Mwezeshaji anaweza kutumia njia zilizomo katika sura hii ili kuendeleza walimu wenyeji. Kama kanisa mahali lilipo halina mtu anayejisikia ana uwezo wa kufundisha, mwezeshaji hawezi kuanza haraka masomo yanayojitegemea. Mwezeshaji lazima amgundue na kumwedeleza mwalimu mtarajiwa. Sura hii inamwelezea mwezeshaji jinsi ya kupata mwalimu mwenyeji.
Mwezeshaji kutayarisha walimu wenyeji jinsi ya kutumia mbinu hii kwa wanafunzi wao. Kama walimu wenyeji wa eneo jipya tayari wana uwezo wa kufundisha, mwezeshaji hahitaji kutumia zoezi katika sura hii. Mwezeshaji anapaswa kujifunza mbinu hii kwa walimu wenyeji ili waweze kutumia mazoezi ya kuwaendeleza washiriki.
Mwalimu mwenyeji kuwandeleza washiriki. Kila mwalimu anapaswa kuwa na juhudi za kuendeleza ujuzi wa huduma ya washiriki. Mbinu zilizoelezwa katika katika sura hii zitafaa kuwasaidia washiriki kuanza kuzumza katika makundi.
Mara nyingine wawakilishi wa SGC wanapotembelea makanisa wanakuta watu walio tayari kuanza kufundisha. Kwa kawaida, walimu hawa watarajiwa ni watu walio na taaluma na wana uzoefu wa kufundisha. Wanaweza kuyaangalia masomo na kuona kuwa ni rahisi kuyafundisha. Maelekezo yamechapwa mwanzoni mwa kila somo. Kuna maswali ya mjadala. Sio kwamba masomo haya ni kitabu tu; yanaweza kufundishwa kama yalivyo.
Masomo yamepangiliwa kiasi kwamba mtu mwenye ujuzi wa kusoma, uelewa wa Biblia, na uwezo wa kufundisha anaweza kujifunza haraka kuvitumia. Walakini, wakati mwingine watu ambao hawana mafunzo ya kitaaluma hujisikia kwamba hawana uwezo wa kufundisha. Wanafikiri kwamba ni watu waliopata mafunzo ya juu tu ndio wanaweza kufundisha.
Mungu amewapa watu wengi ambao hawajapata fursa ya kupitia vyuoni uwezo wa kufundisha. Ni kwa kuwa walimu ni muhimu kwa kanisa, Tunaweza kuwa na ujasiri kwamba kwa kawaida Mungu ana watu wenye uwezo wa kufundisha mahali popote ambapo kuna kanisa (Waefeso 4:11-12).
Watu wengi hawatambui kuwa tayari wamepata ujuzi wa kufundisha kwa kupitia maisha yao ya kila siku. Huwa wanaelezea mambo nyumbani na wakiwa kazini. Wanasaidia watu kutatua matatizo yao. Wanayo sifa njema kuwa wanauwezo wa kuelezea mambo. Walipokuwa wanafunzi mashuleni walikuwa na ujuzi wa kusoma na kuelewa na kueleza. Hawajui kuwa wana uwezo wa kufundisha.
Mwezeshaji anapaswa kuwasaidia walimu watarajiwa kugundua uwezo wao kupitia uzoefu wa kuongea walionao. Kupitia uzoefu, mtu anaweza anaweza kujiamini kuzungumza katika kikundi.
Njia za kupata Uzoefu katika kuongea
1. Wape Zoezi la kuongelea Mada rahisi. Hotuba iwe ya muda wa dakika chache. Kama washiriki wanajisikia aibu kusimama mbele ya kikundi wape fursa kutoa hotuba zao wakati wamekaa katika viti vyao.
Mifano ya mada za rahisi kuzungumzia:
Zungumzia changamoto ulizopitia ukiwa mtoto.
Zungumzia kuhusu ndugu ambaye alikuwa muhimu kwako.
Mulize mshiriki mwingine maswali ndipo mtambulishe mshiriki huyo katika kikundi.
Ni mahali gani ungependa kutembelea? Kwanini?
Zungumzia mstari moja wa Maandiko unaoupendelea.
Zungumzia siku zima inavyokuwa ukiwa kazini kwako.
Unakumbuka nini kutokana na mahubiri uliyosikia hivi karibuni?
2. Katika darasa mwelekezee mtu swali. Swali liwe la kutaka maelezo, sio majibu mafupi ya ndio na hapana. Swali lihusu jambo ambalo mshiriki anaweza kujibu, ili ajiamini zaidi na sio kujisikia amedhalilishwa.
3. Omba mshiriki moja kuelezea mazoezi yao ya kikundi waliyoandika. Masomo yanahitaji mazoezi aina mbalimbali ya kuandika. Hata kama mwezeshaji amekuja kwa siku moja, washiriki wanaweza kupewa moja ya zoezi la kuandika na kuliwasilisha.
4. Wagawe katika vikundi vya watu watatu kwa ajili zoezi la kufundisha. Mpatie kila mtu sehemu fupi afundishe katika kikundi. Hii inafanya kuwa na watu wachache na kuwapatia fursa washiriki kadhaa kufanya zoezi kwa wakati moja.
5. Omba mshiriki aelezee sehemu ya somo. Sehemu nyingi katika somo zina aya chache zinazoelezea dhana husika. Muombe mshiriki mapema kujitayarisha kuelezea sehemu hiyo kwa dakika chache.
6. Omba mshiriki mwenye uelewa mzuri kufundisha mada kutoka moja ya masomo. Utaratibu rahisi kwa mshiriki ni kufundisha mada ambayo amesikia mtu mwingine akifundisha. Mshiriki ataonesha uwezo wake wa juu anapojitayarisha na kufundisha somo ambalo hakuna aliyemfundisha. Mwezeshaji anaweza kujisikia kuendelea kufundisha zaidi kadiri inavyowezekana, na darasa likafurahia kumsikiliza mwezeshaji, lakini kumbuka lengo ni kuwatayarisha wengine kufundisha.
7. Tumia mbinu za “meza ya duara” Washiriki. Wanakaa wakizunguka meza wakiwa na somo lilochapwa. Hakuna mwalimu katika meza hiyo. Washiriki mbalimbali wanaachiana kuzungumza kitu kuhusu mada. Mtu moja katika meza anapewa wajibu kuongoza na kuendeleza mjadala kwa kuuliza mwitikio kutoka kwa washiriki. Kiongozi huyu sio mwalimu. Kikundi kitagundua kuwa kinafanya kazi na kujifunza bila mwalimu. Mbinu hii inawezesha kikundi kujiunda hata mahali ambapo hakuna mtu ambaye anasifa ya kufundisha.
Hitimisho
Maono ya SGC ni kuifanya huduma ya mafunzo kuwa ya wenyeji kila mahali. Mafunzo yanaweza kuwa kila mahali kupitia watu ambao Mungu amewapa uwezo wa vipawa na uelewa wa Biblia. Wawezeshaji wanapaswa kukubuka kuwa kusudi lao sio tu kutoa maarifa lakini pia kuwatayarisha washiriki kuieleza kweli kwa wengine.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.