Kwa nyongeza ya tabia zilizoelezewa katika sura hii, mwanafunzi wa somo la kufunza mwalimu anapaswa kuwa mshiriki wa kanisa la mahali na amependekezwa na mchungaji.
Mwalimu wa SGC anapaswa kuwa mkomavu kiroho, mwenye stadi za kufundisha, na mwenye maarifa ya kibiblia.
Matakwa ya kitaaluma: Mwalimu anapaswa kuwa na uwezo wa kusoma, kuelewa na kuelezea dondoo za somo kwa ufasaha. Ingawa mwenye cheti cha shahada anaweza kumtayarisha mwalimu kwa mbinu na maarifa ya kina, lakini maono ya SGC ni kuendeleza walimu wanaoweza kuhamishia mafunzo hayo kwa wengine. Kwa sababu hii, hatukusudii kutafuta walimu wenye vyeti vya shahada. Tunamtegemea Mungu kwa uaminifu wake atatoa karama za kiroho kwa walimu watarajiwa kila mahali. Tunatarajia kupata na kutayarisha watu ambao wamepewa karama na uwezo wa kufundisha.
Orodha inayofuata hapa chini inajumuisha tabia zingine ambazo ni muhimu pia. Mwalimu sio lazima awe ana sifa hizi zote lakini anapaswa kujiboresha katika zote. Mwalimu anayepungukiwa sifa yeyote kati ya hizi ufanisi wake utakuwa mdogo.
	- 
	
Ukomavu wa kiroho. Mwalimu anapaswa kuwa mfano mzuri wa tabia za kiroho. Kama maisha ya walimu wa kikristo na mitazamo yake hazilingani, hawatakuwa mfano mzuri kwa washiriki.
	 
	- 
	
Kupatikana. Kama ratiba ya mwalimu imejaa tayari na hawezi kuifuata vizuri, atakuwa hapatikani kwa huduma ya kufundisha katika vipindi vyake. Kufundisha kunatakiwa kuwa kipaumbele cha mwalimu. Baadhi ya watu wenye vipawa hawapaswi kupewa huduma hii endapo wanashughuli nyingi kiasi cha kutofanya vizuri kwa kuingiliwa na shughuli zingine.
	 
	- 
	
Kutegemewa. Walimu ni lazima wawe ni watu ambao wanatimiza majukumu yao. Wanapaswa kwenda na muda na kufuata ratiba. Washiriki watakatishwa tamaa kama walimu hawaji au wanakuja darasani kwa kuchelewa.
	 
	- 
	
Kujiamini. Ni lazima walimu waamini kwamba wanaweza kujifunza jinsi ya kuongoza kikundi. Wanaweza kuhitaji usimamizi kwa vitendo ili kuwajengea kujiamini.
	 
	- 
	
Uwezo wa kutatua matatizo. Walimu wanahitaji kuwa na uwezo wa kutunza mitazamo sahihi endapo watu hawataelewana na wanasababisha matatizo. Wanahitaji kusimama katikati ili kusaidia kutatua mgogoro huo.
	 
	- 
	
Uwezo wa kufundisha. Je, watu wanaelewa ufafanuzi wa mwalimu? Mwalimu anapaswa asiwe mtu anayechanganya washiriki.
	 
	- 
	
Njaa ya Neno la Mungu. Walimu wanapaswa kuwa watu wanaolifurahia Neno la Mungu, ili wawaalike wengine kuja kulifurahi pia. Ni lazima waifanye Biblia kuwa ni muhimu katika mahusiano yao na Mungu.
	 
	- 
	
Kumtegemea Mungu. Walimu lazima wafahamu kuwa matokeo ya kiroho yanaweza kutokea tu kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Ni lazima wawe tayari kushirikiana na Roho Mtakatifu. Ni lazima kutegemea upako kutoka kwa Mungu. Hawapaswi kujiamini kuwa ufafanuzi wao utaleta matokeo mazuri kwa sababu ya uwezo wao pake yake.
	 
	- 
	
Kuwa tayari kutumika. Walimu hawapaswi kuwa watu wanaotaka kutumikiwa. Hawapaswi kutafuta huduma kwa kusudi la kuzionyesha talanta zao. Wanatakiwa kuwa jibu la mahitaji na utayari wa kujitolea.
	 
	- 
	
Chini ya mamlaka ya kiroho. Walimu wanapaswa kuwajibika kiroho kwa watu wengine. Wanapaswa kufuata maelekezo ya viongozi wa kiroho.
	 
	- 
	
Mwaminifu katika kanisa. Walimu wanapaswa kuwa washirika waaminfu wa kanisa mahali alipo. Mafundisho yao yanapaswa kusababisha watu kulithamini kanisa na kuwafanya wawajibike kanisani.
	 
	- 
	
Shauku ya kutaka kufanikiwa. Kama walimu wana shauku ya kutaka kufanikiwa, hawatakata tamaa upesi. Watazoea mazingira ya kazi hiyo. Watatafuta taarifa za kuwasaidia kuwa na ufanisi zaidi. Kukitokea tatizo au fursa watachukua hatua stahiki. Watakuwa na nguvu na shauku.
	 
	- 
	
Itikadi sahihi. Kila mwalimu anapaswa awe na msingi mzuri wa kibiblia, kievanjeliko.
	 
	- 
	
Uzoefu katika huduma. Walimu wanapaswa kuwa watu ambao wamekuwa waaminifu katika huduma ya kanisa kwa muda wa kutosha.