Mwalimu anapaswa kupanga darasa mapema kama inawezekana. Washiriki wanapaswa kukaa kwa kutazamana. Mwalimu anapaswa kuhakikisha kwamba kuna nafasi ya kutosha na kuna hakuna vitu ambavyo vitaondoa usikivu na makelele wakati wa somo. Mwalimu anapaswa kujitahidi kuhakikisha kuwa kutakuwa na mkao wa kuridhisha, hewa ya kuridhisha na mwanga wa kutosha. Kusomea nje kunaweza kuwa kuzuri endapo hakuna shughuli za kuharibu usikivu.
Darasa linapaswa kuwa na ubao mkubwa wa kuandikia na kuchorea.
Walimu wanapaswa kujitambulisha, wakielezea kuhusu familia zao, uzoefu wa kihuduma, na historia ya elimu zao. Wanapaswa kuepuka kuorodhesha waliyowahi kufanya kana kwamba wanataka kuonyesha kuwa ni watu waheshimiwa. Wanapaswa kukumbuka kwamba kusudi la kuelezea habari hizi ni kujenga uhusiano na washiriki.
Washiriki wanapaswa kujitambulisha kwa ufupi. Mwalimu anaweza kuongea nao kila mmoja, akiwauliza maswali mmoja au wawili ili kuonesha kuwa anavutiwa na ana jenga uhusiano kati yao.
Baada ya kujitambulisha kunaweza kufuata muda wa maombi. Omba ili Mungu alitumie darasa kukutana na mahitaji ya wanafunzi. Mwalimu anapaswa kuonesha kuwa anamtegemea Mungu kuyafanya mafundisho kufaa na yenye kubadili maisha. Vipindi vya baadaye vya darasa vinapaswa kuanza na maombi na kwa kushirikishana mahitaji kwa ufupi.
Walimu wanapaswa kuwambia washiriki walete vifaa vya aina gani, ikiwa pamoja na Biblia, nakala ya somo lililochapwa na daftari la kuandikia. Walimu wasisitize kuwa washiriki waandike kumbukumbu kwa kuandika ili ziwe faida zao baadaye, sio kwa lengo la majaribio. (Majaribio yote yatatokana na mazoezi yaliyomo katika kitabu cha somo.)
Baada ya utambulisho, muda wa darasa siku ya kwanza unapaswa uwe ndio mfano wa madarasa yanayofuata, ili washiriki wajue wanachotarajia.
Muundo wa Somo
Masomo ya SGC sio tu ni vitini; ni masomo yaliyopangwa kufundishia. Kila somo lina mwongozo wa mwlimu karibu na mwanzoni mwa kitabu. Masomo yanafanana na mengine lakini hayafanani katika muundo.
Masomo mengine yameanza na malengo ya somo. Sio lazima kwa mwalimu kusoma hayo katika darasa.
Masomo mengi yanaanza na swali au simulizi au na mbinu nyingine ya kuvutia na kuwafanya washiriki waone kuwa mada ni muhimu.
Walimu wanaweza kupitia ukurasa kwa ukurasa kwa somo lote, wakielezea habari za aya. Wanapaswa kujitayarisha mapema kwa kuhakikisha wanaelewa taarifa na wanapigia mistari vifungu muhimu ili kuwasaidia kuelezea kila aya.
Maswali ya mijadala yapo katika kitabu chote. Wakati mwingine swali linatambulisha taarifa inayofuata. Wakati mwingine, swali linamuuliza mshiriki kusema kitu kutokana na alichojifunza. Maswali hayahitaji majibu ya “ndio” au “hapana”, bali ni kwa ajili ya ufafanuzi. Mwalimu aruhusu washiriki kadhaa kusema. Sio lazima mjadala kupata jibu la kuhitimisha kila wakati, hasa pale ambapo swali linatambulisha taarifa inayofuata.
Walimu wanahitaji kuwa na maswali yao ya ziada ili kujadili. Wakati wote walimu wanatambue kuwa wamekuwa wakiongea kwa dakika kadhaa bila mrejesho kutoka kwa washiriki, wanapaswa kuwauliza washiriki swali.
Wakati wote huwa changamoto kufanya mijadala isiwe ya kupoteza muda. Walakini, watu wengi hawawezi kujifunza bila kuwa na mjadala. Washiriki huhitaji muda kufikiri na kusikiliza wengine wakisema jinsi dhana iliyoko katika somo inavyoweza kutumika katika mazingira yao na katika maisha ya kanisa.
Masomo mengi yanamalizika kwa mazoezi. Mwalimu anapaswa kuyaelezea mazoezi. Kama darasa la siku hiyo lina mada kadhaa, mwalimu anapaswa kuhakikisha kuwa washiriki wanaelewa mazoezi yote ambayo yanatakiwa kukamilika kabla ya kipindi kingine.
Siku zingine za darasa
Mazoezi yatawasilishwa siku za darasa baada ya siku ya kwanza. Mwalimu anapaswa kukusanya mazoezi mwanzoni mwa darasa. Baadhi ya mawasilisho ya washiriki yanaweza kuwasilishwa mwanzoni, na mengine baadaye ili kuleta utofauti wa shughuli katika siku.
Wakati kuna jaribio au kuandika kitu kutokana na kumbukumbu zao ni muhimu kuhakikisha washiriki wanakaa vizuri wanapoandika ili waepuke kutoangalia kazi za wengine.
Mbali na kazi za uwasilishaji za washiriki, mwalimu anapaswa kuuliza mara nyingi mwanafunzi kuwasilisha sehemu ya habari iliyomo katika somo. Hili linapaswa kupangwa kabla ya muda ili washiriki waweze kujitayarisha.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.