Maono ya Shepherds Global Classroom
Maono ya SGC ni kutayarisha mwili wa Kristo kwa kufanya mafunzo ya huduma ya wenyeji kuwepo ulimwenguni kote.
Kampuni moja ya taksi iitwayo Uber husafirisha abiria wapatao milionio 5.5 kila siku. Hili linahitaji nguvu kazi kubwa ya madreva wenye magari. Uber hainunui maelfu ya magari; badala yake, wanakodisha madreva wenyeji kutumia magari yao wenyewe kubeba abiria wa Ubar. Wanatatua tatizo la kazi kwa kufanya biashara hiyo. Hivyo hivyo SGC inafanya mafunzo kupatikana kila mahali kwa kuwatayarisha waalimu wenye uwezo ambao tayari wapo mahali pale. Mungu amewapa waamini karama, uwezo na hamu ya kufundisha.
