
1. Thamani ya muda. Anza na maliza darasa kwa wakati. Usisubiri kila mtu afike. Kama utaanza kwa kuchelewa utakuwa unapoteza muda wa watu waliokuja kwa wakati. Unapomaliza kwa kuchelewa unaingilia majukumu ya washiriki. Katika tamaduni zingine, kujali wakati sio jambo rahisi. Lakini watu wale wale katika tamaduni hizo wanajua kutunza ratiba kwenye kazi za ajira zao au wanaposafiri. Wanapaswa kuweka uzito wa namna hiyo kwenye darasa.
2. Waketishe washiriki katika mkao wa nusu duara. Ni kwakuwa mjadala ni muhiu, ukaaji unapaswa kupangwa vizuri ili washiriki waweze kutazamana.
3. Lisiliza vizuri wanafunzi wanapoongea. Viashiria vizuri vya kusikilizana ni kutazamana, kuwa makini katika lugha za mwili, kupuza vitu vinavyofanya akili yako kutanga tanga, na mwitikio kwenye ucheshi wa mzungumzaji au hisia zingine.
4. Hakikisha hakuna mwanafunzi ambaye wakati wote yuko kimya. Elekeza swali kwa mshiriki ambaye huwa hasemi sana (“Daudi, unafikiri nini kuhusu hilo?”).
5. Uliza swali ambalo washiriki wanaweza kujibu ili kujenga kujiamini. Kama moja anatoa jibu lisilo sahihi, jaribu kuonesha kitu kizuri katika jibu lake kabla ya kufanya uchambuzi.
6. Jaribu kusema kitu kizuri kwa kila maoni yanayotolewa kabla ya kufanyia uchambuzi. Washiriki watajienga kujiamini endapo maoni yao yatasemewa vizuri.
7. Usiruhusu mshiriki moja kuzungumza sana na kujibu maswali yote. Unaweza kuelekeza maswali kwa washiriki fulani kimakusudi. Au unaweza kuuliza, “wengine mnasemaje?” katika mjadala, unaweza kusema “hebu tusikie kwa mtu ambaye bado hajasema kuhusu hili.”
Kama kuna washiriki bado wanaongea sana kuliko wengine, viongozi wanaweza kusema nao nje ya darasa. Kiongozi anaweza kusema kama hivi “Yeremia, wewe ni mfikiri haraka na unao uwezo wa kujibu haraka katika mijadala, lakini ninaogopa kuwa wengine hawatashiriki ikiwa tutajibu kila kitu haraka. Je, unaweza kunisaidia kuwapa wengine nafasi ya kushiriki?”
8. Usiruhusu washiriki wawili au watatu kuendelea kubishana huku ukisahau wengine walioko kwenye kundi. Kama kuna mtu anataka kuendelea kubishana kwa muda mrefu kuhusu suala Fulani, mwambie kwamba mjadala utamaliziwa baadaye.
9. Usiruhusu yeyote kuingilia kati au kukatisha wengine. Inua mkono wako, kwa ujasiri msimamishe anayeingilia na mruhusu mzungumzaji wa kwanza kumalizia. Vinginevyo, wakati wote mjadala utakuwa umedhibitiwa na mwanakikundi ambaye ana tabia aina hiyo. Watu ambao wana ujasiri kidogo watajisikia kuvunjika moyo kwamba hawawezi kumaliza maneno yao.
10. Sikiliza malalamiko. Kila lalamiko linaweza kuwa dalili ya tatizo ambalo laweza kusahihishwa. Usipuuzie viashiria vinavyoonesha kutoridhika. Kama kuna mtu haridhiki na masomo, anaweza kuwa haelewi kusudi, au anaweza kuwa ana malalamiko ya kweli.
11. Msahihishe mshiriki vurugaji. Kama washiriki binafsi kwa wakati wote wanaonyesha upinzani, vurugu, ubishi, au uchovu, wanaweza kuwa hawakubaliani na masomo. Wanaweza kuwa hawakutazamia darasa la namna hiyo. Zungumza nao pembeni kuwasaidia kuona kusudio la masomo.
12. Kama hujui jibu la swali usijifanye unajua. Mwalimu sio lazima kujua kila kitu. Itakuwa ni sawa ukimwambia mshiriki kuwa utaenda kutafuta jibu.
13. Usiruhusu mijadala iwe fitina au uchochezi. Usiruhusu kikundi kiwe jukwaa la kukosoa kanisa na viongozi. Wachungaji wengi wanaogopa wakati washirika wao wakijiunga na masomo.
14. Wajue washiriki wako. Unaweza kufundisha kwa ufanisi zaidi endapo unajua mazingira yao ya kifamilia, uzoefu wa kihuduma, elimu zao, huduma ya sasa, na malengo ya baadaye. Jaribu kujifunza mambo haya katika mazungumzo ya binafsi.
Maelekezo mengine ya ufundishaji mzuri na tabia za kujifunza kwa watu wazima zipo katika sura ya 6.