Kitabu Cha Taasisi Za Wenyeji
Utangulizi
Kanisa linapaswa kufundisha. Yesu aliliambia kanisa kwenda mahali pote kufundisha amri zake (Mathayo 28:19). Paulo alisema kuwa Mchungaji anapaswa kuwa na uwezo wa kufundisha (1 Timotheo 3:2). Mafundisho haya ni sehemu ya kazi ya kufanya wafuasi. Kanisa linafundisha watu jinsi ya kuishi kama waamini, wanaoishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Mafundisho haya yanapaswa kufanyika kila mahali ambapo kuna waamini. Ki-mkakati makanisa yenye nguvu yanatayarishwa kwa ukweli wa kibiblia na mbinu za kivitendo ili kufundisha watu wao.
Kanisa linapaswa kufundisha.
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine (2 Timotheo 2:2).
Ulazima wa kufundisha huleta ulazima wa mafunzo ya huduma. Paulo alimwambia Timotheo kufundisha watu watakao fundisha wengine (2 Timotheo 2:2). Mafunzo sio suala la kufundisha maarifa tu. Mafunzo sio tu unafundisha waamini kwa faida yao. Mafunzo yanatayarisha waamini kusaidia watu wengine.
Yesu alitoa kipaumbele katika mafunzo ya huduma. Mwanzoni wa huduma yake, alichagua watu wachache ambao wangeweza kuongoza na kupanua kanisa. Hakutumia muda wake wote kuhubiria makutano ya watu; badala yake tunaona mara nyingi alitumia muda wake kufundisha viongozi kumi na wawili. Alipanua huduma yake kupitia wale ambao aliowafundisha.
Shepherds Global Classroom hutoa mafuzo yanayoweza kutumiwa na huduma za wenyeji katika mazingira mbali mbali.
Please select a section from the sidebar.