Utangulizi Wa Elimu Ya Kuitetea Imani
Utangulizi
Jia ni Mkristo mchanga wa Taipei. Amekuwa Mkristo kwa mwaka mmoja. Kwa miezi michache iliyopita, amekuwa akijaribu kushiriki katika Injili na Lee, aliye jirani yake. Lee siyo mwamini na anapenda kumwuliza Jia maswali magumu sana. Mara nyingine Jia anafikiri kwamba Lee ana mashaka ya kweli na anatafuta ukweli; wakati mwingine anafikiri kwamba anataka tu kubishana. Hata hivyo, pamoja na kusudio lake hilo, Jia hujaribu kuwa na heshima na kuonyesha upendo wa Kikristo. Hata akiwa mwamini mchanga, anatambua kwamba siyo tu akili yake, bali hata roho yake, vinavyopaswa kumdhihirisha Kristo kwa jirani yake.
Wiki hii, Lee kwa msisimko alikuja kwa Jia. Kutoka kwenye mtandao, alikuwa amepata orodha ya mambo kumi ya “kuwachanganya Wakristo.” Mtandao unasema, “Hakuna Mkristo atakayeweza kujibu maswali haya. Maswali haya yatadhihirisha kwamba Biblia haiwezi kuaminika.”
Lee akasema, “Jia, nina swali la kukuuliza. Unasema kwamba Biblia ni neno la Mungu na haliwezi kuwa na makosa. Katika Marko 15:25 panasema kwamba Yesu alisulibiwa kwenye muda wa saa tatu, yaani 03:00 asubuhi. Yohana 19:14 anaelezea kwamba Pilato hakuwahi kuitoa hukumu yake hadi ilipofika saa sita, yaani 06:00 mchana. Kama Biblia ni Neno la Mungu, kwa nini aya hizi zinapingana?
► Kama Jia atakuja kwako kwa msaada, utamjibuje? Utakuwa na wasiwasi kwamba Lee amepata kosa katika Biblia? Je, unafikiri kwamba ni muhimu kuwa na uwezo wa kuitetea imani yako?
Please select a section from the sidebar.