Uinjilisti Wa Kibiblia Na Uanafunzi
Utangulizi
► Mwanafunzi atapaswa kusoma Mathayo 28:18-20 kwa ajili ya kikundi.
Baadhi ya watu wanaamini kwamba Agizo hili lilikuwa ni kwa ajili ya mitume tu.
► Je, Agizo hili lilikuwa ni kwa ajili tu ya watu waliolisikia siku ile? Elezea jibu lako.
William Carey aliishi mwaka 1761-1834. Alikuwa mzawa wa Uingereza. Alikuwa mshona viatu aliyekuwa na matamanio makubwa ya kuieneza injili. Kanisa lake halikuwa na shauku kubwa ya huduma ya umisheni wa nje. Waliamini kwamba Mungu tayari alishaamua ni nani atakayemwokoa, na kwamba hakutegemea msaada wa mwanadamu.
Kwenye kongamano la wachungaji, Carey alipendekeza mada ya kujadiliwa: aliuliza kama Agizo Kuu la Yesu ni jukumu la Kanisa hadi mwisho wa dunia, kwa kuwa ahadi aliyoitoa Yesu kwenye Agizo Kuu ni kwamba atakuwa pamoja nao hadi ukamilifu wa dahari. Kiongozi wa lile kongamano akasema, “Kaa chini, kijana mdogo. Wewe ni mtu mwenye shauku sana (msimamo mkali). Wakati itakapompendeza Mungu kuwabadilisha wapagani au makafiri, atafanya hivyo bila ya msaada wako au wangu.”
Tunajua kwamba Agizo hili lilitolewa kwa kanisa hadi mwisho wa dunia. Yesu aliahidi kuwa pamoja nasi tutakaoipeleka injili, hadi mwisho wa dahari, jambo linaloonesha kwamba jukumu la uwajibikaji liko kwa kanisa kwa vizazi vyote. Wanafunzi wa Yesu hawangeweza kulikamilisha jukumu hili katika maisha yao, lakini Yesu alisema kwamba injili itahubiriwa kwa kila taifa (Mathayo 24:14).
Kwa hiyo jukumu la kuhubiri injili linarithiwa na kila kizazi cha kanisa.
► Angalia tena kwa umakini maelezo yaliyoko kwenye Mathayo 28:18-20. Je, ni nini mahususi kinachoagizwa?
Agizo maalumu la Yesu lilikuwa kwamba kanisa liende kila mahali na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake.
Agizo hili ni pamoja na uinjilisti kwa sababu mtu hawezi akawa mwanafunzi wa Yesu hadi pale atakapokuwa ameokoka.
Agizo hili linamaanisha kwamba kanisa ni lazima lifanye uinjilisti na ufuasi kama kipaumbele chake cha kwanza na kuchukua hatua zenye ari kubwa; vinginevyo, halitatimizi sababu za kuwepo kwake.
[1]Fungu la maneno “ulimwenguni mwote” (kila taifa inamaanisha kila kundi la kabila) inaonyesha kwamba kazi ya umisheni wa nje ni agizo, kwa kuwa makundi ya kikabila hayana injili hadi itakapokuwa imepelekwa kwao. Hakuna aina fulani ya watu wanaopaswa kutengwa.
Agizo lenyewe sio kuhubiri injli tu. Mchakato wa kufundisha ni muhimu kwa sababu tunapaswa tufundishe watu wapya waliookoka kila kitu ambacho Yesu aliagiza.
Mwalimu ni lazima adhamirie katika kumtii Kristo kwa sababu ni lazima awe mfano mzuri wa kuigwa, akiwaelezea watu waliookoka jinsi ya kuishi maisha yenye kumtii Kristo.
Mtu aliyeokoka ni lazima adhamirie katika kumtii Kristo kwa sababu kujifunza maagizo ya Kristo tu hakutoshi bila ya kutii anayojifunza. Kama siyo mtiifu kwa yale anayojifunza, anapingana na kazi ya ufuasi. Mchakato wa ufuasi siyo tu wa kielimu, bali kubadilika kitabia.
“Ninajiridhisha zaidi kabisa kwamba kama tungechukua mwelekeo wa Bwana wetu na ahadi za uhakika alizowapa wanafunzi wake wa kwanza kama mwongozo wetu kamili, tungewakuta nao wanastahili kama ilivyo kwa nyakati zetu kama vile walivyokuwa wamepewa awali..”
- J. Hudson Taylor,
“The Call to Service”
Please select a section from the sidebar.