Sifa za kidini
Kwa kuwa masomo ya SGC yana makusudi ya mafunzo ya huduma, washiriki wanapaswa kuwa waamini wa kikristo walio na ushuhuda mzuri na maisha yanayoheshimika. Asiyeamini hataelewa au hatayathamini yale yaliyoko katika masomo.
Washiriki wanapaswa kuamini misingi ya imani ya kikristo katika ukristo wa asili, ikijumuisha itikadi ya kievangeliko. Masomo yamepangiliwa kutumikia mwili wa Kristo kila mahali, hivyo imani za kimadhehebu hazihitajiki.
Mshiriki anapaswa kuwa mshirika wa kanisa ambaye hushiriki katika ibada na ushirika wa kanisa lake. Washiriki ambao hawako tayari kuheshimu makanisa yao hawatakuwa wajumbe wazuri wa mafunzo. Wanatakiwa kuwa sehemu ya makanisa ambayo yatawaruhusu kuyatendea kazi yale wanayojifunza. Baadhi ya mazoezi yatahusisha ushirikishaji wa waamini wengine.
