Maisha Na Huduma Ya Yesu
Maisha Na Huduma Ya Yesu
Audio Course Purchase

Search Course

Type at least 3 characters to search

Search through all lessons and sections in this course

Searching...

No results found

No matches for ""

Try different keywords or check your spelling

results found

Lesson 6: Kufundisha kama Yesu

21 min read

by Randall McElwain


Malengo ya Somo

Kufikia mwisho wa somo hili, kila mwanafunzi atapaswa:

(1) Aelewe maana ya ufalme wa Mungu katika Vitabu vya Injili.

(2) Kutambua kwa pamoja vipengele vya wakati huu na wakati ujao vya ufalme wa Mungu.

(3) Kufuata kanuni za Yesu za maisha katika ufalme kutokana na Mahubiri ya Mlimani.

(4) Kufasiri kwa ukamilifu mifano ya Yesu kuhusiana na ufalme.

(5) Kujikabidhi kwenye masharti ya Yesu kuhusiana na uanafunzi.

Kanuni ya Huduma

Sisi tunahudumu kama mabalozi wanaouwakilisha Ufalme wa Mungu katika ulimwengu wetu.

Utangulizi

Ufalme wa Mungu ndiyo dhamira kuu ya msingi katika Agano Jipya.[1] Neno “ufalme” linaonekana mara hamsini na nne katika Mathayo, mara kumi na nne katika Marko, mara thelathini na tisa katika Luka na mara tano katika Yohana.[2]

Karibia nusu ya mifano ya Yesu inafundisha kuhusu ufalme wa Mungu. Anahubiri kuhusu ufalme. Anaponya na kutoa mapepo kudhihirisha uwezo wa ufalme. Baada ya kupaa, kanisa la mwanzo liliendelea kuhubiri ujumbe wa ufalme (Matendo 8:12; 28:23).

Katika somo hili, tutajifunza kuhusu ufalme wa Mungu katika huduma ya Yesu na matokeo ya ufalme katika huduma leo. Mwisho wa somo hili, nimeweka mahubiri yaliyohubiriwa Nigeria kuhusu ufalme wa Mungu. Mahubiri haya yanaonyesha jinsi ujumbe wa ufalme ulivyo na matokeo kwenye huduma katika dunia yetu.

 

[1] Vianzo vilivyotumika katika sura hii ni pamoja na:

+ D. Matthew Allen, “The Kingdom in Matthew” (1999). Kinapatikana kutoka https://bible.org/article/kingdom-matthew March 22, 2021.

+ Darrell L. Bock, Luke: Baker Exegetical Commentary on the New Testament. (Grand Rapids: Baker Books, 1994-1996)

+ J. Dwight Pentecost, The Words and Works of Jesus Christ. (Grand Rapids: Zondervan, 1981)

+ Martyn Lloyd-Jones, Studies in the Sermon on the Mount. (Grand Rapids: Eerdmans, 1959)

[2] Mathayo kwa kawaida alirejea “ufalme wa mbinguni,” Luka alirejea kama “ufalme wa Mungu.” Wasikilizaji wa kwanza wa Mathayo walikuwa Wayahudi; Wayahudi walikwepa kutumia

Jina la Mungu na mara nyingi wakitumia “mbinguni” kama tasifida ya Mungu. Inaonekana kwamba Mathayo alibadili “Ufalme wa Mungu” kuwa “Ufalme wa Mbinguni” kwa namna nyingi. Katika somo hili, nitatumia “Ufalme wa Mungu” isipokuwa pale ninapokuwa nanukuu kwa Mathayo.

Ufalme wa Mungu

Kuna maswali mawili yanayotambulisha fundisho hili kuhusu ufalme wa Mungu.[1]

1.    Je, Ufalme wa Mungu ni nini?

2.    Je, Ni lini ufalme wa Mungu utaanzishwa?

Je, Ufalme wa Mungu ni nini?

Soma Matendo 1:1-8.

Siku arobaini baada ya kufufuka, Yesu alikuwa na wanafunzi wake “akizungumzia juu ya ufalme wa Mungu.” Muda mfupi kabla ya kupaa, wanafunzi wake walimwuliza, “Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?” Wanafunzi walitegemea yafuatayo:

1.    Ufalme wa haraka: “wakati huu.” Walitegemea Yesu angeanzisha ufalme kwa haraka.

2.    Ufalme wa kisiasa na kijiografia: “unapowarudishia.” Walitegemea kwamba Yesu angeuangusha utawala wa Rumi na kuwarudishia mamlaka ya kisiasa ya Israeli.

3.    Ufalme wa Kitaifa : “ufalme wa Israeli.” Walitegemea Yesu angetawala taifa lao kama ufalme wa wakati wa Daudi kwenye Agano la Kale.[2]

Yesu alijibu,” Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.”

Jibu la Yesu lilionyesha yafuatayo kuhusu ufalme wake:

1.    Ufalme usio na wakati: “nyakati wala majira Baba aliyoyaweka.” Ufalme wa Yesu siyo wa kutegemea nyakati wala majira ya kibinadamu bali wakati wa Baba.

2.    Ufalme usiokuwa wa ulimwengu huu: “nguvu, Roho Mtakatifu akiisha kuwajilia juu yenu.” Ufalme wa Yesu ulijengwa kwenye msingi wa uwezo wa Roho Mtakatifu, na siyo kwenye mamlaka ya kisiasa.

3.    Ufalme wa ulimwwengu wote: “hata mwisho wa nchi.” Ufalme wa Yesu uliwafikia mataifa yote. Haukuwa maalumu kwa ajili ya Iraeli tu.

[3]Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba hawahitaji kujua mambo ya nyakati wala majira. Badala yake, wanapaswa wawajibike na mambo mawili: kupokea Roho Mtakatifu na kuwa mashahidi wake “hata mwisho wa nchi.”

Ufalme wa Mungu utaanzishwa lini?

Miongoni mwa wanazuoni wa theolojia, kuna mitazamo mitatu ya msingi kuhusiana na ufalme wa Mungu.

Ufalme wa Mungu Utakuja.

Baadhi ya wanazuoni wa theolojia wanauona ufalme wa mwisho ukianzishwa na Yesu atakapokuja kuitawala dunia wakati wa miaka elfu moja. Waandishi hawa huangalia maandiko kama Mathayo 24-25 penye msisitizo wa vipengele vya kisiasa na mipaka vya ufalme.

Ufalme Ulishakuja.

Wanazuoni wengine wa theolojia wanafundisha kwamba ufalme wa Yesu ulianzishwa wakati akiwa bado hapa duniani. Wanaweka msisitizo wa maandiko kama ile kauli ya Yesu kwamba “ufalme wa mbinguni umekaribia” na “ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia” (Mathayo 4:17 na Luka 11:20). Mtizamo huu wa ufalme unazingatia asili ya kiroho ya ufalme na utawala wa Mungu ndani ya mioyo ya waumini.

Ufalme tayari ulishakuja, lakini bado haujatambulishwa kikamilifu.

Wanazuoni wa theolojia wengi wanasema kwamba ufalme unahusisha kwa pamoja vipengele vya wakati uliopo na ujao. Mtizamo huu unafundisha kwamba ufalme wa Mungu ulizinduliwa wakati wa huduma ya Yesu hapa duniani; unaendelea kuenea kupitia kazi ya kanisa; utatambulishwa kwa utimilifu wakati Yesu atakaporudi duniani kuja kutawala.[4] Wakati wa kuja kwa Yesu, “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu” (1 Wakorintho 15:24). Huu ndio utimilifu wa ufalme wa Mungu.

► Katika mitazamo hii mitatu wewe unashikilia mtazamo upi? Je, kuna matokeo gani ya kivitendo kwenye huduma kutoka katika kila mtazamo?

Katika somo hili, tutaona vipengele vya ufalme ambavyo tayari vinaonekana na vipengele ambavyo bado vimebakia kutimizwa. Ufalme unahusisha mambo yafuatayo:

  • Mfalme: Kuanzia kwa Mamajusi wakati wa kuzaliwa kwake hadi kubandikwa kwa tangazo la “Mfalme wa Wayahudi” juu ya msalaba, Yesu alikuja kama mfalme.
  • Mamlaka: Yesu alidhihirisha mamlaka yake kupitia miujiza yake na ushindi dhidi ya kaburi.
  • Sheria: Yesu alitoa muhtasari wa sheria za ufalme kwenye Hotuba ya Mlimani.
  • Eneo la nchi: Yesu alifundisha kwamba ufalme wake umeenea hadi miisho yote ya nchi za dunia ikiwa ni pamoja na lugha zote na watu wote.
  • Watu: Watu wote waliokombolewa na Mfalme na wanatawaliwa na yeye ni raia wa ufalme wa Yesu

[1] Kwa ajili ya hotuba za kupitia video kuhusiana na Ufalme wa Mungu, unaweza ukaangalia Scot McKnight, “What and Where is the Kingdom of God?” katika http://www.seedbed.com/where-is-the-kingdom-of-god/ (Iliyopatikana Marchi 22, 2021.)

[2] John Stott, The Message of Acts (Westmont, Illinois: InterVarsity Press, 1990), 41

[3] “Ufalme ulishakuja;

Ufalme unakuja;

Ufalme bado haujaja.”

- Martyn Lloyd-Jones

[4] Watoa maoni hutumia maneno “kuzinduliwa kwa ufalme” wakimaanisha kuanza kwa ufalme wakati wa huduma ya Yesu hapa duniani. “Utimilifu wa ufalme” ni ukamilishwaji wa mwisho wa ahadi za ufalme wakati wa kuja tena kwa Yesu Kristo duniani.

Ahadi ya Ufalme

Soma Mathayo 3:1-12.

Marejeo ya kwanza ya ufalme wa Mungu katika Agano Jipya yanapatikana katika mahubiri ya Yohana Mbatizaji. Akiwa ninabii wa mwisho wa katika Manabii wa Kale wa Agano, Yohana alishutumu unafiki wa viongozi wa dini ya Kiyahudi. Akiwa mjumbe wa kwanza wa Agano Jipya, aliandaa njia kwa ajili ya ujio wa mfalme mpya. “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 3:2). Neno “umekaribia” linaashiria kwamba ufalmeunakaribia kwa haraka. Haujafika bado, lakini uko karibu sana. Yohana alihubiri kuwaandaa Wana wa Israeli katika ujio wa Masihi ambaye ataongoza katika ufalme mpya.

Kitambo kidogo baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alianza huduma yake ya hadharani. Alisafiri kupitia Galilaya “akitangaza injili ya ufalme.” Kama ilivykuwa kwa Yohana Mbatizaji, Yesu naye alitangaza, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 4:17).

Soma Mathayo 10:5-42.

Yesu aliwatuma wanafunzi kumi na mbili kuhubiri ujumbe wa ufalme kwa “kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” Kama ilivyokuwa kwa Yohana Mbatizaji na Yesu, walihubiri wakisema, “Ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 10:5-7).

Huduma ya wanafunzi ilikuwa imekaa katika mpangilio sawa na huduma ya Bwana wao. Kama Yesu, walikuwa watangaze kuhusu ufalme na wahudumie mahitaji ya kimwili ya watu. Kama Yesu, waliponya wagonjwa na kutoa mapepo kama ishara kwamba ufalme wa Mungu sasa umeingia kusambaratisha kwenye mamlaka za Shetani. Yesu aliwatuma wawakilishi wake, “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo” (Mathayo 10:8).

Kuzinduliwa kwa Ufalme

Soma Mathayo 12:22-32.

Ahadi ya ufalme haikuwa mpya. Manabii wa Agano la Kale walikuwa wametabiri kuhusu ujio wa ufalme wa baadaye. Hata hivyo, Yesu alitangaza kwamba ufalme haukuwa tu kwa ajili ya matumaini ya baadaye, lakini ni ukweli wa mara moja. Yesu alitangaza kuzinduliwa kwa ufalmewa Mungu. Ufalme wa Mungu ulikuwepo mahali popote ambapo Yesu alikuwa yupo.

Akiwa na uwezo dhidi ya mapepo, Yesu alidhirisha mamlaka ya mfalme ambaye ameushinda ufalme wa Shetani. Baada ya kumponya mtu aliyekuwa amegandamizwa na pepo, Mafarisayo walidai kwamba Yesu “anatoa pepo” kwa nguvu za “Beelzebuli, mkuu wa pepo.” Yesu alijibu kwamba alikuwa anaushinda ufalme wa Shetani kupitia nguvu za Mungu: “Mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia” (Mathayo 12:24, 28). Yesu alikuwa amevamia ufalme wa Shetani.

Soma Mathayo 11:1-24.

Miujiza ya Yesu ilikuwa ni ishara ya uzinduzi wa ufalme wake.Injili ya Yohana inatumia neno “ishara” kwa ajili ya miujiza ya Yesu. Miujiza ilikuwa ni ishara ya utambulisho wa Yesu na ushahidi wa ufalme mpya.

Yohana Mbatizaji alitangaza kwamba “ufalme wa mbinguni umekaribia.” Alikuwa ametegemea ufalme wa kisiasa utakaoleta ukombozi kwa Israeli.. Badala yake, Yohana akajikuta yuko gerezani akikabiliwa na kifo!. Aliwatuma wanafunzi wake kuuliza, “Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?” Huduma ya Yesu haikuendana na mategemeo ya Yohana Mbatizaji ya Masihi wa kisiasa ambaye angeanzisha ufalme wa kidunia.

Yesu alimjibu kwa kuelezea kazi zake kama Masihi.

Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; Vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.

Yesu alimfundisha Yohana kuwa mtu wa subira kwa ajili ya mpango wa Mungu unaoonekana.

Ingawaje Yesu alimpongeza Yohana kwa nguvu na ujasiri, alitangaza kwamba “aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu” kuliko Yohana. Kwa nini? Yesu alikuwa amekuja kuanzisha agano jipya pamoja na mafao yote yaliyoko kwenye ufalme. Mwamini wa mwisho wa Agano Jipya ana faida kubwa kuliko mtakatifu maarufu sana wa Agano la Kale ambayo hakuwahi kuipata. Waamini wa Agani Jipya wameshuhudia utimilifu wa utabiri wa Agano la Kale. Ufalme uliokuwa umetabiriwa umeshazinduliwa.

Maisha katika Ufalme: Hotuba ya Mlimani

Mahubiri marefu ya wakati mmoja yaliyokwisha rekodiwa katika Vitabu vya Injili ni Hotuba ya Yesu Mlimani. Ufalme wa Mungu ndio dhamira kuu iliyoko katika mahubiri haya. Hii inaonekana kwa njia mbalimbali:

  • Hali ya heri ya kwanza inafundisha kwamba ufalme wa Mbinguni ni “kwa walio maskini wa roho. Hali ya heri ya mwisho inafundisha kwamba ufalme wa Mbinguni ni kwa ajili ya wale “wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki.” Heri hizi mbili zinaifunga bahasha yenye hali zote za Heri zikionyesha kwamba msingi mkuu wa dhamira ya Hali za Heri ni ufalme wa Mbinguni.
  • Yesu anadai mamlaka ya kufasiri sheria (Mathayo 5:21-48). Hiki ni kitendo cha mfalme ambaye ana mamlaka ya kufasiri na kutumia sheria za ufalme wake.
  • Yesu aliwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kuomba, “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni” (Mathayo 6:9-13). Tumeitwa kuomba kwa ajili ya kuendelea kwa ufalme wa Mungu hapa duniani. Watu wa Mungu wanapoishi sawasawa na Hotuba ya Mlimani, ufalme unapanuka na mamlaka ya Mungu yanapanuka kwenda kwa raia wapya wa ufalme.
  • Mwisho wa mahubiri yake, Yesu alifundisha kwamba “matendo mema” peke yake hayatoshi kwa mtu “kuingia kwenye ufalme wa mbinguni.” Ni wale tu “wafanyayo mapenzi ya Baba yangu” ndio watakaoingia kwenye ufalme huo.

Kanuni za Kusoma Mahubiri ya Mlimani

Inatupasa tukumbuke kanuni tatu jinsi tunavyoendelea kusoma Mahubiri ya Mlimani.

(1) Kutii maamrisho ya Hotuba ya Mlimani hakuleti kupewa “uraia“ kwenye ufalme wa mbinguni.

Hatupaswi kufikiri, “Ishi kwa njia hii na utakuwa Mkristo.” Badala yake, tunapaswa tuisome hii Hotuba ya Mlimani kama mwongozo wa maisha kama raia wa ufalme: Ishi kwa njia hii kwa sababu wewe ni Mkristo.” Tumeokolewa kwa neema peke yake; kasha, kama raia wa ufalme wa Mungu, tunatii maagizo yake.

(2) Hotuba ya Mlimani ni kwa Wanafunzi tu na siyo kwa watu wasioamini.

Hii siyo katiba ya nchi ya kidunia. Usishangae wakati majirani zako ambao hawajaamini wakikataa kuishi sawasawa na kanuni hizi! Huu ni ufafanuziwa maisha katika ufalme wa Mungu, na siyo maisha katika falme za mwanadamu.

(3) Hotuba ya Mlimani ni kwa ajili ya kila Mwamini.

Watu wengi wamejitahidi kuepuka kuendana na madai yaliyopo kwenye haya Mahubiri wakidai kwamba kanuni hizi hazifai kwa waamini wa kawaida. Wengine wamesema, “Sheria hizi ni za baadaye kwa ajili ya ule ufalme ujao wa miaka elfu moja. Wengine wamesema, “Hizi sheria ziko kwa ajili ya watakatifu wachache. Wakristo wengi hawana uwezo wa kuzifuata hizi sheria. Wengine wamesema, “Mahubiri haya yanaashiria kwamba kamwe hatuwezi tukazitimiza sheria za Mungu. Tunapojikuta kwamba kamwe hatuwezi tukazitimiza sheria za Mungu, tutategemea neema ya Mungu peke yake.”

Hata hivyo, kanisa la mwanzo liliyasoma Mahubiri haya kama mwongozo kwa kila mwamini. Barua za Yakobo na 1 Petro zina marejeo mengi ya sheria zinazotokana na haya Mahubiri. Yesu alikataa kudhoofisha hadhi ya kiwango cha utakatifu wa Mungu. Badala ya hadhi ya kiwango cha chini kuliko Mafarisayo, Yesu aliwaweka wafuasi wake kwenye hadhi ya kiwango cha juu: “Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:20).

Maisha kwenye Ufalme wa Mungu

Soma Mathayo 5-7.

Kama Ysu alizindua ufalme wakati wahuduma yake hapa duniani, sasa tunaishi kweye ufalme wa Mungu. Hotuba ya Mlimani inafafanua tabia za raia wa ufalme wa mbinguni. Hapa kuna mtazamo mfupi wa dhamira ya haya Mahubiri.

(1) Maadili ya ufalme wa Mungu ni kinyume kabisa na maadili ya ulimwengu huu.

Hakuna mtawala katika ulimwengu huu anayesema kuwa maskini ni kubarikiwa, kuomboleza, kusalimisha haki zetu, au kuteswa. Haki ya Heri zinaelezea kinyume kabisa cha maadili ya Utawala wa Rumi wakati wa Yesu, na ulimwengu wetu wa leo. Ufalme wa Mungu ni tofauti na ufalme wa mwanadamu.

(2) Raia wa ufalme wa Mungu wanapaswa walete mabadiliko kwenye ulimwengu wao.

Kundi la Waesene la wakati wa Yesu lilisema kwamba wenye haki wanapaswa kujiondoa katika jamii na kuanzisha ufalme wa Mungu wakiwa wamejitenga. Yesu alisema, “Hapana! Ninyi ni chumvi ya dunia; ambayo inahifadhi na kuikoleza dunia yenu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu inayoleta utukufu kwa ‘Baba yeu aliye mbinguni’” Wakati ufalme wa Mngu kimsingi ni wa kiroho, dunia yetu inatakiwa ifaidike kisiasa, kiuchumi, na kijamii kutokana na uwepo wa raia wa ufalme.

[1]Tunaweza tukaorodhesha mifano mingi ya Wakristo waliokuwa chumvi na nuru katika jamii ya kidunia. William Wilberforce aliongoza Bunge katika kukomesha biashara ya watumwa katika iliyokuwa Dola ya Uingereza. Uamsho wa Wamethodisti ulileta mabadiliko ya kijamii katika ngazi zote za jamii ya Waingereza. Kuua watoto na kuwachoma wajane pamoja na maiti za waume zao ilikuwa halali nchini India. William Carey alipigana kukomesha uovu huu. Wakristo wameeneza kusoma na kuandika ili kuondoa ujinga, wameanzisha mahosipitali na vituo vya kutunzia watoto yatima na wasoijiweza, na wamesaidia maskini na wahitaji katika mataifa mengi.

(3) Raia katika ufalme wa Mungu wanaenda hata zaidi ya mahitaji ya chini ya Sheria ili kuonyesha upendo wa Baba

Yesu hakuja duniani ili kuitangua Sheria, bali “kuitimiza” Sheria. “Sikuja kutangua, bali kutimiliza.” Kutimiliza kitu ni “kuleta kwenye kukamilika” au “kuhitimisha.” Yesu hakuja kwa ajili ya kuitangua Sheria bali kuidhihirisha roho nyuma ya Sheria. Katika mfululizo wa mifano sita, Yesu anaonyesha kwamba haki ya raia wa ufalme ni lazima “izidi haki ya waandishi na Mafarisayo.”

Sheria

Raia wa Ufalme

Sheria inakataza mauaji.

Raia wa ufalme wanashughulikia chanzo cha uhamasishaji wa chuki.

Sheria inakataza uzinzi.

Raia wa ufalme “hawaangalii kwa nia ya kumtamani mwanamke.”

Sheria inahitaji
“cheti cha talaka.”

Raia wa ufalme wanatafuta njia za kuidumisha ndoa, kuliko kutoa sababu za kutaka kuachana.

Sheria inakataza viapo vya uongo.

“Ndio” au “Hapana” kwa raia wa ufalme inatosha.

Sheria inaweka mipaka ya kulipiza kisasi
("jicho kwa jicho").

Raia wa ufalme wanachukua hatua za upendo, na siyo kulipiza kisasi aact from love, not revenge.

Sheria inataka upendo kwa jirani yako.

Raia wa ufalme wanawapenda hata maadui wao.[2] Wanadhihirisha upendo na huruma za Baba yao wa mbinguni (Luka 6:36).

(4) Raia wa ufalme wanajali zaidi kumpendeza Mungu kuliko kuwapendeza watu wengine.

Mafarisayo walitaka watu waone ukarimu wao; raia wa ufalme wanaweka siri. Wanafiki waantaka watu wengine wasikie sala zao znyekuvutia; raia wa ufalme wanaomba kwa wepesi na kwa kumaanisha. Mafarisayo walitaka watu wengine wawaheshimu kwa ajili ya kufunga kwao kwa muda mrefu; raia wa mbinguni wanafunga tu kwa ajili ya kupata thawabu ya Mungu.

(5) Raia wa mbinguni hawategemei utajiri wao au kuwa na mashaka kuhusu mahitaji yao.

Badala yake, wana imani ya utoaji kutoka kwa Baba yao wa mbinguni.

(6) Raia wa ufalme hawana hukumu dhidi ya watu wengine.

Hata hivyo, ni waangalifu kugundua tunda la uovu la waalimu wa uongo.

(7) Raia wa ufalme wanajiamini katika maombi yao.

Raia wa ufalme wanajiamini katika maombi yao kwa sababu wanajua kwamba “Baba yao aliye mbinguni anatoa yaliyo mema kwa ajili ya wale wamwombao!”

(8) Raia wa ufalme wanaelewa kwamba kuna njia mbili tu.

Wanaelewa kwamba kuna lango pana na lango jembamba. Kuna mti wa mema na mti wa maovu. Kuna mjenzi mwenye hekima na mjenzi mpumbavu. Raia wa ufalme wanatambua hayo.

Kuishi kwa kanuni za ufalme.

[3]Tunawezaje kuishi kwa kanuni za Hotuba ya Mlimani? Msingi ni katika Mathayo 5:48. Raia wa ufalme tumeitwa tumfananie Baba yetu wa mbinguni. Mahubiri ya Yesu ni mepesi – na ni magumu. Ni neema ya Mungu tu inayotuwezesha tuishi sawa na mafundishoya Yesu. Kwa uwezo wetu wenyewe, kamwe hatuwezi kuishi kulingana na mahitaji ya Hotuba. Ni Roho Mtakatifu peke yake anayefanya maisha ya ufalme yawezekane.

Ni lazima tuelewe kanuni hii tunapokuwa tunahubiri Hotuba ya Mlimani. Kama tutahubiri Hotuba hii kama sheria peke yake, tutawaacha watu wakiwa wamechanganyikiwa na kukataa tamaa. Ni pale tu tutakapohubiri hii Hotuba kama mfano wa maisha ya ufalme – yaliyowezeshwa kwa neema ya Mungu, yaliyonunuliwa kwa dhabihu ya Mwanae, na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu – kwamba Hotuba ya Mlimani kweli imekuwa injili, “habari njema.”

► Baada ya kusoma Hotuba ya Mlimani na kutafakari muhtasari huu, jadili:

  • Ni mafundisho gani kutoka katika Hotuba hiyo yanaonekana kuwa magumu kwa Wakristo katika jamii yako?
  • Ni mafundisho gani kutoka katika Hotuba hiyo yanaonekana kuwa magumu sana kwako kama kiongozi wa Kikristo?

[1] “Mwenye moyo safi siyo tu kwamba atamwona Mungu lakini atakuwa barua ambayo jamii itamwona Yeye.”

- Leon Hynson

[2] Agano la Kale halijaamuru Israeli “mchukie adui yako.“ Hii ilikuwa ni kueleweka visivyo kwa Agano la Kale.

[3] "Hotuba ya Mlimani ni onyo dhidi ya kupenda kukiwa na masharti yaliyoambatanishwa, kupenda kwa ajili ya kujpatia faida binafsi, au kukataa wito wa haki ya kweli. Kwa hakika, hotuba hii ni wito wa kuonyesha aina za misamaha, utoaji, upendo wa kushukuru na rehema ambao unamfanania Mungu.”

- Darrell Bock

Siri ya Ufalme: Mifano ya Ufalme

Waalimu wa Kiyahudi walijua kwamba tunakumbuka hadithi zaidi kuliko tunavyokumbuka taarifa za kupendeza. Kwa sababu hiyo, mifano ilikuwa ni aina maarufu ya kufundishia iliyotumiwa na rabi wa Kiyahudi. Yesu alitumia mifano ili kuunganisha kweli za ufalme wa Mungu.

Mapema kwenye huduma yake, matumizi ya mifano ilimruhusu Yesu kufundisha wanafunzi akiwa anakwepa mgogoro wa moja kwa moja na maadui zake. Baadaye, Yesu angekabiliana moja kwa moja na viongozi wa dini Yerusalemu; lakini katika miaka ya mwanzo, fokasi yake ilikuwa ni kufundisha wanafunzi.

Watu wengi waliisikia ile mifano lakini hawakuelewa. “Wanasikia lakini kamwe hawaelewi”; “wanaona lakini kamwe hawajui.” Kwa nini? Kwa sababu wameifanya migumu mioyo yao. Isaya alitabiri:

Mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya (Mathayo 13:15, akinukuu Isaya 6:9).

Kupitia mifano, Yesu aliweza kufundisha wale ambao masikio yao yalikuwa tayari kusikia

Mathayo 13 inawakilisha mfululizo wa mifano kuhusu “siri za ufalme” (Mathayo 13:11). Mifano hii inafichua asili ya ufalme wa Mungu kwa wafuasi wa Yesu, huku ikificha mengi ya mafundisho yake kutoka kwa viongozi wasioamini.

► Kabla ya kuendelea, simama na usome Mathayo 13:1-52. Utakapokuwa unasoma kila mfano, andaa muhtasari wa dhamira ya msingi ya kila mfano kwa mistari miwili au mitatu katika jedwali lililoko katika ukurasa unaofuata. Kwa kila mfano, tafuta matumizi yake kwenye huduma leo. Nimekamilisha mfano wa kwanza kama kielelezo.

Mifano ya Ufalme

Mfano

Dhamira

Somo la kujifunza kwa huduma leo

Mpanzi

Kinachotegemewa kutoka kwa msikilizaji ni kipimo cha utoaji wa matunda

Ninapokuwa ninahubiri au kufundisha, ni lazima nimwamini Mungu kwa matunda. Siwajibiki katika mavuno; ninawajibika katika kupanda mbegu kwa uaminifu

Magugu

 

 

Mbegu ya haradali

 

 

Chachu

 

 

 

Hazina iliyositirika

 

 

 

Lulu ya thamani kubwa

 

 

Wavu (juya)

 

 

 

Bwana wa nyumba

 

 

 

Watumwa kumi

(Luka 19:11-27)

 

 

Mfano wa Mpanzi (Mathayo 13:3-9, 18-23; Luka 8:5-18)

Mfano wa kwanza katika mfululizo huu wa mifano kuhusiana na ufalme unafundisha kwamba kinachotegemewa kwetu katika mbegu kinapimwa kutokana na kuzaa kwa matunda yake. Kwenye ufalme wa mbinguni, baadhi ya watu wataamini na kuzaa matunda hali wengine watakataa kuamini au watakengeuka baada ya kuwa wamekuwa tegemeo la kwanza.

Mfano huu unaweza kuitwa kuitwa mfano wa udongo kwa sababu ni hadithi kuhusiana na aina mbali mbali za udongo, na siyo wapandaji tofauti. Katika kila mfano, mbegu ni ile ile moja, na mpandaji alikuwa ni yule Yule; tofauti ni udongo tofauti. Tunapokuwa tunatangaza ujumbe wa ufalme, hatupaswi kushtuka wakati tunapoona watu wengine wanakuwa wagumu kupokea kuliko wengine. Hatupaswi kukataa tama. Yesu alifundisha kwamba baadhi ya wasikilizaji watakuwa udongo mzuri unaozaa matunda wakati watu wengine watakuwa wagumu dhidi ya Neno.

Uamuzi wa mwisho wa Luka kuhusiana na mfano huu wa mpanzi unaonyesha kwamba huu ni mfano kuhusiana na kusikiliza ukweli. “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho” (Luka 8:18). Wakati mtu anapokuwa na mwitikio chanya wa ukweli, anapokea ukweli wa ziada. Kabla ya kutoa mifano mingine katika hotuba yake, Yesu alifundisha wasikilizaji wake jinsi ya kusikiliza kama udongo wenye kuzaa matunda.

Mfano wa Magugu (Mathayo 13:24-30, 36-43)

Wayahudi walitegemea ufalme wa Mungu ulete hukumu ya haraka dhidi ya wenye dhambi. Yesu aliwaandaa wanafunzi wake kwa ajili ya kipindi cha mpito ambacho kwa pamoja watu walioamini na ambao hawajaamini wataishi kwa pamoja katika dunia. Katika hadithi hii, “lile konde ni ulimwengu” (Mathayo 13:38). Ni katika “mwisho wa dunia tu” malaika watayakusanya magugu na kuyachoma motoni. Ufalme wa Mungu utakuwa katika wakati wa Bwana na siyo katika wakati wa mwanadamu.

Mfano wa Mbegu ya Haradali (Mathayo 13:31-32)

Hakuna hata mtu mmoja aliyeangalia huduma ya Yesu hapa duniani angeweza kubaini usambaaji wa kanisa katika ulimwengu wote. Wanafunzi hawakuwa na elimu, walikuwa masikini,na wenye hofu. Walikosa haiba kubwa, hadhi katika jamii na nguvu ya kisiasa. Walikuwa kama “punje ndogo ya haradali.” Lakini kama vile punje ndogo ya haradali inavyokua na kuwa mti mkubwa au msitu, ufalme wa Mungu ndivyo hivyo utakavyoifikia dunia yote.

Wasikilizaji wa Yesu wangeshituka kumsikia Yesu akilinganisha ufalme wa Mungu na punje ndogo ya haradali. Rabi wa Kiyahudi walitegemea ufalme wa Mungu uje kwa nguvu na utukufu. Walitegemea zitolewe hukumu dhidi ya watenda dhambi; walitegemeamapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wa Rumi; walitegemea mapinduzi ya hali ya kijamii wakati ufalme mpya wa Kiyahudi utakapokuwa umeanzishwa. Badala yake, Yesu aliwaandaa wanafunzi wake kwa mwanzo usiovutia wa ufalme.

Tunaposoma katika Agano Jipya, tunaweza tukasahau umuhimu wa nchi ya Yudea katika karne ya kwanza. Yudea ndio kitovu cha Agano Jipya, lakini ilikuwa mbali sana na katikati ya karne ya kwanza ya dunia. Fikiria kuhusu mji mkuu wa nchi yako. Hili halikuwa jukumu la Yudea katika karne ya kwanza; jukumu hilo lilikuwa la Rumi. Fikiria kuhusu jiji lililo na vyuo vikuu vingi na mfumo mzuri wa elimu. Hili halikuwa jukumu la Yudea katika karne ya kwanza; jukumu hilo lilikuwa la Athene au Alexandria.

Yudea haikuwa muhimu kisiasa; haikuwa muhimu kuichumi; haikuwa muhimu kijamii. Fikiria kuhusu miji isiyokuwa na muhimu wowote katika nchi yako; hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya Yudea wakati wa utawala wa Dola ya Kirumi

Mfano wa punje ya haradali unaonyesha kukua kwa ufalme wa Mungu kutokea kikundi kidogo cha watu kutokea nyuma pembezoni mwa Dola ya Kirumi kuwa mti mkubwa uliofikia mataifa yote.[1] Rabi wa Kiyahudi walifundisha kwamba ufalme wa Mungu utakuwa ni kwa wana wa Israeli tu; Yesu anafundisha kwamba ufalme wa Mungu utafika hadi miisho ya nchi.

Mfano wa Chachu (Mathayo 13:31-32)

Mfano wa chachu unaonyesha pia ukuaji wa muujiza wa ufalme Ingawaje chachu kwa kawaida imekuwa na mtazamo hasi katika Maandiko,  (Mathayo 16:6; 1 Wakorintho 5:6-7). Yesu alitumia chachu kama alama ya kusambaa kwa ufalme. Vipimo vitatu vya shayiri vinatosha kutengeneza mikate ya kutumiwa na watu mia moja. Pamoja na mwanzo wake kutokuwa muhimu, ufalme utakua kwenye kiwango cha nguvu kubwa sana.

Mfano wa chachu unaonyesha kukua kwa kasi kwa ufalme. Chachu siyo kitu cha kuvutia; hailipuki kama baruti kali; inafanya kazi polepole kwenye mkate. Rabi wa Kiyahudi walifundisha kwamba ufalme wa Mungu utatambulishwa kwa ishara mbalimbali duniani; Yesu alionyesha kwamba ufalme utakua polepole, lakini ukiongezeka kwa kasi hadi utakapoifikia dunia nzima.

Mifano ya Hazina Iliyofichwa na Lulu ya Thamani Kubwa (Mathayo 13:44-46)

Mifano hii miwili ni juu ya furaha ya ufalme. Kwa pamoja, mtu alipata kitu cha thamani kubwa kiasi kwamba ilbmbdi “auze vyote alivyokuwa navyo ili akinunue.” Mtizamo wa hii mifano siyo ntu kujitoa mhanga, bali ni furaha yake kwa kupata kitu cha thamani sana, “kwa furaha yake huenda akauza vitu vyote.” Wanafunzi walifurahia kuachana na kila kitu ili wamfuate Kristo.

Mifano hii inaonyesha thamani ya juu sana ya ufalme. Ufalme waMungu unagusa tabia zetu zinazohusiana na maisha yetu yote. Kwenye maeneo mengine, Yesu anasema kwamba “Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum” (Marko 9:47). Kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ni kwa thamani kubwa kuliko dhabihu yeyote ya ulimwengu huu.

Mfano wa wavu (juya) (Mathayo 13:47-50)

Boti za kuvua katika Ziwa la Galilaya hushusha nyavu kwenye Ziwa nyavu (juya) kubwa, wakikamata samaki wanaolika na visivyolika. Baada ya kurejea ufukweni, wavuvi watatenganisha samaki wazuri kutoka katika vitu vibaya vilivyovuliwa.

Kama ilivyo kwa mfano wa mpanzi, mfano huu uliwakumbusha wanafunzi kuhusu hukumu itakayokuja “wakati wa mwisho wa dunia.” Badala ya kutegemea hukumu ya haraka, ni lazima wahubiri habari za ufalme wakijua kwamba mungu, kwa wakati wake mwenyewe, atahukumu wenye dhambi na wenye haki.Kutakuwa na hukumu ya mwisho ambayo itatenganisha mema kutokana na maovu, lakini tunapaswa tuuache wakati huo kwa Mungu mwenyewe.

Mfano wa Bwana wa Nyumba (Mathayo 13:51-52)

Yesu alianza mfululizo wa mifano hii kwa kuwafundisha wanafunzi wake kwamba ni lazima wawe udongo mzuri unaozaa matunda. Alimalizia mifano yake kwa kuwafundisha kuwashirikisha na wengine. “Kila mwanafunzi aliyefundishwa” ni lazima atoe katika hazina yake chochote alicho nacho ili kufundisha wengine. Hatujifunzi kwa ajili ya faida yetu sisi peke yake. Wanafunzi walifundishwa ili waweze kuwafundisha na wanafunzi wengine.

Mfano wa watumwa Kumi (Luka 19:11-27)

Soma Luka 19:11-27.

Mfano huu unatoka kwa Luka, lakini Mathayo 24 anajumuisha mfano unaofanana uliopatikana kutokana na mhadhara wao na Yesu. Yesu aliutoa mfano huu wa watu kumi waliotoka miongoni mwa watumwa alipokuwa karibu na Yerusalemu, “kwa sababu walikuwa wakidhania kwamba ufalme wa Mungu ungekuja kwa haraka.”

Yesu alipokuwa akikaribia Yerusalemu, watu waliongeza hamu yao kubwa katika matazamio yao ya Masihi wa kisiasa. Yesu alitoa mfano huu ili kuwafundisha wanafunzi wake waendelee kuwa waaminifu wakati wakiwa wanaungojea ufalme. Hawakutakiwa kuficha kwa tahadhari yale ambayo Bwana wao aliwapa; badala yake walitakiwa watumie rasilimali zao zote walizokuwa nazo kwa ajili ya maendeleo ya ufalme.


[1] Katika Danieli 4:12 na Ezekieli 31:6, ndege waliojenga viota kwenye mti kunawakilisha ufalme mkuu ukiyafikia mataifa mengi.

Kilele cha Ufalme

Soma Mathayo 24-25.

Mengi ya mafundisho ya mwanzo ya Yesu yalielekezwa kwenye kuzinduliwa kwa ufalme. Alipokuwa anakaribia mwisho wa huduma yake hapa duniani, Yesu alizungumzia zaidi kuhusu wakati wa mwisho wa kilele cha ufalme. Mhadhara ulioko katika Mathayo 24 na 25 ni mwendelezo muhimu sana wa mafundisho ya Yesu kuhusiana na ahadi za ukamilishwaji wa mwisho wa ufalme.

coming

coming

coming

coming

coming

coming

coming

coming