesu wangeliona kuwa ni kukosa heshima kwa hali ya juu kwa mtoto kuomba urithi mapema. Kisha mtoto akaupoteza urithi. Wasikilizaji walifikiri kwamba wakati anarudi, baba yake angemkataa, angekataa kumuona, na labda hata angempiga na kumfukuza. Fikiria mshangao walioupata wasikilizaji wakati ambapo baba alikikibia ili kumkaribisha mtoto wake.
Katika mfano wa Msamaria mwema, wasikilizaji hawakushangaa kwamba Kuhani na Mlawi walimpita aliyejeruhiwa pasipo kumsaidia, kwa sababu waliwaona viongozi wa hekalu kuwa wameharibika na wanafiki. Waliwaheshimu Mafarisayo, na walifikiri ambaye angekuwa mtu wa tatu kumsaidia aliyejeruhiwa angekuwa Farisayo. Hebu fikiria kuhusu mshangao wao kwamba mtu wa tatu ni Msamaria, mtu ambaye walifikiri amedharauliwa kwa ajili ya tabaka lake na kukosa hali ya kidini.
Kwa kadiri unavyoelewa vizuri mazingira ya kiutamaduni ya mfano, ndivyo utakavyoelewa vema ujumbe.
Taarifa za Kina na Alama Katika Mifano
Baadhi ya wahubiri kwa makosa wanafikiri kwamba kila kipengere katika kila mfano ni lugha ya alama. Kwa mfano, katika mfano wa Msamaria mwema baadhi ya watu wamesema kwamba msafiri aliposhuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, alikuwa akifanya uamuzi mbaya kwa sababu alikuwa akienda katika jiji ambalo Mungu amelilaani. Hii si tafsiri nzuri ya mfano huo, kwa sababu kusudi la mfano huo lilikuwa kueleza jinsi mtu anavyoonyesha upendo kwa jirani. Maelezo mengine ni maelezeo na sio ishara ya chochote.
Katika mfano wa Marko 4:30-32, wahubiri wametafakari juu ya kile ambacho ndege kwenye mti wanawakilisha, lakini ndege wanatajwa tu ili kuelezea namna ambavyo mbegu ndogo ilikua na kuwa kitu kikubwa ambapo ndege wangekuja na kuketi kwenye matawi.
Katika mfano wa mwana mpotevu hakuna sababu ya kujaribu kupata maana ya mfano kwa ajili ya kila taarifa. Kwa mfano, nguruwe sio ishara. Nguruwe wanatajwa kuonyesha hali mbaya ya mwana mpotevu: Mvulana wa Kiyahudi kwa kawaida asingeweza kuwa karibu na nguruwe.
Ni nadra kwa maelezo ya mifano kuwa ya kiishara. Mfano mmoja wa maelezo ya alama katika mfano ni katika mfano wa ngano na magugu (Mathayo 13:38-39). Tunajua kwamba maelezo katika mfano huu yalikuwa ni alama kwa sababu Yesu alisema yalikuwa hivyo.
Kuhubiri kwa Mifano
Muhubiri anaweza kutumia mfano ili kuutumia kwa namna inayoeleweka katika utamaduni wake. Hata hivyo, anatakiwa kuchukua muda kuelewa nini ambacho mfano unamaanisha kwa wasikilizaji wa kwanza. Vinginevyo, hatawasilisha ujumbe ule ule kwa wasikilizaji.
Mtafsiri hatakiwi kutumia mfano kama msingi wa kanuni ya imani au matumizi ambayo hayaungwi mkono na maandiko mwengine yaliyo wazi.
Vitabu vingi vya Agano Jipya ni nyaraka kutoka kwa Paulo, Yakobo, Petro, Yohana, na Yuda. Wakati zipo tofauti kati ya nyaraka, baadhi ya sifa ni sawa kwa nyaraka. Nyaraka za Agano Jipya ni:
1. Zenye Mamlaka. Nyaraka za Agano Jipya zilikuwa ni mbadala wa uwepo wa mwandishi. Waraka ulionesha mamlaka ya mwandishi; mamlaka hayo mara nyingi yalioneshwa katika mistari ya ufunguzi.[2]
2. Za Kimazingira. Nyaraka za Agano Jipya mara nyingi zilielekezwa katika hali mahususi au tatizo mahususi. Kwa mfano, Wagalatia iliandikwa kwa kanisa ambalo linafikiri wokovu unategemea kufuata matakwa ya Wayahudi. Paulo anasisitiza uhuru wetu katika Kristo. Kinyume chake, kanisa la Korintho lilichukua uhuru huo kupita kiasi—kuvumilia uasherati. Katika 1 Wakorintho, Paulo anasisitiza wajibu wetu wa utii.
3. Zilielekezwa kwa Waamini. Nyaraka ziliandikwa kwa makanisa ya majimbo (Warumi) au kwa waamini binafsi (Filemoni) au kwa waamini kwa ujumla (Yuda). Si kila wapokeaji wa nyaraka walikuwa wanaishi katika mahusiano mazuri na Mungu. Paulo aliwaita waamini wa kanisa la Korintho kutubia baadhi ya matendo yao; aliwaita Wagalatia kurudi kwenye Injili, na Yakobo anawaambia matajiri wasio wenye haki kutegemea hukumu. Hata hivyo, nyaraka ziliandikwa katika muktadha familia ya imani ya kikristo.
Muundo wa Nyaraka za Agano Jipya
Utangulizi
Jina la mwandishi na nafasi
Wapokeaji
Salamu
Maombi ya Utangulizi
Sehemu kuu (Ujumbe wa msingi wa waraka)
Hitmisho (inahusisha nyenzo kama)
Mipango wa safari (Tito 3:12)
Pongezi na salamu (Warumi 16)
Maelekezo ya mwisho (Wakolosai 4:16-17)
Baraka (Waefeso 6:23-24)
Doksolojia (Yuda 24-25)
Kutafsiri Nyaraka
Unapopokea barua kutoka kwa rafiki, unaketi chini na kusoma barua yote. Soma nyaraka za Agano Jipya kwa namna hiyo hiyo. Soma waraka wote ili kupata muhtasari ya ujumbe wa mwandishi. Unaposoma, tengeneza orodha ya Uchunguzi. Kwa kadiri unavyochunguza kwa kina, unakuwa umeandaliwa vema ili kutafsiri waraka.
Kuna maswali kadhaa ya kuuliza unaposoma waraka katika Biblia:
(1) Nani ni wapokeaji wa waraka?
Kwa kadiri tunavyofahamu zaidi kuhusiana na kanisa au mtu anayepokea waraka, tutaelewa vizuri zaidi waraka huo. Tunaposoma nyaraka za Paulo, itakuwa na msaada sana endapo unatosoma rejea yake katika Matendo ya Mitume kwa kanisa linalopokea. Mara nyingi hii itatoa uelewa mzuri zaido wa waraka. Kwa mfano:
Kanisa la Filipi lilizaliwa katika mateso (Matendo ya Mitume 16:12-40). Hii inaonesha maelekezo ya Paulo kwamba wanapaswa kufurahi hata katika nyakati ngumu.
Waefeso (kama nyaraka nyingine za Paulo) iliandikwa kwa waamini. Wakati Paulo anaomba kwamba waamini wa Efeso wapate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu, (Waefeso 3:19) anaomba kwamba watoto wa Mungu wapokee hata zaidi ya utimilifu wa kimungu. Anaomba kwamba wakristo wafanywe “watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake” (Waefeso 1:4).
(2) Nani ni mwandishi? Anahusianaje na wapokeaji?
Unapo pokea barua katika barua pepe, unataka kufahamu: “Nani ameandika hii?” Kwa kadiri unavyomfahamu vizuri mwandishi, ndivyo barua itakavyovutia. Kwa namna hiyo hiyo, kwa kadiri tunavyomfahamu mwandishi wa waraka wa Biblia, ndivyo tutaelewa vizuri ujumbe wake.
Katika nyaraka zake, mtume Yohana amesisitiza upendo. Yohana mwanzo alijulikana kama mmoja wapo wa “wana wa ngurumo” (Marko 3:17). Huko nyuma, yeye na ndugu yake walimuuliza Yesu awape ruhusa ya kuita moto kutoka mbinguni (Luka 9:54). Nyaraka za Yohana, ziliandikwa baade, zinatuonesha sisi kwamba yeye (Yohana) amebadilishwa sana na ujazo wa Roho Mtakatifu siku ya pentekoste.
Petro aliandika waraka wake kuwatia moyo wakristo walikuwa wanateseka. Aliwahakikishia kwamba wanaweza kuwa jasiri hata katika mashambulizi ya Shetani (1 Petro 5:8-9). Mwanzoni mwa maisha ya Petro, alikana kwamba anamjua Yesu kwa sabau ya hofu (Marko 14:66-72). Nyaraka za Petro zinatuonesha sisi badiliko ambalo lilitokea katika maisha yake.
Kufahamu mahusiano baina ya mwandishi na wapokeaji mara nyingi ni msaada sana katika kusoma waraka. Mahusiano mazuri ya Paulo na kanisa la Filipi yanaonekana wakati wote wa waraka wake wa furaha. Kwa upande mwingine, mzozo kati ya Paulo na Waamini wakorofi wa Korintho unapelekea kemeo la nguvu katika Wakorintho1 na 2.
(3) Ni mazingira gani yalipelekea kuandikwa kwa waraka?
Tunafahamu mazingira yaliyopelekea nyaraka kadhaa za Paulo. Wakorintho 1 na 2 ziliandikwa ili kujibu matatizo na maswali kule Korintho. Filemoni iliandikwa kama maombi kwa niaba ya mtumishi aliyekimbia, Onesmo.
Waraka kwa Wagalatia unaonesha thamani ya ufahamu wa mazingira ya waraka. Mistari michache katika Wagalatia, inaweza kukufanya uulize, “kuna shida gani Galatia?” Paulo anaanza, “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine” (Wagalatia 1:6). Kwa haraka inakuwa wazi kwamba waamini hawa wapya wameiacha Injili ya kuhesabiwa haki kwa neema kupitia imani. Na badala yake wameamini ujumbe wa kuhesabiwa haki kwa matendo. Maneno yenye nguvu na yenye hisia ya Paulo yaliyosukumwa na upendo wake kwa waamini hawa. Ameyatoa maisha yake yote kuhubiri ujumbe wa kuhesabiwa haki kwa imani pekee. Anashangaa kwamba Wagalatia wanaiacha kweli na kukubali Injili potofu.
Aina ya Fasihi: Ufafanuzi
Ufafanuzi ni mafundisho yenye mpangilio maalumu. Yanaenda katika mpangilio wa kimantiki kutoka dondoo 1 kwenda 2. Aina hii ya Fasihi ni ya kawaida katika nyaraka za Agano Jipya, hasa hasa katika Nyaraka za Paulo. Katika nyaraka hizi, Paulo anawasilisha kweli katika namna iliyowazi ya mwalimu mzuri.
Ufafanuzi hutumia maneno kama vile kwa hiyo, na, au lakini. Mara nyingi hujumuisha maswali na majibu. Ufafanuzi hutoa mawasilisho ya kimantiki ya kweli.
Katika Wakolosai, Paulo anawasilisha ufafanuzi kuhusu Kristo. Paulo anafundisha kwamba Kristo ni juu ya wanafilosofia wote wa kibinadamu na utamaduni. Paulo anafuata mpangilio huu wa kimantiki:
1. Paulo anatoa ushahidi kuhusu ukuu wa Kristo (Wakolosai 1:15-23)
Yeye ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
katika yeye vitu vyote viliumbwa.
ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa.
Upatanisho unapatikana kupitia yeye.
2. Paulo anawakumbusha wasomaji wake kusudi la kuandika. Ujumbe wa Kristo aliyetukuzwa ulikabidhiwa kwa Paulo ili kuuleta kwa mataifa (Wakolosai 1:24–2:5).
3. Paulo anaonya dhidi ya mafundisho ambayo yanakataa ukuu wa Kristo (Wakolosai 2:6-23).
Mafundisho kwamba watu wanaokolewa kwa kushika sheria za Mungu.
Matendo hatarishi ya kuwasiliana na roho
Msisitizo usio sahihi wa nidhamu ya kimwili kwa ajili ya matokeo ya kiroho
4. Kwa hiyo, kwa sababu ya ukuu wa Kristo, hivi ndivyo unavyotakiwa kuishi
(Wakolosai 3-4):
Utii kwa Kristo utaleta matokeo katika tabia zetu za kimaadili.
Hatutakuwa na tabia mbaya tena (Wakolosai 3:1-11).
Tutaishi kwa Amani na shukrani (Wakolosai 3:12-17).
Utii kwa Kristo utaleta matokeo katika mahusiano yetu na wengine (Wakolosai 3:18-4:6).
5. Salamu za mwisho zinazo wakumbusha wasomaji kujali kwa Paulo kuhusiana na waamini wa Kolosai (Wakolosai 4:7-18).
Waraka wa Paulo ni ufafanuzi wa mafundisho ya ubwana wa Kristo. Unafundisha kuhusu asili ya Kristo na matokeo ya kweli hii katika maisha yetu kama waamini.
[1]Dhana katika sehemu hii zimechukuliwa kutoka katika J. Scott Duvall na J. Daniel Hays, Grasping God’s Word (Grand Rapids: Zondervan, 2012).
[2]Kwa mfano, Waefeso 1:1 inataja Mamlaka ya kitume ya Paulo: “Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu.”
(1) Tafsiri sahihi inatuhitaji sisi kuelewa aina ya fasihi ya kifungu cha maandiko tunachojifunza.
(2) Baadhi ya aina muhimu sana za fasihi zinazopatikana katika Biblia zinajumuisha:
Historia: historia ya kweli na ya uhakika ya watu halisi na matukio halisi.
Unapotafsiri historia, uliza:
Habari ni nini?
Watu katika habari ni nani?
Je, simulizi hii ya kihistoria inatoa mfano wa kufuata?
Je, ni kanuni gani zinazofundishwa katika simulizi ya kihistoria?
Sheria za Agano la Kale
Agano la Kale ni muhimu kwa ajili ya waamini wa Agano Jipya kwa sababu:
Ni maelezo ya asili ya Mungu.
Linatufanya sisi wenye hekima kwa ajili ya wokovu.
Linatusaidia kufahamu mapenzi ya Mungu.
Inaweza kuwa ya masaada sana kufikiri kuhusiana na Nyanja tatu za Sheria za Agano la Kale:
Sheria za kiibada
Sheria za kiraia
Sheria za kimaadili
Unapotafsiri Sheria za Agano la Kale, uliza:
Andiko hili lilimaanisha nini kwa wapokeaji wa kwanza?
Ni tofauti gani iliyopo baina ya wapokeaji wa Biblia na ulimwengu wetu?
Ni kanuni gani zinazofundishwa katika andiko hili?
Je, Agano Jipya linachukua kanuni hizi kwa namna yeyote?
Ushairi
Sifa za mashairi ya kiebrania:
Usambamba
Tamathali za semi
Mashairi yenye hekima: yanafundisha namna maisha yanavyoenda.
Mithali: uchunguzi wa jumla wa maisha umetajwa kwa ufupi na kwa uwazi.
Unapotafsiri Mithali, uliza:
Ni kanuni gani za jumla zinazofundishwa katika andiko hili?
Je, ni hali gani za zisizo za kawaida zinazoweza kutokea katika kanuni hii?
Ni watu gani katika Biblia ni kielelezo cha kanuni hii?
Unabii wa Agano la Kale: mawasiliano ya ujumbe kutoka kwa Mungu.
Unapotafsiri unabii wa Agano la Kale, uliza:
Nabii alisema nini kwa ulimwengu wake?
watu wake waliitikiaje ujumbe wake?
Ni kanuni gani kutoka katika ujumbe wa nabii inayozungumza katika ulimwengu wetu leo?
Fasihi ya kiapokaliptiki
Unapotafsiri fasihi ya kiapokaliptiki, kumbuka:
Imejaa alama.
Sio lazima ielezee matukio katika mfuatano wa matukio
Inaweza kurudia kuelezea matukio yale yale kwa kutoa taarifa tofauti za kina.
Dhana kuu katika fasihi ya kiapokaliptiki ni:
Changamoto ya kutunza imani katika ulimwengu huu wa uovu
Mungu Mwenyezi ambaye anasaidia watu wake.
Mifano: mafundisho yanayolinganisha kweli ya kiroho na mambo katika asili au mazingira ya maisha. Mara nyingi mifano ilitolewa kama mwitikio ili kujibu swali au mtazamo.
Unapotafsiri mifano, uliza:
Ni kwa namna gani mfano ulitolewa?
Hitimisho la mfano lilikuwa ni nini?
Ni mwitikio gani au mabadiliko gani ya mtazamo ambayo mfano unatoa?
Wapokeaji wa kwanza walikuwa na mwitikio gani?
Waraka
Nyaraka za Agano Jipya ni:
Zenye mamlaka
Za kimazingira
Zilielekezwa kwa waamini
Unapotafsiri nyaraka, uliza:
Nani ni wapokeaji wa waraka?
Nani ni mwandishi? Anahusianaje na wapokeaji?
Ni mazingira gani yalipelekea kuandikwa kwa waraka?
Ufafanuzi: mafundisho yenye mpangilio maalumu
Somo la 6 Zoezi
Katika Somo la 1, ulichagua kifungu cha maandiko ambayo utayasoma wakati wote wa kozi hii. Kifungu chako ni aina gani ya fasihi? Tumia taarifa katika somo hili ili zikusaidie kuelewa zaidi kuhusiana na kifungu chako. Jibu maswali ya tafsiri yanayohusiana na aina mahususi ya fasihi.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.