Search Course
Search through all lessons and sections in this course
Searching...
No results found
No matches for ""
Try different keywords or check your spelling
Mafundisho Na Mazoezi Ya Kanisa
Course Description
Kozi hii inaelezea ubunifu na mpango wa Mungu kwa kanisa na masomo ya kibiblia kama vile uanachama wa kanisa, ubatizo, ushirika, zaka, na uongozi wa kiroho.
Introduction
Maelezo ya Kozi
Kozi hii inawasilisha dhana ya kibiblia kwa ajili ya kanisa kama kiini cha kazi ya Mungu. Mwanafunzi atapata ufahamu wa Umoja wa Kikristo, uanachama wa kanisa, ushirika, msaada wa kifedha kwa ajili ya huduma, utoaji wa zaka, ubatizo, Meza ya Bwana, nidhamu ya kanisa, na alama za ukomavu wa kanisa. Kozi hii inaelezea kanuni na jinsi ya kuzitumia kwa ajili ya maisha na kazi ya kanisa.
Maelekezo kwa ajili ya Viongozi wa Madarasa
Maelekezo kwa viongozi wa madarasa yamewekwa katika kozi nzima pamoja na maelekezo kwa ajili ya sehemu maalumu za masomo. Zimeoneshwa kwa maandishi ya mlalo.
Maswali yanayohitajika kujadiliwa na shughuli za ndani za darasa zimeoneshwa kwa alama ►. Kwa maswali yanayohitajika kujadiliwa, Kiongozi wa darasa atapaswa kuuliza swali na kuwapa wanafunzi muda wa kujadili hilo swali. Kama mwanafunzi huyo huyo kwa kawaida anakuwa mtu wa mwanzo kujibu maswali kwanza, au kama wanafunzi wengine hawapendi kuwajibika katika kujibu maswali, kiongozi anaweza kulielekeza swali moja kwa moja kwa kumlenga mwanafunzi yeyote: mf “Petro, unawezaje kujibu swali hili?”
Maandiko mengi yametumika katika kozi hii. Vifungu ambavyo vinapaswa visomwe kwa sauti katika darasa vimeoneshwa kwa vichwa vya mishale. Wakati mwingine, marejeo ya maandiko yamekuwa kwenye kifungu kwa kutumia alama za mabano. Kwa mfano: (1 Wakorintho 12:15). Alama hizo ni kwa ajili ya kuunga mkono taarifa iliyoko kwenye kifungu husika. Hakuna ulazima wa kusoma aya zilizoko kwenye alama za mabano.
Kila somo lina angalau nukuu mbili kutoka kwa baadhi ya wanatheolojia katika historia. Wakati wanafunzi watakapofika kwenye nukuu hizi, Kiongozi wa darasa anaweza kumtaka mwanafunzi asome na kuelezea nukuu hiyo.
Masomo yote isipokuwa moja yanakamilika kwa kutoa Taarifa Saba kwa Muhtasari. Kusudi la somo ni kwa mwanafunzi kuweza kuzielewa mambo haya. Wanafunzi watapaswa kujifunza na kukariri mambo yaliyoko kwenye muhtasari. Wanafunzi wanapaswa kusoma na kukariri taarifa hizi. Wanafunzi lazima waandike aya moja kuhusiana na kila taarifa katika muhtasari na kisha kuziwasilisha kwa Kiongozi wa darasa Mwanzoni mwa kipindi kinachofuata cha darasa (zitakuwa aya saba). Kwenye kila aya mwanafunzi atapaswa kuielezea taarifa kama ambavyo ingekuwa anamwelezea mtu ambaye hayuko darasani, Pamoja na sababu inayoeleza kwa nini hii ni dhana muhimu. Mwanzoni mwa kipindi kinachofuata, Kiongozi wa darasa anatakiwa aandaye baadhi ya wanafunzi ambao watashirikishana aya zao walizoandaa pamoja na kikundi chote cha darasa.
Pia mwanzoni mwa kipindi kinachofuata, wanafunzi watapaswa kuandika Taarifa Saba kwa Muhtasari kwa kumbukumbu kutoka kichwani tu kama mtihani wa kuandika wa majaribio ya ufahamu wao. Kiongozi wa darasa atahakikisha kwamba wanafunzi hawafanyi nukuu kutoka kwenye kumbukumbu zao walizoandika, au mwanafunzi mmoja kumsaidia mwingine wakati wa kufanya mtihani. Kama mwanafunzi atakuwa hana uwezo wa kuandika hiyo orodha, anaweza akatakiwa kujaribu kuiandika tena baadaye.
Mojawapo ya kusudi kubwa la kozi hii ni kuwaanda wanafunzi waweze kuwa waalimu. Kiongozi wa darasa anapaswa kuwapa wanafunzi nafasi ya kuinua viwango vyao vya kufundisha. Kwa mfano, kiongozi wa darasa mara kwa mara atapaswa kumpa mwanafunzi nafasi ya kufundisha sehemu fupi ya somo katika darasa.
Kazi ya kufanya ya zoezi la kufundisha: Wakati kozi hii ikiwa inaendelea, mwanafunzi atapaswa afundishe somo, au sehemu ya somo, kwa mtu binafsi au kikundi ambacho siyo sehemu ya darasa. Mwanafunzi anaweza akachagua somo la kufundisha. Zoezi hili linatakiwa lifanyike mara tatu, akiwa na masomo tofauti. Kazi hii ya kufanya haijawekewa utaratibu. Mwanafunzi atapaswa atafute nafasi yake mwenyewe na ahakikishe kwamba kazi za kufanya zinafanyika. Mwanafunzi anapaswa atoe taarifa kwa kiongozi wa darasa kila amalizapo kipindi cha kufundisha.
Kazi nyingine za kufanya zitajumuishwa kwenye kozi nzima: mahojiano, kujifunza Maandiko, kuandika au mitihani. Kazi yeyote ya kufanya iliyoandikwa inapaswa iwakilishwe kwa kiongozi wa darasa kwenye kikundi kinachofuata cha darasa. Kiongozi wa darasa siku zote atapaswa aongoze majadiliano ya kazi ya kufanya na awe na baadhi ya wanafunzi ambao watashirikishana yale waliyojifunza au yale ambayo wameandika.
Kama mwanafunzi atahitaji kupata cheti cha kufuzu mafunzo kutoka Shepherds Global Classroom, atapaswa ahudhurie vipindi vyote vya darasa na amalize kufanya kazi zote zilizotolewa. Fomu imetolewa mwisho wa kozi hii kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kazi za kufanya zilizomalizika.
Ready to Start Learning?
Select a lesson from the sidebar to begin your journey through this course.