Kufunza Wachungaji
Wachungaji wanapaswa kufunzwa itikadi, kutafsri Biblia, kuhubiri, na mbinu za kufanya wafuasi. Maelfu ya makanisa duniani kote yanaongozwa na wachungaji walio na vitabu vichache na wasio na mafunzo maalumu. Wachungaji wengi hawana mafunzo na hawana uwezo kuwafundisha wengine.
Wengi wa wachungaji duniani kote hawawezi kwenda chuo cha Biblia. Sio rahisi kwao kuacha familia, ajira, na huduma ili waende kwenye mafunzo mahali fulani kwa miaka kadhaa. Hawa wanahitaji mafunzo mahali waliko.
Kufunza Washuhudiaji 
Mtu yeyote ambaye amejionea neema ya Mungu iokoayo kwenye maisha yake anazo sifa za kueneza injili. Watu wanaweza kusema kile ambacho Mungu amewafanyia. Shuhuda zao zaweza kuwa na ushawishi, hususani kwa watu ambao wanawajua na kuona mabadilio yaliyotokea katika maisha yao.
Hata hivyo, wakati fulani mtu anaweza kuwa hana uwezo wa kuelezea mambo ya msingi yanayohusu injili. Kama wasikilizaji wako tofauti na hawamjui mtoa ushuhuda, wanaweza wasielewe ni jinsi gani wanavyoweza kupata mabadiliko ya aina hiyo.
Hata mtu ambaye amekuwa mwamini kwa miaka mingi anaweza kujiona hawezi kushuhudia watu wa jamii yake kwa sababu hawezi kujibu maswali yanayohusu ukristo. Mwamini huyu anajua jinsi alivyookoka, anavyojisikia anapoabudu, na jinsi ya kushirikiana na wengine katika mwili wa Kristo lakini hana uwezo wa kuelezea mambo hayo.
Wakati mwingine jamii ina uadui na Ukristo. Wakati mwingine wanaheshimu wafuasi wa Kristo ambao wanaishi maisha mema, lakini hata hivyo wanahitaji pia kusikia ufafanuzi wa Imani ya kikristo.
Mtu anaweza kuwa mshuhudiaji mwenye ufanisi kwa kujifunza kanuni za injili na itikadi za msingi zinazo kubalina na injili.
Kulinda Kanisa 
Wachungaji wanawajibika kulinda makanisa yao kwa mafundisho sahihi (Tito 1:9-14). Makanisa ya uongo na dini za uongo hutumia fikira zinazochanganya na kuhadaa watu. Ni huzuni kuwa watu wengi ambao walikuwa wameokoka baadaye hupotoshwa na kuchukuliwa na kanisa la uongo.
Mchungaji anapaswa kufundisha itikadi za kibiblia ili watu wajengwa katika Imani. Mafundisho lazima yawe yenye makusudi, yenye mpangilio na yenye kutolewa katika viwango mbalimbali ngazi ili kuwafikia watu wote wa kanisa.
Kupanua Timu ya Huduma 
Timu za michezo huwa zina mabenchi ya wachezaji ambao wakati wote hawachezi. Wengine wanaweza kuwa bado ni wadogo na wana ujuzi kidogo kuliko wale waliobobea, lakini wako katika mafunzo. Wengine wana uwezo maalumu utakaohitajika wakati fulani.
Kanisa lenye afya, linalokua linapaswa kuwa na “benchi”. Ni kosa kufikiri kuwa kwa sababu nafasi za uongozi kanisani zina watu, basi timu imekamilika. Huduma hufikia mwisho na haiendelei kukua isipokuwa kuna viongozi wanaosaidia kuanza aina nyingine ya huduma.
Kanisa lenye afya linapaswa kuwa na watu kwenye “benchi” ambao wanaendelezwa na wanafanyizwa mazoezi. Hilo linahitaji mafunzo ya kanisa la mahali. Kwa hiyo, huduma ya mafunzo sio tu ni ya watu wanashikilia nyadhifa.
Kazi ya mchungaji ni kuhakikisha mafunzo yanafanyika. Mchungaji hatakuwa na uwezo kutoa mafunzo yote mwenyewe, lakini anapaswa kuyapanga na kutia moyo. Anahitaji timu ya watu wanaotumika katika huduma mbalimbali kanisani.

Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo (Waefeso 4:11-15).
Mungu huwapa watu wa kanisa la mahali karama na vipawa vinavyohitajika kutimiza kazi ya kanisa. Hivyo lazima kanisa lichukue wajibu wa makusudi kuendeleza watu.
Kuimarisha Kanisa la Wenyeji 
Kanisa la wenyeji linaongozwa na watu wake, na ni miliki yao. Halitegemei kupata fedha au kuongozwa kutoka nchi za nje. Uimara wa kanisa la wenyeji ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa makanisa.
Kanisa la wenyeji liko nyumbani katika utamaduni wake. Hili sio kanisa la nchi za nje.
Kanisa la faida kubwa wenyeji lina manufaa mengi:
1. Lina eneza injili kwa ufanisi na kuwafanya watu kuwa wafuasi katika utamaduni wao.
2. Kusanyiko linakuwa komavu na linatenda kazi kama mwili wa Kristo bila kutegemea nchi za nje.
3. Viongozi wake hujijenga na kufikia uwezo unaohitajika.
4. Washirika wa hapo huwezesha na huwajibika kwa ajili ya kazi ya huduma.
Baadhi ya makanisa ya wenyeji hayana afya kwa sababu yanakosa uimara wa itikadi na viwango vya maisha ya kikristo. Yanashindwa kushawishi jamii zao kwa ushuhuda wenye nguvu, na wenye uendelevu. Yanakuwa wahanga wa viongozi wenye vipawa lakini hawana tabia njema. Wanakosa mafunzo ya kuwaendeleza kiuongozi. Hivyo wanahitaji huduma ya mafunzo mahali pao.
Wakati mwingine kanisa linaanzishwa na mishenari kutoka nchi nyingine kwa malengo kuwa baadaye litakuwa la wenyeji. Malengo ya komavu wake hupimwa kwa uwezo wa kujitegemea kwake na uwajibikaji wa viongozi wake.
Mafunzo katika ngazi ya kanisa la mahali ni lazima kwa ajili ya kuendeleza viongozi wa hapo ambao ndio hufundisha itikadi, hutumia imani ya vitendo katika maisha, na kuendeleza namna nzuri ya huduma njema na mbinu njema.
Kupanda Makanisa 
Ni huzuni kuwa makanisa mengi hufanya kazi miaka mingi bila kupeleka injili katika jamii zingine. Makanisa yanapaswa kufunza na kutuma timu za wainjilisti kwenye maeneo ambayo hayana makanisa. Shabaha ya timu hizo ni kuwa na kundi jipya la watu waliokoka na wanakuwa kanisa.
Wainjilisti baadhi wanapaswa kufunzwa kusaidia makundi hayo ya waliokoka ili wawe kanisa. Wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwafanya waamini hawa wapya kuwa wafuasi kwa kuwafunza jinsi ya kuishi maisha ya kikrsito. Wanapaswa pia kuwa na uwezo wa kufunza kueneza injili na kuwajibika kufanya huduma.
Makanisa mengi mapya yataongozwa na mtu mwenyeji, sio na Mchungaji anayetoka kwingine na kuishi katika jamii hio. Wachungaji wengi wenye elimu kubwa hawako tayari kuchunga kanisa jipya au kutumika vijijini au miji midogo. Lazima tupate huduma ya mafunzo kwa mshirika wa mahali kanisa lipo ambaye ameitwa na Mungu kuongoza kusanyiko hilo.
Kutayarisha Wamishenari 
Mishenari ni mtu ambaye anatumwa na kansia kwenda mahali pengine kwa kusudi la kueneza injili. Neno mishenari linatumika hususani kwa mtu ambaye anakwenda katika nchi nyingine na/au jamii ya utamaduni tofauti, lakini wakati mwingine linarejelea kwa mtu ambaye anaenda kwenye jamii nyingine katika nchi yake mwenyewe.
Injili inaenea haraka katika baadhi ya maeneo ya dunia, mengi ya hayo ni yale ambayo wamishenari wenyeji wanaenda kwenye maeneo mengine ya nchi zao. Hivyo mafunzo yangeongeza ufanisi wao na uimara wa itikadi zao.
Dirisha la 10/40 ni eneo la nyuzi 10 kusini mpaka nyuzi 40 kaskazini mwa ikweta, likianzia Africa kaskazini na Asia ya kusini, linajumuisha nchi za China na India. Eneo hili lina jumla ya 2/3 ya idadi ya watu duniani. Zaidi ya 80% ya watu katika dirisha 10/40 hawajafikiwa na na injili.
Baadhi za nchi za dunia hazijafikiwa na injili kwa kiwango cha kutosha ingawa miji yake mikubwa imeshakuwa na makanisa kwa miaka mingi. Mtu anaweza kutumika katika kanisa kwa miaka mingi lakini bado hajui jinsi ya kuanzisha huduma katika eneo jipya. Anajua tu jinsi ya hubiri katika kundi la waamini walioko katika jengo la kansia. Kanisa linapaswa kufunza wamishenari kupeleka ujumbe wakiwa na shabaha ya kuanzisha familia ya waamini katika jamii hiyo.