Masomo ya SGC yanatumika katika mafunzo ya namna tofauti tofauti. Shule za sekondari baadhi zinaweza kutumia baadhi ya masomo. Makanisa kadhaa yanatumia masomo haya katika shule za jumapili kwa watu wazima. Vikundi vya kujifunza Biblia manyumbani huchagua masomo haya na kujifunza. Wachungaji huchagua taarifa kutoka masomo haya na kutumia katika mahubiri na kufundisha.
Maelekezo katika sura hii yanatumika katika utendaji wa taasisi ya wenyeji ambao wanatumia masomo 20 ya SGC katika mafunzo yote.
Masomo yote ya SGC yana masomo muhimu wa mtaala wa chuo cha Biblia. Yameandikwa bila kutumia misamiati migumu.
Mshiriki lazima awe na uwezo wa kusoma, kuandika vizuri na kujifunza masomo kama ilivyokusidiwa.
Masomo haya hayakukusudiwa kwa waongofu wapya, ingawa taarifa nyingi zinafaa kwa kusudi hilo.
Njia nzuri kwa kikundi ni kwamba kila mshiriki kuwa na:
1. Nakala ya somo
2. Kukamilisha mazoezi yote
3. Kupewa nafasi kuwasilisha taarifa katika kikundi
4. Kuwa na mahusiano mazuri na kanisa anakotoka, na
5. Awe na huduma mara nje na kikundi chake
Mwezeshaji anayedumisha vitendo hivi atakuwa anafundisha washiriki kwa ufanisi wa huduma.
Kuna machapisho ya makundi ya wanafunzi ambao hawajitayarishi kwa huduma. Machapisho haya ni muhtasari wa masomo. Yanatumiwa katika shule za sekondari na shule za jumapili za watu wazima. Wanaosoma masomo haya hawahitajiki kufanya mazoezi ya kawaida kwa kuwa hawafanyi mazoezi ya huduma au hawajitayarishi kwa kazi ya huduma. Machapisho haya hayapaswi kutumika kwa wanafunzi wanaojitayarisha na huduma na na na wenye mpango wa kupata cheti cha huduma. Wawezeshaji wa washiriki hawa lazima wafundishe kwa kufuata kitabu cha masomo ya SGC kwa kuwa machapisho hayo hayana taarifa zote.
SGC haitoi shahada ya ki-somi. Mahali pengine taasisi za wenyeji au taifa zinatumia masomo ya SGC kutoa stashahada au cheti kwa kuzingatia vigezo vyao. Mshiriki lazima aandikishwe na kituo na atimize masharti yao.
Mahali ambapo shahada ya kitaaluma haipatikani, masomo haya yatazamwe kama mafunzo ya stadi za kazi. Katika ulimwengu wa kazi mafunzo ya stadi za kazi humtayarisha mtu kufanya kazi za stadi. Masomo hayo huwa hayahitaji shahada, lakini yanamwidhinisha mtu kuwa amepata mafunzo. Hivyo hivyo, masomo ya SGC ni mafunzo ya stadi kwa huduma.
Vifaa Vinavyohitajika
Ni Biblia tu ndiyo inayohitajika kwa ajili ya masomo, lakini masomo yenyewe yanapendekeza kusoma taarifa za ziada. Taasisi za wenyeji zinapaswa kujenga uwezo wa maktaba kwa ajili ya matumizi ya washiriki.
Ratiba ya Darasa
Taasisi ya wenyeji inaweza kuwa na ratiba yake ya masomo, kulingana na mazingira yake. Walakini, muda wa kutosha lazima uzingatiwe. Kama mwezeshaji atafundisha bila kuwa na mjadala na mazoezi ya wanafunzi, muda utakaotumika utakuwa kidogo, lakini ufundishaji huo hautawatayarisha washiriki vizuri. Kama kikundi kitatumia muda kujadiliana taarifa na kukamilisha mazoezi, somo litachukua masaa ya darasani zaidi ya thelathini. Washiriki wanapaswa kutumia muda wa ziada kufanya mazoezi nje ya wakati wa darasa.
Mpangilio wa Masomo
Mtiririko wa aina fulani sio wa lazima. Kila darasa linajitosheleza na halitegemei kuendeleza darasa jingine. Kuna uwezekano kuendesha darasa kwa mzunguko, likiruhusu washiriki wapya kujiunga mwanzoni mwa kila somo. Taasisi inaweza kuendelea kufunza washiriki wapya kuliko kuwafanya wangoje hadi mwanzoni mwa mwaka. Washiriki wanaweza kujiandikisha mwanzoni mwa somo lolote na kuendelea katika mzunguko wote mpaka wamemaliza masomo yote.
Uthibiti Ubora
Mwezeshaji anapaswa kutunza taarifa za mahudhurio ya washiriki. Mshiriki asiyehudhuria ngalau 75% ya muda wa darasa na kukamilisha mazoezi yanayotakiwa kwa 100% hatapewa daraja la somo. Katika mazingira maalumu, mwezeshaji anaweza kutoa masharti ya kujifunza kwa ziada ili kulipiza muda wa darasa uliopotea.
Mwezeshaji anapaswa kutunza kumbukumbu za taarifa zilizokamilika kwa umakini ili kuhakikisha daraja la mwisho liko sahihi na la haki. Mwezeshaji lazima ahakikishe kuwa wanafunzi wanajua binafsi kama mazoezi yao au mahudhurio yao yanasababisha kushuka daraja.
Kama taasisi ya wenyeji ni sehemu ndogo ya umoja wa taasisi nyingi, kumbukumbu za taarifa za mahudhurio na mazoezi yanapaswa yawepo kwa ajili ya kukaguliwa na wakaguzi wa kanda. Cheti hakitakuwa na thamani kama taasisi haifuati matakwa muhimu.
Fedha za Uendeshaji za wenyeji
Kila mahali ilipo taasisi ya wenyeji lazima ijitegemee. Darasa linatolewa na kanisa. Wawezeshaji wanatumika kama sehemu ya huduma ya kanisa la hapo. Gharama za kuchapa masomo itatolewa na kanisa la hapo au wanafunzi. Kama kituo ni sehemu ya umoja wa vituo vingi, uongozi mkuu unaweza kupanga ada kwa washiriki ambayo inaweza kutosheleza gharama ya kuchapa masomo na kusaidia walimu wa hapo.
Ni lazima walimu wa pale wawe waaminifu na wenye uwazi katika masuala yote ya fedha. (2 Wakorintho 8:21). Kila moja anayehusika lazima ajue fedha kiasi gani zimekusanywa na jinsi zilivyotumika. Kamati lazima ihusike katika kudhibiti fedha. Mfano wa masuala ya kifedha ni pamoja na ada wanazolipa washiriki katika taasisi au kituo cha uongozi mkuu, gharama za kuchapisha masomo, kuwapa posho wawezeshaji wa kituo, na fedha zozote zilizokusanywa au au kutumika.
Kwa kuwa uaminifu ni tabia ya msingi ya mkristo, haiwezekani kwa mtu ambaye sio mwaminifu kuwa mkristo wa mfano. Mtu ambaye siye mwaminifu hapaswi kushika nafasi ya huduma yeyote. Aina yeyote ya kutakuwa mwaminifu itaadhiri uhusiano wa kiongozi na SGC.
Shirika la kimisheni/Huduma ya Kitaifa na taasisi ya wenyeji katika kushirikiana
ABC ni jina la kubuni la huduma ya taifa ambayo husaidia makanisa kuimarisha taasisi za wenyeji. Makubalino ya eneo inayotumia ABC kwa taasisi za wenyeji yanapatikana katika ukurasa unaofuata. Mwakilishi wa ABC hutembelea eneo la taasisi ya wenyeji mara kwa mara na kukagua akitumia orodha ya maswali yaliyopo mwishoni mwa sura hii.
ABC hutumia fomu hii kuelezea uhusiano kati ya huduma ya kitaifa na taasisi ya wenyeji.
Kusudi la ABC ni kutumika katika mwili wa Kristo kwa kuliwezesha kanisa kuendeleza huduma ya viongozi. Kanisa la mahali au shirika la huduma linaweza kukubaliwa kuendesha huduma ya mafunzo kwa kutumia masomo ya SGC.
ABC itahifadhi haki ya kuvunja makubaliano haya endapo kanisa la mahali halitatimiza wajibu wake.
ABC hutoa yafuatayo:
Vitabu 20 vya masomo ya mafunzo
Mafunzo ya semina ya wawezeshaji
Wasimamizi kutembelea maeneo ya mafunzo kutia moyo wawezeshaji wenyeji na kuthibiti ubora.
Vyeti vya wanafunzi kwa kila somo waliyomaliza (nakala ya somo ya kila mtu binafsi ni lazima kwa kila mshiriki kupokea cheti)
Cheti cha kumaliza masomo yote
Kibao cha tangazo la ABC kitakachowekwa katika eneo la Huduma
Huduma ya wenyeji watafanya yafuatayo:
Kutoa wawezeshaji mwaminifu, wenye uwezo na kuthibitishwa na uongozi wa ABC
Kuwataka wawezeshaji kushirikiana katika mafunzo na kufuata mwongozo kutoka uongozi wa ABC
Wawakilishi wa ABC wanapokuja kutembeleaeneo, watatumia maswali yafuatayo kutadhimini na kutoa mwongozo wa kuboreshaji.
Je, eneo lina wawezeshaji ambao wamepokea mafunzo ya SGC?
Je, wawezeshaji wanatumia mbinu tofau tofauti za kufundishia?
Je, wawezeshaji wanawahusisha washiriki katika mjadala na kushiriki kweli?
Je, eneo linaendeleza wasaidizi wa mwezeshaji ambao wanafanya mazoezi ya kufundisha darasani?
Je, darasa linafaa kwa kujifunzia (ukaaji, mwanga, hakuna kelele na mwingiliano wa shughuli)?
Je, kila mwanafunzi huwa anapata nakala ya somo lolote linafunzwa?
Je, washiriki wote wanaweza kusoma na kuandika vizuri kiasi cha kukamilisha mazoezi? (Takwa la kupata cheti).
Je, ratiba ya darasa hutoa masaa thelathini kwa kila somo kwa kuongezea muda utumikao katika kukamilisha mazoezi?
Je, mchakato wa majaribio huhakikisha washiriki hawaangaliziani majibu au kuangalia katika makaratasi waliyoingia nayo?
Je, wawezeshaji wanatunza kumbukumbu sahihi za mahudhurio ya washiriki? (Mshiriki akikosa zaidi ya 25% ya masaa ya darasa hapaswi kupokea tuzo za somo.)
Je, wawezeshaji wanatunza kumbukumbu za mazoezi ya wanafunzi ambayo yamekamilika? (Mazoezi yote lazima yakamilishwe ili kupata cheti. Mazoezi kutoka darasa linaloendelea yanatakiwa kuwepo kwa ajili ya tathmini mpaka yatakapo rudishwa kwa washiriki mwishoni mwa somo.)
Je, taasisi ya wenyeji inaweka mfumo wao wa fedha za kuendeshea?
Je, fedha za taasisi za wenyeji zinadhibitiwa na kamati ya wenyeji katika hali ya uwazi na uwajibikaji?
Print Course
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.