Kama tunataka tuhudumu kama Yesu, ni lazima tuwe waombaji kama Yesu.
Utangulizi
Kwenye jujmbe wa mahubiri kuhusiana na maombi, Profesa Howard Hendriki alitoa taarifa hii ya kusadikisha kama ifutavyo:
Shetani hajali kama unasoma Bibilia, ila tu usiombe kwa sababu Andiko haliwezi kubadilisha maisha yako. Linaweza hata likakupa tatizo kubwa la kiburi cha uzima kwa sababu unalijua sana.
Shetani hana cha kujali kama unaishirikisha imani yako kwa wengine, ila tu usiombe kwa sababu anajua kwamba ni jambo muhimu zaidi kuongea na Mungu kuhusu wanadamu kuliko itakavyokuwa kuongea na watu kuhusu Mungu.
Shetani hana cha kujali kama unajihusisha na huduma ya kanisa la mahali, ila tu usiombe kwa sababu utakuwa mshughulikaji sana lakini kwa uhakika hutafanikisha matarajio mengi.[1]
[2]Maombi yalikuwa ndio kiini cha huduma ya Yesu hapa duniani. Hakuna kilichochukua umuhimu zaidi kuliko maombi. Huduma ya Yesu ilizungukwa zaidi na uhusiano wake na Baba wa Mbinguni. Uhusiano huo uliimarishwa kupitia maombi na ushirika wake wa karibu na Mungu.
► Kabla ya kujifunza somo hili, fanya tathmini ya dhima ya maombi katika maisha na huduma yako. Jiulize:
Je! maombi yangu ni endelevu?
Ni lini mara ya mwisho nilipata jibu halisia la maombi?
Kuna changamoto gani kubwa katika maisha yangu ya maombi?
Je! ninaendelea kukua katika maisha yangu ya maombi?
[1]Nukuu kutoka kwa Howard G. Hendricks, “Prayer – the Christian’s Secret Weapon.” Reprinted in Veritas, January 2004
"Maombi ni ukumbi wa michezo ya mazoezi ya roho."
- Samuel Zwemer,
“Mtume kwa Uislamu”
Mfano wa Yesu wa Maombi
Katika kipindi chote cha huduma ya Yesu, tunamwoana akiwa amejikita katika nyakati ngumu za maombi. Vitabu vya Injili vinatoa taarifa za matukio maalumu kumi na tano ambayo Yesu aliomba. Maombi kamwe hayakuwa nafasi ya pili kwake; maombi yalikuwa kiini cha maisha yake.
Luka anaonyesha kwa ufasaha huduma ya Yesu ya maombi kuliko mwandishi mwingine yeyote. Ni Luka peke yake anayetuambia kwamba Yesu aliomba usiku kucha kabla ya kuchagua wanafunzi wake kumi na mbili (Luka 6:12). Ni Luka peke yake anayetueleza jinsi Yesu alivyobadilika mwili wake alipowachukua Petro, Yakobo na Yohana kwenda nao mlimani kwa ajili ya maombi (Luka 9:28). Msisitizo huu unaendelea katika Kitabu cha Matendo kwa Luka kuandika mara thelathini na tano kuhusu majukumu ya maombi katika kanisa la mwanzo.
Maombi katika Maisha ya kila siku ya Yesu
► Soma Marko 1:32-39.
Taarifa hii kutokea mwanzoni mwa huduma ya Yesu inaonyesha jinsi maombi na huduma vinavyohusiana. Chukulia maanani mwendelezo wa masimulizi haya. Jioni iliyopita, watu walikusanyika nje ya nyumba ya Yesu aliyokuwa akiishi, na aliwaponya wengi wao.
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake “mahali pasipokuwa na watu” akaomba huko. Simoni Petro alikuja kumtafuta kwa sababu “Watu wote wanakutafuta.” Yesu akawaambia, “Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea.” Mfumo wa huduma ya Yesu ulikuwa ni maombi yakifuatiwa na kazi ya utumishi.
Hii inatakiwa iwe ndio mfumo wa huduma. Bila ya maombi, huduma yetu inakuwa imechoka kiroho. Bila ya utumishi, maombi yetu yanakuwa niya binafsi ; hatufanyi juhudi ya kuhudumia mahitaji ya wale wote wanaotuzunguka. Yesu ananonyesha kwamba maombi na utumishi ni lazima viunganishwe pamoja.
Maombi katika nyakati za kufanya Maamuzi
► Soma Luka 6:12-16.
Moja ya maamuzi muhimu sana wakati wa huduma ya Yesu ilikuwa wakati wa kuchagua mitume kumi na wawili. Kutoka katika maelfu ya wasikilizaji wa mahubiri yake, wengine walikuwa karibu sana naye hata kuweza kuitwa “mitume” (Yohana 6:60, 66). Wafuasi wake sabini na mbili walikuwa karibu naye sana kiasi cha kuweza kumwakilisha Yesu katika safari yake ya kwenda kuhubiri (Luka 10:1). Lakini Yesu alichagua hapo kumi na mbili tu kuwa “mitume.”
Hawa mitume kumi na mbili walichukuwa muda mrefu kukaa na Yesu. Walikuwa pamoja na Yesu mwishoni mwa huduma yake ya hapa duniani. Baada ya kupaa kwake, mitume kumi na moja walikuja kuwa viongozi katika kanisa la mwanzo. Uchaguzi wa mitume kumi na wawili ulikuwa ni uamuzi uliokuwa mkubwa sana. Yesu hakuwahi kuandika kitabu chochote au kuanzisha mashule. Urithi wake aliwaachia watu hawa.
Yesu alifanya nini kabla ya kuchagua hawa kumi na mbili? Aliomba. Akiwa anakabiliwa na uamuzi mgumu, Yesu alitumia usiku mzima akiwa anaomba. Kama Mwana wa Mungu aliomba kwa kumaanisha kiasi hicho kabla ya kufanya maamuzi magumu, ni kwa jinsi gani maombi yanaweza kutufanyia mambo makubwa katika kufanya maamuzi yetu!
Maombi unapokabiliana na Mateso
► Soma Mathayo 26:36-46.
Masaa machache kabla ya kukamatwa kwake, Yesu alikwenda Getsemane kuomba. Alijiandaa kukabiliana na mateso kwa kuomba. Yesu kamwe hajautumia uungu wake kukwepa mateso ya ubinadamu wake. Badala yake aliyategemea maombi kwa ajili ya kutiwa nguvu za kupambana na mateso.
Maombi ya Yesu kule bustanini ni mfano wetu wa kuigwa leo. Maombi yake hayakuwa ya kinafiki; Yesu alikuwa anakabiliwa na mateso ya kweli. Je, hii inakutia moyo kutambua kwamba Yesu alikumbana na njia zote za maumivu anazopitia mwanadamu? Ili kukabiliana na mateso, Yesu aliomba angalao apatiwe unafuu:
Kule bustanini hajaomba kwamba, “Ee Mungu, ninakushukuru kwamba umenichagua mimi kupata mateso kwa niaba yako.” Hapana. Alijisikia kuelemewa na masikitiko, hofu, kuachwa, na kitu kinachomjia cha kumtaka akate tamaa. Lakini bado, aliendelea kwa sababu alijua kwamba katikati ya dunia Baba yake yupo, Mungu wa upendo ambaye anaweza kumtegemea yeye bila kujali mambo yatakavyojitokeza.[1]
Mbele ya mateso, hatupaswi kujifanya kwamba tunazo nguvu kuliko tulivyo. Kama Ayubu, tunaweza kulia tunapokabiliana na maumivu. Katika hali yake ya kibinadamu, Yesu alifanya vivyo hivyo! Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Yesu, tunaendelea kubakia kuwa waaminifu kwa sababu tunajua kwamba Baba yetu wa upendo aliye mbinguni bado ameshikilia mamlaka yote.
Ni katika maombi tu tunaweza kuyakubalimapenzi ya Mungu. Msingi mkubwa wa maombi ya Yesu katika kukabiliana namateso, na msingi mkubwa wa maombi yetu katika mateso ni kujisalimisha kwenye mapenzi ya Baba: “Hata hivyo, siyo kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.”
[1]Philip Yancey, The Jesus I Never Knew. (Grand Rapids: Zondervan, 1995), 161
Mafundisho ya Yesu kuhusiana na Maombi
Yesu hakuonyesha tu umuhimu wa maombi kwakupitia mfano wake, bali alitumia muda mwingi katika kufundisha kuhusu maombi. Yesu alijua kwamba maisha ya kiroho ya wafuasi wake yangetegema sana maisha ya maombi. Kwa sababu ya hiyo, aliwafundisha wanafunzi wake kuomba
Mafundisho ya Yesu katika Hotuba ya Mlimani
► Soma Mathayo 6:1-18.
Katika hotuba ya mlimani, Yesu alifundisha maeneo matatu yanayohusiana na utendaji wa kiroho: kutoa kwa ajili ya maskini, kuomba na kufunga kwa maombi. Ni wazi kutokana na mafundisho yake kwamba Yesu alitegemea haya yawe ni harakati za kawaida kwa wafuasi wake. Yesu hakusema, “kama mtatoa kwa ajili ya maskini,…” au “kama mtaomba…” au “kama mtafunga kwa maombi…” alikuwa anawategemea wafuasi wake wawe watoaji kwa hiari, waombaji na wanafunzi wenye nidhamu binafsi.
Yesu alionyesha kwamba shughuli zote hizi nzuri zinaweza zisiwe na maana yeyote kama zitatokana na malengo mabovu. Katika ulimwengu wa zamani, “mnafiki” au “hypocrite” ni jina la muigizaji aliyekuwa akivaa vinyago mbalimbali ili aweze kucheza kwenye nafasi mbalimbali. Inawezekana kabisa “kucheza kwenye nafasi ya kidini” mbele ya watu wengine.
Inawezekana kutoa kwa ajili ya maskini ili kuwavutia wengine na ukarimu wetu. Yesu alisema, “Wameipokea thawabu yao.”
Inawezekana kuomba ili kuwavutia wanaotuangalia kwa maneno yetu ya kupendeza. Yesu alisema, “Wameipokea thawabu yao.”
Inawezekana kufunga kwa maombi ili kuwavutia wengine kwa uchamungu wetu na nidhamu binafsi. Yesu alisema, “Wameipokea thawabu yao.”
Katika kila kipengele, mtu aliyetoa kwa ajili ya maskini, aliyeomba au kufunga kwa maombi amefanya hivyo kwa ajili ya watu wengine. Watu walivutiwa; hiyo ndiyo thawabu yake. Kwa hiyo, hatapokea thawabu kutoka kwa Mungu.
Makusudio katika harakati hizi za kiroho ni lazima ziwe zenye kumpendezesha Baba yetu wa mbinguni. Aidha iwe ni kutoa kwa ajili ya maskini, kuomba au kfunga kwa maombi, thawabu yetu ni Mungu mwenyewe. Hatupaswi kuzifanya harakati hizi za kiroho kwa ajili ya kuufurahisha ulimwengu. Badala yake, ni lazima tuyafanye haya kutoka katika kina chetu cha ndani cha matamanio na maombi yetu kwa Mungu.
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake jinsi ya kuomba kwa njia rahisi na iliyo wazi:
Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele (Mathayo 6:9-13).
Haya siyo maombi ya kufanywa kiholela tu bila kufikiria kama zile “aya tupu” Yesu alizoshutumu katika Mathayo 6:7-8. Badala yake, maombi haya hutengeneneza maadili ya tabia ambazo zinapaswa ziongoze maombi yetu:
Mahusiano
“Baba yetu uliye mbinguni” inaonyesha uhusiano wetu wa karibu uliopo na Mungu. Kuliko kuonekana ni Mungu aliye mbali, tunamtambua kama Baba anayetupenda na anayetupa mema kama watoto wake (Mathayo 7:11). Kifungu hiki kwa pamoja kinaonyesha ukaribu (“Baba Yetu”) na mamlaka (“uliye mbinguni.”) Mungu ni adhimu na aliye binafsi.
Heshima
“Jina lako litukuzwe” linaonyesha tofauti iliyopo kati yetu sis na Baba yetu “aliye mbinguni.” Ingawaje Mungu ni wa upendo, yeye ni mtakatifu.[1] Kama mwenye hekima katika kitabu cha Wimbo ulio bora alivyojifunza, ni lazima uende mbele za Mungu kwa heshima na hofu (Wimbo Ulio Bora 5:2).
Kujisalimisha
“Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni,” kunawakilisha kujisalimisha kwetu kwa hiari kwenye mamlaka yake. Kama vile mapenzi ya Mungu yanavyotimizwa kwa ukamilifu huko mbinguni, tunapaswa na sisi tuombe yatimizwe kwa ukamilifu hapa duniani.
Utoaji
“Utupe leo riziki yetu” kulikuwa na umuhimu maalumu katika dunia kabla ya kuwepo kwa majokofu au umeme. Chakula kilitolewa mara moja kwa siku. Kifungu hiki kinaonyesha uaminifu wetu kwa Baba wa kila siku. Kama watoto wake, tunamwamini kwa utoaji wa mahitaji yetu.
Kukiri
“Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Katika Luka 11:2-4, ombi hili hili limetamkwa, “Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye.” Kwa kuwa dhambi yetu ni “deni” tunalowiwa kwa Mungu, maana zote ni sawa katika Mathayo na Luka (Wakolosai 2:14).
Kwa kuunganisha msamaha wetu kwa watu wengine na ule wa Mungu kwetu, Yesu hajatufundisha kwamba “tufaidi” msamaha. Badala yake, sisi ambao tumesamehewa kwa mapenzi ya hiari, tuwasamehe wale wote wanaotukosea. Mfano wa Yesu wa yule mtumishi aliyekataa kusamehe unaonyesha uhusiano uliopo kati ya msamaha wetu sisi na hiari yetu ya kusamehe watu wengine (Mathayo 18:21-35).
Ushindi
“Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu” ni maombi ya ushindi dhidi, ya majaribu na mitihani ya maisha. Mungu kamwe hawajaribu watoto wake, (Yakobo 1:13) lakini kila mmoja wetu atakabiliwa na nyakati za majaribu na mitihani ya maisha (1 Petro 1:6-7). Katika nyakati hizo, Mungu hawezi kuruhusu sisi tujaribiwe kupita vile tuwezavyo kustahimili (1 Wakorintho 10:13).
Mafundisho ya Yesu kuhusiana na Kuomba kwa Bidii
► Soma Luka 11:1-13.
Luka anaifuatilia Sala ya Bwana kama mfano unaotufundisha sisi jinsi ya kuomba kwa bidii kwa Baba ambaye anapenda kuwapa watoto wake thawabu nyingi. Katika Mashariki ya Mbali, ilikuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kukopa kutoka kwa jirani kwa ajili ya kumhudumia mgeni. Kama mtu mhitaji ataomba kwa bidii, jirani yake atampa chochote kilichokuwa kinahitajika. Kwa mila hii, ilikuwa inachukuliwa kama ni ukatili kusema “Hapana” kwa ombi lililotolewa. Hata kama huyo jirani hakutaka aisumbue familia, hataweza kukataa wito wa kusaidia.
Katika hatua nyingine ya juu zaidi, Mungu anapenda kuwapa thawabu njema watoto wake wanaoomba kwa bidii. Kama vile iliyokuwa kwa huyu mtu katika huu mfano alivyoomba kwa bidii, tunaweza kumwendea Baba yetu wa mbinguni kwa ujasiri. Kwa nini? Siyo kwa sababu Mungu ataona aibu kuyakataa maombi yetu, bali ni kwa sababu tumepewa kibali cha “kuomba, kutafuta na kubisha hodi.”
[1]Neno “kufanywa wakfu” linamaanisha “takatifu” au “kilichotengwa”
Angalia kwa kuzingatia: Mitindo ya Kufundisha ya Kiebrania
Katika Luka 11:1-13, Yesu anaelezea habari ya mtu mmoja ambaye hataki kuamka kitandani ili amsaidie jirani yake aliyekuwa anahitaji kukopa kwa ajili ya mgeni wake.
Ili kuelewa fumbo hili, ni lazima uelewe mtindo wa kufundisha wa Kiebrania – hoja ya “ndogo kuwa kubwa.” Aina hii ya ufundishaji inasema kwamba, “Kama A (ndogo) ni kweli, basi ni kiasi gani cha B (kubwa) lazima kitakuwa kweli.” Kwa wakati wa leo, tunaweza kusema. “Kama mtu atamlisha chakula mgeni mwenye njaa (A), ni kwa jinsi gani zaidi Mungu wa upendo anaweza kuwalisha watoto wake (B).”
Unaposoma mfano huu, usifikiri kwamba, “Mungu ni kama jirani mkaidi. Ni lazima nimshawishi yeye aweze kujibu maombi yangu.” Badala yake, Yesu anamlinganisha rafiki mkaidi na Baba wa mbinguni aliye tayari. Kama jirani wa duniani anaweza kushughulika na ombi lililoombwa kwa bidii, ni kwa jinsi gani zaidi Baba wa mbinguni anaweza kushughulika kwa ajili ya watoto wake!
Mafundisho ya Yesu kuhusiana na Maombi (Inaendelea)
Mafundisho ya Yesu kuhusiana na Kuomba kwa Bidii (Inaendelea)
Maombi ni mahusiano
Mungu anataka ajibu maombi ya watoto wake, ni kwa nini mara nyingine majibu yake huchelewa? “Kuomba, kutafuta na kubisha hodi” ni maagizo ya wakati uliopo.Hii inamaanisha kwamba tunapaswa tuendelee “kuomba, kutafuta na kubisha hodi.” Kwa nini?
[1]Sababu mojawapo ni kwamba maombi ni zaidi ya kutoa orodha ya msururu wa mahitaji. Maombi ni uhusiano endelevu kati yetu na Baba wa Mbinguni. Kama vile Paulo alivyotuamuru “tuombe bila kukoma,” (1 Wathesalonike 5:17). Yesu naye anatuamuru sisi tuendelee kuomba, kutafuta na kubisha hodi. Kutokana na mazungumzo endelevu na Mungu, mahusiano yetu na Mungu yanzidi kukua zaidi. Maombi ni zaidi ya orodha ya msururu wa mahitaji; maombi ni mahusiano.
Mfano wa Maombi ya Kung’ang’ania
Katika Luka 17, Mafarisayo walimuuliza Yesu ufalme wa Mungu utakuja lini. Aliwajibu akawaambia kwamba wasitegemee kuuona kwa kchunguza alama. Badala yake, “ufalme wa Mungu umo ndani yenu” (Luka 17:20-21). Ufalme wa Mungu tayari ulikuwa ndani ya wale ambao walikuwa wamemfuata Yesu.
Kisha Yesu aliwageukia wanafunzi wake na kuanza kuwafundisha kuhusu ufalme wa Mungu. Walimtegemea Yesu aanzishe kwa haraka ufalme wa kisiasa, lakini Yesu aliwaandaa kusubiri hata baada ya kifo chake. Wakati wa kungojea, walipaswa kuendelea na maombi siku zote na “siyo kukata tamaa.” Kisha Yesu akawaelezea habari iliyohusiana na maombi ya uaminifu
► Soma Luka 18:1-8.
Katika miji mingi ya zamani, makadhi walikuwa wadhalimu. Hakuna aliyeweza kusikiliza shauri bila ya kupokea rushwa. Huyu mjane hakuwa na fedha za kumpa rushwa huyu kadhi, kwa hiyo alikataa kusikiliza shauri lake. Hata hivyo, dada huyu mng’ang’aniaji hakutaka kabisa kukataa tama. Mwishowe, yule kadhi dhalimu akasema, “kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake.”
Mfano huu unatumia mtindo wa “ndogo kuwa kubwa” kama mfano ule wa jirani aliyeomba kwa bidii. Unapousoma mfano huu, elewa kwamba:
[2]Mungu siyo mwamuzi asiyetenda haki. Mungu wetu anapenda “kutoa haki kwa kila mteule wake.”
Sisi siyo wajane. Yeye alikuwa mgeni, sisi ni watoto wa Mungu.
Hakuweza kupata kibali kwa yule kadhi; kupitia kwa Yesu, tunacho kibali kwa Mungu.
Huu ni mfano wa ulinganifu. Kama kadhi madhalimu ataweza kumskiliza mjane aliyeng’ang’ania, ni kwa jinsi gani zaidi Baba yetu wa mbinguni anaweza kujibu maombi ya watoto wake?
Mfano kuhusu Maombi ya Unyenyekevu
► Soma Luka 18:9-14.
Mfano mwingine wa Yesu kuhusu maombi ulitolewa kwa “watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.” Mfano huu unafundisha tabia halisi katika maombi.
Msingi mkubwa wa mfano huu uko pale mwishoni: “kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” Mafarisayo walidhania maombi yanajibiwa kwa sababu ya kuwa na haki yao wenyewe. Yesu anaonyesha kwamba maombi yanajibiwa kwa sababu ya neema ya Mungu kwa wale ambao hawana haki yao wenyewe. Hakuna hata mtu mmoja anayestahili maombi yake yajibiwe; Mungu hujibu maombi kwa sababu ya neema yake tu kwa wale wasiostahili lolote.
"Maombi siyo kushinda Mungu kuchelewa kujibu. Maombi ni kuweza kijishikilia kwenye mapenzi ya Mungu.”
- Martini Luther
Matumizi: Maombi katika Maisha ya Mkristo
Watu wanaomfanania Kristo ni watu wa maombi. J.C. Ryle, Askofu wa Liverpool wa karne ya kumi na tisa, alijifunza maisha ya Wakristo maarufu katika historia. Alisema kwamba baadhi yao walikuwa matajiri, wengine walikuwa maskini, waengine walikuwa wasomi; wengine hawakusoma kabisa. Wengine walikuwa Wakalvini; wengine walikuwa Waarminia. Baadhi yao walitumia liturugia, wengine walikuwa huru. “Lakini walikuwa na jambo moja la pamoja. Wote walikuwa watu wa maombi.”[1]
Wakati wote wa historia ya Kanisa, watu waliomfananaia Kristo wamekuwa ni watu wa maombi. E.M.Bounds, Kiongozi mashuhuri wa Kikristo, aliomba kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa moja asubuhi. Aliandika kitabu kilichopewa jina “Roho Mtakatifu hashuki kupitia taratibu zilizowekwa bali kupitia wanadamu. Hashuki kwa mashine bali kwa wanadamu. Haachilii upako wake kwenye mipango bali kwa wanadamu – tena wanadamu wa Maombi”[2]i
George Müller alisimamia vituo vingi vya yatima vya maelfu ya watoto. Aliamua kwamba kamwe hataomba msaada kutoka kwa mwanadamu mwingine lakini atategemea maombi peke yake. Alipokea zaidi ya dola 7,000,000 za Kimarekani kupitia maombi peke yake. Siyo tu kwamba aliweza kutoa msaada kwa vituo vyake vya yatima wake, bali Müller alitoa maelfu ya dola kwa ajili ya huduma nyingine. George Müller aliijua nguvu iliyoko katika maombi.
Kwa nini tunaomba?
[3]Tunaomba kwa sababu sisi ni tegemezi kwa Mungu.
Katika ubinadamu wake, Yesu alitegemea maombi kama kiunganishi cha mawasiliano kati yake na Baba yake. Maombi ni kitendo cha kuwa tegemezi kwa Mungu. Inaonyesha kwamba hatujitegemezi wenyewe kwa maombi bali kwa Mungu.
► Soma Mathayo 26:31-46.
Kuanguka kwa Simoni Petro kunaonyesha umuhimu wa maombi. Yesu aliwaonya wanafunzi wake kwamba, “Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu.” Kwa uwazi zaidi, Yesu alimwonya Simoni Petro, “Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi” (Luka 22:31). Petro alianguka kwa sababu ya madhaifu mawili:
1. Petro alijiamini kupita kiasi. Alisisitiza, “Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe,… Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe!” (Mathayo 26:33, 35). Kiburi kilimpa Petro kujiamini sana kwa kutegememea nguvu zake mwenywe.
2. Petro alishindwa kuomba. Kwa sababu alijiamini sana katika nguvu zake mwenyewe, Petro hakumtegemea Mungu. Adala ya kuungana na Yesu katika maombi, Petro alilala. Tunaomba kwa juhudi tunapotambua utegemezi wetu kamili kwa Mungu. Dick Eastman aliandika, “Ni katika maombi tu tunasalimisha matatizo yetu kabisa kwa Mungu”[4]
Tunaomba ili kumjua Mungu kwa ukamilifu Zaidi.
Mojawapo ya madhaifu makubwa ya kanisa la leo ni upeo wetu mdogo wa kuwa na ufahamu kuhusu Mungu. Mara nyingi, haja za maombi yetu zimehusika tu na mahitaji ya vitu na utoshelevu wa mambo binafsi. Tulio wengi tunatumia muda wetu mwingi tukiomba, “Mungu, nakuomba uwasaidie watoto wangu waweze kupata kazi” kuliko kuomba, “Mungu, saidia kuwatengeneza watoto wangu wawe katika mfano wako.” Tunaomba kwa juhudi sana kwa ajili ya kupata uponyaji wa mwili kuliko uponyaji wa kiroho. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tulivyo na ufahamu mdogo kuhusiana na maana halisi ya maombi.
[5]Mojawapo ya makusudi ya msingi ya maombi ni kumjua Mungu kwa ukamilifu zaidi. Katika maombi, tunapatanishwa na moyo wa Mungu. Maombi siyokumtaka Mungu afanye kama tunavyotaka sisi afanye. Maombi hutupa ufahamu mpana wa moyo wa Mungu hadi tutakavyopata kama vile atakavyo yeye.
Tunapofikia katika hatua hii, Yesu alisema, “Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” (Marko 11:24). Kwa kuwa mioyo yetu iko kwenye uelewano na moyo wa Mungu hatutaomba kutoka katika malengo yasiyofaa, au katika mambo yanayopingana na mapenzi ya Mungu (Yakobo 4:3 and 1 Yohana 5:14). Ufahamu huu wa moyo wa Mungu unakuja kupitia maombi thabiti.
Watu wa Tohara husema kwamba ni lazima “kuomba hadi tuwe tumeomba.” Kwa maneno mengine, tunapaswa kuomba kwa muda mrefu na kwa uvumilivu mkubwa ili kupita kutoka maneno matupu hadi kuingia kwenye uwepo wa Mungu. Ni lazima tuombe hadi tufurahishwe katika Bwana.
► Elezea kuhusu wakati ambao maombi yaliweza kukupa wewe ufahamu wa ndani kuhusiana na Mungu pamoja na mapenzi yake.
Tuombe kwa namna gani?
Kwa kujifunza mfano wa Yesu kuhusiana na maombi, tunajifunza masomo muhimu kuhusiana na maombi yenye ufanisi.
Tunaomba kwa uvumilivu.
[6]Yesu alikuwa Mwana wa Mungu.Mtu anaweza kutarajia maisha yake ya maombi kuwa ni jambo rahisi la kusema, “Baba, unataka mimi nifanye nini? Na kutarajia kupata jibu la haraka! Badala yake, tunamwona Yesu akiwa katika maombi ya usiku kucha kabla ya kuchagua wanafunzi wake Kumi na mbili. Tunamwona aking’ang’ana na maombi katika bustani ya Getsemani. Maombi, hata kwa upande wake Yesu, yalihitaji uvumilivu na muda. Maombi ni kumngojea Mungu.
Akiandika kuhusu umuhimu wa kungojea katika maombi, Glenn Patterson alisema, “Kitu Mungu anachofanya ndani yetu wakati tukiwa tunangojea ni muhimu kama kile tunachongojea. Kungoja ni sehemu ya mchakato wa Mungu wa kutufanya tuwe kama atakavyo yeye.” Kwa jinsi tunavyoendelea kumsubiri Mungu, tunazidi kujifunza kumjua vyema zaidi.
Zaburi ya 37:1-9 inafundisha masomo muhimu kuhusiana na maombi. Angalia maamrisho haya:
Usikasirike.
Umtumaini Bwana.
Ujifurahishe kwa Bwana.
Umkabidhi Bwana njia yako.
Umtumaini yeye.
Ukae kimya mbele za Bwana.
Umngojee kwa saburi.
Ukomeshe hasira.
Usikasirike. (kwa mara nyingine tena!)
Maamrisho haya yanalenga katika uaminifu wenye uvumilivu kwa Mungu anayekujali wewe na ambaye “atakupa haja za moyo wako.” Kupitia maombi yenye saburi, tunakuwa watu tunaoaminika ambao ndiyo Mungu anatutaka sisi tuwe.
Mfano wa kuigwa wa Maombi Endelevu
Mapema kabisa kwenye masisha yake ya Ukristo, George Müller alianza kuomba kwa ajili ya kuongoka kwa mafiki zake watano. Baada ya miezi mingi, mmojawapo miongoni mwa wale rafiki zake akakubali kumpa Bwana maisha yake. Miaka mingine kumi baadaye watu wengine wawili waliongoka. Ilichukua takribani miaka mingine ishirini na tano kabla yule rafiki yake wa nne hajampa Yesu maisha yake.
Müller aliendelea katika maombi hadi alipofariki kwa ajili ya rafiki yake wa tano.Kwa miaka hamsini na mbili, hakukata tamaa kumwombea huyu rafiki yake ili aweze kumkubali Kristo! Siku chache baadaye baada ya mazishi ya Müller, rafiki yake wa tano aliokoka. Müller aliamini katika maombi endelevu.
Tunaomba kwa Unyenyekevu.
Yesu aliomba, “Walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:42). Yesu alijua kwamba anaweza kumtegemea Baba yake katika mapenzi yake kamili.
Maombi ni kitendo cha unyenyekevu. Tunaomba kwa ajili ya watu wengine kwa sababu hatuna uwezo wa kuwasaidia katika hekima zetu; ni lazima tumtegemee Mungu. Tunajiombea wenyewe kwa sababu hatuwezi kuyamudu maisha kwa nguvu zetu wenyewe; ni lazima tumtegemee Mungu.
Maombi yanatambua haja yetu ya kupata msaada wa Mungu. Tunapojisikia tuna uthabiti katika uwezo wetu kukabiliana na matatizo ya maisha, haipingiki kwamba hatuwezi kuomba kwa kumaanisha. Tunapojitambua kwamba hatuwezi kuyakabili maisha kwa nguvu zetu wenyewe, tunaomba kwa unyenyekevu.
Maombi yetu ni lazima yafanyike kwa “unyenyekevu wa ujasiri.” Tunapokuwa tunamngojea Mungu kwaajili ya majibu, tunaweza kuwa na uhakika na amani kwa sababu tunaomba kwa Baba yetu wa mbinguni ambaye anatupenda na anatutakia yaliyo mema kwa ajili ya watoto wake. Katika msongamano wa maisha na huduma, maombi ya unyenyekevu yanatupa tumaini la utulivu kwa Mungu.
Tunaomba Kibinafsi.
Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuanza maombi yao kwa kumtanguliza Mungu kibinafsi., “Bab yetu.” Maombi ya kweli ni ya binafsi. Paulo Miller aliandika kwamba, “Watu wengi wanajitahidi kujifunza kuomba kwa sababu wanazingatia juu ya maombi na siyo juu ya Mungu.”[7] Mara nyingi “tunaongea maombi” kuliko kusema na Mungu. Hili lilikuwa onyo la Yesu kutoka moyoni juu ya kutumia “misemo mitupu” (Mathayo 6:7).
Fikiria mtu anayekuja kwenye meza ya chakula cha jioni akiwa na kundi la hotuba zilizokaririwa. Anasema, “Ninataka kufanya mazungumzo na familia yetu, kwa hiyo nimeandaa maneno yaliyokaririwa.” Haya siyo mazungumzo ya kweli! Tunategemea mtu awe na mazingatio na watu walioko mezani na siyo juu ya maneno atakayotumia.
Ni kwa njia hiyo hiyo, maombi yanazingatia juu ya Mungu kuliko juu ya mafungu ya maneno yaliyokaririwa. Maombi siyo mfumo; maombi ni mahusiano. Maombi ni lazima yawe ya binafsi.
Ni kwa jinsi gani tunafanyika kuwa Watu wa Maombi?
Katika karne ya tano, Anicia Faltonia Proba, mwanamke aliyepewa heshima ya juu wa Kirumi aliomba ushauri kuhusiana na maombi. Proba alitaka kujua jinsi ya kuwa mtu wa maombi. Augustine aliandika barua ndefu ikiwa na ushauri wa hekima kuhusu maombi.[8] Katika sehemu hii, tutaichunguza kanuni ya Augustine kuhusu maombi.
Ni aina gani ya mtu anayeweza kuwa mtu wa maombi?
Kwanza, Augustine anasema kwamba mtu wa maombi ni lazima awe mtu asiyekuwa na vianzo vingine. Mtu mwombaji ni mtu anayetumainia maombi peke yake.
Proba alikuwa mjane wa mmoja wa wanaume matajiri na wenye nguvu sana wa Roma. Wanawe watatu wa kiume walitumika kama Mabalozi wadogo wa Kirumi. Augustine alianza kwa kumwambia Proba kwamba “ni lazima ajihesabu mwenyewe kama aliyejitenga na ulimwengu.” Haijalishi sisi ni matajiri, au wenye nguvu au tuliofanikiwa kwa kiasi gani, ni lazima tujitambue kwamba sisi tutambue kutokuwa na uwezo wowote mbele za Mungu. Vinginevyo, maombi yetu yatakuwa kama maombi ya Mfarisayo badala ya maombi ya Mtoza Ushuru.
Mambo gani tunapaswa kuombea?
Augustine anatoa jibulakushangaza kwa Proba. Anasema, “ Omba kwa ajili ya maisha ya furaha.” Hii inawezekana kuonekana kama ni ubinafsi, lakini Augustine anaelezea kwamba furaha ya kweli inatoka kwa Mungu peke yake. Mtu “ana furaha ya kweli ambayo ana yote anayotamani kuwa nayo, na hataki kuwa na kitu ambacho haipaswi kukitaka.”
Mkristo ana furaha kwa sababu anaye Mungu, na anataka asiwe na kitu ambacho Mungu hangetaka awe nacho. Kama mtunga Zaburi, tunaridhika na uwepo wa Mungu.
Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake (Zaburi 27:4).
Kama kweli tunatamani uwepo wa Mungu juu ya mambo yote, tunaweza tukaomba kwa ajili ya furaha tukijua kwamba Mungu atatosheleza matamanio yetu ya ndani kwa kujitoa mwenyewe kwetu!
Tunapaswa kuombaje katika nyakati za shida?
Augustine anamkumbusha Proba kwamba Paulo alitambua kuna nyakati zitakazokuwepo ambazo “hatujui kuomba jinsi itupasavyo” (Warumi 8:26). Tunapaswa kuombaje tunapofikia hatua ya kutokuwa na msaada?
Augustine anaangalia katika Maandiko matatu. Kwanza, anaelezea mfano wa Paulo wakati alipoomba kwa ajili ya ukombozi wa “kutokwa na mwiba katika mwili wake.” Badala ya ukombozi, Mungu akamwahidi, “Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.” Paulo akashuhudia, “Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu… Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu” (2 Wakorintho 12:8-10).
Pili, Augustine anaangalia mfano wa Yesu pale Getsemane. Yesu alikabidhi haja zake zote kwa Mungu. Yesu aliomba kwa ajili ya ukombozi: “Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke.” Lakini akahitimisha, “Walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe” (Mathayo 26:39).
Mwisho, Augustine anaangalia kutoka katika Warumi 8:26. Tunapokuwa hatujui jinsi ya kuomba, Roho Mtakatifu huongoza roho zetu. Roho “hutusaidia katika madhaifu yetu” na “hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” Wakati tunapokuwa tumekosa maneno ya zaidi ya kuomba, Roho Mtakatifu huyapeleka maombi yetu kwa Baba, ambaye anayapokea na “katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake” (Warumi 8:26-28).
[1]Imenukuliwa kutoka Matt Friedeman, The Accountability Connection. (Wheaton, Illinois: Victor Books, 1992
[2]Edward M. Bounds, Power Through Prayer. (Kenosha, Wisconsin: Treasures Media, n.d.), 2
[3]“Kama unaweza kufanya jambo lolote bila ya maombi, je, inafaa kufanya hivyo?”
- Dr. Howard Hendricks
[4]Dick Eastman, The Hour That Changes the World. (Grand Rapids: Baker Book House, 1995
"Tunayaangalia maombi kama njia ya kujipatia chochote kwa ajili yetu wenyewe; wazo la Biblia kuhusu maombi ni kwamba tuweze kumjua Mungu Mwenyewe."
- Oswald Chambers
[6]"Mwanadamu anaweza kukataa kwa dharau rufaa zetu, akatupilia mbali meseji zetu, akapingana na hoja zetu, akawanyanyasa watu wetu; lakini hawawezi kufanya lolote kinyume na maombi yetu."
- J. Sidlow Baxter
[7]Paulo E. Miller, A Praying Life: Connecting with God in a Distracting World. (Colorado Springs: NavPress, 2009
[8]Philip Schaff, ed. The Confessions and Letters of St. Augustine: Nicene and Post-Nicene Fathers, First Series, Volume 1. (Buffalo, New York: Christian Literature Publishing Company, 1886), 459-469
Hitimisho: Unapojitambua kwamba hujui jinsi ya kuomba
Mara nyingine ukimya ndio jambo bora unaloweza kufanya.[1] Unataka kuomba, lakini hujui ni kwa jinsi gani; maombi hayatakuja. Katika hili ufanyeje? Siri moja ni kuelewa kwamba Kristo ndiye Kuhani wetu Mkuu.
Kama Wakristo wa kiinjili, tunaamini katika ukuhani wa waamini wote. Mafundisho haya makuu ya marekebisho yanafundisha kwamba kila mmoja wetu ana uwezo na njia ya kufika kwa Baba. Hata hivyo, kama haieleweki, mafundisho haya yanaweza kusababisha matatizo ya kiroho. Ninaweza nikashikwa na fadhaa: Je! Niliomba yakutosha? Je! Nilitimiza kwa uhakika sehemu yangu?”
Kwenye kongamano la mwaka 2013, Profesa Alan Torrance alitoa ushuhuda huu kuhusu matatizo aliyokumbana nayo katika maswali haya.
Mnamo Januari 2008, mke wangu Jane alikufa kwa ugonjwa wa Saratani. Alikuwa mwanamke Mkristo wa ajabu sana, mke na mama. Nilipokuwa nikimwangalia akifa kwa maumivu ya saratani iliyoenea katika mwili wake wote, ilikuwa hali ngumu sana na nikiwaangalia watoto wetu wakishuhudia mateso yake ilikuwa ni hali ngumu sana. Kulikuwa na nyakati nyingine, katika huzuni yangu, nilitatizika kujua niombe kwa namna gani na niombe nini. Sikujua jinsi ya kuomba.
Kwa wakati ule, ukuhani wa Kristo ulikuwa ni wa maana zaidi kuliko ninavyoweza kuanza kuelezea. Nilipokuwa nimemshikilia Jane kwenye mikono yangu, kuhani aliyepaa juu (Yesu Kristo) alikuwa akiomba kwa niaba yangu. Tulijisikia tumepumzika kwenye uwepo wake.
Maombi niliyokuwa nikishikilia na kuomba hadi wakati ule ilikuwa ni Sala ya Bwana. Sikuachwa niombe peke yangu. “Baba yangu uliye mbinguni –nimeondolewa mbali na mahali nilipo.” Badala yake kupitia Roho Mtakatifu, Niliomba, “Baba yetu, uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe.”
Kugundua umuhimu wa ukuhani endelevu wa Kristo nikugundua ijnjili katika njia inayobadilisha kila sehemu ya maisha yetu na kuabudu.
Tunashindwa kuelewa ukuhani wa waumini wote tunapofikiri ina maana kwamba nilazima tumwendee Baba kupitia nguvu zetu wenyewe za kiroho. Hili ni kosa. Ukuhani wa waumini wote unasisitiza kwamba hatuhitaji mpatanishi mwingine zaidi ya Yesu. Yeye ndiye anayetuombea, akikubaliana na majaribio yetu yaliyovunjika katika sala, na kuyawakilisha kwa Baba kama dhabihu ya kukubalika. Maombi yetu yanawezeshwa na Roho Mtakatifu na kupatanishwa na Kuhani wetu Mkuu, Yesu Kristo
Wakati unapokuwa hujui jinsi ya kuomba, usikate tamaa. Tunaye mmoja aliye mwombezi wetu, akipiga magoti pembeni mwetu, akituombea kwa Baba, akisema yale ambayo hatuwezi kuyasma.
[1]Sehemu hii imenukuliwa kutoka kwa Marc Cortez, Everyday Theology
(1) Kwa kutumia kitabu cha mpangilio wa maneno cha upatano au programu ya kupekua Biblia, pata mifano mitatu ya maombi katika Biblia. Linganisha kila ombi na Sala ya Bwana, Kuna vipengele gani vya Sala ya Bwana vinavyopatikana katika maombi yaliyoko katika maeneo mengine ya Biblia? Tumia jedwali lifuatalo hapa chini kuweka kumbukumbu za yale utakayoyaona.
(2) Weka jarida la maombi yako kwa mwezi mmoja. Weka taarifa za maumivu yako katika maombi, ushindi wako katika maombi, na majibu ya Mungu kutokana na maombi yako. Tumia jarida hili kuimarisha ukuaji wako katika maisha ya maombi.
SGC exists to equip rising Christian leaders around the world by providing free, high-quality theological resources. We gladly grant permission for you to print and distribute our courses under these simple guidelines:
No Changes – Course content must not be altered in any way.
No Profit Sales – Printed copies may not be sold for profit.
Free Use for Ministry – Churches, schools, and other training ministries may freely print and distribute copies—even if they charge tuition.
No Unauthorized Translations – Please contact us before translating any course into another language.
All materials remain the copyrighted property of Shepherds Global Classroom. We simply ask that you honor the integrity of the content and mission.